Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Mimi sidhani kama Zito kakosea hapa. Alikuwa na nia ya kugombea, lakini kasoma upepo kaona achukue busara nyingine. Ni utu bora kutohukumu kabla hujamsikiliza mtuhumiwa.

Huenda kwa kujitoa kunaweza kuwa faida zaidi si tu kwa CHADEMA bali pia kwa upinzani. Hicho kiburi cha Zitto kiko wapi? Tutarajie viongozi wetu kuwa kama robbot? Kwamba wakisema leo wang'ang'anie hata kama wataona harufu mbaya mbele yao katika maamuzi hayo?

Leka
 


Mkuu mi naomba nisikubaliane na wewe.

Hili swala la Zitto liko clear cut kabisa. Argument yako nadhani haina mashiko. Hebu nipe mwanasiasa ambaye amekuwa consistent katika historia? Siasa ni upepo ndo maana wenzetu wana opinion polls huko majuu. Leo ukiangalia upepo unaweza sema nitagombea...ukifika point ukaona mambo hayaendi vizuri unaweza sema nitagombea and V/V. Huwezi tegemea conditions za juzi ziwe sawa na leo. So sioni ubaya wa Zitto kusema sitagombea..I want to do this..later akarudi na kusema jamani ehhee..nimeamua kugombea. Mambo yamebadilika. Mfano..ni wangapi wanasema "next year naenda kufanya Masters au PhD"..lakini katikati mambo yanabadilika wanarudi walikokuwa? Maisha ndivyo yalivyo na kwenye siasa ndo ilivyo. Mpaka hapa sijaona kosa la ndugu Zitto.

Zitto is a politician..you cant expect him to maintain similar positions on some issues as mundane as kuamua kugombea au kutogombea.

Naomba niseme kwamba hili swala by all accounts..lazima watu wataliangalia katika prism ya Uchagga vs..nini sijui. Hata kama hawana hiyo nia. Its simply a human nature to connect the dots. Baba mkwe alikuwa mwenyekiti..akamuachia mkwe..leo..baba mkwe ndo anaongoza kikao cha kuwaengua wagombeaji wengine....simply say..Numbers dont add up. Mzee Mtei angelijua hili angejiengua kabisa. Harafu kwa maamuzi haya ya Chadema ndo yanamfanya Zitto aonekane formidable hata kama kweli Mbowe alikuwa na nafasi ya kushinda. Hivi unafikiri Mbowe akishinda atajisikiaje kuona mgombea mwenzake..'ameenguliwa kwa kulinda mshikamano wa chama'?

Again, nasema hii issue walioifikisha hapa ni Chadema. Mpaka hapa sijaona kosa la Zitto..unless uniambie kwamba wanachadema wana "utaratibu waliojiwekea" wa kuachiana nafasi za wagombea. Kama hilo lipo. Basi nitakuelewa kwamba Zitto ameruka "que" wakati wenzake waliomtangulia bado wako msitarini.
 
Katiba hiyo hiyo ndiyo inyotambua uwepo wa mabaraza mbalimbali ndani ya CHADEMA, Kazi ya mabaraza hayo hutofautiana kuendena na umri na jinsia...mfano kuna baraza la vijana , baraza la wanawake na baraza la wazee.
Baraza la wazee lilimshauri Zito wala halikumlazimisha, na yeye akapima busara yake akajitoa, hapo baraza la wazee lilikua limetimiza jukumu lake la ushauri kwa chama.
Zito anambwembwe nyingi, anapenda kulambwa miguu,anadeka, anajidai,mjivuni...ila mwisho wa yote amewaangusha walio nyuma yake, mwenyewe amenukuliwa akisema amejitoa ili kuleta mshikamano kwa Chama.
Zito akipenda anaweza kwenda akamfuata Kabouru. maana kama anadhani umaarufu ni siraha akamuulize mrema na NCCR ,TLP
 
Haka kamjamaa kanataka kwenda sisiem hiyo ndio bottomest of the bottomest of lines..watch my words.
 
Very Interesting to Compare with What is happening at CHADEMA, I mean the so called CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MEENDELEO.

 
Vijana makini wa CHADEMA sasa hivi wapo kimya kabisa kwakuwa wanajua kilichotokea ni aibu kwao na Demokrasia kwa ujumla.
 
Haka kamjamaa kanataka kwenda sisiem hiyo ndio bottomest of the bottomest of lines..watch my words.
hata mimi naamini hivyo ,na anachotafuta ni sababu ya kulindia umaarufu na heshima yake, aende tu CCM, CHADEMA inajengwa na wanachama na sio umaarufu wakada mmoja-mmoja...
AENDE TU AKUTAKAPO...huenda akapata mkate wake wenye siagi zaidi.
 
Huu mchakato waliotumia CHADEMA hadi kufikia maamuzi ya mwisho..at least kwenye nafasi ya m/kiti.. kwa kweli umenigusa binafsi.

Ulikuwa ni MTEGO katika jina la DEMOKRASIA.
Kwa mazingira ya TZ, kiukweli demokrasia bado ni changa, bado inakuwa. Na si haba kwa CHADEMA.
Kwa hali iliyojitokeza CHADEMA, wangesema waache mambo yaende kufuata mkondo wa demokrasia ya Marekani, Japan, Ujerumani au Uingereza..ambayo tumehubiriwa hapa na wengi; uwezekano mkubwa ulikuwa kukigawa chama katika makundi na hivyo kukidhoofisha zaidi.

Maamuzi yaliyofikiwa yamenishawishi niamini kuwa kweli CHADEMA ni chama makini.
Tupende au tusipende, ule usemi kwamba palipo na wazee wenye busara haliharibiki neno, umejidhihirisha.

Ninawatakia kila la kheri wanaCHADEMA kwenye uchaguzi wenu na mustakabali mwema wa chama chenu hapo baadaye.

Tunatarajia Zitto/Slaa/Mbowe watarudi bungeni na kuwa 'The Lions of parliament' kama alivyokuwa marehemu Edward (Ted) Kennedy 'The Lion of senate' huko ughaibuni.

NB:Ujumbe kwa Dr.Slaa
mkimaliza uchaguzi huu wa ndani, uniandalie KADI ya CHADEMA. Nataka kujiunga rasmi sasa.
 


Zitto naomba ujitokeze hapa utufafanulie yasemayo hapo juu. Je ni kweli ulilazimishwa (shurutishwa) kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho? Na ni nani aliyekulazimisha kufanya hivyo?? Kama ulikubali je, hiyo ndiyo demokrasia kwako?? Tafadhali tupatie majibu!!!
 

Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!!
 
nani kakwambia kuwa alishinikizwa kujitoa? Statement ya zitto haisemi hivyo wewe umeyatoa wapi hayo maneno kuwa alilazimishwa kujitoa?
ushindwe na ..........


Alegee. Akose pumzi afe fiiii!!!
 

Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!! Kwa kituko walichofanya we are starting to see the true color of CHADEMA
 
Nyerere hakuondoa jina la JK kumpitisha Mkapa. Mtei angekuwa anajua siasa kulikuwa na njia nzuri tu za kumpa ushindi mkwe wake bila kuondoa jina la Zitto.
 
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.
 
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.
 
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.

Asante mkuu kwa kunielewa na tumai na wengine wasiopenda ubabaishaji wa kivyama na kuficha makucha watazidi kuelewa
 
hata mimi naamini hivyo ,na anachotafuta ni sababu ya kulindia umaarufu na heshima yake, aende tu CCM, CHADEMA inajengwa na wanachama na sio umaarufu wakada mmoja-mmoja...
AENDE TU AKUTAKAPO...huenda akapata mkate wake wenye siagi zaidi.

Jamaa analeta janja ya nyani kula indi bichi, lakini wengine tulishamshtukia kitambo. PESA ya (yetu walipa kodi kwa kupitia mikono ya) RA si ya kitoto. Kweli adui yako muombee njaa na njaa kweli ni mwanakharamu.

Hii ndio bongo, kila kitu ni usanii. Siasa za kuku!
 

Kama kuwa critical thinker ndiko huku unakofanya kwenye thread hii? Heri ya sisi mafundi tunatwanga nyundo bila kufikiri mara mbili.

Rufiji kwenye hii thread unaongea pumba; hapo nimekuheshimu sana kwasababu michango yako mingine inakuwa ya maana. Vinginevyo ningetumia neno hata bata kuliko hilo.
 
Hivi wajumbe wa mkutano wa mkoa mzima wa Kilimanjaro (ngome kuu) ni 50 tu? Hata kule CUF huo ni uchaguzi wa kata!

Halafu mnajiita chama m-badala, safari mnayo...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…