Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
CHADEMA tudhihirishieni kama nyie sio chama cha kaskazini mbona mna woga kiasi hicho,eti mpaka kwenye press conference ndo suluhu au ukuu wa chama ni wa watu flaflani..,sikutegemea.....MNATUPA WASIWASI VIPI MKITWAA NCHI???? JIREKEBISHENI TUWAAMINI TENA
 
Invisible,
Mkuu wangu yaani wee niache tu..sina pumzi hapa nilipo..
 
Emotional Intelligence is lacking in some person that's why all this happen.
 
Kwangu network imekatika katika ubongo... Sielewi nini kinaendelea mkuu Mkandara!
Mkuu Invisible, nimeshasema hapo juu kuwa kama Mheshimiwa hajapiga ulabu (mvinyo) kabla ya kuandika post hiyo, basi something wrong somewhere. Acha Mkandara achukie kiasi hicho! na sidhani kuwa ni yeye tuu, wako wengi ambao ni kama wamepigwa ngumi ya utosi ghafla na kuona kiza kimetanda mchana kweupe
 


Kwa maneno haya Zitto unakiri kwamba CHADEMA in ukabila ndo kisa cha kukutosa?? Naomba ufafanuzi hapa tafadhali mimi kama mwanachama.
 
Nina mashaka kama Post hii kaandika Zitto mwenyewe ninayemfahamu. Nahisi kuna mtu ana Password yake ndio kaweka haya maneno hapa.
Ila kama niyeye mwenyewe na hajapiga mvinyo (NAJUA HUU NI MWEZI MTUKUFU) basi something wrong somewhere.

Kaamuwa kutubu mbele ya wananchi ,sasa mnachoshangaa ni nini.

Mtikila alitwaambieni ukweli lakini kwa ugumu wa nyoyo zetu tukamuona hafai tukamponda na mawe kama Yesu vile.

Hakika hakuna jiwe lilo fanya uovu juu ya marehemu litabaki bila kupinduliwa,tuliwaambia tangu mwanzo mkatuona sie wahuni ,tumetumwa lakini ukweli unabaki palepale hakika damu ya maremu inawalilia.

Zitto kaamuwa kutubu kwa nini munamwandama ,mwacheni aseme anayoyajuwa kama kweli mwatafuta demokrasia ama damu za watu.
 
niliombwa kujitoa na nikajitoa kama ilivyotangazwa.
Wakina Zitto Mnatutia aibu kubwa sana, Sikidhani kama watu kama nyinyi mtafanya mambo ya ajabu sana katika kipindi kama hiki. Jaribuni kuwa makini na mambo haya kuyamaliza ndani na sio kama mnavyofanya. Tunahuzuni kubwa sana
 
Mimi bado naomba Zitto tafadhali nijibu thread yango hapo juu ili nirudishe kadi, kwani CHADEMA siyo mama yangu.
 
Nawashangaa sana CHADEMA kwa uamuzi wa kumuondoa Zito kwenye ugombea na kumuacha Mbowe kama mgombea pekee. Nina maswali mengi:
1. Hivi wao hawataki kiongozi bora?
2. Kama wangegombea Zito na Mbowe, nadhani yule aliye bora kati yao ndiye angechaguliwa. Au labda wenzangu hawa wasingefanya hivyo?
3. Na kama kati ya Zito na Mbowe kuna mmojawao ambaye ndiye angependwa na wengi hivyo kuibuka mshindi, wanaona shida gani kupata kiongozi kwa mtindo huo, yaani yule aliyekubalika kwa wengi katika kura?
4.Na maswali mengine mengi tu, naona hii CHADEMA sasa sijui imefuliaaa?
 
Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Zitto,

Can you please "Put the records clear" on the paragraph above?
 

Duh, Zitto haya ungemezea ingekuwa powa sana. Anyway akina Makamba ndo usiseme. Hapa wakulaumiwa ni wewe na Slaa kama sikosei. Anyway sijui katiba yenu inasemaje ila simply kuna UFISADI CHADEMA. Kesho magazetini watakunukuu.

Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!

Eehh, Malizeni halafu Zitto usisahau kuangalia pia friends and advisors wako. at this stage you should have advisors in sectorial. Your future is bright and people especially your friends wanakutumia kama ngazi. si kwa matakwa yao ila kwa priorities zao. Review wote ikiwezekana piga wote chini. Katika kipindi cha miaka mitatu hii wakubomoa ila naamini umejijenga wewe binafsi. cheki ishu ya DOWANS, kugombea tena ubunge, afrika mashariki na sasa uenyekiti. People have these in their mind. they will judge you.....Hizi siasa za upepo ni kwasababu tu watu wamechoka ila zikija siasa za kimarekani utakuwa kama vumbie, waaa haupo.

Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.

Mimi binafsi nakuelewa but tusifikishane kutoelewana.
 
CHADEMA Vunjeni makambi yenu haraka sana inatia aibu kubwa sana
 

Wewe kwa nini unaropoka tu bila kufanya utafiti,inamaana baraza zima la wazee ni wachaga na viongozi wengine waliopo kwenye uongozi chadema ni wachaga.Huu ni upotoshwaji tuu na sio bure umepewa hela na mafisadi ili uchafue hewa hapa jamvini.Kama huna ka kusema si ukae kimya uache wenye data wazungumze.
 

Hakuna napingana na wewe.
Sauli leo paulo alitubu na akawa kiongozi mzuri,mtu anayetenda mabaya na kuja kuyakiri huyu twamhitaji.

Hii move ni sahihi kabisa kwa Zitto hatujui watakuja kufanya nini na plan C baad ya plan B.

Si sahihi kwa zitto kukaa kimya saizi kama anaona dalili za kumwoondoa kutokuwa mwenyekiti bado kuna harakati za kwenda mbali zaidi.

Wewe Mkandara kaa kimya muonja, asali haonji mara moja hujikita na kuchonga mzinga.
 
Wakina Zitto Mnatutia aibu kubwa sana, Sikidhani kama watu kama nyinyi mtafanya mambo ya ajabu sana katika kipindi kama hiki. Jaribuni kuwa makini na mambo haya kuyamaliza ndani na sio kama mnavyofanya. Tunahuzuni kubwa sana

Tell them please. Mambo hayo ya mnayaleta hapa JF kwani JF ni forum ya chamema bana? Mbona mnaharibu sasa? I want to strongly believe that sisiM strategist wanaelekea kufanikiwa kukibomoa na kukimaliza hiki chama. Hatutafika popote kwa style hizi alizoanza mweshimiwa. Suppose JJ nae aje, Mbowe nae aweke yake,Slaa aandike si ndio itakua kwishnei? Mliobaki plz msije kujibu hizi hoja hapa. Kaeni kama kamati fanyeni vikao vya ndani malizeni mambo haya. Msitutie aibu kama mwenzenu Zitto alivyotutia aibu ya karne hii!
 

Unamaana hiyo plan C ni ya kutaka kumuwangwe zitto?
 


Mh. Zitto nafikiri kama ni kweli ulikuwa na nia ya kuchukuwa uwenyekiti ili kuimalisha chama halfu badaye ugomebee ukuu wa nchi nafikiri timing haikuwa nzuri. Sababu yangu ni kwamba umri wako ni mdogo kwa hiyo mpaka ufikie umri wa kugombea urais unahitaji miaaka 12 zaidi. Sasa kama ungechukua leo hakika katika kipindi cha miaka 10 ijayo ungeweza kufanya makosa mambayo angekuharibia. Timing is very important kwenye politics, hiyo jaribu kuangalia when is the right time for you!!! Ila hii haikuwa wakati mzuri kwa mtizamo wangu!!
 
 
MH,Zitto

Poleni na mambo ya uchaguzi,Ila nina mambo kadha nataka kukueleza,kwanza usilalamike sana kuhusu mama yako mzazi kuongelewa kwenye mambo yaliondelea inavyonekana na kwa jinsi ulivyoandika inaonyesha dhairi kabisa mama yako anashiriki kwa karibu saana kwenye mambo yako yakisiasa kwa hiyo ujue kama anajiusisha basi iko siku hata mbeleni atazungumziwa tu,hilo huwezi kulikataa,mpaka labda siku ikiamua kutojiusisha na mambo ya siasa kiundani saana.


Mifano tunayo kama pale tulipoona wakati wa uchaguzi kule marekani ,wakati Obama alipolalamika kuwa wamuache kuongelea familia yake ,ndipo watu walipoibuka nakusema kama hutaki tusimuongelee mkeo basi asipande majukwaa,kwa hiyo bwana mkubwa vumilia tu.

Mh, punguza mambo ya kumwaga data za mambo yanayoendelea kwenye chama chenu !!. yani umeamua hata kutangaza matokeo humu wakati ulitakiwa utulie mpaka wahusika watangaze halafu wewe ndio labda uibuke na kutueleza unachojua ,ila nimegundua kila kikitokea kitu kwenye chama chenu wewe unaibuka na ka breaking News kako, anagalia saana hiyo ni siasa na unapambana na wanene wa hicho chama !!

Hayo mambo ya chuki na fitna inabidi uyazoee ndio siasa usianze kulilia mapema mambo bado saana kama ni bado utakua unania ya kuusaka uonngozi wa juu zaidi ''you have not seen nothing yet''

politics is a dirty game

Take care
 
Wazee nini kimetokea


teh teh teh teh teh teh
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…