Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Chadema ina wanachama wengi na sio Zitto peke yake. Kama Zitto anakipenda Chadema, basi natumaini atamuunga mkono yeyote yule atakayepewa nafasi ya uenyekiti wa chadema.

Atakayepewa na nani? Wazee wa CHADEMA au kina nani? Maana kwa mambo yalivyo mpaka sasa huwezi kusema kutakuwa na uchaguzi, bali itakuwa "mkusanyiko" wa wana-CHADEMA kumpitisha rasmi ndugu Mbowe! Sijui itakuwa ni kura zile za mgombea against kivuli kama enzi za chama kushika hatamu....kwi kwi kwi....kweli CHADEMA wamechemsha!
 

Hilo limeongelewa sana hapa na consensus ya wanachama wengi kama sio wote ilikuwa ni kwamba CHADEMA wamechemsha sana kwenye hili. Sidhani kama kuna sehemu yoyote ile mimi nimeunga mkono walichofanya chadema kwenye suala la mgombea wa mwenyekiti.

Katika hili nakubaliana nawe asilimia mia moja.
 

Yeyote atakayetoa uamuzi kwenye chama. Katika hili umenikumbusha sana wakati wa uchaguzi wa Democrats kati ya Obama na Clinton ambako kuna watu ndani ya Democratic Party walikuwa wanamtaka Obama amwachie mama Clinton kwenye uraisi ili Obama apewe umakamo (bila kujali kuwa Obama alikuwa anaongoza kwa delegates kuliko Clinton).

Vyama vya siasa na process zao hunichukua muda sana kuvielewa.
 

Jamaa mmoja alienda kanisani kwa Walokole na kuanza kutafuta mlo.
Akasema kuwa yeye zamani alikuwa ni kibaka na sasa ametubu na anataka kumrudia Mungu. Wakampokea na kumpa kila aina ya msaada. Jamaa akawa mtu wa dini kweli huku akisali na kufanya kila jambo jema.

Siku moja jumapili akaja na kusema kuwa alikuwa anataka KUSUJUDIA. Akasema jinsi yeye alivyokuwa mchawi na kutembea sehemu kibao akiloga usiku na mchana akijifanya mlikole. Baada ya kuishi kwa udanganyifu wa namna hii kwa muda mrefu, nimeona hii tabia niiache.

Walokole walichukia, wakachukua vitu vyake na kuvitupilia mbali na yeye mwenyewe wakamfukuza. Jamaa akalia saana na mwisho akasema:
"Niliwadanganya, mkanipokea. Nimewaambia ukweli, mmenifukuza....."
 

Ha ha haa .. kwa hiyo unataka kusema kuwa ZItto ni mlozi?
 
What Zitto has done can simply be described as a political suicide. I have lost every kind of respect for this man; this guy simply doesn't have neither morals nor values. According to Zitto, he participated in spewing lies and venoms against the late Chacha Wangwe which is totally reprehensible. I think DCI's office will conduct a thorough investigation to get to the bottom of this, since there are a lot of things that we don't know about Wangwe's mysterious death. On the other hand, Zitto's decision to call out Chadema's dirty laundry on this platform says all one needs to know about his persona. To make a long story short, with members like Zitto, Chadema doesn't need enemies.

In order to stop the on going fighting, Mbowe must step aside also ; and if Chadema will ignore our call for the incumbent resignation then should be ready to face ………
 
Wazee,

Kwa mtazamo wangu Chadema, sio kama inavyodhaniwa, inajijengea demokrasia.
Pamoja nakuwa kuna ukiritimba wa 'Wazee', Chadema wameonyesha kuanza kukomaa kidemokrasia, I stand to be corrected.

MB. Zitto Hao wazee wapo kwenye 'Mitandao' history will tell, bado una mda take your time. Detest them.

Hapa nilipo kama sio kunyweshwa maji ya bendera, Chadema ni Chama mbadala wa CCM. Huu bado mtazamo wangu.

Tuombee amani katika kukua kwa demokrasia yetu, tulumbane, tukubaliane tofauti zetu, tuweke mbadala, Tanzania daima tutakuwa na amani.

Vinginevyo tutawakaribisha ndugu zetu wa nje wakatusambaratisha kwa kigezo cha kuimarisha njia za 'Demokrasia'

Halafu tuanze kunyosheana vidole we mdini we mnafiki we spinin we dogo we fisadi we mkabila we mzee wewe wewe wewe; Wenye demokrasia zilizobobea sasa watapata mda wa kunywa kahawa kwenye lazy boy na kutuangalia tunavyovurugana pasipo mwelekeo. Tuusikaribishe ukoloni mamboleo.

Ningependa kuona Demokrasia nchini kwangu, kwenye CCM, Chadema, CUF NCCR-mageuzi sijui wapo? Yaani sehemu zote za siasa na Jamii.

Nitarudia, tulumbane lakini tuwe na mbadala utakao leta tija kwa Mwananchi anayehitaji kuondokana na umasikini na ufukara.

Atanaye Kijiko
 

sio lazima afanye siasa,wao waliosema ametumwa na ccm na kutoa rushwa mbona hamuwaoni kama wana jazba ama wametoa siri?
 
Pamoja mkuu
 

Mzee hii kali sana inabidi ni inote.
 
 
sio lazima afanye siasa,wao waliosema ametumwa na ccm na kutoa rushwa mbona hamuwaoni kama wana jazba ama wametoa siri?

Hapana kaka

Mbona hujakaa kimya dhidi ya RA na Lowasa?? zitto anachofanya ni kupingana na ufisadi ambao mwingine na yeye pia kashiriki,sasa amekuwa mtumwa wa mda sasa ameamuwa kuushusha mzigo.

Kukaa kimya mana yake umekubaliana na ufisadi unaoendelea juu yake na juu ya wananchi.
 
Ingebidi uitumie kule Kyela labda kampeni Mwakalinga isingekuwa kwenye limbo kama ilivyo sasa hivi.

Damu ya Wangwe ya kulilieni udongoni .na hakika hakuna jiwe litalobaki juu ya jiwe jingine.
 
Nimekusoma mkuu..Pa1
 
Mbona ccm wanapolinda mambo yao mnawashambulia??

Huu sasa ni uhuni

Mkuu, CCM ni chama tawala wakati CHADEMA ni chama kinachokuwa. Ni matamanio yangu kuwa na chama ambacho kinaweza kuwa na nguvu kubwa kama ilivyo CCM ili kiweze kusaidia kuleta ustaarabu mpya na utawala bora nchini.

Maamuzi ya CCM si tu kuwa yana manufaa au madhara kwa Taifa zima, bali pia hupelekea mabadiliko ya haraka sana katika maisha ya kila mtanzania bila kujali imani yake kisiasa. Ndio maana ni lazima kusema sana endapo CCM (Chama kikongwe kabisa nchini) kinapofanya mambo yasiyoeleweka. Nakuhakikishia Mkuu, hata Kiongozi wa juu wa CCM angefanya aliyofanya Zitto leo hapa, response ingekuwa kama hii au zaidi kidogo.
 

Kwa sababu hao ni mafisadi .... na wanajaribu kumtoa Mwakyembe kule Kyela ili waweke fisadi mwenzao
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…