Yesu anawalaumu walimu wa Sheria na Mafarisayo
(Marko 12:38-39; Luka 11:43,46; 20:45-46)
3 Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao
wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye
maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
6 Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika
masunagogi.
7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na
watu: <Mwalimu.>
11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.
12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
Yesu analaumu unafiki
(Marko 12:40; Luka 11:39-42,44,52; 20:47)
13 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga
mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.
Baadhi ya makala zina aya ya 14: Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
15 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri
baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu.
Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.
23 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu
zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku
mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
24 Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza
ngamia!
25 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha
kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
26 Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa
safi pia.
27 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama
makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini
kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
Adhabu inakuja
29 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga
makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
30 Mwasema: <Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu
hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!>
31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu
waliowaua manabii.
32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!
33 Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?
34 Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima
na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema
iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya
mambo haya.