Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
CHADEMA kuweni macho na mapandikizi wa SISIEM ambao watachukua fomu iliwawavuruge mwakani. Kumbukeni ya Marehemu Wangwe.
 
Nina watakia wanachadema Uchaguzi wa amani na upendo katika kukuza demokrasia ya kweli. Tubadilishane uongozi bila chuki na vinyongo na baada ya uchaguzi tukijenge Chama. Ni vyema kuchagua wenye uwezo na tayari kukijenga Chama.
 
Huu ni uchaguzi muhimu kwa Chadema kwa namna ya pekee:

a. NI wakati wa kuwaonesha Watanzania kuwa wamejiandaa kuongoza taifa; yaani timu itakayoingia madarakani ndiyo ambayo itakiongoza chama hiki kuelekea uchaguzi mkuu na hivyo ni lazima iwe timu ambayo inaweza kuunda serikali.

b. Ni wakati muafaka wa kumaliza kabisa migongano ma malumbano yoyote ndani ya Chama hicho kama wanataka wawe na nafasi yoyote ya kuliongoza taifa. Endapo mkutano huu utaingia madudu kama ule wa CUF au kwa namna yoyote kutokea migongano ya binafsi (siyo ya kiitikadi au kikampeni) basi utakuwa ni mwisho wa chadema kama tunavyoijua.

c. Uongozi huo mpya ndio bila ya shaka utaandaa agenda ya uchaguzi mkuu kwa Chadema; hivyo ni lazima uwe ni uongozi ambao unaweza kukubaliana na kutokubaliana kwa hoja na pale wanapokubaliana basi wawe ni viongozi ambao hawatodhoofishana. Hiyo ajenda ndiyo itaamua chama kitakuwa na nafasi gani 2010.
Mzee Mwanakijiji,unalionaje hili la CHADEMA kutumia neno kupinga ufisadi ,kama kauli mbiu,is it, in the long run, a sustainable war cry? itakuwaje Kikwete akiwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi kabla ya uchaguzi mkuu na akawasweka lupango (which is a real possibility when the push will come to a shove and the guy is forced into a survival mode)?
 
kikwete hawezi kukamata mafisadi, Kusila amedhibitisha hilo.
 
CHADEMA Msitufanyie Kiini Macho hivi Kwanini Mnavuruga DEMOKRASIA ya Chama kiasi hiki kwa Ubinafsi wenu tu uliokuzongeni? na baya zaidi Msajili wa Vyama JOHN TENDWA amekaa kimyaaaa akiangalia CHADEMA inavyoivunja katiba yake ya CHAMA.

Tuna Mtaka Msajili wa Vyama azuie mara Moja Mkutano Mkuu wa CHADEMA hadi pale CHADEMA itakapo fanya CHAGUZI zake Kikatiba Kuanzia MATAWI, KATA, WILAYA, MKOWA na Mwishowe ndio TAIFA.
Hivi uhalali wa Viongozi haowanaotaka Kuchaguliwa utakuwa upo wapi? ikiwa wale wanaokuja kuchakuwa hawakuchaguliwaa kihalali? kwa mijibu wa Katiba ya CHADEMA.

Uongozi huu wa sasa ulopo wa CHADEMA ni BOMU au ni MAMLUKI Kwani kwa Taarifa RASMI Chadema haijafanya CGhaguzi zake za ngazi ya chini kikatiba ndani ya hii TANZANIA yetu BARA na VISIWANI na hili ni KOSA ambalo litatumika KIsheria Kuwapinga WAGOMBEA WOTE WA CHADEMA 2010 WATAKAO AMUWA KUGOMBEA KUANZIA UDIWANI, UBUNGE, URAIS KWA SABABAU HAWAKUCHAGULIWA KISHERIA KWA KUWA VIKAO VILIVYOWACHAGUWA HAVIKUWA HALALI KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHADEMA, TENA MUTALIA NA NANI? NA HILI LIPO NA LITAFANYIKA.

WACHENI KUENDESHA CHAMA KAMA KAMPUNI TANZU YA MBOWE NA SLAAA, KAJIFUNZENI KWA WENZENU VIPI CHAMA KINAVYOUNDWA, MKIONA VINAELEA VIMEUNDWAA.
Hii kali,Mdau Kiberengo, una maana delegates watakaokuja kwenye convention watakuwa hawakuchaguliwa na mikoa/wilaya zao? sasa hiyo mandate ya ku attend convention watakuwa wameipata wapi? Duniani kote chaguzi za vyama vyote si huwa zinaanzia grassroots ili kuwapata delegates wa mkutano mkuu,unataka kutuambia CHADEMA hili halikufanyika? no way! anyway katika kila chama kuna ambao huwa wanadai ndo wenye chama lao maana hata CCM huo ni wimbo wa kawaida 'CCM INA WENYEWE,UKIONA VYAELEA,ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI,MUASISI KASEMA ETC ETC ETC.
 
CHADEMA Msitufanyie Kiini Macho hivi Kwanini Mnavuruga DEMOKRASIA ya Chama kiasi hiki kwa Ubinafsi wenu tu uliokuzongeni? na baya zaidi Msajili wa Vyama JOHN TENDWA amekaa kimyaaaa akiangalia CHADEMA inavyoivunja katiba yake ya CHAMA.

Tuna Mtaka Msajili wa Vyama azuie mara Moja Mkutano Mkuu wa CHADEMA hadi pale CHADEMA itakapo fanya CHAGUZI zake Kikatiba Kuanzia MATAWI, KATA, WILAYA, MKOWA na Mwishowe ndio TAIFA.
Hivi uhalali wa Viongozi haowanaotaka Kuchaguliwa utakuwa upo wapi? ikiwa wale wanaokuja kuchakuwa hawakuchaguliwaa kihalali? kwa mijibu wa Katiba ya CHADEMA.

Uongozi huu wa sasa ulopo wa CHADEMA ni BOMU au ni MAMLUKI Kwani kwa Taarifa RASMI Chadema haijafanya CGhaguzi zake za ngazi ya chini kikatiba ndani ya hii TANZANIA yetu BARA na VISIWANI na hili ni KOSA ambalo litatumika KIsheria Kuwapinga WAGOMBEA WOTE WA CHADEMA 2010 WATAKAO AMUWA KUGOMBEA KUANZIA UDIWANI, UBUNGE, URAIS KWA SABABAU HAWAKUCHAGULIWA KISHERIA KWA KUWA VIKAO VILIVYOWACHAGUWA HAVIKUWA HALALI KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHADEMA, TENA MUTALIA NA NANI? NA HILI LIPO NA LITAFANYIKA.

WACHENI KUENDESHA CHAMA KAMA KAMPUNI TANZU YA MBOWE NA SLAAA, KAJIFUNZENI KWA WENZENU VIPI CHAMA KINAVYOUNDWA, MKIONA VINAELEA VIMEUNDWAA.
Ushauri wa Bure; FICHA UPUMBAVU WAKO USIFICHE HEKIMA ZAKO
 
CHADEMA huu ni wakati wa kuweka mambo sawa. Kujipanga kwa kuchagua viongozi bora maana naamini viongozi bora mnao hivyo hao ndiyo wanachama na waTZ wanawahitaji. Khali si nzuri kabisa tunaitaji watu makini wenye vision na wasio waoga na wabinafsi. Kila la kheri kwenye mkutano mkuu.
 
CHADEMA kama Yanga na Simba! Wanachaguana KITAIFA tu. Ndio maana Wabunge wao pia wanahangaika zaidi na masuala ya KITAIFA tu! Wajumbe wa kuja kuwachagua mmewapataje au ni walewale wa siku zote?
 
CHADEMA Msitufanyie Kiini Macho hivi Kwanini Mnavuruga DEMOKRASIA ya Chama kiasi hiki kwa Ubinafsi wenu tu uliokuzongeni? na baya zaidi Msajili wa Vyama JOHN TENDWA amekaa kimyaaaa akiangalia CHADEMA inavyoivunja katiba yake ya CHAMA.

Tuna Mtaka Msajili wa Vyama azuie mara Moja Mkutano Mkuu wa CHADEMA hadi pale CHADEMA itakapo fanya CHAGUZI zake Kikatiba Kuanzia MATAWI, KATA, WILAYA, MKOWA na Mwishowe ndio TAIFA.
Hivi uhalali wa Viongozi haowanaotaka Kuchaguliwa utakuwa upo wapi? ikiwa wale wanaokuja kuchakuwa hawakuchaguliwaa kihalali? kwa mijibu wa Katiba ya CHADEMA.

Uongozi huu wa sasa ulopo wa CHADEMA ni BOMU au ni MAMLUKI Kwani kwa Taarifa RASMI Chadema haijafanya CGhaguzi zake za ngazi ya chini kikatiba ndani ya hii TANZANIA yetu BARA na VISIWANI na hili ni KOSA ambalo litatumika KIsheria Kuwapinga WAGOMBEA WOTE WA CHADEMA 2010 WATAKAO AMUWA KUGOMBEA KUANZIA UDIWANI, UBUNGE, URAIS KWA SABABAU HAWAKUCHAGULIWA KISHERIA KWA KUWA VIKAO VILIVYOWACHAGUWA HAVIKUWA HALALI KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHADEMA, TENA MUTALIA NA NANI? NA HILI LIPO NA LITAFANYIKA.

WACHENI KUENDESHA CHAMA KAMA KAMPUNI TANZU YA MBOWE NA SLAAA, KAJIFUNZENI KWA WENZENU VIPI CHAMA KINAVYOUNDWA, MKIONA VINAELEA VIMEUNDWAA.
Dah! hapa kweli pananitia wasi wasi kwani hizi tetesi za Lwakatare kuw atakuwemo ktk safu ya uongozi,inanibidi niamini point hii,kwani sijui atakuwa amepitia tawi gani na ktk chaguzi gani.. Lkn kila la kheri chadema ktk chaguzi zenu,mapambano kwenda mbele,mpaka ccm ingoke..
 
naamini Lwakatare ataingia mahali fulani hapa

So far hana mchango wowote kwenye chama kwanini apewe madaraka haraka sana?

Watu kama Tundu Lissu na Kitila Mkumbo wapewe nafasi.
pia Mwana mama Chiku Abwao na wasisahau watu wa visiwani kama Asha Abdallah ambaye ni mwana Chadema na Jf.
wasifanye utumbo kama wa Viti maalum vya ubunge hakuna mwakilishi toka Zanzibar.
 
Dah! hapa kweli pananitia wasi wasi kwani hizi tetesi za Lwakatare kuw atakuwemo ktk safu ya uongozi,inanibidi niamini point hii,kwani sijui atakuwa amepitia tawi gani na ktk chaguzi gani.. Lkn kila la kheri chadema ktk chaguzi zenu,mapambano kwenda mbele,mpaka ccm ingoke..
Ni makosa makubwa kumpa mtu cheo bila kupitia process ya wanachama wengine. matokeo yake ndio Chadema walikuwa na wanachama kama JOHN GUNINITA.
 
Mzee Mwanakijiji,unalionaje hili la CHADEMA kutumia neno kupinga ufisadi ,kama kauli mbiu,is it, in the long run, a sustainable war cry? itakuwaje Kikwete akiwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi kabla ya uchaguzi mkuu na akawasweka lupango (which is a real possibility when the push will come to a shove and the guy is forced into a survival mode)?

VITA YA KUPINGA UFISADI Vs VITA YA UFISADI

Lakini uwe UFISADI wa NJE na wa NDANI pia...

omarilyas
 
Ni makosa makubwa kumpa mtu cheo bila kupitia process ya wanachama wengine. matokeo yake ndio Chadema walikuwa na wanachama kama JOHN GUNINITA.

Nakuunga mkono asilimia 100%...Lakini si unakumbuka DEALS za nyuma ya panzia kama zile za JK na LOWASSA hadi ikatulazimu kuliingiza taifa hasara ya mabilioni na karibia kupoteza nchi kwa pamoja ndipo tukaweza (watanzania) kuondokana naye.....

omarilyas
 
So far hana mchango wowote kwenye chama kwanini apewe madaraka haraka sana?

Watu kama Tundu Lissu na Kitila Mkumbo wapewe nafasi.
pia Mwana mama Chiku Abwao na wasisahau watu wa visiwani kama Asha Abdallah ambaye ni mwana Chadema na Jf.
wasifanye utumbo kama wa Viti maalum vya ubunge hakuna mwakilishi toka Zanzibar.

Waache wafu wazike wafu wao...
 
Mbowe anagombea Uenyekiti tena?
 
*Ni wa nafasi ya mwenyekiti wa chama Mkoa Mara
*Ukumbi wageuka uwanja wa mapambano, viti vyarushwa
*Msimamizi avunja mkutano, aahirisha uchaguzi

Na Raphael Okello, Bunda

UCHAGUZI Mkuu wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara jana ulivunjika baada ya wagombea kuchapana makonde ukumbini mbele ya wasimamizi wa uchaguzi baada ya kutokea kutofautiana katika kipengele cha katiba ya uchaguzi.

Wagombea hao wa nafasi ya Mwenyekiti Mkoa wa Mara, Bw. Machage Machage ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime na Bw. Mwita Mikwabe ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Uenezi CHADEMA, walitofautiana msimamo katika moja ya kipengele cha katiba ya uchaguzi ambacho kinamtaka mshindi kufikisha nusu ya idadi ya kura za wajumbe halali baada ya kutakiwa zirudiwe kati yao ili mshindi halali apatikane.

Vurugu hizo zilianza baada ya kipindi cha awali cha kuhesabu kura kumalizika ambapo msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Charles Mwera ambaye ni Mbunge wa Tarime na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutangaza kuwa katika nafasi zote zilizogombewa, isipokuwa Ukatibu, hakuna mgombea aliyefikisha nusu ya kura ya wajumbe.

Kwa mujibu wa katiba ya uchaguzi wa chama hicho, wagombea wawili wa kwanza walioongoza kwa idadi kubwa ya kura, walilazimika kurudia ili kupata mshindi halali.

Msimamo huo wa Bw. Mwera kusimamia katiba ulionekana kuwakera baadhi ya wagombea na wapambe wao hususan wale walioongoza kwa idadi ya kura katika awamu ya kwanza ambapo Bw. Machage aliongoza kwa kura 26 huku Bw. Mwikwabe akiwa na kura 24 na Bw. John Koyi akikusanya kura 14 kati ya 64 za wajumbe halali.

Baada ya malumbano marefu, mkutano ulifikia muafaka na upigaji kura kurudiwa kwa nafasi zote ambapo wakati shughuli ya kuhesabu kura awamu ya pili ikinaendelea, Bw. Machage na wapambe wake walionekana kumsonga songa Bw.
Mwikwabe kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono katiba iliyosababisha kura hizo zirudiwe.

Akionekana kupandwa jazba, Bw. Machage alimfuata Bw. Mwikwabe aliyekaa upande wa pili wa ukumbi na kumrushia makonde na kumshambulia kwa viti ambapo alikwepa kwa kusaidiwa na baadhi ya wajumbe.

Kutokana na vurugu hizo, kabla ya kusoma matokeo ya awamu ya pili, Bw. Mwera alisimama na kuahirisha uchaguzi huo hadi utakapotangazwa tena ambapo aliwaeleza wajumbe kuwa yeye hawezi kuendelea kusimamia uchaguzi ambao unakiuka katiba ya chama kwa maslahi ya watu binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhairisha uchaguzi huo, Bw. Mwera ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la CHADEMA, alisema alitumwa na uongozi wa chama hicho ili asimamie uchaguzi kwa kuilinda katiba.

Alinukuu kanuni ya uchaguzi wa CHADEMA ibara ya 6:3:1(C) kinachomtaka mgombea atangazwe mshindi kwa kufikisha nusu ya idadi ya kura za wajumbe halali waliopiga kura.

“Nimesikitika sana kuona viongozi wanaotakiwa kuongoza watu wanakuwa na utovu wa nidhamu kwa kuvunja katiba ya chama kwa sababu hiyo imenilazimu kuahirisha uchaguzi huu wa viongozi hadi itakapotangazwa tena na chama,”alisema Bw. Mwera.

Kuhusu malalamiko ya baadhi ya wagombea na wajumbe kwamba chaguzi zingine za viongozi
wa chama hicho ngazi ya matawi, kata na wilaya zilikiuka kanuni, Bw. Mwera alisema hana ushahidi huo na kudai kuwa hata kama zilikiuka katiba si kigezo cha kukubali kuvunja katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu ya kutotaka kipengele hicho cha katiba kutumika katika uchaguzi huo, Bw. Machage alidai kuwa katika chaguzi zote za kuwapata viongozi wa ngazi ya tawi, kata na wilaya mkoani humo walishindi walitangazwa kwa kufuata wingi wa kura na kwamba haikuwa lazima kufikisha nusu ya kura za wajumbe wote na kudai kuwa wasimamizi hao, walilenga kumhujumu.

“Kama wasimamizi wa uchaguzi huu wa leo hawawezi kuwatangaza washindi walioongoza kwa idadi kubwa ya kura hadi wafikishe nusu za kura za wajumbe wote basi hata chaguzi zingine za ngazi ya chini zilivunja katiba nazo ni batili zirudiwe ! ”Alilalamika Bw. Machage.

Naye Bw. Mwikwabe ambaye awali aliwahi kuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga aliyejiunga na CHADEMA wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo Jimbo la Tarime kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, marehemu Chacha Wangwe, alisema suala muhimu ni kuzingatia katiba.

Alieleza kusikitishwa na baadhi ya wajumbe na wagombea kushabikia kile alichosema uvunjaji katiba katika chaguzi ndani ya chama hicho.

Kutokana na sakata hilo baadhi ya wajumbe waliohudhuria uchaguzi huo walieleza kusikitishwa na vitendo hivyo na kueleza kuwa kimechafua chama kwa kuzingatia kuwa kila siku CHADEMA kimekuwa makini na kusisitiza maadili mema.

Waliitaka Kamati ya Maadili kuchunguza chanzo cha vurugu hizo na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watakaobainika kuhusika.

SOURCE: Majira
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom