Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Sio kweli mkuu tatizo jamaa alilinda masrahi ya DOWANS maana Zito sasa hivi dhambi hii ndio inayo mtafuna kwa taarifa yako asingejihusisha na hili alikuwa na kila sababu ya kuwa Mwenyekiti.

Mimi sidhani kama alichosema ZITTO kuhusu Dowans ndicho kinamponza. No kwa upande wangu mim nadhani jamaa bado hajakomaa vya kutosha kuongoza taasisi anakurupuka kwenye baadhi ya maamuzi. Anaitaji busara zaidi thats why nikasema kuwa wamuandae ka baadaye. Chadema sasa hivi iko kwenye matatizo je ataweza? au ndiyo wataogeza mengine?
 
No kwa upande wangu mim nadhani jamaa bado hajakomaa vya kutosha kuongoza taasisi anakurupuka kwenye baadhi ya maamuzi.

Yeah hata kwenye DOWANS nako alikurupuka mpaka watu wakashangaa anatetea masrahi ya nani?
 
Demokrasia si photocopy wadau, kumbukeni katika nchi maskini kama tanzania mchakato wa demokrasia ya kweli unajumlisha vitu vingi, hatuwezi tu kuamua mambo eti kwa vile demokrasia inaruhusu mtu yeyote mwenye sifa husika agombee nafasi husika...tanzania haijafikia demokrasia ya kiwango hicho, ndio maana kwa maendeleo ya kweli na dhati anahitajika dikteta ama kikundi cha watu wenye dira sahihi...ili kukuza demokrasia, kwa hatua tuliyopo, alichofanya zitto ni sahihi kabisa, kaonyesha anaweza, lakini pia kaonyesha ana usikivu na busara....kwa kifupi, kajiwekea imani kubwa sana ya baadae....chadema inatakiwa ikuze demokrasia nchini, hivyo inahitaji utulivu wa kweli, mbowe na zitto nadhani wamelielewa hilo...chadema msituangushe baada ya hili tukio, tunawategemea kwa sababu tu mnazo busara na mnajua kusoma nyakati....
Hapa hakieleweki kitu baba, Lugha ni moja tu: Uongozi ubaki moshi, nukta. Chimungunyi wala chitemi.

Hekima itakuja baada ya kuelewana hilo. Mganga wa kienyeji CHINGA kingia mtini, maana kawaelimisha watanzania mpaka amechoka. Lakini huu ni wakati muafaka kwake kurudi ulingoni. Jamani tusidanganyane, CHADEMA ni NGO ya wenyewe wangine ni wasindikizaji tu.

Kinachofanya CCM ishinde ni kwamba vyama vingi vya upinzani havina Long term vision, ama vimejikita kwenye ukabila ama dini, nukta. Mengine yote ni gelesha.
 
Jibu ni moja tu, hawawezi kukubali hicho chama kiongozwe na mtu ambaye sio Mchaga au hajaoa Uchagani. Hicho ni chama cha Wachaga na mashemeji zao.

Akina Zitto, Kitila, Wangwe na wengine ni vibarua tu. Wakijiona wamekua na kutaka kuwanyang'anya wenye mali chama chao watakiona cha mtema kuni.

Waongeze tu kwenye katiba yao hayo maneno badala ya kuwadanganya Watanzania.

Hata jimbo la Mbeya vijijini mlilokuwa na nafasi ya kulichukua sasa hamtalipata tena. Huku mikoa ya kusini inabidi msahau kabisa.

Kuna moderator kazi yake kufuta posts zangu, sijui naye ni Mchaga Ha haaaaa! Nifungieni tu mwaka huu kwasababu nasema ukweli. Mimi toto tundu nitapata njia nyingine ya kutoa mawazo yangu.
 
Sio kweli mkuu tatizo jamaa alilinda masrahi ya DOWANS maana Zito sasa hivi dhambi hii ndio inayo mtafuna kwa taarifa yako asingejihusisha na hili alikuwa na kila sababu ya kuwa Mwenyekiti.

Sawa tu assume ni Dowans ndio inamtafuna.
Lakini hiyo dowans angeamuliwa na wapiga kura kwa kumnyima huo uenyekiti ama tuhuma zote mnazommwelekezea zingetumika ktk saduku la kura, na si vinginevyo.
 
Nyie wachagga kama wakikuyu tu mumelawiti demokrasia changa
 
Haya yanayotokea ndani ya Chama Cha CHADEMA ni Mkakati wa Siku Nyingi sana wa Kukifanya Chama hicho kuwa ni Cha watu wa KASKAZINI, wengine wote ni wa KUTUMIWA hii ni dalili Mbaya sana Kwa Demokrasia ya Vyama vingi na Inasikitisha sana Watu Waliojifanya kuwa wako Mbele Kupambana na MAFISADI kumbe wao ni Mabingwa wa UFISADI mbaya zaidi wa KUIBANA DEMOKRASIA ya Mawazo Mbadala yatakayo waletea WATANZANIA NEEMA.

Lakusikitisha zaidi ni hii Kamati ya WAZEE ambayo haina mamlaka kikatiba kuingilia U huru wa mtu, pahala pekee panapo maamuzi ya KIKATIBA ni Mkutano Mkuu wa Taifa ambao unakusanya wajumbe kutoka kila Mkowa ambao wao wanapaswa kufanya maamuzi ya kikatiba ya Kupiga KURA na kutowa Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na wengine lakini wamenyimwa haki yao hiyo ya Kikatiba kwa Uwamuzi wa Kihafidhina ulijilita katika misingi michafu ya UZAWA uLIOKITHIRI Ndani ya Chama. Lakusikitisha na Kuhudhunisha ni Kwa ZITTO Kujimaliza kisiasa na najuwa kuwa sasa yale matumaini ya Watanzania Wengi juu yake yatakatika na nihatari ya Kuwa na Viongozi kama Zitto katika Taifa hili.

Kiongozi makini na Mahiri ni Yule anaesimamia maamuzi yake na hasa yakiwa ni Magumu hadi anahakikisha kuwa Maamuzi yake yanafika pale alipokusudia sio Kuyaacha njiani kama hivi alivyofanya Msaliti huyu wa Demokrasia.
Naamini zitto hajaharibika akili kwani alipoamuwa kuwa anataka kuwa Mwenyekiti alijuwa kuwa Mbowe nae yupo na nataka kama yeye kwani hatukupa kumsikia Mbowe akisema kuwa Anastaafu? na atastaafu vipi kwenye Chama mali yake, lakusikitisha ni Kwa zitto kuwasaliti Waliomuunga Mkono ama kisiri au hadharani wakiwemo Viongozi wenzake Kutoka Mikowani na hata makao Makuu hawa amewaweka katika hali mbaya sana kwani tayari amewatengenezea Uadui na Wakubwa wa Mkao Makuu na Wapambe wao hata itapelekea kutoaminiwa na hata kufikia kufanyiwa vitimbwi ili waachie nafasi zao yote haya Kwa USALITI wa Zitto kabwe alieyavulia MAJI NGUO AKASHIDWA KUYAKOGA alie amuwa KUMUONEA HAYA MKE NDUGU HAKIKA HATOZAA NAYEEEEEE.
 
Hii nilidhani ni uzushi.... Invisible sasa naamini kwamba hakuna tofauti....

Kwangu mimi sasa naona umuhimu wa ule msemo wa 'Its better the devil you know than an angel you dont know"...
CHADEMA wametumia mbinu za ajabu sana hata kumtengenezea mambo/kashfa nzito huyu kijana Zitto ili tu aondoe jina lake!!

Huu ni upuuzi mtupu
 
Mimi sidhani kama alichosema ZITTO kuhusu Dowans ndicho kinamponza. No kwa upande wangu mim nadhani jamaa bado hajakomaa vya kutosha kuongoza taasisi anakurupuka kwenye baadhi ya maamuzi. Anaitaji busara zaidi thats why nikasema kuwa wamuandae ka baadaye. Chadema sasa hivi iko kwenye matatizo je ataweza? au ndiyo wataogeza mengine?
Wapiga kura wataliona hilo, kwani hawamjui Zitto. DJ ndio kakomaa. Alikabidhiwa chama hakuwa na uzoefu na CV kama ya Zitto leo hii. Tusidanganyane. Moshi, kituo, hakuna mjadala.

Tusidanganyane Hii ni NGO ya wenyewe. Zitto ameshawaonya kuwa ili kukinusuru chama au kukiunganisha chama basi lazima Mbowe ajiengue.

Na lugha yake mbona nyepesi sana: tujiengue sote wawili, sasa anachoshindwa Mbowe ni nini?

Halafu angalia, Mwanakijiji naye kaingia mtini, atacoment nini na mambo yameshaeleweka?
 
Je, Kujitoa Kwako Kugombea Uenyekiti Kunajenga au Kunabomoa Chama?

Ndugu Zitto Kabwe (MB),

Nimeamua kukuuliza swali hili la wazi kwa faida ya Jamii ya Kitanzania kwa ujumla. Ningeweza kukuuliza kwa faragha ila kufanya hivyo kungenisaidia mimi binafsi. Naamini suala hili linapaswa kujadiliwa kwa uwazi na ukweli.

Nilikuwa safarini hivyo nilipitiwa na hizi taarifa za wewe kujitoa kugombea Uenyekiti. Leo baada ya kusoma taarifa hizo katika za Vyombo vya Habari nimepigwa na butwaa. Swali kuu nalojiuliza ni, je, kujitoa kwako kutasaidia kuleta huo umoja ndani ya chama chenu au ndio utakigawa zaidi?

Swali hilo kuu linazaa maswali haya mengine ambayo naomba uyajibu:

1. Je, hukuona kuwa utakigawanya chama ulipochukua fomu?
2. Je, huoni kuwa ni hatari kubadili msimamo mzito kama huo?
3. Je, haionekani kuwa umewasaliti waliokuomba ukagombee?

Ndugu nitashukuru kama utanijibu maswali hayo ili nisibaki naamini kuwa hata hicho 'chama kina wenyewe'!

Wasalaam,
Mpiga Kura
 
Last edited:
Acheni uzushi wenu huo maana kila wakati chadema sio chama cha kikabila. Wanafanya kazi nzuri sana

Kweli wanafanya kazi nzuri sana ya kupendelea Wachaga.

Wangwe alisema, mkamwambia ametumwa na CCM.

Zitto kaamua kuwavaa, mnasema katumwa na CCM. Ni nani amefaidika na serikali ya CCM zaidi ya mkoa wa Kilimanjaro?

Tatizo hapa ni kwamba mmeamua kuua demokrasia kwasababu tu ilikuwa inaenda kuchagua mtu ambaye hafanani na viongozi wengi wa CHADEMA. Ni yale yale ya SALIM na CCM mwaka 2005.

Kama mnaamini kwenye demokrasia ni budi kuilinda muda wote.
 
Nyamizi labda Magufuli wao lazima chama lishinde na tushike dola.SHY,MZA na TBR bado watani zetu hawaaingia ndani lazima ushindi
FL,nina mpango wa kumshawishi kaka yangu Sikonge ili atuongoze,maana haya ya Kaskazini mwa TZ yanatuchosha sasa.Huyo Magufuli mwache abaki huko huko alikozoea! WE NEED CHANGE na itoke kwa watu tofoauti na hawa waliopo sasa (Magufuli et al).
 
Lidhwani, JK na Salma wote wako ndani ya CCM na wote viongozi .

Mleta habari umesema Ndesa alipata kura 49 na hakuwa na mpinzani , sasa kama hakutokea mtu kupingana naye je ? Ukiona mzee anapita means anakubalika ambao ndiyo ukweli .Kwamba wapare hawakusimama sasa hii ni shida kubwa ya ukabila naona unakubana sana kaka .Sisi twende tukalazimishe makabila kuingia Siasa nakuoma kugombea ?
kwani wapare wanatokea moshi????
 
Mzee Mtei ana haki ya kushauri pale anapoona mambo yana kwenda vibaya hasa ikizingatiwa yeye ni mwanzilishi wa CHADEMA.Mzee Mtei ni miongoni mwa wanasiasa wachache sana waadilifu na wabunifu ambao taifa hili limewahi kuwanao.Mzee Mtei kutokana na uzoefu wake alishajua CHADEMA ingeweza kugawanyika kama hali ingeachwa iendelee kama ilivyo.Busara na hekima za mzee Mtei ni hazina kubwa kwa CHADEMA,chama cha TLP na NCCR Mageuzi vilikosa na vinaendelea kukosa wazee wa hekima na busara kama kina mzee Mtei,Bob Makani, na prof Mweisiga Baregu.CCM walikuwa na Mwl J K Nyerere baada ya mwalimu kutangulia mbele ya haki hakuna tena mtu wa kutuliza mambo yanapokuwa yamearibika zaidi ya kina Kingunge ambao vitendo vya ufisadi vimewafanya kudharaulika mbele ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Mheshimiwa Zitto Z Kabwe bado ni kijana mdogo sana anayo safari ndefu katika siasa za Tanzania kama atataka kujifunza naamini anaweza kufika mbali.
 
Last edited:
mimi nafikiri ni sahihi kwa zitto kujitoa kwa sababu chama ni institutions na lazima ilindwe hata ikibidi kwa watu fulani kutopata wanachokitaka katika hili linaloitwa demokrasia. mbona hata CCM wanafanya hivyo. Dr. Gharib Bilal alivyochukua fomu zanzibar 2005 wazee walikaa wakamuomba aondoe jina. tusiitafsiri demokrasia kufikiri kila mtu anaweza kufanya lolote na kwa wakati wowote, lazima maslahi ya chama kama institutions yalindwe. wazee wa Chadema ndio wanakijua chama kuliko sisi tulio nje na nafikiri Zitto si mjinga kukubali ushauri wa Wazee. Kwani kuna maslahi gani kama chama kitaingia katika mgawanyiko wakati ni takribani mwaka umebaki kutakuwa na uchaguzi mkuu.

Inabidi tuangalie demokrasia katika uhalisia wake na sio katika falsafa tu.
 
Wachaga wamebaka demokrasia,wasitudanganye eti CHADEMA hiyo ni NGo yao.
Najiuliza ZItto anasema kajitoa ili kulinda mshikamano kwenye chama ina maana wakati anachukua fomu hakulitambua hio?Zitto umetuangusha kwa nini umeshindwa kusimamia maamuzi yako kama ndivyo bora usingechukua fomu
 
Wapiga kura wataliona hilo, kwani hawamjui Zitto. DJ ndio kakomaa. Alikabidhiwa chama hakuwa na uzoefu na CV kama ya Zitto leo hii. Tusidanganyane. Moshi, kituo, hakuna mjadala.

Tusidanganyane Hii ni NGO ya wenyewe. Zitto ameshawaonya kuwa ili kukinusuru chama au kukiunganisha chama basi lazima Mbowe ajiengue.

Na lugha yake mbona nyepesi sana: tujiengue sote wawili, sasa anachoshindwa Mbowe ni nini?

Halafu angalia, Mwanakijiji naye kaingia mtini, atacoment nini na mambo yameshaeleweka?

Kazi kweli kweli
 
owenya%281%29.jpg

Lucy Owenya.

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na mtoto wake, Lucy Owenya, wamechaguliwa bila kupingwa kukiongoza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ndesamburo alichaguliwa tena kukiongoza chama hicho mkoani hapa baada ya kuibuka na ushindi wa kura 49 kati ya 50 za wajumbe wa mkutano huo wakati mtoto wake, Lucy, aliibuka na ushindi wa idadi ya kura kama hizo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana mjini hapa.

Katika uchaguzi huo, Basil Lema, alichaguliwa kuwa Katibu wa chama hicho huku Deogratius Munishi, akichaguliwa kuongoza Baraza la Vijana wa chama hicho na Seranus Mushi alichaguliwa kuongoza Baraza la Wazee wa chama hicho.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Ndesamburo alisema ushindi wake ni ishara kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba bado anakubalika na kamwe hata katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu hapo mwakani, atajitahidi kutetea kwa udi na uvumba kiti chake cha ubunge.

Alisema anashangazwa na propaganda za viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakidai kuwa yeye ni mzee na hivyo hatagombea tena kiti cha ubunge Jimbo la Moshi Mjini jambo ambalo si la kweli.

"Eti wanasema mimi ni mzee, kibabu nimechoka sitagombea tena ubunge...Huo ni uzushi wao na ushindi wangu wa leo ni indiketa ya kwamba uchaguzi mkuu ujao nitatetea jimbo langu na kumbwaga mgombea wa CCM,” alisisitiza Ndesamburo.

Naye Lucy Owenya ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) akizungumza na waandishi wa habari baada ya ushindi huo, alitoa wito kwa wanawake mkoani Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Owenya alisema wanawake hawana budi kuacha woga wa kuwania nafasi za uongozi kuanzia serikali za mitaa, madiwani na hata ubunge ili kuweza kufikisha uwakilishi wa asilimia asilimia 50 bungeni na halmashauri.





CHANZO:

Ndesamburo na Mtoto wake hawakuwa na wapinzani kama itakavyokuwa kwa Mbowe hatakuwa na Mpinzani.

kingine wagombea wote ni wachagga kwani Kilimanjaro si kuna wapare pia?
kwa hiyo mkuu ulitaka msukuma akagombee moshi halafu kwao amwachie nani?????
 
Jamani tusijisahau na kuanza kuzungumzia Ukabila! Kwani Tarime ni wachaga? Mbona chama kinafanya vizuri kule!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom