lililofanyika kumuomba zitto ajitoe, kidemokrasia si jambo la afya sana, ila kwa chama kichanga kama chedema jambo hili lina mantiki yake.
wengi tunakubaliana kuwa baba wa taifa mwl. Nyerere alikuwa kiongozi mzuri aliyelipenda taifa lake ni kulifanyia mengi mazuri.
ebu tuangalie yeye alifanya nini wakati tanzania ikiwa changa ili kuiepusha na watu ambao wangeweza kuiangusha. Je ilikuwaje akawa rais na mwenyekiti kwa muda mrefu? Wakati wake si tulikuwa tunapigia kura yeye na giza? Yote haya aliyafanya ili kuhakikisha watu wanakuwa na msimamo mmoja, maana unapokuwa mchanga ukiruhusu mchanganyiko wa uongozi basi unaweza kuleta mkanganyiko kwa unaowaongoza.
ni hadi alipoona taifa limeanza kukomaa ndipo mfumo uliopo hivi sasa akauruhusu. Tunakumbuka kura za kutaka mfumo huu zilikuwa 20% lakini nyerere akashikia bango kuwa hao 20% wapewe nafasi.
nadhani hata kwa chadema walivyofanya vina logic hiyo. Kwamba pembeni kuna ccm, jitu kubwa sana linataka kuwameza, nyinyi mkianza kugongana mnalipa nafasi jitu hili kujipenyeza. Ngoja waendelee kukua tutaona demokrasia ya kweli baadae ila wakati huu ulikuwa ni wa hatari. Kama zitto mwenyewe alivyosema kuwa wote wawili yeye na mbowe wana wafuasi wengi hivyo kutoondoa jina lake kungekigawa chama katika mapande mawili makubwa je makundi hayo yangeanza kutafunana kama ilivyo ndani ya ccm hivi sasa kweli chadema ingenusurika?
je baba wa taifa alinusuruje mgawanyiko ndani ya ccm mwaka 1995. Si kiuungwana malecela aliondoa jina lake? Si mnakumbuka hali ilivyokuwa? Kama malecela angekataa si ccm na ukomavu wake wote ingegawanyika?
kama ccm na ukomavu wa miaka 35 (wake wakati huo miaka) na kuwepo kwa baba wa taifa, waliogopa mgawanyiko, itakuwaje kwa chadema chenye umri wa miaka 15 tu?