Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Hii mambo ya u-chagga this and uchagga that ni uzamani, tuelekee mbele na tujadili mambo ya msingi, U-mbadala upo wapi katika chaguzi za CHADEMA? Mnyika yuko wapi kutoa fafanuzi endelevu kwetu siye wa nje ya chama? Hivi hii ni ile CHADEMA iliyokuwa inanipa matumaini ya kuwa mwanangu ataishi katika neema ya demokrasia ya kweli? nahitaji maelezo zaidi ya 'NAKINUSURU CHAMA', sitaki kuamini kuwa huo mwelekeo wa kusubiriana miaka 12 ndio u-mbadala mliotuhubiria
 
Mwanakijiji au Kitila MKUMBO huwa wanajadili CCM wao ni CCM?Lowassa au spika Sitta tunamjadili kwanini wakati sio wana CCM?
Field Marshal ES anawajadili watu wa Chadema wakati yeye sio mwana Chadema.

Mwiba ni CUF anawajadili CCM kila siku kwanini hukumuuliza swali hili?
swali langu ni la kisheria zaidi ndio maana nikaweka jukwaa la sheria. kisheria Mzee Mtei hakutakiwa kushiriki kikao kile kwa ajli ya kuwa mzazi wa mmoja wa wagombea-Mbowe.

Makani hakutakiwa kushiriki kikao kile kwa vile ana mahusiano ya kikazi na MBOWE walipokuwa BOT.

hakukuwa na FAIRNESS kutokana na sababu hizo mbili.kifupi maamuzi ya hao wazee ni batili.

Rafiki
Hao ni madikiteta wenda kuliko ccm,kama kujadiliwa wanalazimisha mpaka uwe chadema ndio ujadili wewe bado unashaka tu kwanini Zitto kapigwa nokauti.

Wao wameshasahau kabisa huwa wanawajadili CUF akina safari,mtikila,akina makamba na chilingati.

Kweli inatia shaka sana wenda bado hatujui nini hasa tunakitaka ktk mustakbali wa taifa letu.
 
mafisadi ni kina nani? hili swali huwa najiuliza bila majibu na hadi imefikia kipindi nimekuwa mshabiki wa wapinga ufisadi lakini bila kujua maana halisi ya ufisadi
 
ila ameamua kujitoa kwa lengo la kukinusuru chama ni wazo zuri ukiangalia sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu tunatakiwa tuwe wamoja wenye mshikamano
 
nahitaji maelezo zaidi ya 'NAKINUSURU CHAMA', sitaki kuamini kuwa huo mwelekeo wa kusubiriana miaka 12 ndio u-mbadala mliotuhubiria
Chama kimeshazama na kwa bahati mbaya kimejizamisha chenyewe. Kukinusuru katika hali kama hii inahitaji muda, nguvu na fedha nyingi... tusitarajie hilo kutokea siku za karibuni
 
KizitoMbowe.jpg

Chadema top brass shake hands to show solidarity, moments after briefing journalists at the party’s headquarters in Dar es Salaam yesterday. They are from (R) national chairman Freeman Mbowe, secretary general Dr. Willibrod Slaa, the party`s founder, Edwin Mtei and deputy secretary general Zitto Kabwe who withdrew from the contest for the party chairmanship against Mbowe.

Hon. ukimaliza hizi PR jongea jamvini tafadhali ujibu hoja zetu.

Hapa picha inaonesha nani mnafiki,
 
Shalom hajana na hoa Wachagga na chadema yao.Imeishaeleweka Chadema ni ya Wachagga.Nasisi inabidi tuanzishe chama chetu kule nyanda za juu kusini na tunaweza kuungana na akina SIKONGE.Mtasema ukabila lakini mbona kanisa letu la moravian lilikuwa kwetu tu na kwa kina Sikonge?We Mkwe Fungua Macho

Duh, Kaazi kweli kweli
 
kujitoa kwa zitto kuna onesha jinsi gani ame komaa kisiasa

Naona maandiko ya kibanda tayari kila kitu kilikuwa kimeshaandaliwa.
Nayaona jinsi ma B52 yalivyokuwa yameandaliwa.Yani

1.akiendelea kugombea wazee walikuwa wammalize kwamba anatumiwa na RA.

2.wamshauri kujitoa ,na akijitoa tu hana msimamo ni mbabaishaji,ukitaka liona hilo ni njisi inavyokwenda
(a).ushauri uliotolewa si wa kibabaishaji lakini aliyeupokea huo ushauri amepokea ushauri wa kibabaishaji.

(b) wazee walimshauri ajiodoe ili akinusulu chama, wazee waliosema hayo wao wako sahihi ,ila waliyemwambia akisema waliyosema wazee kwamba ajiondoe akinisulu chama ,basi yeye akisema wao wanahoji ana maana gani anaposema hayo.

Yeye Zitto kajitoa sio kwa uamuzi wake toka awali ila kajitoa baada ya kupokea ushauri na sababu zake, sasa inashangaza kwamba anapohojiwa na waandishi wa habari sababu zake za kujitowa watu wanataka asisema sababu zilizosemwa na wazee wa busara ila wanataka aseme hivi "mimi Zitto nimejitowa kwa sababu nimeona sina uwezo wa kukiongoza chama".

hii ya pili ni sahihi tu kama angelijitoa bila kuitiwa mkutano na wazee wa busara.
 
mafisadi ni kina nani? hili swali huwa najiuliza bila majibu na hadi imefikia kipindi nimekuwa mshabiki wa wapinga ufisadi lakini bila kujua maana halisi ya ufisadi

Tanzama uchambuzi huu hapa; good for beginners.

UFISADI na MAFISADI


•Kutekwa kwa Dola: Dhana

•Ufidadi ni msamiati mpya kabisa katika dhana ya siasa za Tanzania.

•Awali kabla ya 2006, ufisadi ulimaanisha
‘ufataki’

• Chimbuko la msamiati ni nchini Kenya (Ushirikiano wa Jumuiya ya EAC?

•Mwanzo kurasmisha msamiati ufisadi: Mwembeyanga Septemba 2007.



Dhana ya Kutekwa kwa Dola

•Ufisadi ni wasilisho la mtazamo/maoni ya wananchi juu ya vitendo vya kutekwa kwa dola.

•Ainisho la kutekwa kwa dola

–
‘Mtandao’ wa ‘rushwa kubwa’ unaoshirikisha viongozi wakuu wa serikali.

–Sheria sera na taratibu za utawala zinawekwa/
’zinagandishwa’ kunufaisha ‘wanamtandao’ wa ufisadi.

–Vyombo vya dola na/au habari vinadhaifishwa

–Wananchi wanakosa mtetezi na/au sauti.

–Hali ya maisha inakuwa mbaya kwa wananchi wa kawaida.

Dhana
….

–Sharia za nchi zinatumika kwa kutegemea hadhi na mahusiano ya mhusika na na matandao wa ufisadi.

–Nchi inaendeshwa kwa utawala wa sheria mwitu,
‘Rule of law of the jungle.’

–Usalama na amani kwa wananchi unayoyoma, kupotea kwisha kabisa.

–Nchi inaingia kwenye machafuko; rushwa kubwa na rushwa ndogo vikiendelea

Mjadala wa Ufisadi Tanzania, Utambuzi

•Mwembe yanga 2007 na baadaye;

–Rushwa kubwa za Tangold, Meremeta, Deep Green.

–Mtandao wa wizi/ufisadi wa EPA

–Buzwagi na mikataba nyingine ya madini.

–Commodity Import Support (CIS) na Debt Conversion Programme (DCP)

–Mkataba wa kujenga Twin Towers, BoT.

–Manunuzi ya Ndege ya Rais, rada, vifaa vya jeshi (magari, helicopter na zana nyinginezo) na huduma (Alex Stewart Assayers G B)

–Mikataba ya Richmond na Dowans

–Ubinafsishaji mashirika ya umma
– Kiwira, TTCL, KIA, NBC, Williamson Diamond na mengine

Utambuzi
…

–Matumizi mabaya ya madaraka na uchuuzi katika ofisi za serikali (ANBEM, EOTF, Net Group Solution na kashifa nyinginezo)

–Mikopo kutoka taasisi za fedha za umma bila kufuata taratibu zilizopo (NSSF 8bn/-, CRDB 17bn/-)

–Mikataba ya kujenga na kuuza majengo ya Ubungo EPZ

Tathmini

•Kiasi kikubwa cha pesa kinahusika

•Uhalali kisheria ni mashaka matupu.

•Kulindwa na dola/dola kushindwa kuwajibisha wahusika (visingizio)

•Wahusika wanajulikana; ni mtandao wa watu walewale.

•Maisha ya wananchi yanaendela kuwa mabaya

•Serikali haionekani kuchukua hatua madhubuti na stahili

Washiriki wa, na agenda za Mjadala wa ufisadi

•Vyombo vya habari

–Vinavyomilikiwa na kuhudumiwa na wanaopinga ufisadi

–Vinavyomilikiwa na kuhudumiwa na wanaotetea ufisadi

•Wananchi na Viongozi wa Serikali

–Wananchi na wabunge/mawaziri/viongozi wa vyama vya siasa wanaopinga ufisadi

–Wananchi na wabunge/mawaziri/viongozi wa vyama vya siasa wanaotetea/kushabikia ufisadi.

•Mgawanyiko unaonekana bayana (maslahi)

Mwitikio wa Serikali

•Kamata-kamata; kesi 3 ziko mahakamani (EPA 1, BoT Twin Towers 1, Matumizi mabaya ya ofisi ya umma 1)

•Kulaani matumizi mabaya ya vyombo vya habari

•Kulaani kuingilia kesi zilizoko mahakamani

•Kualaani wanaokiuka haki za binadmu kwa kuwataja mafisadi hadharani.

•Kutaka wapelekewe ushahidi (Polisi)/kujibaraguza?

•Kuleta dhana ya ubaguzi wa rangi na ushindani wa kibiashara katika hoja za mapambano dhidi ya ufisadi.

•Kukiri hadharani kuwa mafisadi wana nguvu sana, pengine zaidi ya dola.

•Kuonya vyombo vya habari na wananchi wasiendeleze mjadala dhidi ya mafisadi na ufisadi (kufunga mjadala).



Mkakati Unaofaa

•Kutumia fursa hii kuhamasisha umma (social movement)

•Kutumia fursa kupaza sauti za wananchi

•Kutumia ushahidi uliopo; vyombo vya habari, tafiti za wanataaluma, ripoti za Serikali (CAG), na ripoti za kamati teule za Bunge (Richmond) kuendeleza mjadala dhidi ya mafisadi na ufisadi.

Tufanye Nini?

• Tuhitishe maandamano?

•Tufanye mkutano na waandishi wa habari?

•Tutangaze bayana kuunga mkono upande mmojawapo katika vita dhidi ya ufisadi na mafisadi? Tunajitambulisha kuunga mkono upande gani?
’

•Tutoe
‘Taarifa kwa vyombo vya habari’?
 
Je, Kujitoa Kwako Kugombea Uenyekiti Kunajenga au Kunabomoa Chama?

Ndugu Zitto Kabwe (MB),

Nimeamua kukuuliza swali hili la wazi kwa faida ya Jamii ya Kitanzania kwa ujumla. Ningeweza kukuuliza kwa faragha ila kufanya hivyo kungenisaidia mimi binafsi. Naamini suala hili linapaswa kujadiliwa kwa uwazi na ukweli.

Nilikuwa safarini hivyo nilipitiwa na hizi taarifa za wewe kujitoa kugombea Uenyekiti. Leo baada ya kusoma taarifa hizo katika za Vyombo vya Habari nimepigwa na butwaa. Swali kuu nalojiuliza ni, je, kujitoa kwako kutasaidia kuleta huo umoja ndani ya chama chenu au ndio utakigawa zaidi?

Swali hilo kuu linazaa maswali haya mengine ambayo naomba uyajibu:

1. Je, hukuona kuwa utakigawanya chama ulipochukua fomu?
2. Je, huoni kuwa ni hatari kubadili msimamo mzito kama huo?
3. Je, haionekani kuwa umewasaliti waliokuomba ukagombee?

Ndugu nitashukuru kama utanijibu maswali hayo ili nisibaki naamini kuwa hata hicho 'chama kina wenyewe'!

Wasalaam,
Mpiga Kura


Nashindwa elewa nini maana ya neno demokrasia. na kama demokrasia ni kubomoa au kupasua basi ili kujenga umoja wa nchi yetu tumuache JK awe mgombea pekee wa Urais kwa Tanzania mwaka kesho.
 
Baada ya kumlazimisha zitto asigombee uenyekiti wa CHADEMA bila sababu za msingi eti chama kitapasuka..
leo hii WAZEE hao hao wametoa mpya kwa kuufuta uchaguzi wa baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA)
sasa ndugu zangu hawa wazee ndio katiba yao au?
kama hari ikiendelea kuwa hivi,hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mageuzi nchini
 
Tatizo walioshinda sio chaguo la Mbowe.kila chama kina wenyewe bwana.
 
Baada ya kumlazimisha zitto asigombee uenyekiti wa CHADEMA bila sababu za msingi eti chama kitapasuka..
leo hii WAZEE hao hao wametoa mpya kwa kuufuta uchaguzi wa baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA)
sasa ndugu zangu hawa wazee ndio katiba yao au?
kama hari ikiendelea kuwa hivi,hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mageuzi nchini

Usiseme sana Wazee ila sema Baba Mkwe wake Mbowe, maana huyo ndio Mwenyekiti wao na ni dikteta kinoma. Hata Marehemu Wangwe aliwahi mwambia ya kwamba ni kweli yeye ni muasisi wa chama lakini kwa chama kilipofikia maamuzi yawe yanafanywa na wanachama na si yeye kwa kisingizio cha wazee wamesema. na isitoshe hakuna close katika katiba ya chadema inayowapa mamlaka wanayo ya -exercise, ukisoma kitabu cha: Chacha Zakayo Wangwe: MPAMBANAJI MTETEZI WA WANYONGE, utaona ni jinsi gani hawa wazee walitumia hila kumuondoa ili kumnusuru Mbowe na kuendesha chama kama mali yake binafsi, ukabila na ufamilia.
na hapohapo nimegundua kama tunataka kuona mbali basi ni heri tuanzishe chama cha vijana maana hivi vingine ni remote controled ya Wazee bila kuangalia maslahi ya makundi mengine katika jamii.
 
Mbowe & family wamekijenga chama from the grass root kwa taabu na gharama kubwa, iweje leo waje watu wa nje na kupora madaraka kwa mgongo wa demokrasia? no way!

Mwenyekiti Mbowe yupo sahihi kwenye hili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom