Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Wakati namsubiri Zitto aje kujibu barua yangu ya wazi, ngoja niendelee na dhahania:

Inawezekana Zitto alijua fika lililotokea litatokea wakati anajaza na kurudisha fomu.

- Kama alijua inawezekana basi alichukua fomu ili kulifanya lililotokea litokee
- Kama hakujua inawezekana basi hakuujua uzito wa Wazee na Mwenyekiti
- Na kama alifanya akijua basi inawezekana alifanya hivyo kufikisha ujumbe
- Na kama alifanya bila kujua basi inawezekana hakijui vyema chama chake

Swali la kujiuliza ni: Je, Viongozi na Wazee wa Chama wanajua walitendalo?

Pengine kuna umuhimu pia wa kuwasamehe wale wote wasiojua walitendalo!
 
Jembe Ulaya,na wanachadema wenzako,kwa hakika sasa mmefikia mahali pabaya,chadema kama vyama vyote vya upinzani tanzania sio maarufu bila ya kuweposome figures amazo wananchi wanazikubali,,,kama mnafanya character assassination ya kumuuwa zitto ,kitila etc soon mtakosa mvuto wa kisiasa na mtakuwa chama dhaifu....chadema kigoma ilidhoofishwa sana na mbowe as ugomvi wake na kabouru ulipelekea hata alipoenda kigoma asipande kumnadi kwenye mkutano wa hadhara.matokeo yake jama akarudi ccm.zitto kajitoa sasa mnadai kuwa anatoa rushwa....chadema mnahitaji mabadiliko walau mpunguze ata idadi ya madereva wachaga makao makuu yenu.
 
Zitto hongera sana wanajamii na watanzania wapenda demokrasia tupo pamoja wameyakoroga na watayanywa.
 
hahahah! jamni nafikiri yule ndugu yetu hajafikia umri. Unakumbuka usemi wa Baba wa Taifa alivyomsikolifai mheshimiwa mwenye nchi ile 95, watu tumeshupaaa nae sasa angalia inavyoendelea. Kuna watu wanaona mbali jamani tuwape chances zao.

Nafikiri Mtei yuko sahihi, ZItto awe mpole
 


mbowe "hakumnadi" kaburu kwasababu kaburu aliamua kusafiri katikati ya kampeni kwenda afrika kusini wakati anajua ratiba ya mbowe kulitembelea jimbo lake. Alimwombea kura lakini presence ya kaburu haikuwepo kwenye jukwaa, kosa la nani? na hio ndio sababu kaburu ahamie ccm???

zitto kajitoa sasa mnadai kuwa anatoa rushwa

Wajumbe wa mkutano wamedai kuna rushwa imetolewa na kambi ya Kafulila nyumbani kwa Zito. Wewe unashauri vipi? Watangaze matokeo bila kufanyia uchunguzi tuhuma?


....chadema mnahitaji mabadiliko walau mpunguze ata idadi ya madereva wachaga makao makuu yenu.

Kwanza tungeanza na serikali kupunguza madereva ambao ni wachaga halafu ndio tuje chadema. tatizo la tanzania wewe hulioni unaliona ni tatizo la chadema tu?
 
Last edited:
Omary ni nini kimekusukuma na ukaamua kuanzisha "Thread" ya uchochezi kama hii ilhali kilichotokea BAVICHA jana kule Mbezi kinafahamika na wajumbe na wanachama wote ambao walikuwepo pale. Naona hii ni direct attack kwa Mbowe na Baraza la Wazee.

Naamini wewe ni Muumini wa Zitto na hili halijaanza leo. Lakini ukiwa kama MwanaChadema (Kama ni Mwanachama) ulikuwa na jukumu la kuhamasisha Mshikamano na Umoja katika Chama badala ya kwa makusudi kabisa katika hii habari yako kuzidi kutengeneza mgawanyiko katika Chama kwa kuwaelezea watu kama Wafuasi wa Mbowe na Wafuasi wa Zitto.

Na mbona matokeo ya Baraza la Wazee yalikuwa yameshatangazwa na sehemu pekee ambayo ilikuwa na walakini ni BAVICHA. Ama hizo taarifa nazo hukupewa? Kaka jaribu kuweka personal interest pembeni unapojaribu kumtumikia Boss wako kwa maslahi ya Wanachadema na Taifa kwa Ujumla.
 
Tatizo ni ukaskazini, na ninashangaa watanzania walio wengi hawaliangalii hili,lazima apatikane Mwenyekiti asiye na chembe ya ukabila, au anatoka kabila ambalo kubebana si jadi yao, MAMBO NI MENGI YA AJABU YANAONEKANA, kwa sababu tunataka chadema iwe ndo tumaini, hata tulioko nje tupigeni kelele kieleweke.
 
We uchagga umekujaa mpaka umekuwa lijinga.
 
 
Zitto,
Umemjeruhi sana Mh Mbowe na Mzee Mtei. Hata kama umeondoa jina kwenye kugombea usidhani utafanya kazi naye kwa kuaminiana, kuelewana na kuheshimiana kama ilivyokuwa kabla haujachukua fomu na kuijaza kwa nia ya kutaka kugombea nafasi hii.
Binafsi ningekushauri upumzike SIASA kwa sasa. Utakaporudi, uje na msimamo usioyumba kwa mambo muhimu kama haya. JK alikatishwa tamaa sana kugombea Uraisi wa Nchi hii tangu 1995. Hakuyumba.
Kwa sasa kaa mbali kidogo na vyombo vya habari.
 
Kibanda na Ngurumo wamejadili hoja kwa kupitia matukio ya Zitto, Mbowe na CHADEMA.
Endeleza mkondo huo wa fikra na mtindo ya kujadili hoja;si watu na ushabiki.
Wakhtanabahu,
 
Rafiki yangu hiyo ndio inaitwa SIASA. Ukishaingia huko uwe tayari na mambo kama haya. Haya yanatokea hata huko CCM, walivyomwambia John Cigwiyemisi ajitoe haikuwa kwenye kikao, bali aliitwa na kushurutizwa kuchomoa fomu yake.

Nadhani Zito ameshayaona mengi kwenye siasa (hasa uozo ndani ya ChaDeMa) lakini njia anayotaka kukimbilia kuyatatua anafanya haraka. Atafute political analysts wamsaidie. You cant fight alone, you need commandas, battalion, section, volunteers etc. He should be strategic rather than opportunist.
 
Mkuu Kanda2 mbona hii makala ipo tayari hapa, kulikuwa na sababu ya kuipost upya mkuu? ipo kwenye thread ya Invisible tayari kuhusu chadema na Zitto
 
CHADEMA bwana! mara hii Zitto keshakuwa mtoa rushwa? Kweli hii Tanzania mtu mdogo hutakiwi kugusa maslahi ya wakubwa.

ZITTO umeambiwa ni fisadi, njoo CCM kwenye chama cha mafisadi uje ule kuku zako. Siasa za Kaskazini mtu wa bara huko Kigoma utaziweza? Mwishowe watakuambia wewe ni Mkongo.
 

Yangu Macho, inawezekana Kibanda yuko sahihi, na Ngurumo je? anyway maswali magumu mara nyingi majibu yake ni Muda tu. Tutasikia mengi mwaka huu. Ni mwaka ambao Kondoo watajipambanua na Mbwa Mwitu hali kadhalika.
 

Tukiwa na Wahandisi wa Fikra Ndogo kama zako Basi hatutaweza kujenga hata visima.

Wakaskazini wanakutisha sana ee, Usiwaogope ndugu yangu, they are just aggressive na si kingine
 

Umejuaje kama ni Wachagga, Unajua mtu mzima na Familia yako unapokuwa Mbeya ni jambo la aibu hata kwako mwenyewe.

Wachagga ni NOMA, kila sehemu wapo, na watu wanawahara si mchezo
 
Kakwangu ni kajiswali kwa Dr. Hosea,Boss wa TAKAKURU:Kwa kuwa CHADEMA ni Taasisi ya Kitaifa,na kwa kuwa sio siri tena chaguzi nyingi nchini mwetu zinahusishwa na rushwa,je ni jitihada gani ofisi yako ilifanya/inafanya ili kudhibiti vitendo vya rushwa au vinavyoashiria rushwa katika uchaguzi unaoendelea CHADEMA?Nauliza hivi kwa sababu Taasisi yako ndio inatakiwa iwe msemakweli katika masuala nyeti kama haya kwani bila ya hivyo Watanzania tutakuja kutoana ngeu kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi wa kitaalam kama ule ambao Taasisi yako imekuwa equiped na pesa za walipa kodi kuutafuta.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…