Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Chadema ina wanachama wengi na sio Zitto peke yake. Kama Zitto anakipenda Chadema, basi natumaini atamuunga mkono yeyote yule atakayepewa nafasi ya uenyekiti wa chadema.

Atakayepewa na nani? Wazee wa CHADEMA au kina nani? Maana kwa mambo yalivyo mpaka sasa huwezi kusema kutakuwa na uchaguzi, bali itakuwa "mkusanyiko" wa wana-CHADEMA kumpitisha rasmi ndugu Mbowe! Sijui itakuwa ni kura zile za mgombea against kivuli kama enzi za chama kushika hatamu....kwi kwi kwi....kweli CHADEMA wamechemsha!
 
Mkuu,na hili la CHADEMA kuwa na mgombea mmoja wa uenyekiti wa Taifa unalizungumziaje???,si bora Zitto angebaki tu ili kuleta ushindani na kuangalia kama Mwenyekti wa sasa anakubalika miongoni mwa wana CHADEMA badala ya kuwachagulia wana CHADEMA Mwenyekiti(kwangu mimi kitendo cha Zitto kujitoa na kumwacha Mbowe peke yake ni sawa na kuwachagulia wana CHADEMA Mwenyekiti),kuna nini hapa???,ama ndo tunarudi enzi zilee za kupigia kura Sura na kivuli...Inasikitisha sana,demokrasia iko wapi hapa??,CHADEMA kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinatakiwa kiwe mfano wa kuigwa katika suala zima la democracy(Ijitofautishe na vyama vingine ambavyovenyewe na demokrasia ni sawa na mbingu na ardhi)

Hilo limeongelewa sana hapa na consensus ya wanachama wengi kama sio wote ilikuwa ni kwamba CHADEMA wamechemsha sana kwenye hili. Sidhani kama kuna sehemu yoyote ile mimi nimeunga mkono walichofanya chadema kwenye suala la mgombea wa mwenyekiti.

Katika hili nakubaliana nawe asilimia mia moja.
 
Atakayepewa na nani? Wazee wa CHADEMA au kina nani? Maana kwa mambo yalivyo mpaka sasa huwezi kusema kutakuwa na uchaguzi, bali itakuwa "mkusanyiko" wa wana-CHADEMA kumpitisha rasmi ndugu Mbowe! Sijui itakuwa ni kura zile za mgombea against kivuli kama enzi za chama kushika hatamu....kwi kwi kwi....kweli CHADEMA wamechemsha!

Yeyote atakayetoa uamuzi kwenye chama. Katika hili umenikumbusha sana wakati wa uchaguzi wa Democrats kati ya Obama na Clinton ambako kuna watu ndani ya Democratic Party walikuwa wanamtaka Obama amwachie mama Clinton kwenye uraisi ili Obama apewe umakamo (bila kujali kuwa Obama alikuwa anaongoza kwa delegates kuliko Clinton).

Vyama vya siasa na process zao hunichukua muda sana kuvielewa.
 
Binafsi naona Kosa la Zito ni kuanika Siri za Chama hadharani(JF),ndo maana anashambuliwa kama mpira wa kona.Pia ikumbukwe kwamba mara baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombe Uenyekiti wa CHADEMA na kujitoa mengi mabaya juu yake yamesemwa hadharani ambayo kwa namna moja ama nyingine yamemchafua machoni mwa jamii(tuhuma kama anatumiwa na mafisadi,mtoa rushwa nk),na mbaya zaidi baadhi ya tuhuma hizi zilikuwa zikitolewa na viongozi/wazee wa CHADEMA...Zitto aliona kila mtu anamtenga/anamuona msaliti,kwamba jambo lolote baya litakaloitokea CHADEMA yeye ndo ataonekana chanzo..So ili aisulubiwe peke yake akaamua kumwaga ukweli wa yote yaliyo nyuma ya pazia hapa jamvini(Watoto wa mjini wanasema,wewe ukimwaga ugali mi namwaga mboga,ngoma inakuwa droo),mambo ambayo kimsingi yalitakiwa yabaki kuwa ni siri ya chama,hayakutakiwa kutoka nje...Zitto wewe ni mwanasia mzuri sana ndugu yangu,cha msingi punguza jazba,ukiendelea na jazba hautafika kokote(huu ni mtizamo wangu tu),tafuta washauri wazuri na uwatumie ipasavyo....

Jamaa mmoja alienda kanisani kwa Walokole na kuanza kutafuta mlo.
Akasema kuwa yeye zamani alikuwa ni kibaka na sasa ametubu na anataka kumrudia Mungu. Wakampokea na kumpa kila aina ya msaada. Jamaa akawa mtu wa dini kweli huku akisali na kufanya kila jambo jema.

Siku moja jumapili akaja na kusema kuwa alikuwa anataka KUSUJUDIA. Akasema jinsi yeye alivyokuwa mchawi na kutembea sehemu kibao akiloga usiku na mchana akijifanya mlikole. Baada ya kuishi kwa udanganyifu wa namna hii kwa muda mrefu, nimeona hii tabia niiache.

Walokole walichukia, wakachukua vitu vyake na kuvitupilia mbali na yeye mwenyewe wakamfukuza. Jamaa akalia saana na mwisho akasema:
"Niliwadanganya, mkanipokea. Nimewaambia ukweli, mmenifukuza....."
 
Ha ha haa .. kwa hiyo unataka kusema kuwa ZItto ni mlozi?
 
What Zitto has done can simply be described as a political suicide. I have lost every kind of respect for this man; this guy simply doesn't have neither morals nor values. According to Zitto, he participated in spewing lies and venoms against the late Chacha Wangwe which is totally reprehensible. I think DCI's office will conduct a thorough investigation to get to the bottom of this, since there are a lot of things that we don't know about Wangwe's mysterious death. On the other hand, Zitto's decision to call out Chadema's dirty laundry on this platform says all one needs to know about his persona. To make a long story short, with members like Zitto, Chadema doesn't need enemies.

In order to stop the on going fighting, Mbowe must step aside also ; and if Chadema will ignore our call for the incumbent resignation then should be ready to face ………
 
Wazee,

Kwa mtazamo wangu Chadema, sio kama inavyodhaniwa, inajijengea demokrasia.
Pamoja nakuwa kuna ukiritimba wa 'Wazee', Chadema wameonyesha kuanza kukomaa kidemokrasia, I stand to be corrected.

MB. Zitto Hao wazee wapo kwenye 'Mitandao' history will tell, bado una mda take your time. Detest them.

Hapa nilipo kama sio kunyweshwa maji ya bendera, Chadema ni Chama mbadala wa CCM. Huu bado mtazamo wangu.

Tuombee amani katika kukua kwa demokrasia yetu, tulumbane, tukubaliane tofauti zetu, tuweke mbadala, Tanzania daima tutakuwa na amani.

Vinginevyo tutawakaribisha ndugu zetu wa nje wakatusambaratisha kwa kigezo cha kuimarisha njia za 'Demokrasia'

Halafu tuanze kunyosheana vidole we mdini we mnafiki we spinin we dogo we fisadi we mkabila we mzee wewe wewe wewe; Wenye demokrasia zilizobobea sasa watapata mda wa kunywa kahawa kwenye lazy boy na kutuangalia tunavyovurugana pasipo mwelekeo. Tuusikaribishe ukoloni mamboleo.

Ningependa kuona Demokrasia nchini kwangu, kwenye CCM, Chadema, CUF NCCR-mageuzi sijui wapo? Yaani sehemu zote za siasa na Jamii.

Nitarudia, tulumbane lakini tuwe na mbadala utakao leta tija kwa Mwananchi anayehitaji kuondokana na umasikini na ufukara.

Atanaye Kijiko
 
Binafsi naona Kosa la Zito ni kuanika Siri za Chama hadharani(JF),ndo maana anashambuliwa kama mpira wa kona.Pia ikumbukwe kwamba mara baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA na kujitoa mengi mabaya juu yake yamesemwa hadharani ambayo kwa namna moja ama nyingine yamemchafua machoni mwa jamii(tuhuma kama anatumiwa na mafisadi,mtoa rushwa nk),na mbaya zaidi baadhi ya tuhuma hizi zilikuwa zikitolewa na viongozi/wazee wa CHADEMA...Zitto aliona kila mtu anamtenga/anamuona msaliti,kwamba jambo lolote baya litakaloitokea CHADEMA yeye ndo ataonekana chanzo..So ili aisulubiwe peke yake akaamua kumwaga ukweli wa yote yaliyo nyuma ya pazia hapa jamvini(Watoto wa mjini wanasema,wewe ukimwaga ugali mi namwaga mboga,ngoma inakuwa droo),mambo ambayo kimsingi yalitakiwa yabaki kuwa ni siri ya chama,hayakutakiwa kutoka nje...Zitto wewe ni mwanasiasa mzuri sana ndugu yangu,cha msingi punguza jazba,ukiendelea na jazba hautafika kokote(huu ni mtizamo wangu tu),tafuta washauri wazuri na uwatumie ipasavyo....

sio lazima afanye siasa,wao waliosema ametumwa na ccm na kutoa rushwa mbona hamuwaoni kama wana jazba ama wametoa siri?
 
Hilo limeongelewa sana hapa na consensus ya wanachama wengi kama sio wote ilikuwa ni kwamba CHADEMA wamechemsha sana kwenye hili. Sidhani kama kuna sehemu yoyote ile mimi nimeunga mkono walichofanya chadema kwenye suala la mgombea wa mwenyekiti.

Katika hili nakubaliana nawe asilimia mia moja.
Pamoja mkuu
 
Jamaa mmoja alienda kanisani kwa Walokole na kuanza kutafuta mlo.
Akasema kuwa yeye zamani alikuwa ni kibaka na sasa ametubu na anataka kumrudia Mungu. Wakampokea na kumpa kila aina ya msaada. Jamaa akawa mtu wa dini kweli huku akisali na kufanya kila jambo jema.

Siku moja jumapili akaja na kusema kuwa alikuwa anataka KUSUJUDIA. Akasema jinsi yeye alivyokuwa mchawi na kutembea sehemu kibao akiloga usiku na mchana akijifanya mlikole. Baada ya kuishi kwa udanganyifu wa namna hii kwa muda mrefu, nimeona hii tabia niiache.

Walokole walichukia, wakachukua vitu vyake na kuvitupilia mbali na yeye mwenyewe wakamfukuza. Jamaa akalia saana na mwisho akasema:
"Niliwadanganya, mkanipokea. Nimewaambia ukweli, mmenifukuza....."

Mzee hii kali sana inabidi ni inote.
 
sio lazima afanye siasa,wao waliosema ametumwa na ccm na kutoa rushwa mbona hamuwaoni kama wana jazba ama wametoa siri?[/QUOTE]
Kukaa kimya pia ni busara aisee,Zitto angekaa kimya tu,maana nijuavyo mimi ukiargue na fool na wewe utaonekana fool pia(nimequote tu msemo huu simaanishi kuna mtu ambaye ni fool katika mada hii) maana watu watashindwa kuwatofautisha miongoni mwenu wawili nani ni fool na nani si fool.Zitto angekaa kimya ingemsaidia sana aisee
 
sio lazima afanye siasa,wao waliosema ametumwa na ccm na kutoa rushwa mbona hamuwaoni kama wana jazba ama wametoa siri?

Hapana kaka

Mbona hujakaa kimya dhidi ya RA na Lowasa?? zitto anachofanya ni kupingana na ufisadi ambao mwingine na yeye pia kashiriki,sasa amekuwa mtumwa wa mda sasa ameamuwa kuushusha mzigo.

Kukaa kimya mana yake umekubaliana na ufisadi unaoendelea juu yake na juu ya wananchi.
 
Ingebidi uitumie kule Kyela labda kampeni Mwakalinga isingekuwa kwenye limbo kama ilivyo sasa hivi.

Damu ya Wangwe ya kulilieni udongoni .na hakika hakuna jiwe litalobaki juu ya jiwe jingine.
 
Hapana kaka

Mbona hujakaa kimya dhidi ya RA na Lowasa?? zitto anachofanya ni kupingana na ufisadi ambao mwingine na yeye pia kashiriki,sasa amekuwa mtumwa wa mda sasa ameamuwa kuushusha mzigo.

Kika kimya mana yake umekubaliana na ufisadi unaoendelea juu yake na juu ya wananchi.
Nimekusoma mkuu..Pa1
 
Mbona ccm wanapolinda mambo yao mnawashambulia??

Huu sasa ni uhuni

Mkuu, CCM ni chama tawala wakati CHADEMA ni chama kinachokuwa. Ni matamanio yangu kuwa na chama ambacho kinaweza kuwa na nguvu kubwa kama ilivyo CCM ili kiweze kusaidia kuleta ustaarabu mpya na utawala bora nchini.

Maamuzi ya CCM si tu kuwa yana manufaa au madhara kwa Taifa zima, bali pia hupelekea mabadiliko ya haraka sana katika maisha ya kila mtanzania bila kujali imani yake kisiasa. Ndio maana ni lazima kusema sana endapo CCM (Chama kikongwe kabisa nchini) kinapofanya mambo yasiyoeleweka. Nakuhakikishia Mkuu, hata Kiongozi wa juu wa CCM angefanya aliyofanya Zitto leo hapa, response ingekuwa kama hii au zaidi kidogo.
 
Hapana kaka

Mbona hujakaa kimya dhidi ya RA na Lowasa?? zitto anachofanya ni kupingana na ufisadi ambao mwingine na yeye pia kashiriki,sasa amekuwa mtumwa wa mda sasa ameamuwa kuushusha mzigo.

Kukaa kimya mana yake umekubaliana na ufisadi unaoendelea juu yake na juu ya wananchi.

Kwa sababu hao ni mafisadi .... na wanajaribu kumtoa Mwakyembe kule Kyela ili waweke fisadi mwenzao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom