Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Mimi sidhani kama Zito kakosea hapa. Alikuwa na nia ya kugombea, lakini kasoma upepo kaona achukue busara nyingine. Ni utu bora kutohukumu kabla hujamsikiliza mtuhumiwa.

Huenda kwa kujitoa kunaweza kuwa faida zaidi si tu kwa CHADEMA bali pia kwa upinzani. Hicho kiburi cha Zitto kiko wapi? Tutarajie viongozi wetu kuwa kama robbot? Kwamba wakisema leo wang'ang'anie hata kama wataona harufu mbaya mbele yao katika maamuzi hayo?

Leka
 
Msauzi,

Please be advised that I am not here to defend neither Mbowe nor Zitto. I am just analyzing this issue critically and give each side a fair shake. Trust me, Zitto must change his attitude if he wants to become a formiddable in Tanzania's politics.


Mkuu mi naomba nisikubaliane na wewe.

Hili swala la Zitto liko clear cut kabisa. Argument yako nadhani haina mashiko. Hebu nipe mwanasiasa ambaye amekuwa consistent katika historia? Siasa ni upepo ndo maana wenzetu wana opinion polls huko majuu. Leo ukiangalia upepo unaweza sema nitagombea...ukifika point ukaona mambo hayaendi vizuri unaweza sema nitagombea and V/V. Huwezi tegemea conditions za juzi ziwe sawa na leo. So sioni ubaya wa Zitto kusema sitagombea..I want to do this..later akarudi na kusema jamani ehhee..nimeamua kugombea. Mambo yamebadilika. Mfano..ni wangapi wanasema "next year naenda kufanya Masters au PhD"..lakini katikati mambo yanabadilika wanarudi walikokuwa? Maisha ndivyo yalivyo na kwenye siasa ndo ilivyo. Mpaka hapa sijaona kosa la ndugu Zitto.

Zitto is a politician..you cant expect him to maintain similar positions on some issues as mundane as kuamua kugombea au kutogombea.

Naomba niseme kwamba hili swala by all accounts..lazima watu wataliangalia katika prism ya Uchagga vs..nini sijui. Hata kama hawana hiyo nia. Its simply a human nature to connect the dots. Baba mkwe alikuwa mwenyekiti..akamuachia mkwe..leo..baba mkwe ndo anaongoza kikao cha kuwaengua wagombeaji wengine....simply say..Numbers dont add up. Mzee Mtei angelijua hili angejiengua kabisa. Harafu kwa maamuzi haya ya Chadema ndo yanamfanya Zitto aonekane formidable hata kama kweli Mbowe alikuwa na nafasi ya kushinda. Hivi unafikiri Mbowe akishinda atajisikiaje kuona mgombea mwenzake..'ameenguliwa kwa kulinda mshikamano wa chama'?

Again, nasema hii issue walioifikisha hapa ni Chadema. Mpaka hapa sijaona kosa la Zitto..unless uniambie kwamba wanachadema wana "utaratibu waliojiwekea" wa kuachiana nafasi za wagombea. Kama hilo lipo. Basi nitakuelewa kwamba Zitto ameruka "que" wakati wenzake waliomtangulia bado wako msitarini.
 
Papa sam sikubariani na wewe kwa sababu zifuatazo.Kwanza nafahamu kwamba CHADEMA ina katiba na katiba inasema wazi kuhusu utaratibu wa kugombea nafasi ya uongozi uhuru na haki ya mwanachama kugombea na hii ndiyo Demokrasia na demokrasi na ushindani katika mchakato wa kupata viongozi unazaa viongozi bora pasipo ushindani tunapata viongozi dhaifu.Unaposema ya kwamba hana shukurani kwa waliomfikisha hapo alipo ni kosa vile vile kwani CHADEMA ilipofika sasa mchango wa Zitto ni mkubwa na nimatumaini yangu kama angelipewa nafasi ya kugombe angelishinda na kuleta manufaa zaidi kwa CHADEMA.Unapozungumzia mambo ya kulipana fadhira haya ndiyo matatizo yanayomkabili Mh.Rais JK. analipa fadhira za mafisadi waliomuweka madarakani.Kwa hiyo kwa kiongozi yeyote makini anapoamua kugombea anachopashwa kuangalia ni sifa za uongozi,katiba ya chama chake na uwezo wake katika kukisaidia chama chake.Ni kanuni gani aliyoivunja Mh.Zitto?Uamuzi wa Wazee na uongozi wa juu wa CHADEMA umetutisha na kutusikitisha Tunashindwa kukitofautisha CHADEMA na CCM!Kumbe chama kinawenyewe wao ndio wanaoamua nani awe nani nilikua nikichukulia upuuzi madai ya mgongano kati Chacha Wangwe na viongozi wa juu sasa naamini baadhi ya madai yaliyotolewa.INASIKITISHA!MUNGU IBARIKI TANZANIA
Katiba hiyo hiyo ndiyo inyotambua uwepo wa mabaraza mbalimbali ndani ya CHADEMA, Kazi ya mabaraza hayo hutofautiana kuendena na umri na jinsia...mfano kuna baraza la vijana , baraza la wanawake na baraza la wazee.
Baraza la wazee lilimshauri Zito wala halikumlazimisha, na yeye akapima busara yake akajitoa, hapo baraza la wazee lilikua limetimiza jukumu lake la ushauri kwa chama.
Zito anambwembwe nyingi, anapenda kulambwa miguu,anadeka, anajidai,mjivuni...ila mwisho wa yote amewaangusha walio nyuma yake, mwenyewe amenukuliwa akisema amejitoa ili kuleta mshikamano kwa Chama.
Zito akipenda anaweza kwenda akamfuata Kabouru. maana kama anadhani umaarufu ni siraha akamuulize mrema na NCCR ,TLP
 
Haka kamjamaa kanataka kwenda sisiem hiyo ndio bottomest of the bottomest of lines..watch my words.
 
Very Interesting to Compare with What is happening at CHADEMA, I mean the so called CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MEENDELEO.

Yesu anawalaumu walimu wa Sheria na Mafarisayo

(Marko 12:38-39; Luka 11:43,46; 20:45-46)

3 Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.

4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao
wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.

5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye
maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.

6 Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika
masunagogi.

7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na
watu: <Mwalimu.>

11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.

12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.

Yesu analaumu unafiki

(Marko 12:40; Luka 11:39-42,44,52; 20:47)

13 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga
mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.

Baadhi ya makala zina aya ya 14: Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.

15 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri
baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu.
Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.

23 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu
zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku
mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

24 Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza
ngamia!

25 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha
kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.

26 Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa
safi pia.

27 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama
makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.

28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini
kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

Adhabu inakuja

29 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga
makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.

30 Mwasema: <Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu
hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!>

31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu
waliowaua manabii.

32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!

33 Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

34 Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima
na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.

35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema
iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.

36 Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya
mambo haya.
 
Vijana makini wa CHADEMA sasa hivi wapo kimya kabisa kwakuwa wanajua kilichotokea ni aibu kwao na Demokrasia kwa ujumla.
 
Haka kamjamaa kanataka kwenda sisiem hiyo ndio bottomest of the bottomest of lines..watch my words.
hata mimi naamini hivyo ,na anachotafuta ni sababu ya kulindia umaarufu na heshima yake, aende tu CCM, CHADEMA inajengwa na wanachama na sio umaarufu wakada mmoja-mmoja...
AENDE TU AKUTAKAPO...huenda akapata mkate wake wenye siagi zaidi.
 
Huu mchakato waliotumia CHADEMA hadi kufikia maamuzi ya mwisho..at least kwenye nafasi ya m/kiti.. kwa kweli umenigusa binafsi.

Ulikuwa ni MTEGO katika jina la DEMOKRASIA.
Kwa mazingira ya TZ, kiukweli demokrasia bado ni changa, bado inakuwa. Na si haba kwa CHADEMA.
Kwa hali iliyojitokeza CHADEMA, wangesema waache mambo yaende kufuata mkondo wa demokrasia ya Marekani, Japan, Ujerumani au Uingereza..ambayo tumehubiriwa hapa na wengi; uwezekano mkubwa ulikuwa kukigawa chama katika makundi na hivyo kukidhoofisha zaidi.

Maamuzi yaliyofikiwa yamenishawishi niamini kuwa kweli CHADEMA ni chama makini.
Tupende au tusipende, ule usemi kwamba palipo na wazee wenye busara haliharibiki neno, umejidhihirisha.

Ninawatakia kila la kheri wanaCHADEMA kwenye uchaguzi wenu na mustakabali mwema wa chama chenu hapo baadaye.

Tunatarajia Zitto/Slaa/Mbowe watarudi bungeni na kuwa 'The Lions of parliament' kama alivyokuwa marehemu Edward (Ted) Kennedy 'The Lion of senate' huko ughaibuni.

NB:Ujumbe kwa Dr.Slaa
mkimaliza uchaguzi huu wa ndani, uniandalie KADI ya CHADEMA. Nataka kujiunga rasmi sasa.
 
Edwin Mtei ambaye aliongoza kundi la wazee wanne wa Chadema ambao walimshurutisha Zitto Kabwe kujitoa kwenye uchaguzi wa Chadema na kumpa nafasi Mbowe.

swali la kisheria Mzee Mtei kuongoza kikao hicho na kuwa upande wa Mtoto wake/Mkwe bwana Mbowe inakubalika kisheria?hakuna mgongano wa kimaslahi?

maamuzi ya wazee hawa ni halali? jee kazi ya CC na mkutano mkuu wa Chadema ni nini? kwanini CC ya Chadema isifanye kazi hii ya wazee wanne kuwanyima haki wanaChADEMA wengi?


Zitto naomba ujitokeze hapa utufafanulie yasemayo hapo juu. Je ni kweli ulilazimishwa (shurutishwa) kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho? Na ni nani aliyekulazimisha kufanya hivyo?? Kama ulikubali je, hiyo ndiyo demokrasia kwako?? Tafadhali tupatie majibu!!!
 
Zito amejaa kiburi,dharau na amekua mjivuni....analeta dharau hata kwa walio mfikisha hapo, fikiri anaongea na baraza la wazee, kisha amekubaliana nao maswala fulani yeye anatoka mbio katika vyombo vya habari kuelezea yale ambayo yamezungumziwa kwenye vikao halali vya chama, bado kama raia wakawaida wa Tanzania huu ni mwanzo wa mwisho wakija wetu huyu, kama CHADEMA anadhani hawajamtendea haki anapaswa aende mbele kwa mbele akiwaachia vijana wengine wenye moyo....
CHADEMA inawaheshimu wazee, na hao ni nguzo ya nguvu zake...akina Mtei,Bob Makani na wengineo, hata leo hii WANGEKUWEPO HAI WAZEE KAMA mzee Brown Ngwilulupi ,RIP, bado nidhamu ya chama ni muhimu kuliko kumpoteza muasi mmoja....

Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!!
 
nani kakwambia kuwa alishinikizwa kujitoa? Statement ya zitto haisemi hivyo wewe umeyatoa wapi hayo maneno kuwa alilazimishwa kujitoa?
ushindwe na ..........


Alegee. Akose pumzi afe fiiii!!!
 
Zito amejaa kiburi,dharau na amekua mjivuni....analeta dharau hata kwa walio mfikisha hapo, fikiri anaongea na baraza la wazee, kisha amekubaliana nao maswala fulani yeye anatoka mbio katika vyombo vya habari kuelezea yale ambayo yamezungumziwa kwenye vikao halali vya chama, bado kama raia wakawaida wa Tanzania huu ni mwanzo wa mwisho wakija wetu huyu, kama CHADEMA anadhani hawajamtendea haki anapaswa aende mbele kwa mbele akiwaachia vijana wengine wenye moyo....
CHADEMA inawaheshimu wazee, na hao ni nguzo ya nguvu zake...akina Mtei,Bob Makani na wengineo, hata leo hii WANGEKUWEPO HAI WAZEE KAMA mzee Brown Ngwilulupi ,RIP, bado nidhamu ya chama ni muhimu kuliko kumpoteza muasi mmoja....

Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!! Kwa kituko walichofanya we are starting to see the true color of CHADEMA
 
Nyerere hakuondoa jina la JK kumpitisha Mkapa. Mtei angekuwa anajua siasa kulikuwa na njia nzuri tu za kumpa ushindi mkwe wake bila kuondoa jina la Zitto.
 
Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!! Kwa kituko walichofanya we are starting to see the true color of CHADEMA
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.
 
Zitto hana kiburi wala nini, Je wewe ungekuwa nafasi hiyo ungefanyaje na Mizee hiyo ya Chadema inamng'akia asigombee.....Sasa tumeshapata wasiwasi na hiki chama yaani wamefuliaaaaa mbayaaaa!!!! Kwa kituko walichofanya we are starting to see the true color of CHADEMA
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.
 
Daima msomi,mwanaharakati,mwanamapinduzi ambae hawezi kusimamia anachokiamini huyo ni hayawani na msaliti wa mawazo yake, mwanaume jasiri husimamia kile anachokiamini hata kama anabaki peke yake.

Asante mkuu kwa kunielewa na tumai na wengine wasiopenda ubabaishaji wa kivyama na kuficha makucha watazidi kuelewa
 
hata mimi naamini hivyo ,na anachotafuta ni sababu ya kulindia umaarufu na heshima yake, aende tu CCM, CHADEMA inajengwa na wanachama na sio umaarufu wakada mmoja-mmoja...
AENDE TU AKUTAKAPO...huenda akapata mkate wake wenye siagi zaidi.

Jamaa analeta janja ya nyani kula indi bichi, lakini wengine tulishamshtukia kitambo. PESA ya (yetu walipa kodi kwa kupitia mikono ya) RA si ya kitoto. Kweli adui yako muombee njaa na njaa kweli ni mwanakharamu.

Hii ndio bongo, kila kitu ni usanii. Siasa za kuku!
 
Msauzi,

Please be advised that I am not here to defend neither Mbowe nor Zitto. I am just analyzing this issue critically and give each side a fair shake. Trust me, Zitto must change his attitude if he wants to become a formiddable in Tanzania's politics.

Kama kuwa critical thinker ndiko huku unakofanya kwenye thread hii? Heri ya sisi mafundi tunatwanga nyundo bila kufikiri mara mbili.

Rufiji kwenye hii thread unaongea pumba; hapo nimekuheshimu sana kwasababu michango yako mingine inakuwa ya maana. Vinginevyo ningetumia neno hata bata kuliko hilo.
 
Hivi wajumbe wa mkutano wa mkoa mzima wa Kilimanjaro (ngome kuu) ni 50 tu? Hata kule CUF huo ni uchaguzi wa kata!

Halafu mnajiita chama m-badala, safari mnayo...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom