Hivi ukiwa kama Kiongozi Mkuu kwenye Ukatibu Mkuu Makamu hivi huoni kuwa umeingilia huo uchaguzi kwa kusema wewe mwenyewe kuwa ulifanya kampeni wazi wazi kwa vijana hawa wadogo huoni kuwa ukutenda kosa??
Hivi mtu ukishakuwa naibu katibu mkuu unakosa haki ya kumpigia kampeni mgombea unayemwamini hata kama umejivua majukumu yote ya kusimamia uchaguzi? Hivi hawa vijana wadogo kwa Zitto mwenye umri wa miaka 33 ni wapi hao? Kama Zitto alijitoa katika shughuli za kusimamia uchaguzi na yeye ni mjumbe wa mkutano wa vijana ni wapi amekosea? Na kati ya Zitto na ninyi ni kina nani ambao wamo katika timu ya kusimamia uchaguzi lakini pia wanakuwa mbele kupiga kampeni chafu dhidi ya Zitto na sasa mmekimbilia kwa watu wanaomuunga mkono?
Kwa taarifa yenu Zitto hakuwa na nia ya kufanya kampeni zaidi yakumsaidia kimawazo Kafulila hadi mlipojikusanya wote na baadhi yenu mkiwa wasimamizi wa uchaguzi kuenda kuanza kumfanyia kampeni mtu "wenu" eti kumuonyesha siasa Zitto. Hapo ndipo mlipo likoroga. Zitto alishakuwa tayari kujishusha na kum-approach Mbowe for genuine reconciliation lakini kwa utoto wenu mkajiona kuwa mmemshinda na mtaweza "kummaliza". That wa a big mistake kwenu lakini pia kwa maslahi ya chama chenu.
Mh Zitto! kwenye kipindi kama hiki kizito kwa chama kwanini usiwe na moyo kama wa mwenyekiti wako Mbowe ukakaa kimya kwa masrahi ya chama kwanza, unapoanza kusema mambo ya Fedha (CAG) huoni kuwa hapo kuna mushkeli,
Hivi Mbowe amekaa kimya? Yaani mtu anayeongea nyumba ya pazia ndio amekaa kimya na huyu anayeongea bila ya kujificha ndiye amekuwa mbaya. Tatizo vijana mnakurupukia profession za watu. Unaibuka huko ulipo unajidanganya kuwa unajua spining bia ya kutambua uwezo na uthubutu wa unayemfanyia spining katika kujibu mashambulizi. Ulitaka uj umwage sumu yako halafu Zitto anyamaze afe kisabuni? Tena hapa Zitto amejicontroal sana maana ninyi ndio mnaojua ni nani na kutoka upande gani wamekuwa wakitumia rushwa katika uchaguzi huu.
Pia kuja hapa kwenye JF forum kumwaga razi lote hilo ambalo kuna utitiri wa wanaCCM kibao, huoni kuwa unavujisha siri??
Siri, yaleyale wtu wanatoka ndani ya CCM kushutumu ufisadi kina Makamba wanasema washugulikiwa kwa kuvuja siri za chama. Uozo na uvundo hauwezi kuwa siri na kuuficha ni kuwalaghai watanzania.
Mimi sina chama ila picha unayoonyesha ni ile ya mapindikizi ya CCM tuliyozoea kuona!!!
Yale yale, wanatokea watu wanawaeleza uovu wa MASIHA FEKI wenu wanaonuka ufisadi na kujidai kuwa wanapiga vita ufisadi huohuo, mnakimbilia kusema kuwa wanaosema uchafu wao watakuwa wametumwa na mafisadi. Hivyo hivyo ndani ya chama chenu mnapofanya mambo ya maovu yaliyopita kiwango cha uvumilivu wakitokea wenzenu kuyasema mabaya hayo mnakimbilia kutafuta mchawi nje ya nyumba...Hapa CCM msiwahusishe kwani ni wenyewe mmeamua kujigeuza asusa yao.
Kubalini makosa yenu, jifunzeni kujisahihisha halafu muanze upya na sio kutaka kushambulia mliowkosea ili kuhalalisha makosa mliyoyafanya na mnaendelea kuyafanya kama spining hii mliyoleta hapa
omarilyas