Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Sijasema jamaa ni kama gambler, nimetumia lyrics za Gamblers song kufikisha ujumbe wa kujua kila kitu kinataka timing, hiyo hata that badazz general Patton alikijua.

Hapa hujaiona psychology na pragmatism iliyo katika hii gambling. Kitu chochote kinachojumuisha an unknown outcome kina degree ya gambling.
Mkuu wangu nafanya utani tu najua ulichoandika ndio maana nikaongezea kuwa wanitisha!..
 
Haki ya nani walai

Ni jamii ya Tanzania tu niliyopata kuiona ya kwamba mtendewa ndiye wakulaumiwa, hakiyanani hata ukienda Lagos hutakuta jamii ya namna hii.

Kosa la mtendewa ni lipi hapa jamani? Kama alikuwa na makosa ama mapungufu si zingetumika kanuni kumwekea pingaminzi.

Na kama amekubali ushauri wa wanaojiita wazee kwanini watoa waliotoa waonekane wana busara na aliyeupokea ushauri uonekane tendo lile ni la kuhujumu.

Hakuna kanuni hata moja ktk mahesabu inayokubaliana na theory hii.

Zitto si-muingi kama chama, ila inanisikitisha tunavyomtia msalaba mtanzania mwezetu msalaba asiostahili ila waliostahili wanakula kuku kwa mrija.

Mkitoka hapo mwendelee na sera ya kuwaelimisha watu wa vijijini.
 
nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Watu watofautishe kuwa somebody katika bunge na kuwa somebody katika Chama.Mwakyembe ni somebody katika bunge lakini he is nobody katika CCM akigombea uenyekiti leo CCM pamoja na umaarufu wake katika bunge usishangae akatoka na kura mbili akabwagwa na kingunge au makamba who are nobodys katika Bunge.

Vivyo hivyo Zitto Kabwe is a heavyweight katika bunge lakini katika Chadema he is nobody.Wengi wana fikra kuwa if somebody is somebody katika bunge au serikali basi akienda na kwenye chama atakuwa somebody vilevile.Hapana.Ingekuwa ni hivyo Waziri Magufuli au Mwakyembe wangekuwa ndio makatibu wakuu wa CCM na Makamba angekuwa mjumbe wa tawi la CCM kwa wakweze .

Mnaodhani Zitto Kwa kuwa ni somebody kwenye Bunge aweza kuwa somebody every where you are wrong.

Wazee wa CHADEMA nawasifu wanajua wanachofanya na ni wasikivu na wanajua kuchuja mambo kwa umakini mkubwa wakizingatia mstakabali wa maslahi ya chama ya muda mrefu ujao tofauti na CCM ambao huangalia maslahi ya muda mfupi ujao wa uchaguzi unaofuata tu.Wazee wa CCM hawajui kazi yao zaidi ya kusubiri kuhutubiwa Diamond Jubilee na mwenyekiti wa CCM anapojisikia lakina hawana ROLE yoyote ya maana ndani ya CCM kama akina MTEI wa CHADEMA..CCM ingekuwa na wazee kama akina Mtei,Makani,N.K saa hizi akina Lowasa na akina Rostam Azizi wangekuwa kwenye chama cha CCM walishatimuliwa sikui nyingi lakini CCM haina wazee wenye akili na upeo mkubwa kama CHADEMA na ambao wanasikilizika.CCM ni kama chama cha MA-CHECK BOB WA KIJIWENI ambao vijiwe vyao kazi kubwa ni kujadili na kuwazia chaguzi tu na kujadlili nani agombee wapi na akishagombea apewe cheo gani.

CCM toka afe nyerere haina mwenyewe .Chadema ina wenyewe (INNER CIRCLE) wakati CCM haina wenyewe (INNER CIRCLE).Nyerere alikuwa na INNER CIRCLE alipofariki hakuna INNER CIRCLE hata jangili laweza ingia ndani ya CCM likawa kesho mwenyekiti wa Taifa wa CCM hakuna Inner CIRCLE kama ya akina Mtei inayoweza kuchuja.KABWE amekataliwa kwa kuwa hatakiwi kuingia ndani ya INNER CIRCLE sababu si kwa kuwa demokrasia haimuruhusu inamruhusu sana ila kilichozuia ni DOWANS,DOWANS,DOWANS.

Sasa kama kumzuia mtetezi wa DOWANS asiwe mwenyekiti ni kudharau demokrasia sidhani nadhani ni kuheshimu demokrasia.Wazee wa CHADEMA I SALUTE YOU.

Uamuzi waliofanya hawa wazee utakiimarisha chama zaidi na kukijengea hadhi mbele ya umma wa watanzania wenye hasira na DOWANS lakini kwa wapenzi na watetezi wa DOWANS poleni kwa maumivu mkatafute Panadol dawa ya kupunguza maumivu mnywe siyo mara tatu kutwa kama wanavyoshauri madaktari bali nyie mnywe mara tatu tatu kutwa.
 
True true....he's a flip-flopper. He can't make his damn mind about what he wants. One minute he says he's quitting politics to focus on school...the next minute he says no..I'm going to run....now he wants to run for the chairmanship of his party....then he withdraws his name....

I don't know which is which with him. Decide on one thing and stick with it. Come on Zitto...you need to make up your damn mind and stop confusing folks.

Nyani Ngabu nadhani kusoma na kuanalyse siasa kwa misingi na mitizamo ya kimarekani imekuaathiri sana. Hii siasa ya flip-flopper ambayo ni maarufu miongoni mwa wahafidhina inaweza kuwa na mshiko katika taifa kama marekani ambalo lina mifumo iliyokomaa na yenye nguvu ya kupambana na athari za misimamo mgando lakini sio katika kataifa ketu ambako ndio kwanza tupo katika hatua za kuanzisha miundo mbinu ya kisiasa na uongozi kama vile mfumo wa siasa za ushindani ambazo tunataka zituzalishie siasa za kidemokrasia. Hivyo kwa mwanasiasa mwenye kutambua na kuthamini ni mchango gani anaotaka kuutoa katika zoezi zima la kujenga miundombinu ya kiuongozi na kisiasa katika nchi yenye mifumo legelege kama yetu, mbapo demokrasia inaendelea kubaki kauli mbiu tu na sio imani wala utamaduni, kubadili mawazo kwa ajili ya kufanikisha lengo kuu (vision) yake ni kitu muhimu.

Pia ningependa kukurekebisha katika hili suala la Zitto kuacha siasa.
Kamwe Zitto hawezi kupumzika na wala kuacha siasa na hajawahi kutamka nia ya kufanya hilo kamwe.

Alichosema yeye na hadi sasa ndio msimamo wake ingawa siku za hivi karibuni amekuwa akitafakari sana, ni kuwa ataacha jukumu la ubunge (hatagombea mwaka 2010) kwa sababu kadhaa.

Moja ni kuwa anaamini aspokuwa mbunge atapana nafasi zaidi ya kufanya kazi za chama kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha kuwa anatoa mchango zaidi katika kujenga chama kiasasi na kukiandaa kuwa kama mbadala makini wa chama tawala inapofika hapo mwaka 2015. Kwake yeye muhimu sio mradi chama chake kuchukua madaraka tu ama kuiondoa CCM madarakani tu, bali kuwa na chama chenye nia ya dhati na uwezo wa uhakika wa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo yawawezesha watanzania kutumia potentials zilizojaa nchini kuifanya nchi yetu kuwa yenye demokrasia makini na yenye kuleta tija kwa maisha ya mtanzania.

Zitto anaamini kuwa ni muhimu sasa chama chake kujiongezea nguvu katika vyombo vya maamuzi nchini yaani bunge na mabaraza ya serikali za mitaa ili kuwa na nafasi ya kujijenga zaidi kwa wananchi, kuwaexpose wanachama wao katika nafasi za uongozi kwa mapana zaidi na pia kuwa na nguvu za ushawishi za kufanya mabadiliko ya kimfumo ambayo yanahitajika kufanyika sasa wakati wanajiandaa kuchukua jukumu la kuongoza nchi. Ndio maana anaamini uwa endapo hatagombea 2010 ataweza kutumia muda na nguvu zake zote kusaidia shughuli za kampeni kikamilifu na kuwezesha chama chake kupata viti vingi zaidi haswa kwa wagombea vijana na ama kuondoa ukiritimba wa CCM bungeni ama hata kulazimu kuunda serikali ya mseto kwa kulazimisha waziri mkuu kutokea chama pinzani. Zitto ni gradualist inapokuja katika suala la mustakabali wa taifa letu.Kwake yeye muhimu ni mabadiliko bora na sio bora mabadiliko.

Pia anaamini kuwa kujipunguzia majukumu ya ubunge atakuwa na nafasi ya kujenga zaidi uwezo wake kiuongozi. Anaamini ili kuweza kuwa kiongozi mzuri ni lazima awe na upeo mpana wa masuala ya kiuongozi, kiuchumi , kisiasa na kidunia. Hivyo angelipenda kuchukua muda wake kuanzia sasa kujiongezea elimu na pia kufanya selfreflection/tafakuri binafsi ya miaka mitano ya ubunge wake ili kujipambanua na kuongeza ujuvi katika masuala hayo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu lakini pia chama chake.

Hivyo ni muhimu kutambua tofauti ya kupumzika siasa na kupumzika ubunge kama ambavyo Zitto alionyesha nia mapema kabisa na hadi sasa bado anaamini kuwa nia hiyo ni bora Hata hivyo endapo ataona kuwa UBUNGE ni muhimu ili kufanikisha malengo yake kwa chama na nchi yake ni wazi hataogopa Nyani ngabu kumuita flip-flopper.

omarilyas
 
Rejea makala ya Ngurumo kwenye gazeti la jana la Tanzania Daima!! Hivyo kama yeye amesoma hizo na kuamua kujitoa

Nyie shangilieni tu hizi spinning kwa sasa wakati zinakidhi matakwa yenu. Zitakapowageuke nawashauri mzishangilie pia.......

Ngurumo ametumia ukaribu wake na Zitto kuspin against him tena ukiangalia jinsi alivyokuwa akijichanganya kujaribu kuuma na kupuliza ni wazi kuwa alifanya kazi hii huku roho na nia yake ikimsuta.

Uzuri wa uthabutu kama wa Zitto ni kuwa unakupa nafasi ya kuwajua vizuri wale unaowaamini....ni nafasi kwake kama kiongozi kujifunza na kujua nia na uthabiti wa unaowaona wenzio katika mapambano....

Nasubiri kwa hamu spining hovyohovyo za yule KALUMANZILA wa Mafia akitekeleza jukumu lake alilopewa pamoja na wenziwe likitoka kwa hao anaojidanganya kuwa ni WAPIGANAJI WENZIWE. Siku watakapomgeuka kama anavyowageuka wenzake waliomjenga na kumlinda pale alipowahitaji, ndipo atakapopata wasaa wa kuelimika uzeeni.

omarilyas
 
Kwangu mie mambo mawili yalitokea na moja wapo likasababisha huu mtafaruku.

1. Zitto alikurupuka na uamuzi huo bila ya kufanya utafiti wa kutosha na kupata baraka kutoka kwa wazee.
Hii ilisababisha wazee wa Chadema wafanye uamuzi wa 1.b kumuomba (kumlazimisha) ajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho cha kugombea cheo cha Mwenyekiti.
Wazee kwa kufanya hivyo kwa kweli wameonyesha chama hakina demokrasia ya kweli.
2. Hii yote ilipangwa ili kuifanya CHADEMA iwe namba moja kwenye media zote. Sasa hivi hamna ufisadi wala nini, ni Chadema tu. Kama ni tangazo la biashara basi kwa kweli wamefanikiwa sana. Ila sema sasa kazi kuitoa hiyo negative na kuutumia huu umaarufu walioupata kwa kusemwa kila sehemu.

Mbowe kama Mwenyekiti: Inawezekana kweli kakijenga chama ila bado anatawala kwa mgongo wa Wazee. Kama kiongozi wa karne ya 21, hana njia za kumfanya yeye mwenyewe asimame na kukitetea chama chake. Hata umaarufu uliopo sasa hivi Chadema, umeletwa zaidi na Dr. Slaa na Zitto. Zitto umaarufu wake umekuja kama bahati pale alipofungiwa bungeni. Toka alipofungiwa na kuanza kupita mikoani, zomea zomea ikaanza na Zitto akawa maarufu bila ya CCM kutegemea.
Mbowe inabidi awe kiongozi wa kweli kama Mwenyekiti. Asingeligombea Urais na akabaki kuwa Mbunge, angelikuwa na yeye mlipuaji mabomu na hii ingelimpa na yeye umaarufu zaidi. Na yeye pia alikurupuka kwenda kugombea Urais. Heri angelibaki Mbunge na kuongeza vita bungeni. Ndiyo maana katishwa na Zitto akaanza kubabaika. Hadi nashindwa kuamini kama alitaka kuwa Rais wakati hata ndani ya Chadema kwenyewe hana uhakika kama anaweza kushinda. Vinginevyo, basi wangelimuacha Zitto agombee na agonge mwamba.
Sidhani enzi za JKN mtu angelitaka kugombea anglishinda. Na hii hata haikuhitaji kuiba kura.
KUTUMIA NJIA ZA CCM: Napinga kwa nguvu zote kutumia WIZI wa kura ili kumpasisha Mbowe. Hii kitu itaendelea kuiumiza CCM milele na milele hadi siku moja watakuja kuzipiga kavu kavu. Heri kuongea na kuyamaliza ndani kuliko kuiba kura.

Nimalizie kwa kuonyesha njia mbaya kabisa waitumiayo CCM. Watakuacha ugombee na ushinde. Jina lako liende NEC/CC na huko wanakaa wazee ambao ni Maprofesa wa kubadili Risasi kuwa Maji. Jina lako likienda la Tatu (kama dada yangu Tatu Ntimizi wa Nzega) linaweza likarudi la kwanza. Na la kwanza likawa la mwisho. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Heri hao CC/NEC wakae mapema na kumwambia fulani, wala usipoteze muda wako kugombea maana hapa lazima apite FULANI. Kwa hili naona bado Chadema ni wa kweli kuliko Fisadi CCM.
 
Nyani Ngabu nadhani kusoma na kuanalyse siasa kwa misingi na mitizamo ya kimarekani imekuaathiri sana. Hii siasa ya flip-flopper ambayo ni maarufu miongoni mwa wahafidhina inaweza kuwa na mshiko katika taifa kama marekani ambalo lina mifumo iliyokomaa na yenye nguvu ya kupambana na athari za misimamo mgando lakini sio katika kataifa ketu ambako ndio kwanza tupo katika hatua za kuanzisha miundo mbinu ya kisiasa na uongozi kama vile mfumo wa siasa za ushindani ambazo tunataka zituzalishie siasa za kidemokrasia.

Omari, hiyo ya "flip-flopper" ni description tu. Mtu unaposema hutagombea tena kiti chako cha ubunge ili urudi shuleni kuongeza elimu yako halafu unarudi na kusema utagombea tena hicho kiti chako, huo ni ugeugeu (flip flopper). Umeflip na kuflopp na hujui hata unataka nini. Kwa hiyo haijalishi wewe uko wapi. Unapokuwa geugeu kwenye mambo hususan ukiwa kwenye nafasi ya uongozi, wewe ni flip-flopper tu uwe Marekani, Albania, Kandahar au Tanzania.
 
Katika hali ya mshangao na kuonyesha kuchanganyikiwa kuna taarifa zinazosema kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameshinikiza kughairishwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi ya Baraza la Vijana na Baraza la wazee ambayo yanaonyesha ushindi mkubwa wa wanachama ambao wanaaminiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto Kabwe.

Wakati katika uchaguzi wa Baraza la Vijana unaonyesha kuwa Kafulila ambaye ni msaidizi wa Zitto ambaye amekuwa akimtayarisha kugombea ubunge Kigoma Kusini (sio kigoma kaskazini kwa Zitto) amemshinda kwa kura zilizojitosheleza ndugu Henche ambaye ni chaguo la wafuasi wa Mbowe ambao jana baada ya kumlazimu Zitto kujito walihamishia nguvu zao zote dhidi ya wagombea wanaomuunga mkono Zitto.

Katika matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Wazee yanaonyesha kuwa bwana Shilungeshela ambaye pia anasemekana ni mfuasi wa Zitto na ambaye jana usiku Zitto alikuwa akitpita kumuombea kura naye pia ameshinda kwa kura nyingi.

Ukweli ni kuwa haya yanaweza kuwa makosa makubwa zaidi kwa upande wa wafuasi wa Mbowe kwani nahofia nguvu hizi za ushindi wa waliokuwa wakimuunga mkono Zitto zikageuka kuwa kura ya HAPANA kwake na kujikuta akikosa kabisa uhalali wa kiuongozi. Hali ambayo jana usiku Zitto alikuwa akijaribu kuizuia kwa kuhofia kuumiza maslahi ya chama chao.

Cha ajabu na kinachoonyesha kupanick ni kuwa wasimamizi wa chaguzi zote mbili wamezuiwa hata kutangaza matokeo kama zilivyo taratibu....Inaelekea siasa za CCM zimeathiri sana psych ya watanzania.....

Ama kweli hawa jamaa wanajua kukabaka kademokrasia ketu....Mwataka tuende wapi....NYUMBANI kumeota magugu na kumejaa many'agau...

omarilyas
 
Yep..kama yeye sio CHADEMA atakuwa hana input. Maana huenda hata haujui mchakato wao wa uchaguzi..sasa post kama hizi zinaweza hata kufikia page ya 50 lakini ukichunguza hamna input..Hii ndio hatari niliyoiona.

Mwanakijiji au Kitila MKUMBO huwa wanajadili CCM wao ni CCM?Lowassa au spika Sitta tunamjadili kwanini wakati sio wana CCM?
Field Marshal ES anawajadili watu wa Chadema wakati yeye sio mwana Chadema.

Mwiba ni CUF anawajadili CCM kila siku kwanini hukumuuliza swali hili?
swali langu ni la kisheria zaidi ndio maana nikaweka jukwaa la sheria. kisheria Mzee Mtei hakutakiwa kushiriki kikao kile kwa ajli ya kuwa mzazi wa mmoja wa wagombea-Mbowe.

Makani hakutakiwa kushiriki kikao kile kwa vile ana mahusiano ya kikazi na MBOWE walipokuwa BOT.

hakukuwa na FAIRNESS kutokana na sababu hizo mbili.kifupi maamuzi ya hao wazee ni batili.
 
Una uhakika na hili? basi kuna uwezekano wa KURA za maruhani kutokea kwenye kura za Mwenyekiti wa Taifa.
 
baada kuungana zidi ya ccm wanaanza kutengana wenyewe kwa wenyewe kweli mafisadi watatutawala milele na milele.
 
Pamoja na uhuru wa kusema na ukajikuta huna la kusema ni vema ukanyamaza kuliko kuongea pumba hizi.

kama pumba za wazee wanne wa Chadema,walichokifanya wameharibu kila kitu, utabnikumbuka.mmonyoko huu sio rahisi Chadema kuuziba.chukua wapenzi wa Wangwe bado hawajasahau kiongozi wao kushambuliwa wazi, baada ya hapo wanachama kama 15 wakafukuzwa na sasa wafuasi wa Zitto kama kina KITILA hawatakubali.sasa maadui wa Mbowe aliowazalisha toka kwa wangwe,na wale wa wanachama 15,na wa Zitto ni mgawanyiko kamili wa Chama. huu unaweza kuwa mwisho wa Chadema.

kama Zitto ni mtoto kwenye siasa basi msimtumie kwenye kampeni.
naamini watu wengi watapiga kura ya hapana kwa MBOWE.
 
baada kuungana zidi ya ccm wanaanza kutengana wenyewe kwa wenyewe kweli mafisadi watatutawala milele na milele.
Mbowe atakuwa na wakati mgumu sana kwani hawezi kupata kura toka kwa wajumbe wa kutoka mikoa ya Mara kutokana na sakata la Wangwe,
Kigoma kwani mwenyekiti wa huko ni mjomba wake Zitto Kabwe.
Singida huko ni ngome ya KITILA na LISSU ambao wako kwa Zitto.
Iringa ambako Chiku ambwao alinyimwa ubunge wa viti maalum akapewa mtu wa KILIMANJARO.
TUSUBIRI.
 
Chama cha ubabe na longolongo imefika wakati wa kudhihirisha makucha walokuwa wameficha.

TANZANIA HAKUNA CHAMA CHA UPINZANI KILICHO IMARA.

UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM.
 
Hivi huyu jamaa akishindwa kutetea kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao, mustakabali wake wa kisiasa utakuwaje?

Nasema hivi kwa sababu nasikia kuna uwezekano asishinde tena kiti chake cha ubunge kutokana na tuhuma kwamba kawatelekeza wananchi wa jimbo lake kimaendeleo kwa kutumia muda mwingi kujihusisha zaidi na masuala (na mijadala) ya kibunge na kitaifa. Nadhani ndiyo maana wiki iliyopita alikuja humu ndani na kuposti mada ndefu iliyojaribu kuorodhesha mafanikio lukuki Ubunge wake bila shaka kwa nia ya kujisafisha dhidi ya tuhuma za kuwatupa Wananchi wa jimbo lake.
 
Zitto ataweza?
ban.maswali.jpg


Ansbert Ngurumo

amka2.gif

NIMEFARIJIKA kusikia na kusoma kwamba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameamua kugombea uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa shinikizo la wapambe, si kwa hiari yake;
kwani maswali ya awali niliyokuwa najiuliza niliposikia anagombea uenyekiti, si kama ana weza au la.
Nilitaka kujua Zitto ana haraka gani, na kama anagombea kwa uamuzi wake binafsi au kwa shinikizo la watu wengine; na kama ni kweli, ni kina nani.

Nilitaka kujua pia kama anajua athari ya uamuzi wake huo kwa muda mfupi na mrefu kwenye chama chake na yeye binafsi.
Vile vile, nilitaka kujua kama chama chake kilichomtambua, kikamlea na kumfunda kisiasa kimemwandaa kugombea nafasi hiyo au anakwenda kama ‘mgombea binafsi' ndani ya chama.

Lakini kwa sababu ameshajibu swali moja hapo juu, na kwa kuwa bado yapo maswali mengi yanaulizwa juu yake, hasa kwa kuwa ameibua mjadala kitaifa, nimeona leo niandike makala hii kumlinda na kumsaidia kama mdogo wangu, msomi mwenzangu, mwanaharakati mwenzangu, kijana mwenzangu na rafiki yangu; na kwa kuwa mimi na Zitto tuna mengi tunayokubaliana na kutofautiana.
Zitto amethubutu kufanya kile ambacho vijana wengi wa umri wake wanaogopa kufanya. Anajaribu kuutumia umaarufu wake karama yake na mvuto wake wa kisiasa vikiwa bado juu ili asonge mbele na kujijenga kisiasa.

Tumzuie? Tumruhusu? Tumpinge? Tumuunge mkono? Tumshabikie? Tumshauri au tumwache? Tumjali au tumpuuze? Je, tuna uwezo wa kufanya lolote miongoni mwa hayo hapo juu?

Jambo moja liko wazi.
Kila anayemjadili Zitto leo, si tu kwamba anamjadili Mbunge wa CHADEMA, bali anamjadili pia mbunge wa taifa.
Uamuzi aliochukua na athari au hatima yake vina mwangwi mkubwa kitaifa.

Kwa sababu hiyo, hatuwezi kumpuuza Zitto. Na mimi nitajaribu kufanya nitakaloweza katika hayo niliyoyataja hapo juu.

Bahati nzuri kuna walionitangulia. Rafiki yangu mwingine, ambaye pia ni rafiki ya Zitto, Absalom Kibanda, katika safu yake ya Tuendako, wiki hii, amemsema sana mbunge huyo katika kile alichokiita ‘anguko la Zitto.'

Mimi nitajadili anguko la CHADEMA. Lakini kabla ya kwenda mbali, hatuna budi kujiuliza: Nani angependa na kushabikia anguko la Zitto au la CHADEMA? Kwa manufaa gani? Je, kuna watu wanaomwandalia Zitto na kumsindikiza katika anguko lake au la chama chake? Je, anguko la Zitto ni kuupata au kuukosa uenyekiti wa CHADEMA? Je, Zitto kuupata au kuukosa uenyekiti wa CHADEMA ni heri kwa Tanzania?
Maswali ni mengi, lakini lipo hili ambalo Kibanda amelidokeza katika makala yake, akalichochea na kulifafanua zaidi katika barua pepe kwa umma; la kusema Zitto anatumiwa na CCM bila kujua ili kuivuruga na kuibomoa CHADEMA, mithili ya NCCR-Mageuzi na CUF.

Nataka kumtetea Zitto kidogo. Naamini kwamba hatumiwi na CCM bila kujua. Kwangu mimi, Zitto ameshavuka viwango vya kutumiwa bila kujua. Zitto ni mjanja vya kutosha, kiasi kwamba akiamua kutumika, atafanya hivyo kwa hiari yake.
Kwa vyovyote vile, Zitto anajua analofanya. Hivyo, wanaomlaumu na wanaomtetea wasizunguke mbuyu; waseme kile wanachokusudia kusema. Wamwambie.

Kama wanakerwa na vikao vya siri anavyofanya na vigogo kadhaa wa CCM, waseme; na watutajie majina. Kama ni Joseph Sinde Warioba au Dk. Ahmed Salim au Rostam Azizi au Edward Lowassa au Rais Jakaya Kikwete au Lawrence Masha au William Ngeleja; waseme wazi.

Kilicho wazi ni kwamba Zitto anajaribu kujenga himaya yake kisiasa ndani na nje ya CHADEMA. Wakati mwingine anajisikia fahari kuzungukwa na kushauriwa na vigogo kama hao.
Katika umri wake mdogo, anaona heshima na fahari ya pekee kupata joto na ushauri wa vigogo kama hao, hata kama baadhi yao hawana majina mazuri kisiasa na kijamii. Kwake, kisiasa, anaona kama anawekeza kwa malengo ya muda mrefu.
Maana kinachozungumzwa sasa ni kwamba mojawapo ya ajenda za Zitto kuutaka uenyekiti ni ahadi aliyopewa na baadhi ya vigogo wa CCM kwamba wanatamani kujiengua na kujiunga na CHADEMA iwapo tu, ataweza kumwangusha Freeman Mbowe katika nafasi ya uenyekiti.

Uongo wanaotumia ni kwamba wakishajimega kutoka CCM wataiwezesha CHADEMA kupata wabunge wengi mwaka 2010, na hata kuipa uwezekano wa kuwa na waziri mkuu kutoka chama cha upinzani.

Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.

Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.

Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.

Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.

Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyang'anyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.

Tunajua mbinu walizokuwa wanatumia, na tumeshuhudia wakifurukuta tangu mwaka 2007; lakini wameshindwa kwa sababu CHADEMA imekuwa na watu shupavu na mahiri, huku ufisadi wa wanamtandao ukichangia kuwamaliza ‘makabakaba' na kusaidia harakati za kuwabana.
Zitto amekuwa mmoja wa mashujaa katika vita dhidi ya ufisadi, lakini akiwa mkweli atatuambia bila kificho kuwa watu wale wale waliokuja kufahamika baadaye kuwa mafisadi, ndio waliokuwa wanaomba CHADEMA iwape nafasi walipokuwa hawajaipata CCM.

Kwa hiyo, kupata kwao nafasi katika CCM ndio ulikuwa wokovu wa CHADEMA, maana leo hii ndiyo ingekuwa inashambuliwa kwa ufisadi kama wanamtandao wangejiunga nayo, hata kama wasingefaulu kushika madaraka.
Ndiyo maana wengi wetu tunatarajia kwamba Zitto angepaswa kuwa mwangalifu sana anapoletewa masharti ya namna hii na vigogo wa CCM wanaomuahidi kujiunga CHADEMA kwa kishindo iwapo atamuondoa Mbowe.

Hili ni sharti lenye hila; na woga wao kwa Mbowe unapaswa utumiwe kama nguvu ya CHADEMA dhidi ya CCM, na sifa ya ziada ya kiuongozi ya Mbowe.

Wana CCM hawawezi kuwachagulia wana CHADEMA kiongozi bora. Na kama kweli wanamtuma Zitto (ingawa yeye amekanusha) wanajua wanachokitaka.

Pili, Zitto na wapambe wake wanapaswa wajue kuwa nguvu na uhai wa CHADEMA haviwezi kutoka CCM. Na kama ikitokea hivyo, vigogo wa CCM wakameguka na kujiunga CHADEMA, hilo ndilo litakuwa anguko la kwanza la CHADEMA.

Sababu ni moja. Baadhi ya hao wanaoionea ‘huruma' CHADEMA kwa staili hiyo, ni makapi ya kisiasa huko waliko. Siamini kama ni jambo jema kutarajia kuijenga CHADEMA kwa kutumia makapi ya CCM.
Wanaotaka kuijenga CHADEMA bora wawekeze katika damu mpya, kizazi kipya kisicho na mawaa ya ufisadi.

Kazi ile ile iliyofanyika kuwatambua kina Zitto, John Mnyika, John Mrema, Halima Mdee, Mhonga Ruhwanya na vijana wengine wengi wanaoendelea kuchangamsha siasa za CHADEMA na kuchochea harakati, iendelee kufanyika kuendeleza kazi nzuri iliyokwishaanza chini ya uongozi wa sasa wa kina Mbowe, Dk. Willibrod Slaa na Zitto mwenyewe.

Kwa hiyo, kama makundi haya ya wana CCM yanamwaminisha Zitto kwamba njia pekee ya kuijenga CHADEMA ni kumwondoa Mbowe, kumweka Zitto na kuwaruhusu wao kujiunga, Watanzania wanaoona mbali watamuonya yeye na watu wake kwamba sasa wanavuka mipaka ya demokrasia, wanajiingiza katika uhujumu, usaliti na uhaini ambao unamfanya Zitto sasa aanze kuwashambulia viongozi wenzake kwa maamuzi yaliyofanyika ndani ya vikao halali (kwa mfano kuhusu kuwasimamisha watu uanachama au kuwafukuza kabisa), wakati naye alishiriki, tena kama kiongozi mwandamizi wa chama.

Na jambo hili linazua hoja kwamba labda akifanikiwa kuwa mwenyekiti hatachukua hatua zozote dhidi ya wazembe, wasaliti, mafisadi na watovu wa nidhamu ndani ya chama.
Ikumbukwe kuwa ni vigumu Zitto kukiri kuwa anatumiwa na CCM. Inawezekana watu wanamuonea tu kwa sababu ya hisia, lakini ninavyokumbuka mimi tuhuma hizi zimetokana na mambo kadhaa.

CCM wanaogopa nguvu ya CHADEMA; na wanatafuta pa kupumulia, baada ya kuthubutu na kushindwa kwa miaka mitatu mfululizo.

Wanadhani wakifanikiwa kuwapambanisha vigogo wa chama unaweza kuwa mwanya wa kujenga ufa ndani ya chama na wao kupona.

Wanahofia umaarufu wa Zitto unaweza kuwadhuru wasipokuwa karibu naye. Njia rahisi wanayodhani inaweza kumlainisha ni kukiri umaarufu wake, kuutambua na kumfanya ajisahau, alewe umaarufu wake, wamtumie.

Ndiyo maana Zitto alipojisahau akaanza kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans, akidhani umaarufu wake ungeweza kubadili mjadala wa kitaifa na upepo wa kisiasa,

wapambanaji wenzake walimsikitikia sana, na tuhuma za waziwazi zikaanza kurushwa dhidi yake kwamba 'kuna waliomharibu.'

Hata leo, kauli yake kuhusu Dowans imemjeruhi sana kisiasa, hasa inapochangiwa na kile wachunguzi wanachokiita vikao vyake vya siri na wabaya wa CHADEMA. Na kama baadhi yao ndio wanaojitokeza leo kumshabikia na kumpongeza hadharani kwa hiki anachofanya, ni vigumu kuzuia hisia za wananchi dhidi yake. Itamchukua muda mrefu kujisafisha.

Na katika siku za hivi karibuni, Zitto amesikika akizungumza katika Radio Sauti ya Ujerumani akidai kwamba tofauti ya msingi kati yake na Mbowe katika kinyang'anyiro cha uenyekiti ni kwamba ‘Mbowe ni bepari, Zitto ni mjamaa!'
Lakini Zitto anajua kuliko wengi wetu kuwa kiitikadi CHADEMA haijawahi kuwa chama cha kijamaa.

Anajua kuwa watu pekee wanaojidai kuwa na itikadi ya ujamaa hapa nchini ni CCM, ingawa nao wanaishi kwa siasa za ubepari wenye ulemavu.

Katiba ya CHADEMA, ambayo Zitto ameshiriki kuiandika upya mwaka 2006, akiwa mbunge na kiongozi mwandamizi, inaeleza vema itikadi ya chama chake. Miaka mitatu baadaye, Zitto amegeuka na kuwa mjamaa katika chama cha kibepari? Lipi limemsibu Zitto?

Zaidi ya hayo, Zitto amepata bahati ya kukosolewa na vyombo vya habari visivyomilikuwa na CCM, huku akisifiwa na kupongezwa na kupewa moyo na vyombo vya CCM au vinavyomilikiwa na makada wa CCM.

Ikumbukwe pia katika migogoro mingine iliyopita ya uongozi ndani ya CHADEMA, ya kweli na ya kupandikizwa, vyombo hivyo hivyo vilikuwa vinawaunga mkono na kuwashabikia waliojitokeza kuisumbua CHADEMA au Mbowe.

Hii si neema ya kisiasa kwa Zitto. Wana CCM wanamsifu makusudi ili kumchafulia jina mbele ya wana CHADEMA na wananchi wengine waliomwamini kwa muda mrefu, ili baada ya muda naye awe kapi la kisiasa kama wao.

Sisi wengine tungependa kumzuia asiende huko – kama atasikiliza. Vinginevyo, iwapo atakifikisha chama chake katika unyonge, udhalili na hatimaye kifo kama kilichowakuta NCCR-Mageuzi, au kama hataki kujikumbusha jinsi CCM ilivyoisambaratisha CUF, anaweza kuchagua kutumia ubishi na umaarufu kukuza haiba yake kisiasa na kuua taswira ya taasisi iliyomlea na kumkuza.

Nimekuwa nafuatilia wanasiasa wanaompongeza. Ni vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na TLP; vile vile ambavyo vimeshughulikiwa na CCM, na baadaye vimekuwa katika ushindani na wivu dhidi ya CHADEMA, ambayo inakua, vyenyewe vinafifia, kiasi cha kuathiri hata ushirikiano wa kisiasa uliokuwa umeanzishwa.

Hizi ndizo pongezi anazotafuta Zitto? Anazihitaji? Anapochanganya hizi na za CCM, anapata jawabu gani?
Kwa elimu na uzeofu wake, Zitto anapaswa kuelewa kwa nini watu wanapigia kelele uamuzi wake wa kugombea uenyekiti sasa, katika mazingira haya, na kwa staili aliyoamua kutumia.

Watanzania hawako tayari kumsamehe binadamu yeyote atakayeshiriki kwa kujituma au kutumiwa kudhoofisha nguvu iliyopo sasa ya CHADEMA Bara na CUF Visiwani. Na kama yupo, asiwe Zitto.

Ni haki yake kugombea na kuongoza. Lakini lazima atumie busara inayomlinda yeye na taasisi yake. Nyota yake kisiasa bado ni changa na inawaka. Hana sababu ya kujiingiza katika jitihada za kuizima mapema hivi.

CHADEMA inaweza kumwandaa Zitto kuwa kiongozi mkubwa kitaifa baadaye, iwapo atakubali kufanya kazi na viongozi wenzake na kujijenga pole pole.

Naamini kwamba hata Mbowe asingefika hapo alipo kama angekurupuka au kama angegombea kwa mbinu zinazotiliwa shaka, na katika mazingira kama haya ya sasa. Tungemshauri kama tunavyofanya kwa Zitto leo.

Hata hivyo, ninapotafakari mbinu alizotumia Zitto, nafika mahali nadhani Zitto hajadhamiria kushinda, bali anataka kumtikisa Mbowe na chama, kuleta msisimko wa kitaifa kuhusu uchaguzi ndani ya CHADEMA, kujenga hisia na ufuasi wa hapo baadaye, ili atakapokuwa amefuzu, na chama kiko tayari, iwe rahisi kwake kupitishwa, kugombea na kushinda.
Kwa sasa naona anatumia njia ile ile iliyotumiwa na Jakaya Kikwete kuusaka urais mwaka 1995, ambao aliupata baada ya miaka 10 ya kujijenga, kujitangaza na ‘kukua kidogo.'

Tuombe tu kwamba umaarufu uambatane na uwezo; maana kama alivyosema Kibanda, ya Augustine Mrema na Kikwete yametufundisha ukweli kwamba kuna tofauti kati ya kutoa hotuba nzuri, kuhamasisha umma na kuwa kiongozi.

Navijua CHADEMA na CCM; nawajua vizuri Mbowe na Zitto. Najua uwezo na udhaifu wao, na sababu ya CCM kuiogopa CHADEMA ya Mbowe.

Kama CCM wamehangaika kwa miaka mitatu mfululizo wakashindwa, na kama wataweza kuibomoa CHADEMA hii kabla ya Uchaguzi Mkuu 2010, ibilisi awape nini!

Si lazima wamwangushe Zitto, maana anaweza kujikwaa, au hata akaanguka na kusimama pale pale alipo au akasimamia pengine. Lakini iwapo CHADEMA itaanguka haitaamka; na itatuchukua muda mrefu sana kupata nguvu nyingine na uwanja wa mapambano; walau si kabla ya 2010.

Wasioona anguko la CHADEMA katika mpambano wa Zitto na Mbowe, waendelee kutafakari, na wajiulize sababu za ushabiki wa wazi wa wabaya wa CHADEMA katika pongezi wanazompa Zitto. Natambua kuwa Zitto amefanya kazi nzuri bungeni na majukwaani. Aendelee kuifanya, maana anaiweza, na taifa linamhitaji kuelekea 2015 akiwa na viongozi wenzake waandamizi wa CHADEMA.

wiki iliyopita alinadika Kibanda gazeti hili hili jumapili kaandika NGURUMO ambaye alipelekwa Ulaya na Mbowe, ni salamu kwa wajumbe wa mkutano mkuu kumchafua Zitto, unafiki wa Chadema wakati mzee Mtei kasema vijana ni taifa la leo,hapa wanamwambia Zitto awe na subira hadi 2015 kwani ni mchanga.wanasema MBOWE alikuwa na subira swali angeweza vipi kushindana na baba yake/mkwe wake? Ngurumo umetumwa na bosi wako ambaye pia bosi wa Kibanda?
 
My take so far is as follows:

  • I thank Invisible for his update. It makes the point that Zitto was not forced to abandon his move. Advising him to remove himself from the contest was not undemocratic.
  • Chadema has been bruised in this saga. So has Zitto. Both can emerge with minor injuries, but they have given ammunition to many detractors.
  • Tribalists and their CCM manipulators are using this difficulty to claim that Chadema is a tribal party. That is not true. It was founded by a most distinguished Tanzanian (Edwin Mtei) who, through no fault of his, happens to be Mchaga. I hate to see well educated groups of Tanzanians, like the ones we have here, being so tribal in their outlook.
  • It is not a sin for the son in law of a leader to be a leader. Freeman Mbowe was elected Chadema leader. He was not simply given the chairmanship by Mzee Mtei. In fact, Mzee Mtei was succeeded by Bob Makani, and after Makani, Chadema elected Freeman. What is so sinister about that? Freeman’s association with the founder of Chadema may have helped him, but that there is nothing undemocratic about that.
  • Those who would like to see CCM continue to misrule Tanzania some more will do all they can to exploit this episode. They have already began to try to dismantle the support that those who aim for change give to Chadema here at JF. Their argument that what transpired in Chadema was undemocratic has run out of steam, so they have now reverted to naked tribalism.
  • Change must come to Tanzania. As Obama puts it, we cannot continue to do the same things over and over again and expect a different result. We cannot afford to re-elect CCM. We must build up the opposition, and it seems to me, Chadema is the focal point of that.
 
Last edited:
buttonone.gif
Wachungaji kuiombea Kenya ipate mvua
buttonone.gif
Walimu waliopigwa viboko kudai fidia kortini Date::8/31/2009Zitto: Nilikataa kurubuniwa kwa cheo
kabwezube.jpg
NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyoro
cha Uenyekiti wa chama hicho.
broken-heart.jpg
ADAI AWALI ALIKATAA MPANGO WA WAZEE WA KUMPA MADARAKA ZAIDI ILI AJITOE

Salim Said

NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema kuwa awali alikataa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa chama hicho baada ya kuona anarubuniwa cheo, lakini akasisitiza kuwa uamuzi wake wa kuachia ngazi ni kwa ajili ya kukinusuru chama hicho.

Zitto alisababisha kizaazaa kwenye chama hicho baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti, kitendo ambacho kingemfanya apambane na mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe ambaye amefanya kazi kubwa ya kukijenga chama hicho.

Wengi waliona kuwa uamuzi wa Zitto ungegawanya wanachama na hivyo kusababisha makundi ambayo yangekifanya kidhoofike, lakini juzi mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini aliwasilisha barua ya kujiengua kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti na jana aliiambia Mwananchi sababu za kujitoa.


"Naelewa watu wengi wameumia, lakini wazee waliniambia chama kitapasuka iwapo nitagombea nafasi ya mwenyekiti, kwa sababu chama ni zaidi ya Zitto," alisema mwanasiasa huyo kijana.


"Najua nimewaangusha wengi, lakini chama ni zaidi ya Zitto. Zitto atapita Chadema itaendelea kuwepo, nimezingatia umoja wa chama kuliko maslahi yangu."


Alisema awali alishawishiwa kuondoa jina lake kwenye nafasi hiyo kwa kuwa angepewa cheo kingine kwenye chama, lakini alishikilia msimamo wake wa kupambana na Mbowe kwenye uchaguzi.


"Niliwaambia wazee wa chama kwamba lengo langu si vyeo, bali ni kutumikia chama ndio maana nilikataa kujitoa ‘in exchange for cheo' (ili nilifidiwe kwa kupewa cheo), lakini nimekubali kwa maslahi ya chama,"alisisitiza Zitto.


"Kama chama kitaona bado nahitajika katika kujenga chama, nitakubali nafasi yoyote nitakayopewa, lakini si kuwa na lengo la kutaka vyeo."


Mwananchi iliripoti Jumamosi iliyopita kuwa wazee wa Chadema walikuwa wamepanga kukutana na Zitto ili wamuombe aondoe jina lake kwenye nafasi ya uenyekiti na kwamba, angepewa cheo cha katibu mkuu wa chama baada ya anayeshikilia nafasi hiyo, Dk Willibrod Slaa kuripotiwa kuwa anataka kujiweka pembeni na majukumu ya chama, ili awatumikie kwa karibu wananchi wa jimbo lake la Karatu.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa wazee walimshauri Zitto ajitoe na kumuachia Mbowe aendeleze harakati zake za kukijenga chama na kwamba, walimtaka agombee nafasi ya makamu mwenyekiti, lakini habari zinasema kuwa alikataa.


Badala yake, kwa mujibu wa habari hizo, Zitto alisema katika kikao hicho kuwa angejitoa iwapo na Mbowe naye angejitoa, wazo ambalo liliwakuna vichwa zaidi wazee hao.

Miongoni mwa wanaounda Baraza la Wazee la Chadema ni waasisi wawili wa chama hicho, Edwin Mtei na Bob Makani, na habari zaidi zinasema kuwa katibu mkuu, Dk Willibrod Slaa pia alihudhuria mkutano huo na Zitto.


Zitto, 33, aliiambia Mwananchi juzi kabla ya mkutano huo na wazee kuwa yuko tayari kupokea ushauri wowote kutoka kwa wazee hao na haikuwa ajabu jana alipotangaza kuwa amejitoa kwenye kinyang'ayiro cha uenyekiti.


Akifafanua kuhusu uamuzi wake wa kumwachia Mbowe agombee peke yake nafasi ya uenyekiti na hivyo kuwa kwenye nafasi ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha pili, Zitto alisema lengo lake lilikuwa ni kuitumikia Chadema kwa maslahi ya wanachama na Watanzania wote na hakuwa na lengo la kutafuta cheo au ukubwa.


Zitto alisema kuwa amekubali ushauri wa wazee ambao walimwambia kuwa akiendelea na nia yake ya kugombea uenyekiti, chama kitapasuka na hivyo akaona ajiondoe ili kuinusuru Chadema.


Lakini mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliponda uamuzi huo wa Zitto akisema kuwa kama ni maslahi ya chama alipaswa kuyafahamu mapema na hivyo asingechukua fomu ili apambane na Mbowe.


"Zitto ni kiongozi makini, si tu kwamba namsifia bali kazi zake ndio zinaonekana. Ni fundi wa kujenga hoja, kwa hiyo nastaajabu kama amejitoa kwa sababu ya maslahi ya chama. Kwa nini hakujua hilo tangu mwanzo kwamba kugombea kwake kungesambaratisha chama," alihoji Profesa Lipumba.


Profesa Lipumba alifafanua kwamba, kitendo cha yeye kuchukua fomu na baadaye kujitoa katika kinyang'anyiro mwishoni na kukubali kusimama kwa mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti, taswira ya chama katika demokrasia inaweza kuvurugika.


"Alituambia kwamba, ameamua kugombea kwa sababu ya ushauri wa wanachama wake ambao ni wazee wanachama, sasa inashangaza leo kusema wanachama wake hao hao wamemwambia chama kitasambaratika iwapo atagombea," alisema Profesa Lipumba.


Mwenyekiti huyo wa CUF aliweka bayana kwamba ikiwa kutakuwa na mgombea mmoja katika nafasi ya mwenyekiti, demokrasia ambayo tunaipigania haitakuwapo na kwamba Watanzania wataona alishinikizwa kujitoa, jambo ambalo ni kinyume na misingi ya kidemokrasia.


"Jambo ambalo hata mimi kama mwenyekiti wa CUF nililikataa sana wakati wa uchaguzi wa chama changu... kama kuna jambo nililikataa, basi ni kusimama mgombea mmoja katika nafasi ya mwenyekiti. Ndio maana nilikuwa mtu wa mwisho kuchukua na kurudisha fomu, ili kulinda demokrasia ya chama na wala hakukuwa na shinikizo la waliojitokeza kujitoa," alisema Profesa Lipumba.

"Sitaki Zitto aonekane si mtu na si kiongozi makini, lakini hii ya kuchukua fomu na kujitoa na kukubali kusimamisha mgombea mmoja ndani ya Chadema, itaathiri sura ya demokrasia ndani ya chama."


Naye katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza alipata kigugumizi kuzungumzia uamuzi wa Zitto kujitoa, akiomba asitoe maoni yake.


"Naomba 'nisi-comment' (nisizungumze) chochote kuhusu hilo kwa sababu 'comment' yangu yoyote inaweza kujeruhi na kusambaratisha chama chao, ukizingatia kwamba kinaelekea wakati wa uchaguzi mkuu," alisema Ruhuza.


"Unajua vyama hivi vina mifumo tofauti. Kila mwanachama ana haki ya kugombea na kila mmoja ana haki ya kujitoa pengine huo ndio mfumo wao."


"James Mbatia Mwenyekiti wetu alishasimama na Mabere Marando, lakini hakujitoa licha ya kushauriwa ajitoe na pia akasimama tena na jamaa mmoja anaitwa John Dodo, hatuna kawaida ya kumuogopa mwenyekiti sisi."

Kwa upande mwingine maandalizi ya mkutano mkuu wa Chadema unaotarajiwa kuanza Septemba 3 mwaka huu, yamepamba moto. Mwananchi ilishuhudia wajumbe kadhaa wa mkutano huo kutoka Bara na Visiwani wakiwa makao makuu ya chama hicho.
Leo hii Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), linafanya uchaguzi wa viongozi wake katika hoteli ya Keys iliyo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.




Contact Us DISCLAMEREmail:webmaster@mwananchi.co.tz© Mwananchi Communications Ltd 2006- 2009
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom