Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Tukiendelea na WOGA huu, CCM itatawala kwa KARNE nyingi zijazo! Tulimjadili sana Chacha, tumwache apumzike tu huko aliko kama kweli kuna maisha mengine baada ya kifo.

Woga gani !! Kutoa jina sio woga pengine ni strategy nzuri !! ukitaka kuingia vitani jihakikishie una silaha za kumwangamiza adui sio unaenda kupigana ukijuwa utashindwa.

Hiyo nec ya chadema kama haimuungi mkono wewe unategemea nini hata akiwa mwenyekiti watampiga chini tu kama alivyopigwa chini makamu mwenyekiti.

Sema waambieni waache unafiki wa kuhubiria demokrasia,mimi binafsi sina soni kwa hili li lungu huwa nalilusha napoona panastahili.

CHADEMA ni wanafiki hili ndilo neno linalowastahili.
 
Lililofanyika kumuomba Zitto ajitoe, kidemokrasia si jambo la afya sana, ila kwa chama kichanga kama Chedema jambo hili lina mantiki yake.
Wengi tunakubaliana kuwa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alikuwa kiongozi mzuri aliyelipenda taifa lake ni kulifanyia mengi mazuri.
Ebu tuangalie yeye alifanya nini wakati Tanzania ikiwa Changa ili kuiepusha na watu ambao wangeweza kuiangusha. Je ilikuwaje akawa Rais na Mwenyekiti kwa muda mrefu? Wakati wake si tulikuwa tunapigia kura yeye na giza? Yote haya aliyafanya ili kuhakikisha watu wanakuwa na msimamo mmoja, maana unapokuwa mchanga ukiruhusu mchanganyiko wa uongozi basi unaweza kuleta mkanganyiko kwa unaowaongoza.
Ni hadi alipoona Taifa limeanza kukomaa ndipo mfumo uliopo hivi sasa akauruhusu. Tunakumbuka kura za kutaka mfumo huu zilikuwa 20% lakini Nyerere akashikia bango kuwa hao 20% wapewe nafasi.
Nadhani hata kwa Chadema walivyofanya vina logic hiyo. Kwamba pembeni kuna CCM, jitu kubwa sana linataka kuwameza, nyinyi mkianza kugongana mnalipa nafasi jitu hili kujipenyeza. Ngoja waendelee kukua tutaona demokrasia ya kweli baadae ila wakati huu ulikuwa ni wa hatari. Kama Zitto mwenyewe alivyosema kuwa wote wawili – yeye na Mbowe wana wafuasi wengi hivyo kutoondoa jina lake kungekigawa chama katika mapande mawili makubwa – je makundi hayo yangeanza kutafunana kama ilivyo ndani ya CCM hivi sasa kweli Chadema ingenusurika?
Je baba wa Taifa alinusuruje mgawanyiko ndani ya CCM mwaka 1995. Si kiuungwana Malecela aliondoa jina lake? Si mnakumbuka hali ilivyokuwa? Kama Malecela angekataa si CCM na ukomavu wake wote ingegawanyika?

Kama CCM na ukomavu wa miaka 35 (wake wakati huo miaka) na kuwepo kwa baba wa Taifa, waliogopa mgawanyiko, itakuwaje kwa Chadema chenye umri wa miaka 15 tu?
 
Mwaka huu mtaongea mengi sana waacheni wana CHADEMA kama mnavyo waacha wana CCM. CHADEMA haitaki mamluki ili wakibomoe chama kwa mgongo eti wa domokrasia wapi na wapi jama tumeshtukia janja ya nyani.[/QUOTE

Aibu aibu..huuu ni ubakaji wa demokrasia Chadema wamefanya
 
lililofanyika kumuomba zitto ajitoe, kidemokrasia si jambo la afya sana, ila kwa chama kichanga kama chedema jambo hili lina mantiki yake.
wengi tunakubaliana kuwa baba wa taifa mwl. Nyerere alikuwa kiongozi mzuri aliyelipenda taifa lake ni kulifanyia mengi mazuri.
ebu tuangalie yeye alifanya nini wakati tanzania ikiwa changa ili kuiepusha na watu ambao wangeweza kuiangusha. Je ilikuwaje akawa rais na mwenyekiti kwa muda mrefu? Wakati wake si tulikuwa tunapigia kura yeye na giza? Yote haya aliyafanya ili kuhakikisha watu wanakuwa na msimamo mmoja, maana unapokuwa mchanga ukiruhusu mchanganyiko wa uongozi basi unaweza kuleta mkanganyiko kwa unaowaongoza.
ni hadi alipoona taifa limeanza kukomaa ndipo mfumo uliopo hivi sasa akauruhusu. Tunakumbuka kura za kutaka mfumo huu zilikuwa 20% lakini nyerere akashikia bango kuwa hao 20% wapewe nafasi.
nadhani hata kwa chadema walivyofanya vina logic hiyo. Kwamba pembeni kuna ccm, jitu kubwa sana linataka kuwameza, nyinyi mkianza kugongana mnalipa nafasi jitu hili kujipenyeza. Ngoja waendelee kukua tutaona demokrasia ya kweli baadae ila wakati huu ulikuwa ni wa hatari. Kama zitto mwenyewe alivyosema kuwa wote wawili – yeye na mbowe wana wafuasi wengi hivyo kutoondoa jina lake kungekigawa chama katika mapande mawili makubwa – je makundi hayo yangeanza kutafunana kama ilivyo ndani ya ccm hivi sasa kweli chadema ingenusurika?
je baba wa taifa alinusuruje mgawanyiko ndani ya ccm mwaka 1995. Si kiuungwana malecela aliondoa jina lake? Si mnakumbuka hali ilivyokuwa? Kama malecela angekataa si ccm na ukomavu wake wote ingegawanyika?

kama ccm na ukomavu wa miaka 35 (wake wakati huo miaka) na kuwepo kwa baba wa taifa, waliogopa mgawanyiko, itakuwaje kwa chadema chenye umri wa miaka 15 tu?

watu wanalinganisha demokrasia ya usa na ya kwetu hapa. Huwezi kupewa nafasi sensitive kihivyo lazima uwe umeandaliwa. Chadema bado kina safari ndefu hivyo lazima kikue kwanza. Msilinganishe ya obama na hillary yakitokea chadema itakufa na hapo tutakuwa tumewapa ccm turufu.
 
Mkuu japo nimechelewa kuchangia mada na inawezekana baadhi ya mambo yameisha fanyiwa maamuzi lakini wacha niweka mawazo yangu kidogo.

Mimi nijuavyo Demokrasia inapokuja issue ya kuchagua ni kuwa kila mmoja ana haki ya kuchaguliwa sidhani kama umri ni kikwazo. Lakini inabidi tujiulize je kweli ZITTO KABWE ameiva vya kutosha kuweza kuongoza taasisi inayokua kama CHADEMA?

Watu wamechangia mengi ya kuponda lakini tujiulize kama kweli ZITTO alikuwa na nia ya dhati mbona hata viongozi wake wamemshangaa? Maana mtu unapokuwa unataka kufanya kitu kizito kama hicho lazima uombe ushauri ili kama kuna tatizo liweze kuwekwa sawa. ZITTO BADO ANATAKIWA KUANDALIWA ILI AWEZE KUWA MWENYEKITI MZURI atakaye kipeleka chama kinakotakiwa kwenda. Lakini kwa sasa jamaa bado mbichi sana. Ametumia tu umaarufu wake sidhani kama alikuwa amedhamilia kiukweli kugombea. WAPAMBE NDIYO WAMEMSHINIKIZA.

KAMA ZITTO KWELI AMEAMUA MWENYEWE BILA KUSUKUMWA NA WATU FULANI ASITOE JINA LAKINI KAMA KUTUMWA KUFANYA HIVYO AFANYE HIVYO AONDOE JINA LAKE.

SIASA ZA BONGO ZIMECHAFUKA HIVYO INABIDI TUANGALIE MAMBO KWA MAPANA YAKE SIYO KURUKIA VITU KWA JUU TU.

Labda kwa kuweka jina alitaka kutumia turufu kama ya kikwete 1995 lakini vinginevyo bado jamaa ni kijana mdogo anatakiwa kupikwa ili aweze kuwa kiongozi shupavu zaidi na mwenye maamuzi ya busara. Siyo ya kukurupuka kama alivyofanya.

Pia kuna ukweli mwingine kuwa CHADEMA wanamtegemea sana MBOWE kwenye mambo yao (sidhani kama kuna makubaliano kuwa mpaka awe mwenyekiti) na pia CCM wanamgwaya jamaa kwani irrespective ya mashambulizi yote wameshindwa kumjeruhi na much less CHADEMA yenyewe. Hivyo ZITTO kujiingiza kichwa kichwa kawapa jamaa turufu kwani SIASA za vyama sasa ni very delicate. Uamuzi wowote unaweza kuleta balaa kama ilivyotokea. Sidhani kama CHADEMA wangekuwa na nia mbaya ya kutowapa VIJANA nafasi hao wote wanaowika sasa tungewajua ikiwemo na ZITTO mwenyewe. Lakini kwa nafasi sensitive kama hizi lazima jamani watu waandaliwe vizuri.

Mimi sisupport ZITTO kuwa mwenyekiti kwa sasa bado ajapevuka vya kutosha. Anaitaji miaka kama mitano zaidi kukaa sawa. Kama ambavyo imevumishwa kuwa no. 1 wanawasiliana naye sasa maamuzi kama haya lazima yaangaliwe vizuri.

jamani kama hmana vya kusema kukaa kimya is best solution, kupevuka maana yake nini? ukisema hivyo ndugu kila kitu kisimame kwa wakati fulani kwani havijapevuka, yees, haukutakiwa kwa senior member kwani bado haujapevuka, au siyo??
 
Wewe kweli ni MACHO MDILIKO.

Wewe kila wazo la mtu ni Shetani?

Usiwe na wasiwasi. Siku Wanyamwezi/Wasukuma tutaanzisha chama chetu basi nyie wengine mtakuwa na hali mbaya sana. Nilifikiri UTAKUWA na akili ya kuliona hilo ila lohh. Sipendi Wanyamwezi waungane na kuwa na chama kimoja maana hakutakuwa na balance. Ila kwa mwenendo wa Chadema na CUF kwa kweli ni au tuwe na chama chetu au TURUDI CCM.

Kuanzia leo NARUDI CCM tukabanane hukohuko na MAFISADI huku nikisubiri Chama cha Ngoshas.
Sikonge,
Chonde usirudi huko for heaven sake! Naungana na wazo lako,Tuanzishe chama letu la NGOSHAS,lakini ni nani atatuongoza? Tusijikute Kina Chenge tena wamedandia.
 
Lililofanyika kumuomba Zitto ajitoe, kidemokrasia si jambo la afya sana, ila kwa chama kichanga kama Chedema jambo hili lina mantiki yake.
Wengi tunakubaliana kuwa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alikuwa kiongozi mzuri aliyelipenda taifa lake ni kulifanyia mengi mazuri.
Ebu tuangalie yeye alifanya nini wakati Tanzania ikiwa Changa ili kuiepusha na watu ambao wangeweza kuiangusha. Je ilikuwaje akawa Rais na Mwenyekiti kwa muda mrefu? Wakati wake si tulikuwa tunapigia kura yeye na giza? Yote haya aliyafanya ili kuhakikisha watu wanakuwa na msimamo mmoja, maana unapokuwa mchanga ukiruhusu mchanganyiko wa uongozi basi unaweza kuleta mkanganyiko kwa unaowaongoza.
Ni hadi alipoona Taifa limeanza kukomaa ndipo mfumo uliopo hivi sasa akauruhusu. Tunakumbuka kura za kutaka mfumo huu zilikuwa 20% lakini Nyerere akashikia bango kuwa hao 20% wapewe nafasi.
Nadhani hata kwa Chadema walivyofanya vina logic hiyo. Kwamba pembeni kuna CCM, jitu kubwa sana linataka kuwameza, nyinyi mkianza kugongana mnalipa nafasi jitu hili kujipenyeza. Ngoja waendelee kukua tutaona demokrasia ya kweli baadae ila wakati huu ulikuwa ni wa hatari. Kama Zitto mwenyewe alivyosema kuwa wote wawili – yeye na Mbowe wana wafuasi wengi hivyo kutoondoa jina lake kungekigawa chama katika mapande mawili makubwa – je makundi hayo yangeanza kutafunana kama ilivyo ndani ya CCM hivi sasa kweli Chadema ingenusurika?
Je baba wa Taifa alinusuruje mgawanyiko ndani ya CCM mwaka 1995. Si kiuungwana Malecela aliondoa jina lake? Si mnakumbuka hali ilivyokuwa? Kama Malecela angekataa si CCM na ukomavu wake wote ingegawanyika?

Kama CCM na ukomavu wa miaka 35 (wake wakati huo miaka) na kuwepo kwa baba wa Taifa, waliogopa mgawanyiko, itakuwaje kwa Chadema chenye umri wa miaka 15 tu?

Sikubaliani na mambo yako mengi kama sio yote.

Mimi ninavyoona Nyerere alichofanikiwa ni kutuunganisha kuwa wamoja pia Nyerere hakuwa mra rushwa na kujilimbikizia fwedha.

Lakini mengine yote Nyerere alifeli.Na yeye alikili haya baada ya kung'atuka.

Na hata hivyo era za Nyerere sio tena era hizi ,huu utegemezi wa fikra eti Nyerere hivi na vile mie nafikiri umepitwa na wakati,tuwe wabunifu kuya modify nyerere mazuri aliyoyaacha na kuleta mazuri mapya.Na sio kuya implement kama yalivyo mambo mazuri ya Nyerere ya wakati huo.
 
Woga gani !! Kutoa jina sio woga pengine ni strategy nzuri !! ukitaka kuingia vitani jihakikishie una silaha za kumwangamiza adui sio unaenda kupigana ukijuwa utashindwa.

Hiyo nec ya chadema kama haimuungi mkono wewe unategemea nini hata akiwa mwenyekiti watampiga chini tu kama alivyopigwa chini makamu mwenyekiti.

Sema waambieni waache unafiki wa kuhubiria demokrasia,mimi binafsi sina soni kwa hili li lungu huwa nalilusha napoona panastahili.

CHADEMA ni wanafiki hili ndilo neno linalowastahili.
Zitto anayumba sana. Sielewi kama ni huo UMRI au UMAARUFU umeanza kumtafuna taratibu! Ametusaidia kumwelewa zaidi. CHADEMA ikiendelea hivi kama akina CUF na Seif, Lipumba na TLP na Mrema basi ile dhana kwamba hii ni CCM B itakubalika. Dr Slaa alisema kwamba hakuna UNTOUCHABLES ndani ya CHADEMA. Sakata hili analionaje?
 
kupevuka maana yake nini? ukisema hivyo ndugu kila kitu kisimame kwa wakati fulani kwani havijapevuka, yees, haukutakiwa kwa senior member kwani bado haujapevuka, au siyo??

Mkuu watu bado wanakumbuka ishu ya DOWANS wamenidokeza hivyo kwa hiyo hawana imani naye ndo maana wengi wanahisi katumwa na wale wale wa huko upande wa pili.
 
Unajua huwa najiuliza kila siku , sawa CCM mafisadi, uongozi mmbovu na mengineyo mengi. seriously am not planning to giv any of them ma vote but the question is WHO IS READY TO TAKE THE WHEEL? kama ambao niliokuwa na imani nao kidogo kwamba waweza kuleta mabadilikko kwenye demokrasia ya nchi hiii ndo wanapalaganyika hivi.......... NANI ATAWEZA?
 
jamani kama hmana vya kusema kukaa kimya is best solution, kupevuka maana yake nini? ukisema hivyo ndugu kila kitu kisimame kwa wakati fulani kwani havijapevuka, yees, haukutakiwa kwa senior member kwani bado haujapevuka, au siyo??

Nashukuru sana kwa mawazo yako kuwa mimi sijapevuka. Lakini hay6o ndiyo mawazo yangu. ZITTO KAKURUPUKA TU NA TATIZO KUBWA LA WATZ NI KUFUATA UPEPO. Hivyo wewe kama unaona kuwa ZITTO kafanya uamuzi sahihi thats u not me. Na pia kwa vigezo vyako kama sijapevuka kuwa senior member mwambie MODERATOR anishushe niwe junior is na gonna change my stand.

ACHENI KUFUATA UPEPO CHADEMA BADO SANA HAIJAFIKA KAMA MNAVYOFIKIRI KUJENGA CHAMA NI PROCESS. Hivi unadhani kama MBOWE na ZITTO wakichuana then mmoja wao akashindwa yakaanza malimbano ndiyo tunachotaka kujenga?

Chadema bado tena sasa hivi iko kwenye delicate state na pia ndiyo kama jicho kwa sasa hivyo wakufanya maamuzi ya hovyo kama kumruhusu ZITTO tutaona yatakayotokea mbeleni.
 
Sikonge,
Chonde usirudi huko for heaven sake! Naungana na wazo lako,Tuanzishe chama letu la NGOSHAS,lakini ni nani atatuongoza? Tusijikute Kina Chenge tena wamedandia.
Nyamizi labda Magufuli wao lazima chama lishinde na tushike dola.SHY,MZA na TBR bado watani zetu hawaaingia ndani lazima ushindi
 
Hii inaonyesha kuwa Demokrasia ya kweli Bongo haipo kabisa. Nadhani kunahaja ya kuwepo na kanuni ama taratibu za ukomo wa madaraka ktk vyama vya siasa, nikiwa namaanisha Mwenyekiti awe anagombea kwa miaka 5 or 10 halafu anapisha wenginge nao wagombee hivyo hivyo kwenye nasafi nyinginezo ndani ya chama,katibu mkuu,mtunza hazina... nawengineo hii inaweza kusaidia kuwa sie tulio nje ya chama hicho tuone kweli ni demokrasia na sio vinginevyo. Hatuwezi kuwa na chama mwenyekiti ni huyo huyo weeeeee hadi chama kinakufa ama mweyewe anakufa hii sio demokrasia inatakiwa tubadilike tupokezani vijiti kuongoza chama na wananchi wake.

Uenyekiti wa chama ni sawa na kiti cha daladala unakaa ukifika unachuka na mwingine naye anakaa akifika mwisho wa safari yake nae anashuka ss ukingangania kukaa ktk kiti cha daladala hushuki ww wazunguka na gari tuuu hufiki hiyo safari yako? Shuka nawengine nao wasafiri wakalie kiti.

Mbowe onyesha Demokrasia nawewe utoke kwenye kiti nawengine nao wakae waanze safari, kondakta na dereva wamekuchoka kuzunguka na gari lao bila kushuka hata kama walipa nauli.
 
Mkuu watu bado wanakumbuka ishu ya DOWANS wamenidokeza hivyo kwa hiyo hawana imani naye ndo maana wengi wanahisi katumwa na wale wale wa huko upande wa pili.

Fidel80
Husiwe mjinga hivyo ishu hapa sio DOWANS bali the real ishu hapa ni UCHAGGA
 
Nani kakwambia kuwa alishinikizwa kujitoa? Statement ya Zitto haisemi hivyo wewe umeyatoa wapi hayo maneno kuwa alilazimishwa kujitoa?
USHINDWE NA ..........
 
Inaonekana Zitto kalazimishwa ajitoe,na kwa jinsi nilivoongea na baadhi ya watu ambao wamemuona jana ktk taarifa ya habari ya usiku wanasema hakuwa ktk hali yake ya kawaida,halafu wanasema hata ktk maelezo yake kulikuwa kuna kautata hivi, sasa haya ndo yale ya kina Gharib bilali jitoe au*********???? CCM B. Nilibahatika kufatilia uchaguzi wa Cuf,nilichoona ni kuwa Pr Lipumba alimpongeza Pr safari na yule jama mwengine kwa kuchukua form,hivi ndivo inavotakiwa Democrasia,sio kuogopana.
 
Zitto mwenyewe amekaririwa akisema hakushurutishwa, wewe hilo umelitoa wapi? Kwa mtazamo wangu Mtei kama mwasisi wa CHADEMA ana haki na wajibu wa kuingilia kati pale anapoona kuna dalili ya tatizo kujitokeza ndani ya chama. Ni kama alivyokuwa anafanya Mwalimu wakati CCM ilipokuwa ikielekea kuyumba.
 
Fidel80
Husiwe mjinga hivyo ishu hapa sio DOWANS bali the real ishu hapa ni UCHAGGA

Sio kweli mkuu tatizo jamaa alilinda masrahi ya DOWANS maana Zito sasa hivi dhambi hii ndio inayo mtafuna kwa taarifa yako asingejihusisha na hili alikuwa na kila sababu ya kuwa Mwenyekiti.
 
Nakubaliana na uamuzi wa Zitto; tukifanya tathmini ya hasara vs faida ya yeye kugombea uenyekiti tutaona hasara ni kubwa kuliko faida hasa katika chama. Demokrasia kukua si kwa Zitto kugombea uenyekiti au Mbowe kutogombea kuna mambo mengi zaidi ya hayo. Je wanachedema wameandaliwaje kukabiliana na mabadiliko ya kiuongozi. Tusisahau Chadema bado ni chama kichanga sana, inabidi tuwe na subira ili chama kikue!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom