Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Acha propaganda, Wazee wale ni wakina Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Wakili Makani, Mzee Kasisiko nk. Kasisiko ni Mwenyekiti wa Zitto Kigoma na Makamu Mwenyekiti wa Wazee na ndugu wa damu wa Zitto bado hakutaka Zitto kugombea uenyekiti. Kuna siri nzito, labda ipo siku wazee wataisema au Zitto mwenye ataropoka. Siri hii haihusiani kabisa na uchaga, inahusu ufisadi!

asha

This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.
 
Mmekazana Demokrasi demokrasia hivi CCM kuna demokrasia? Maana kuna mizee mle toka nazaliwa ipo kwenye chama mpaka leo hii....hiyo ndo demokrasia mnayo hubiri?
 
Undoeni ukabila kama mnataka kudumisha chama. Chama hakiendeshwi kikabila. Alijaribu Cheyo na akashindwa, mtaweza nyinyi. Maana Cheyo alikuwa na mtaji wa wasukuma 5 milioni lakini hakupata kitu, sasa wenzangu mtaji wenu mdogo sana ndio mtapata nini? Kalaga baho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Fikra zile zile zenye utando wa kutoelewa.
Mara ngapi mmeshapata ufafanuzi wa kina kuwa Chadema hakuna ukabila? Hao akina Makani, Baregu,Ngaiza nk ni wachaga? Huna cha kusema kalale!
 
CHADEMA sasa demokrasia imekuwa bora kwenye chama cha Savimbi.

Kwa heshima na taadhima naomba msimfuate tena Mzee makame.

Mnyika baba kinehe ahenaho "?
 
Mbowe & family wamekijenga chama from the grass root kwa taabu na gharama kubwa, iweje leo waje watu wa nje na kupora madaraka kwa mgongo wa demokrasia? no way!

Mwenyekiti Mbowe yupo sahihi kwenye hili

Eebo!! Kwahiyo Familia ya Nyerere nayo wafanye kama ya Mbowe?? Je tutafika??
Hapa tunachotaka ni demokrasia ya kweli kwama chama ni cha kifamilia basi wawe wanafamilia pekeyao ijulikane moja? Eti walitumia garama kubwa so what??

Huu ni ujinga na mawazo finyu kwa hao wanaofikiria chama ni mali yao.Chama ni mali ya wananchi wote wenye mapenzi mema na chama.

Mwalimu Nyerere (RIP) alisema tukianza kubaguana kwa ukabila na udini tutakwisha tutatafunana wenyewe. Ndio maana ya dhambi ya ukabila na udini huo. sasa chadema wnaelekea huko.
 
Zitto
user_online.gif

Zitto has no status.
JF Senior Expert Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Fri Mar 2007
Posts: 541
Thanks: 160
Thanked 1,431 Times in 324 Posts
Rep Power: 64
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

icon1.gif
Re: Zitto na Mama yake wawazidi kete vijana CHADEMA
Ndugu zangu,

Katika kipindi hiki sikutaka kabisa kuingia na kujibu hoja yeyote ndani ya JF kuhusiana na uchaguzi wa vijana Taifa. Hata hivyo mtaniwia radhi kujibu hili ili kuweka rekodi sahihi kutokana na upotoshaji ambao unafanyika kwa makusudi kabisa ili kushusha heshima yangu katika jamii.

Moja, mimi ni mumbe wa Baraza la Vijana la CHADEMA kwa nafasi yangu ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu wa kuchaguliwa kuwakilisha vijana na nikiwa Mbunge mwenye umri wa ujana (miaka 33). Hivyo kushiriki kwangu kwenye vikao ni jambo la kawaida kabisa kwani nina haki ya kupiga kura. Vile vile nina haki ya kuamua mgombea gani wa kumuunga mkono katika uchaguzi. Niseme waziwazi kuwa David Kafulila ndiye mgombea niliyemwunga mkono na kumfanyia kampeni waziwazi bila kificho chochote kile. Hii inatokana na tabia yangu ya kutokuwa mnafiki. Nilimwunga mkono David Kafulila na alishinda kwa kupata kura 99 dhidi ya kura 73 ambazo alipata mgombea mwingine John Heche ambaye alikuwa anaungwa mono na kundi lililonipinga kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Huyu aliyeandika post hii ni mmoja wa vijana wa makao makuu ya CHADEMA ambaye amekuwa akinipinga siku zote kwa chuki tu ya kuwa mimi nimepaata umaarufu wa kisiasa kuliko yeye na kundi lake.

Mama yangu mzazi ni mwanachadema. Ni kiongozi mwandamizi wa CHADEMA kutoka mkoa wa Kigoma na amekuwa msaada mkubwa wa chama katika Manispaa ya Kigoma. Ninaomba sana masuala yangu ya kisiasa na mahasimu wangu wasimhusishe mama yangu mzazi. Ninaomba sana sana mumuweke mama yangu pembeni. Mwandishi wa post hii tafadhali naomba usimhusishe mama yangu na tofauti zetu za kisiasa. Ninaomba sana hili liheshimiwe.

Pili, ni dhahiri kulikuwa kuna makundi katika uchaguzi wa BAVICHA. Mimi niliweka wazi msimamo wangu wa kumwunga mkono kafulila. Wakurugenzi wa Makao makuu ya chama kuanzia Katibu Mkuu mpaka wakurugenzi kama John Mnyika, John Mrema na hata maafisa kama Halima Mdee walikuwa wanampinga David Kafulila. Hawa wanaogopa uwezo wa Kafulila wa kukataa kutumika na kuwa independent katika maamuzi yake.
Hii sio mara ya kwanza kwa Kafulila kuzuiwa haki yake. Kijana huyu alipitishwa kugombea Ukurugenzi wa vijana na jina lake kwenda katika Kamati Kuu. Ajenda ya uteuzi wake ikasitishwa baada ya kuhofia kuwa atashinda. Mtindo huo huo wameutumia sasa kufuta uchaguzi na kuupeleka mbele mpaka baada ya miezi 6. Mimi nimekataa

1. Uchaguzi umefanyika.
2. Matokeo hayakutangazwa
3. Hakuna aliyekata rufaa

Hivyo, wazee wanapata wapi 'locus' ya kufuta uchaguzi?

Hata hivyo wenye mamlaka ya kufuta uchaguzi ni Kamati Kuu ya chama maana kuna taratibu za rufaa ndani ya chama chetu. Nimetaka Kamati Kuu iitishwe ili taratibu zifuatwe.

Huyu mtu aliyeleta post hii hapa anataka kuspin ili kupinda ukweli bila aibu.

David Kafulila kashinda round ya kwanza zaidi ya 50%. Wamekataa kutangaza matokeo na kuleta fujo kwenye mkutano.

Kuna tuhuma dhidi yangu kuwa nimetoa rushwa. Huku ni kutapatapa kwani tuhuma hizi zinatolewa bila ushahidi. Hivi huyu mwandishi na akili zake timamu anaweza kuweka akilini kwake kuwa mimi naweza kutoa rushwa hadharani? Eti nimevuta kiti na kuita watu kutoa rushwa. Bila adabu anamhusisha mama yangu mzazi.

Mama yangu ana maamuzi yake binafsi na mfano dhahiri ni uchaguzi wa chaha wangwe ambapo mimi nilimwunga mkono arfi na yeye akamwunga mkono Chacha wangwe waziwazi na bila kificho.

Uchaguzi wa vijana haukua na rushwa. Uchaguzi wa vijana wa chadema umefanyika kwa amani kabisa na matokeo hayakutangazwa kwa kuwa mgombea 'wao' hakushinda.

Wanasema eti Mtemelwa aliyekuwa ananiunga mkono alishindwa Temeke. Hawasemi watu waliowatuma kwa kutumia fedha za chama kugombea mikoa 15 na kutupwa chini na watu wanaoniunga mkono. Ukiwemo mkoa wa Dodoma na Shinyanga ambao walitumwa wakurugenzi wa chama kama Benson Kigaila na Erasto Tumbo na kushindwa. Habarindiyohiyo nakuomba ukumbuke kuwa baada ya uchaguzi kinachofuata ni ukaguzi wa fedha za chama katika kipindi hiki na jinsi zilivyotumika. Nashukuru Mungu kuwa ukaguzi huo sasa utafanywa na CAG

Katika spirit ya umoja na mshikamano wa chama tutamaliza suala hili katika Kamati Kuu ya chama.

Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.

Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.

Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!

Haya ambayo nimeyaandika hapa JF nimewaambia vijana hawa 'face to face' ili waache uwongo, uzandiki, majungu, fitna na chuki.

Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.

Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.
 
yaani hata siamini........kinachoendelea huko Chadema....duuh

John Mnyika wewe ni mwanachama hapa JF, hebu tuweke sawa........
 
Politics of patronage ndo sasa zinaonekana sahihi. Hakuna enzi nilizokuwa naziona kama za chaguzi za kihuni kama enzi za mgombea pekee wa chama!! Kwa nini mgombea pekee? Kwa sababu wakiwa zaidi ya mmoja chama kitagawanyika!!

Effectively hii maana yake ni kuwa NEC ya CCM ndiyo iliyokuwa ikichagua, full stop. Wananchi wanaitwa kuweka muhuri!!

CHADEMA imeamua kwenda njia ile ile. Yaani kikundi cha wateule fulani ndani ya Chama ndo wanaamua nani awe nani. Reasons ni kuwa watu wana very low level ya emmotional competence. Wakishindanishwa, badala ya kushindana, wanabomoana. I can understand this.

Lakini hii itatutofautishaje na vyama vya kikomunisti?? Tumekubali kuwa hatuwezi kuwa mabepari!! Kwenye ubepari core value ni competition, kazi ya vyama ni kuhakikisha kuwa hii value inalindwa. Badala yake kwetu sisi kazi ya vyama imekuwa ni kuzuia competition kwa sababu competition inaonekana ni hatari kwa uhai wa vyama!!! SAD!

Madhara ya siasa hizi ni makubwa kuliko tunavyodhani. Hii hangover ya mifumo ya kikomunisti bado imejaa. Tunaogopa competition kwa sababu kwenye vyama personalities ni muhimu kuliko vyama. Hii ni shida kubwa. Tunaendelea kujenga watu, badala ya kujenga vyama. watu huja na kupita! Vyama vinaishi. Inatakiwa tufikie mahala watu wanaoviongoza vyama waviheshimu vyama na kuviacha vikue.

Sheria ya ushindani hutaka mapambano ya fikra, ili fikra bora zisimame. Wapo watakaoanguka kutokana na hii. Na vipo vyama vitakavyoanguka kutokana na hii. Lakini ndo test ya ubora wenyewe!

ikiwa Chadema haiwezi kuhimili mikiki mikiki ya mapambano ya ndani, ni afadhali kife ili kizaliwe kingine kitakachoweza kuhimili. Vinginevyo kulea hiki kilichotokea ni kujenga CCM nyingine. Hatuichukii CCM kwa sababu tunawachukia kina Kikwete na viongozi wengine wa CCM. Tunakichukia CCM kutokana na kukosekana uwazi katika maamuzi yake. Kukosekana kwa uwazi huku ndo kumelea donda ndugu la ufisadi. Kukosekana kwa uwazi huku ndo kunafanya iwe ngumu kulishugulikia donda ndugu la ufisadi katika nchi hii.

Kulea chama kingine kinachofanya maamuzi yake kama CCM si jambo la kheri kwa nchi hii na watu wake!!!
 
Thanx Zitto kwa maelezo yako,

CHADEMA inakoelekea imeanza kuwatia wasi wasi wananchi wanaoiunga mkono na kufikiri kwamba ndio kitatoa upinzani madhubuti 2010. Ila kwa sasa sivyo ilivyo na sipendi kuwa mtabiri ila naanza kupata maono ya kusambaratika kwenu hasa mnapoanza kuanika siri zenu za ndania kama ulivyofanya hapa.

Ok, wanakuchafua, ila nafikiri ingekuwa sahighi kwako kutojibu hadharani kama hivi bali kutafuta namna nyingine ya kutatua. Nawahakikishia CHADEMA hamtafika popote na nafikiri kuna nguvu kubwa ya CCM kuendeleza machafuko haya kwa manufaa yao.

CHADEMA imepata sifa ilizonazo si kwa sababu ya mbowe au Zitto ila ni kwa muunganiko wa kila mmoja wenu kuanzia juu mpaka chini. Naanza kuhisi anguko la Chadema kama lile la NCCR maneno ya Nyerere yatatimia kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM. Unasema wewe ni maarufu kuliko Mnyika, so what? .

Maneno uliyosema hapo ni ya vikao vya ndani
 
Nashukuru nimekusoma Mh. Zitto lakini ninacho omba ufafanuzi ni hapo unaposema wamekataa kutangaza matokeo kwa sababu kafulia kashinda, je, yeye hakutakiwa kushinda? au alikiuka taratibu za uchaguzi?

Lapili, mimi kama mwanachama naona ninyi viongozi wa CHADEMA mmenivunja moyo kwa matendo yenu yanayoendelea. Naomba Zitto unihakikishie kama kweli wewe, mbowe, mnyika, slaa, ndesamburo bado mwaweza kukaa pamoja na kuturudishia imani sisi wanachama ambao tulitaraji makubwa kutoka kwenu lakini sasa mnatuhadaa.
 
Baada ya kumlazimisha zitto asigombee uenyekiti wa CHADEMA bila sababu za msingi eti chama kitapasuka..
leo hii WAZEE hao hao wametoa mpya kwa kuufuta uchaguzi wa baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA)
sasa ndugu zangu hawa wazee ndio katiba yao au?
kama hari ikiendelea kuwa hivi,hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mageuzi nchini

Zitto hajalazimishwa. Ameshauriwa kama Bilal alivyoshauriwa 2005 asimpinge Karume. Hiki sio kitu cha ajabu katika Siasa. Hata 2004 katika Kinyanganyiro cha Urais kule Marekani Bush hakuwa na mpizanzani katika mchakato ndani ya chama chake cha Republican. Ni busara ilitumika ili kuepuka utengamano hasa kwenye wakati kama huu ambapo Chadema inakua. Kuhusu uchaguzi kufutwa, nadhani tusibiri tuambiwe kwa nini wazee wameamua kuufuta uchaguzi wa BAVICHA.Mimi nadhani kuna sababu labda kama hawa wazee wetu wamechanganyikiwa?!
 
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.

Zitto asiku shughulishe huyo m-kaskazini anaejidai ni Mzanzibari, ndio haoa hao.

Msimamo wako ume eleweka hao hawataki mabadiliko lakini banana nao humo humo mpaka kieleweke!
 
Thanx zitto kwa maelezo yako,

Chadema inakoelekea imeanza kuwatia wasi wasi wananchi wanaoiunga mkono na kufikiri kwamba ndio kitatoa upinzani madhubuti 2010. Ila kwa sasa sivyo ilivyo na sipendi kuwa mtabiri ila naanza kupata maono ya kusambaratika kwenu hasa mnapoanza kuanika siri zenu za ndania kama ulivyofanya hapa.

Ok, wanakuchafua, ila nafikiri ingekuwa sahighi kwako kutojibu hadharani kama hivi bali kutafuta namna nyingine ya kutatua. Nawahakikishia CHADEMA hamtafika popote na nafikiri kuna nguvu kubwa ya CCM kuendeleza machafuko haya kwa manufaa yao. Chadema imepata sifa ilizonazo si kwa sababu ya mbowe au Zitto ila ni kwa muunganiko wa kila mmoja wenu kuanzia juu mpaka chini. Naanza kuhisi anguko la Chadema kama lile la NCCR maneno ya Nyerere yatatimia kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM. Unasema wewe ni maarufu kuliko Mnyika, so what? .Maneno uliyosema hapo ni ya vikao vya ndani

nilishawahi kusema huko nyuma kuna watu wana tatizo la kutaka watu waamini kuwa wao ndio vinara wa mambo fulani............hili ni tatizo ndani hii Chadema na Mkuu Shangazi nashukuru sana kwa kuliona hilo na.............. Maneno yako ni mazito sana hayo Mkuu, tuko UKURASA MMOJA.........
 
yaani siasa, kweli mchezo mchafu. maana ni kuzidiana kete tu. haya jamani sijui kama tutafika mwisho mzuri, mie yangu macho
 
Pasco,

Ni muhimu mno uwe na uhakika kabla ya kutoa accusations nzito kama hizo za kwamba Zitto atahamia CCM. Asipohamia sijui utamwomba msamaha mara ngapi?

Nafikiri ifike mahali tutofautiane kwa hoja; hizi dalili za kila aliye na mawazo tofauti basi anatumiwa au anataka kutimkia CCM mimi nafikiri hazitasaidia kujenga demokrasia ndani ya hivi vyama.

Kumbukeni hizi accusations zilielekezwa kwa Wangwe pia pale alipoonyesha nia kwamba huenda angempinga Mbowe.

Hivi kwanini tunaogopa sana mabadiliko? Kwanini tusiamini busara za wananchi au wanachama kufanya maamuzi ya maana?

Politics is a dirty game, zangu sio accusation ni predictions ndani ya huo huo mchezo mchafu. Tatizo langu ni uwepo wa maswali mengi bila majibu, kunapelekea mimi na wengine wa aina yangu kushindwa kumwelewa Zitto mpaka leo. Haya ni baadhi ya maswali1. Alichukua fomu kwa kificho kupitia kwa wapambe. akajaza na kurudisha kupitia hao hao wapambe ni kwa nini?.2. Kwa nini hakushauriana na viongozi waliopo kabla hajataka kumuembarass Mbowe?.3. Anatoka Kogoma, ya Kabourou anayajua fika, ya Wangwe anayajua, kwa nini na yeye bado alitaka kurudia yale yale?.4. Chadema kilianzishwa na nani, akakabidhiwa nani na aliyepo ni nani na mlolongo wa wabunge ndugu, bado na yeye akataka kupenyesha shingo mpaka kwenye mizizi ili angoe kisiki huku anaejua fika atakikwaa kisiki na sasa yuko kwenye hati hati kuanguka, hakuyaona hayo yote?.5. Alisema hagombei hata ubunge, yeye amepania kurejea kwenye academia, mara ameshauriwa akabadili msimamo, kumbe sasa sio ubunge tuu, ni mpaka uenyekiti wa chama?! kwa nini lakini?.Hayo ni baadhi tuu ya maswali ambayo yananifanya nijiulize Zitto kweli ni pragmatist ama naye ni opportunist?.Kama ni opportunist, Chadema is a wrong party kwa sababu CCM ndio chama tawala, wanasiasa uchwala wote na waganga njaa lazima waelekeze nguvu zao huko sambambamba matamanio ama kushibisha matumbo yao ama kuendekeza njaa zao, bahati nzuri, Zitto hayuko kundi hili, lakini kwanini ameyafanya hayo aliyoyafanya?.Angalizo, CCM pamoja na uoza wote, CCM kama chama ni safi, tatizo ni baadhi ya wanachama na baadhi viongozi wake tena sio wote, miongoni mwao bado kuna viongozi safi, waadilifu ambao wanachafuliwa na vale waliolowea kwenye tope la uchafu.Chadema ni chama safi, kina baadhi ya viongozi wazuri tuu, lakini ni ukweli usiofichika, hata kikishinda uchaguzi leo, kina safu gani ya kuongoza nchi, hili Zitto analielewa na labda ndio kusudio lake kutoka kupanda gorofani kwa kutegemea ngazi mbovu!.Kama ni demokrasia ndani ya vyama, kwa Tanzania safari bado ni ndefu, ya Chadema tumeyaona, tena kwa ushauri, wasipoteze tena muda kumchagua mwenyekiti, keshapita bila kupingwa, uchaguzi wa nini?.Mgombea wa CCM mwakani nae tayari, ni utaratibu tuu wa kutuzuga kwa demokrasia kufuatwa.Ya CUF mliyaona ambapo Frof Safari yalimkuta na akatimua.Swali ambalo ndilo prediction baada ya kukumkuta Zitto yaliyomkuta, bado anauzito huyu au ni tayari mwepesi anasubiri ama kupeperushwa na upepo ama kupulizwa na wenyewe, ambapo he is left with no choices, apeperuke, apae aishie, ama anendelee kusimama, apulizwe, aanguke na kuflushiwa down the drain.
 
Last edited by a moderator:
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.

im failing to believe that wewe ni zito im sure sio wewe kama ni wewe basi huu ndo mwisho wako kisiasa na kweli hela za mafisadi zimekukolea baba,asante sana,sasa tusubiri mkombozi wa nchi hajachaguliwa,huna maana hata kidogo,sikutegemea km maneno haya ni yako,well if sio wewe samahani kwani humu ndani waeza watu kuingia kama wewe,so please jitokeze magazetini na everywhere uukane upuuzi huu,laa unaangamia kisiasa baba!unafulia taaaratibu kama mbatia
 
Thanx zitto kwa maelezo yako,

Chadema inakoelekea imeanza kuwatia wasi wasi wananchi wanaoiunga mkono na kufikiri kwamba ndio kitatoa upinzani madhubuti 2010. Ila kwa sasa sivyo ilivyo na sipendi kuwa mtabiri ila naanza kupata maono ya kusambaratika kwenu hasa mnapoanza kuanika siri zenu za ndania kama ulivyofanya hapa.

Ok, wanakuchafua, ila nafikiri ingekuwa sahighi kwako kutojibu hadharani kama hivi bali kutafuta namna nyingine ya kutatua. Nawahakikishia CHADEMA hamtafika popote na nafikiri kuna nguvu kubwa ya CCM kuendeleza machafuko haya kwa manufaa yao. Chadema imepata sifa ilizonazo si kwa sababu ya mbowe au Zitto ila ni kwa muunganiko wa kila mmoja wenu kuanzia juu mpaka chini. Naanza kuhisi anguko la Chadema kama lile la NCCR maneno ya Nyerere yatatimia kwamba upinzani wa kweli utatoka CCM. Unasema wewe ni maarufu kuliko Mnyika, so what? .Maneno uliyosema hapo ni ya vikao vya ndani

Tangu mh. Zitto alipokuwa akijigamba kuwa anamagari 5 n.k. mimi nilianza kuishiwa imani, lakini nae ni binadamu atueleze ekweli lakini.

Mimi kwanza sioni kama hata CCM inamkono hapo, ila ni yale yale ya uchu wa madaraka. kwamba zitto anamuunga mkono kafulia n.k. na wengine na kambi zao isho ni kukosa hata jimbo moja mwakani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom