Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Ninasema tena na tena Chadema mpeni Zitto fomu ya kugombea uenyekiti tena now, msituletee ngonjera hapa JF sio mahali pa ngonjera ni mahali pa kumkoma nyani tu giladi! hatuwezi kushusha standard zetu hapa JF kuwa-commodate Chadema tu no way, mimi ninasimamia policies sio jina la mtu, Zitto is not an ishu hapa the ishu ni demokrasia makini ambayo hapa mmeibana na kuivuruga kwa visingizio ambavyo havi-make a sense at all, Zitto apewe fomu na aruhusiwe kugombea wanachama waamue kuwa hafai, ya kuchafuana kati yenu huko Chadema hapa JF we could care less sisi tunasimamia demokrasia makini that is all!

FMES

I am speechless, siamini kama ni wewe uliyeandika haya! huwa uko analytical mzuri, ila kwa hili ur impartial. Nadhani ungesoma hii thread tokea mwanzo ungekuja kivingine kabisa, hoja yako hapo haina mshiko hata kidogo!Ur sounds very authoritative vipi kaka hapa ni kujadiliana hoja, unakuwa kama unatoa tamko la JF, hope not!!? Msome vizuri Mkadara na wengine....

Kamanda it seems u have missed the whole issue hapa! calm down get to normal

Respect Masa
 
[/SIZE]

Mhh hii kali kweli.

Mhh

Unapingana na Zitto anayesema kuwa amejitoa kwenye kugombea?

Huyu ni the same Zitto ambaye ulimwita kuwa Zitto wa Dowans baada ya kumuita tingatinga kuwa ni Bajaji?

Sidhani kama wewe ndiye unatakiwa uwaamulie hao CHADEMA cha kufanya.

Ukiita wanachoandika wenzako kuwa ni pumba, je hiki ulichoandika wewe ni nini?

Haya ni mawazo yako binafsi na sio tamko na JF au sio?

- Zitto hakujitoa angejitoa kusingekua na matusi na kejeli za kumdhihaki kutoka kwa viongozi wa Chadema, pumba ni kumlazimisha mgombea arudishe fomu kwa manufaa ya wachache ndani ya chama na kujaribu kuutetea huo ujinga kwa nguvu zote, that is pumba.

- Msimamo wetu hapa JF siku zote ni kurekebisha uozo kama huu wa Chadema, mlichokifanya ni uozo tena wa ajabu sana kwanza mmeharibu demokrasia halafu mmejiabisha kujaribu kumharibu Zitto maana na yeye amewaharibu.

- Demokrasia ya kweli na makini ni kwa Zitto kuruhusiwa kugombea huu haupaswi kuwa msimamo wa JF, isipokuwa ni political fact inayoweza kutambuliwa JF tu badala ya media ya bongo ambayo siku zote inakuwa imenunuliwa na wanasiasa, ya Zitto kuwa dowans au kutokua hayana uhusiano wowote na yeye kutaka kuwa Mwenyekiti wa Chadema, kama mlijua amenunuliwa na Dowans then kwa nini hamkumfukuza?

Zitto hakuondoa jina lake kwa hiari yake angekuwa asingekuja hapa kuwachafua na nyinyi Chadema msingekuja hapa kumchafua, wote sasa mmechafuka na demokrasia zenu za uchwara uchwara, sasa msituletee ngonjera hapa! Kumbe mkuki ni kwa nguruwe kujifanya mnajua kuchambua ya CCM, yakiwakuta tizama mnavyohangaika aibuu sana hii!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Msimamo wetu hapa JF siku zote ni kurekebisha uozo kama huu wa Chadema, mlichokifanya ni uozo tena wa ajabu sana kwanza mmeharibu demokrasia halafu mmejiabisha kujaribu kumharibu Zitto maana na yeye amewaharibu

Unanichanganya hapa itabidi niwasiliane na invisible atoe clarification !
 
Pamoja na maoni mengi toka kwa wana JF dunia nzima;lkn kwangu ukweli unabaki palepale;SIUTAMBUI WALA SITAKUJA KUUKUBALI UCHAGUZI WENYE HILA WA CHEDEMA WA TAREHE 4 SEPTEMBA UTAKAOMRITHISHA MADARAKA MWENYEKITI MBOWE NA WENZAKE!

Ni uchaguzi wa kiimla mbao haufai hata kufikirika kama umewahi kutokea kwa chama kama CHADEMA ambako viongozi wake wamekuwa wakijinadi kama wao ndiyo "baba wa demokrasia nchini tz"

Je hiyo ndiyo demokrasia kutumia wazee kumuomba mgombea halali kisha kumlazimisha kujitoa?SIWEZI KUTAMBUA WALA KUYAKUBALI WALA KUMTII KIONGOZI ALIYESHINDA KWA MATOKEO YA KUPIKWA!

Natetea katiba,sitetei nguvu za wazee ndani ya CHADEMA akina Mtei!

- Mkuu Malafyale, tupo pamoja sana hapo, heshima juu na salute!

Respect.

FMEs!
 
FMES

I am speechless, siamini kama ni wewe uliyeandika haya! huwa uko analytical mzuri, ila kwa hili ur impartial. Nadhani ungesoma hii thread tokea mwanzo ungekuja kivingine kabisa, hoja yako hapo haina mshiko hata kidogo!Ur sounds very authoritative vipi kaka hapa ni kujadiliana hoja, unakuwa kama unatoa tamko la JF, hope not!!? Msome vizuri Mkadara na wengine....

Kamanda it seems u have missed the whole issue hapa! calm down get to normal

Respect Masa

- Masa kweli unategemea nijibu this? yaani niache the subject na kuingia kwenye personal analysis, pole sana mkuu mimi ninasimamia demokrasia makini tu na sio ubinafsi na sio wote hapa JF tunaolipwa na Mbowe katika maisha yetu au ndugu zetu wanafanya kazi kwake,

- Naona ndugu yangu unaandika tu bila kuelewa motives za watu hapa, tulia kijana usiyoyajua uliza usaidiwe, wengi hapo juu wanatetea milo yao na ya ndugu zao wanaofanya kazi kwa Mbowe! acha kuingia kichwa kichwa mkuu wenzako wanatetea mlo!

- Naona ndugu yangu unaandika tu bila kuelewa motives za watu hapa, tulia kijana usiyoyajua uliza usaidiwe, wengi hapo juu wanatetea milo yao na ya ndugu zao wanaofanya kazi kwa Mbowe!

Respect.

FMEs!

Sorry mzee am out!

Ila hakuna personal hapa, unajua mzee sipati chochote kwa Mbowe

unaweza kuwa sahihi kuna motives nisiyo ijua. Nadhani siihitaji time will tell.

Regards

M
 
- Zitto hakujitoa angjitoa kusingekwua na matusi na kejeli za kumdhihaki kutoka kwa viongozi wa Chadema, pumba ni kumlazimisha mgombea arudishe fomu kwa manufaa ya wachache ndani ya chama na kujaribu kuuttetea huo ujinga kwa nguvu zote, that is pumba.

Zitto amejitoa kwenye kugombea. Hayo ni maneno yake mwenyewe na siyo ya kwangu. Hayo ya kejeli ni sehemu ya siasa nadhani hata wewe unaelewa hilo.

- Msimamo wetu hapa JF siku zote ni kurekebisha uozo kama huu wa Chadema, mlichokifanya ni uozo tena wa ajabu sana kwanza mmeharibu demokrasia halafu mmejiabisha kujaribu kumharibu Zitto maana na yeye amewaharibu.

Kama hujagundua bado, kinachoendelea hapa ni kurekebisha uozo kama huu wa Zitto. Au wewe unaonaje?

- Demokrasia ya kweli na makini ni kwa Zitto kuruhusiwa kugombea huu haupaswi kuwa msimamo wa JF, isipokuwa ni political fact inayoweza kutambuliwa JF tu badala ya media ya bongo ambayo siku zote inakuwa imenunuliwa na wanasiasa, ya Zitto kuwa dowans au kutokua hayana uhusiano wowote na yeye kutaka kuwa Mwenyekiti wa Chadema, kama mlijua amenunuliwa na Dowans then kwa nini hamkumfukuza?

Sidhani kama kuna yeyote aliyepingana nawe katika hili. Katika siku ambazo hukuwepo hapa, kulikuwa na thread iliyoanzishwa na invisible ambayo ilipinga sana kitendo cha CHADEMA kumzuia Zitto kugombea na wachangiaji karibu wote walikubaliana na Invisible katika hili.

Zitto hakuondoa jina lake kwa hiari yake angekuwa asingekuja hapa kuwachafua na nyinyi Chadema msingekuja hapa kumchafua, wote sasa mmechafuka na demokrasia zenu za uchwara uchwara, sasa msituletee ngonjera hapa! Kumbe mkuki ni kwa nguruwe kujifanya mnajua kuchambua ya CCM, yakiwakuta tizama mnavyohangaika aibuu sana hii!
Respect.

Field Marshall Es!

Zitto kaondoa jina lake mwenyewe. Kama una habari za ndani ya vikao vya chadema unaweza kuzileta hapa otherwise wewe ndiye unaleta ngonjera hapa.
 
Siwezi kuficha kuwa labda naye anatumiwa katika hili.. umefikia hatua ya kutoa tuhuma mpaka kwa wakina Mnyika??

Acheni kujiuliza maswali mepesi haya....ina maana mtu ana haki ya kufikiria kivyake ama kufanya makosa kivyake hadi atumiwe. Mradi ninyi mnajioda ni wepesi wa kutumiwa basi kila mtu atakuwa anatumiwa....

No wonder we keep blaming umasikini na ujinga wetu kwa wazungu.....

Also, Mnyika anaweza kuwa smart na ambaye Zitto alimuamini sana na hata hivi juzi alikuwa akifikiria jinsi gani ya kushirikiana naye hapo mbeleni. Lakini haimanishi kuwa hana makosa na ni malaika asiyeweza kufanya maovu anayotuhumiwa kuyafanya...unadhani kila anayeandika haa anatumia jina lake kama mimi, zitto na wengineo?

omarilyas
 
- Masa kweli unategemea nijibu this? yaani niache the subject na kuingia kwenye personal analysis, pole sana mkuu mimi ninasimamia demokrasia makini tu na sio ubinafsi na sio wote hapa JF tunaolipwa na Mbowe katika maisha yetu au ndugu zetu wanafanya kazi kwake,

- Naona ndugu yangu unaandika tu bila kuelewa motives za watu hapa, tulia kijana usiyoyajua uliza usaidiwe, wengi hapo juu wanatetea milo yao na ya ndugu zao wanaofanya kazi kwa Mbowe! acha kuingia kichwa kichwa mkuu wenzako wanatetea mlo!

Respect.

FMEs!

Mkuu nilidhani umeacha ngonjera lakini kumbe wapi ... au ndiyo yale yale ya kutetea mlo wako wa Rostam Azizi?
 
Acheni kujiuliza maswali mepesi haya....ina maana mtu ana haki ya kufikiria kivyake ama kufanya makosa kivyake hadi atumiwe. Mradi ninyi mnajioda ni wepesi wa kutumiwa basi kila mtu atakuwa anatumiwa....

No wonder we keep blaming umasikini na ujinga wetu kwa wazungu.....

Also, Mnyika anaweza kuwa smart na ambaye Zitto alimuamini sana na hata hivi juzi alikuwa akifikiria jinsi gani ya kushirikiana naye hapo mbeleni. Lakini haimanishi kuwa hana makosa na ni malaika asiyeweza kufanya maovu anayotuhumiwa kuyafanya...unadhani kila anayeandika haa anatumia jina lake kama mimi, zitto na wengineo?

omarilyas

Omar ndugu yangu,

Mnazidi kulikoroga hapa na kulitia sukari. Kama Zitto anaona chadema iko vibaya hivi, anaweza:

1. Kuanzisha Chama
2. Kujiunga na CCM
3. Kujiunga na CUF au vyama vingine
4. Au kwenda kusoma kama alivyokwisha sema.

Haya mengine ya frame throwing sioni kama yanajenga nafasi yake ndani ya CHADEMA.
 
[/SIZE]

Zitto amejitoa kwenye kugombea. Hayo ni maneno yake mwenyewe na siyo ya kwangu. Hayo ya kejeli ni sehemu ya siasa nadhani hata wewe unaelewa hilo.

Kama hujagundua bado, kinachoendelea hapa ni kurekebisha uozo kama huu wa Zitto. Au wewe unaonaje?

Sidhani kama kuna yeyote aliyepingana nawe katika hili. Katika siku ambazo hukuwepo hapa, kulikuwa na thread iliyoanzishwa na invisible ambayo ilipinga sana kitendo cha CHADEMA kumzuia Zitto kugombea na wachangiaji karibu wote walikubaliana na Invisible katika hili.

Zitto kaondoa jina lake mwenyewe. Kama una habari za ndani ya vikao vya chadema unaweza kuzileta hapa otherwise wewe ndiye unaleta ngonjera hapa.

- Yaani inazidi kuchekesha, Zitto kaondoa jina lake mwenyewe lakini yupo hapa akilia lia na viongozi wa Chadema wapo hapa wakilia inachekesha sana, huku wote wanajua kuwa Zitto aliondoa jina kwa hiari yake mwenyewe!

- Demokrasia haijawahi kusema kwamba kumrekebisha kiongozi dawa ni kumnyima uongozi bila ya kura za wananchi, sasa Chadema mnamnyima Zitto fomu kule CCM Nchimbi anamnyima Nape fomu, halafu mnasema nini sasa hapa hivi huoni hiyo balance kwamba hakuna tofauti!

- Kwa hiyo kwa sababu alisema Invisible mimi sitakiwi kusema? Aaahgggrrr inachekesha sana, mmelikoroga sasa mlinywe tu, walikubaliana na Invisible kwa hiyo wengine tusiseme tena, hapana ninasema hivi Chadema wameharibu sana na hawana tofauti kabisa na CCM, dawa ni kufuta vyama vyote vya siasa Tanzania, na kupiga marufuku viongozi wote wa sasa kugombea tena, kwa sababu wote hawafai!

- Habari za vikao vya Chadema za nini na zote zipo hapa kwenye hii thread tena mpaka za Wangwe zipo, saafi sana unafiki siku zote una mwisho wake na sasa umefika aibu iliyoje siku inapofika kama hii, siku moja miaka ya 90s, niliwahi kuhudhuria mkutano wa Mtei, pale Sheridan Street New York nyumbani kwa Mkuu wa NICCO Mzee Felix Mosha, I mean Mtei alinipatia muongozo mmoja mrefu wa Chadema ninao mpaka leo ambao unapingana kabisa na haya yaliyofanyika, tena kwa mbali sana sasa eti mnaweza ku-spin hapa mkajisafisha na hii aibuu?

Eti Chadema mko better kuliko CCM after this aibuuu?

Respect.

Field Marshall Es!
 
Acheni kujiuliza maswali mepesi haya....ina maana mtu ana haki ya kufikiria kivyake ama kufanya makosa kivyake hadi atumiwe. Mradi ninyi mnajioda ni wepesi wa kutumiwa basi kila mtu atakuwa anatumiwa....

No wonder we keep blaming umasikini na ujinga wetu kwa wazungu.....

Also, Mnyika anaweza kuwa smart na ambaye Zitto alimuamini sana na hata hivi juzi alikuwa akifikiria jinsi gani ya kushirikiana naye hapo mbeleni. Lakini haimanishi kuwa hana makosa na ni malaika asiyeweza kufanya maovu anayotuhumiwa kuyafanya...unadhani kila anayeandika haa anatumia jina lake kama mimi, zitto na wengineo?

omarilyas

- Mkuu Omar, saafi sana na salute tupo pamoja sana hapo!

Respect.

FMEs!
 
Wanajamvi,
Hatimaye nimebaini kuwa hapa jamvini watu wengi wanajiofanya wapinga ufisadi sio wa wakweli na kauli aliyoitoa Kadinali Pengo kuhusu wapinga ufisadi ni ya kweli. Kwamba watu wengi wanajidai kupinga ufisadi kwa maslahi yao.

Yaani kama mtu X anatuhumiwa kwa ufisadi lakini kwa vile mimi Y ni jamaa yangu au nina maslahi naye, basi nimtatetea X hata ikibidi kwa kuhalalisha huo ufisadi anaotuhumiwa nao. Mifano hai nilimeiona mingi tu kama juu ya utata wa urai wa Mhe. Mukasa, watu kuumunga mkono Mwakalinga (Kyela) ambaye ukweli kuwa anatumiwa na baadhi ya watuhumiwa ufisadi liko wazi kabisa. Pia nimeliona katika suala la Mhe. Zitto ambapo watu kadhaa wamekuwa wakimtetetea wakati ukweli upo peupe kabisa kuwa kitendo chake cha kugombea na kuamua kujitoa vyote vilikuwa well calculated chini ya usimamizi wa hao hao wenye kuhusishwa na ufisadi au wale wenye kukitakia mabaya CHADEMA.

Jambo moja ambalo wengi wameshindwa kulibaini ni kuwa hapa hesabu zote mbili zilipigwa mapema kabisa kuwa Zitto akichukua fomu na kwa vile umaarufu wake ni mkubwa na kwa vile wanachama na watu wengi (wakiwemo hata hapa JF) wanamuamnini sana hawatashtukia hii move kuwa anatumika.

Wapangaji wa mchezo huo wanajua kuwa kuwa kutokana na ufahamu mdogo wa wanachama au ushabiki uliopitiliza, jina la Zitto lingefika kwa wanachama (walalahoi) lazima angeshinda tu maana jina lake liko juu sana na wanachanma wengi hawamjui vizuri kiundani. Siwalaumu hao wanachama wa kawaida kwa kukosa ufahamu huo, endapo watu wasomi hata wenye shahada za uzamili na uzamivu hawajaweza kumjua vizuri Mhe Zitto vipi mwanachama anayetoka Ntambaswala au Mangaka au Ifwenkenya?

Bahati nzuri kwa CHADEMA ni kuwa viongozi wengine na wazee wa chama walishamfahamu hyu kijana kuwa anatumikia mabwana wawili wakaona hakuna njia isipokuwa kumfanya achomoe jina lake. Uamuzi wa kuamua kumshinikiza bila shaka ulikuwa mgumu lakini waliona njia hii ina maumivu kidogo kwa chama kuliko kumuachia kijana agombee

Zitto alijua kuwa akishindwa au jina lake likichomolewa kama ilivyotokea basi ataanzisha mizengwe yake ya kukichafua chama ili kikose sifa mbele ya watanzania, na ndilo analolifanya sasa. Kwa hiyo yote anayoongea sio jazba wala hasira ni jambo liliokuwa limeandaliwa vizuri sana.

Kimsingi Zitto anaelewa hata mwisho wake wa hili saga, kuna njia mbili moja atajitoa CHDEMA na kusema anapumzika siasa za vyama, na njia ya pili ambayo nasikia imeshika kasi ni kuondoka nchini kwenda kusoma kwani hata chuo naambiwa kipo tayari.

Inaaminika akirejea toka masomoni hatarudi CHADEMA. Jambo moja aliliosahau ni kuwa watanzania sio mabwege tena, watazipima kauli zake za kuanzia miezi 18 iliyopita na kulinganisha na tukio lilitokea sasa na kauli anazoendelea kuzitoa watambaini kuwa kuna mushkeli katika msimamo wake kisiasa.

Nadhani sasa hata wale waliokuwa wanamshabikia tangu wiki iliyopita, kwameanza kurudi nyuma kutoka na kauli alizozitoa siku mbili hizi. Katika thread hii au nyingine nilitoa mtihani huu kwa Zitto ambao ndio swali alilokuja kuulizwa kwenye kikao cha wazee na kushindwa kutoa jibu.

Anachofanya sasa ni kuwachokonoa CHADEMA na kutoa siri za chama chake ili hatimaye chama kishindwe kumvumilia na hatimaye kimuchukulie hatua kisha aanza kusema mnaoona..........ya Chacha Wangwe yamejirudia

Ushauri kwa Zitto:katika maisha sote huwa tunakosea kwa mawazo yetu au kwa influence ya watu wengine, Zitto toa kauli ya mwisho unusuru mageuzi nchini ili wananchi tuendelee kuwa na imani na upinzani. CHADEMA pia jaribuni kuwa na pamoja na Zitto anapitia kipindi kigumu, matamko anayotoa vumilieni tu, magazeti nayo kazi yake wakati fulani ni kuharibu zaidi kuliko kujenga au kuhabarisha.

Nawasilisha

Ntambaswala!
Unajua sisi Watanzania (au niseme Waafrika?) kitu kinachoturudisha nyuma ni kuwa wavivu wa kudadisi? Tukio likitokea hatutaki kujishughulisha hata sekunde mbili kuchunguza kiini hasa ni nini bali tunafwata mkumbo. Hivi kweli inaingia akilini mtu kama Zito afikikie hatua ya kuiambia kadamnasi eti yeye alishiriki kumwangamiza marehemu Wagwe kisiasa na ikabidi aiombe maiti
yake radhi kabla hajazikwa? Anachofanya Zito ni mkakati maalumu alioandaa na Kikwete ili amnusuru kwenye uchaguzi wa 2010 (baada ya kuona maji yako shingoni). Chaguzi zooote ndogo zilizofanyika CHADEMA imewakaba koo mafisadi wa CCM na sasa wanatumia gharama yoyote kuiangamiza... wanataka iwe kama NCCR. UKWELI NI KUWA ZITO YUKO CHADEMA KIMWILI LAKINI KIROHO ALISHATOKA SIKU NYINGI SANA KWA KUNUNULIWA NA SERIKALI YA KIKWETE. AMEAHIDIWA VITU VINGI TU IWAPO ATAWEZA KUISAMBARATISHA CHADEMA KABLA YA UCHAGUZI WA 2010.
 
RAIA MWEMA ya leo:

NILIIPOKEA vizuri taarifa ya uamuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe (Mb) kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika leo Jumtano.

Nilimwuunga mkono Zitto kwa moyo wangu wote, kumpongeza, na kumwombea dua apambane vyema na Mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe katika kinyang'anyilo hicho. Najua si mimi peke yangu, bali na Watanzania wengine kadhaa walifurahia uamuzi huo adimu wa Zitto; ingawa wapo pia waliouona kama usio sawa sawa.

Binafsi nilimuunga mkono Zitto kwa sababu kuu nne. Kwanza, nilijua kwamba uamuzi wake ungeleta msisimko mkubwa katika siasa za Tanzania kwa mwaka huu, msisimko wenye mwelekeo tofauti na msisimko wa muda mrefu katika siasa za Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili sasa.

Kwa miaka kama miwili sasa, siasa za Tanzania zimekuwa na msisimko mmoja tu – Ufisadi, na ndani ya huo, makundi ndani ya CCM na kusumbuka kwa Serikali ya Rais Kikwete kupambana nao.
Kwa maoni yangu, sio jambo jema sana kwa siasa za nchi kuegemea agenda moja tu kwa muda mrefu sana. Upepo wa kisiasa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, lakini lazima uvume kwa muda na kisha kupisha mawimbi mapya!

Madhara ya agenda moja kuvuma kwa muda mrefu sana bila kupitwa na wakati, ni pamoja na kujenga usugu kwa yule anayeelemewa na agenda hiyo, kuwafanya wengine wajisahau katika mapungufu waliyonayo kwa kuwa hayaguswi kwa muda mrefu; maana taifa lote linakuwa linang'ang'ana tu na udhaifu wa aina nyingine isiyowagusa wao kwa wakati huo, na kisha kujenga viwango vikubwa vya visasi miongoni mwa jamii.

Siamini kwamba CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ni vitakatifu. Nina uhakika vinayo mapungufu na mengine tunayajua. CCM ina mapungufu mengi, tena yanaonekana kwa uwazi zaidi kwa sababu ya ukubwa wa chama, na ‘u-kioo' wa chama kwa vile ndicho kina serikali.

Yanapotokea mashambulizi ya kukisakama CCM, kwa maoni yangu, inakisaidia kujirekebisha (iwe kwa kupenda au kwa kulazimika), na kujiweka katika nafasi bora zaidi kisiasa. Siyachukii hata kidogo mashambulizi ya kisiasa.

Lakini kusukwasukwa kisiasa kunakoikabili CCM ni muhimu kuvikabili pia na vyama vingine vya kisiasa vya upinzani; hata kama ni kwa kiwango pungufu.

Nasema hivi kwa sababu chama kinachojitahidi kama CHADEMA, ni chama ambacho kinaweza wakati wowote kuwa mbadala wa CCM na kukamata dola.

Ni kwa maana hiyo hatuwezi kujivunia kukiacha chama hiki ambacho wakati wowote kinaweza kuiongoza nchi yetu bila kupata changamoto za kukumbushwa mapungufu yake, kusukwa sukwa japo kidogo ili kijiweke bora zaidi kisiasa.

Maana; ieleweke wazi kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Chama kikiwa na mapungufu kikiwa kwenye kambi ya upinzani kikabembelezwa mapungufu yake yasiguswe, kikishashika dola itakuwa vigumu zaidi kukibana kwa mapungufu yale.

Kwa mfano, pale ambapo chama kinatuhumiwa kwa ukabila au ukanda kikiwa bado kiko kambi ya upinzani, yafaa kibanwe sana na kikikaidi umma ukiadhibu kwa udhaifu huo kabla hakijatwa dola ili kikitwaa dola kiwe kinajua wazi kwamba kinaweza kupoteza dola ikiwa kitaendekeza ukabila.

Yatupasa kukumbuka kwamba Watanzania hatujawahi kushuhudia chama tawala kikinyang'anywa dola kwenye uchaguzi. Hivyo hatujajua umuhimu wa kukiandaa chama pinzani kuwa chama tawala makini kwa mahitaji ya wananchi, na siyo tu kwa ilani na sera zilizoandikwa kwenye makaratasi na chama chenyewe.

Sasa kwa kuwa udhaifu wa chama huweza kukabiliwa vizuri zaidi kutoka ndani kuliko nje, ilikuwa muhimu sana kwa CHADEMA kupita kwenye uchaguzi wenye ushindani mkubwa wa mitazamo ili wao wenyewe wakosoane sera na mielekeo yao.

Wote tumeshuhudia kwamba wakati wabunge wa upinzani wakiongozwa na DK. Slaa na Mh. Zitto wakiishambulia Serikali ya CCM kwa ufisadi, chama hiki tawala hakikuweweseka kwa kiwango kikubwa kama kilivyokuja kuweweseka juzi baada ya wabunge wa CCM wenyewe wakiongozwa na kina Mh. Anne Kilango, Spika Sitta, Dk. Mwakyembe, nk.
Ni kwa sababu vita ya kutoka ndani huwa makini na yenye mashiko zaidi kuliko ya kutoka nje!

Sababu ya pili ya kumuunga mkono Zitto Kabwe ilikuwa imani yangu kwamba Zitto ni mpinzani bora zaidi nchini kwa sababu rekodi zake zinamweka kama mtu pekee ndani ya kambi ya upinzani ambaye siasa zake za upinzani hazina agenda ya siri zaidi ya ile moja ya kuitafutia Tanzania serikali mbadala wa serikali ya chama kilicho madarakani.

Maana tumekuwa tukiwashuhudia wapinzani ambao ishara zinaonyesha, tetesi zinaaminisha, na hata uchunguzi unasisitiza kwamba kuibadili CCM madarakani ni agenda ya juu tu, lakini agenda kamili ndani ni ama utajiri, biashara, utukufu, au kitu kingine kifananacho na hivyo.

Sababu ya tatu ya kumuunga mkono Zitto ilikuwa tamaa yangu ya kuishuhudia CHADEMA ikitekeleza kwa vitendo kile ambacho imekuwa ikikikemea sana dhidi ya CCM; nacho ni kwamba CCM imekuwa na utamaduni wa kuvumiliana na kusulubiana kwenye kinyang'anyilo cha ugombea urais ili aliye madarakani kwa miaka mitano ya kwanza aachiwe kumalizia kipindi cha pili; na kwamba rais wa nchi atokanaye na CCM asipingwe inapofika wakati wa kugombea uenyekiti wa chama.

CHADEMA wamekuwa wakiuponda sana utaratibu huu kwamba ni wa kizamani, unaokandamiza demokrasia, na unaoinyima CCM na nchi nafasi ya kupata viongozi bora.

Hili nalikumbuka zaidi miezi kadhaa iliyopita, viongozi kadhaa wastaafu wa CCM wakiongozwa na Mzee Pancras Ndejembi walipowashauri wana CCM wasijitokeze kuchukua fomu kumkabili Rais Kikwete mwaka 2010. CHADEMA waliwapinga na kuwazomea sana wazee hawa.

Makada wawili maarufu wa CHADEMA wanaotekeleza ukada wao kwa njia ya uandishi, kaka zangu Absaloom Kibanda na Ansbert Ngurumo waliandika makala nzito gazetini kuwashambulia wazee wale na CCM yao; huku wakijitahidi kuuonyesha umma ‘uhafidhina' wa CCM.

Ndiyo maana niliposikia Zitto kachukua fomu kupambana na Mwenyekiti wake Mbowe, nikajua sasa CHADEMA wamepata nafasi ya kutuonesha kwa vitendo kile walichokuwa wanakikemea kwa maandishi na matamshi.
Nilisubiri kwa hamu kuwasoma tena kina Kibanda na Ngurumo, na wengine wakimtia moyo Zitto na kuwakemea wote ambao wangemwambia Zitto amekosea kumkabili mwenyekiti wake!

Sababu ya nne ilikuwa hamu yangu ya kuiona CHADEMA, kwa mara ya kwanza, ikipokezana kijiti cha uenyekiti kwa mtu ambaye hana uhusiano wa zaidi ya ule wa kisiasa na mwenyekiti aliyemtangulia. Mtu ambaye hana undugu wa kifamili, wala wa ukwe wala historia ya kufanya kazi pamoja Benki Kuu miaka ya nyuma, na mwenyekiti aliyemtangulia!

Faida ya jambo hili ni mwanya wa chachu ya mawazo yenye mtiririko tofauti na yenye uzoefu tofauti, na hata yenye makuzi tofauti na mtangulizi wake. Hii ni muhimu kwa ukuaji wa chama na upana wa vionjo vya kisiasa.

Tofauti na Mh. Hamad Rashid aliyenukuliwa akisema alitarajia Zitto asingefika mbali na nia yake, mimi niliamini sana Zitto angegangamala na kumkabili Mbowe kikweli kweli.

Lakini sivyo ilivyotokea; kwani dakika za mwisho Zitto alijitoa kugombea akisingizia ushauri kutoka kwa wazee wa CHADEMA!
Hiyo ni mara yangu ya kwanza kumuona Zitto akikosa msimamo na kuweweseka kimaamuzi. Niliamini Zitto asingesikiliza kelele za chura, angeendelea kuyanywa maji mpaka akate kiu yake.

Nilitambua uwezekano wa Zitto kushinda au kushindwa kwenye uchaguzi, lakini nilitamani ashindwe kwa idadi ya kura na siyo kwa ‘ushauri wa wazee'.

Nafsi yangu ilianza kupigwa bumbuwazi niliposoma makala ya kaka Kibanda akimtisha Zitto kwamba uamuzi wa kumkabili Mbowe ni anguko lake mwenyewe. Nikajua kaka Kibanda kapitiwa tu akasahau kwamba kwa kuandika hivyo anaikana tahariri yake mwenyewe aliyopata kuiandika dhidi ya kina mzee Ndejembi!

Nilishangaa zaidi kuona kaka Ngurumo naye anaipigilia zaidi msumalr ‘Demokrasia ya CHADEMA' kwa kumponda rafiki yake wa karibu Zitto, na kumuunga mkono Kibanda!

Ndipo kilipoibuka kitu ambacho majigambo ya siku zote ya CHADEMA yalinifanya nisitarajie kukiona kikiibukia CHADEMA. Kwamba demokrasia ya chama na mwanachama ikatelekezwa kwa njia ya ‘ushauri wa wazee'.
Wazee wale wale waliokianzisha chama na kukiwekea katiba inayompa mtu uhuru wa kugombea uongozi bila uhuru wake kuathiriwa na msukumo toka ndani au nje ya chama!

Hivi ikitokea leo Mwalimu Nyerere akafufuka akawakusanya wazee wenzake kina Kawawa alioasisi nao taifa hili; Wakawaweka kikao CHADEMA na kuwapa ‘ushauri wa wazee' kwamba kwa kuwa ni chama chenye umri mdogo sana kuliko CCM, basi, wasiwe na haraka kugombea dola (urais) wala ubunge, waiachie kwanza CCM nafasi na wao watapewa dola wakati wao ukifika; watakubali?

Watamwelewa Mwalimu akiwashauri kwamba wasiipinge CCM ili kuzuia mpasuko wa nchi? Maana ni kweli CHADEMA kuipinga CCM kunasababisha sasa hivi nchi iwe ya moto. Kama wazee hawa wanaona changamoto ambazo CHADEMA inaipa CCM ni muhimu, kwa nini waone ni makosa Zitto kumpa Mbowe changamoto?

Tutakosea tukipata mashaka kwamba huenda hapa wazee walikuwa wanalinda tu heshima ya ‘mkwe', na siyo maslahi ya chama?
Nilisononeka zaidi nilipomwona, kwa mara ya kwanza, Zitto akizungumza na waandishi wa habari huku akijiumauma. Sikuwahi kumwona akiwa katika unyonge huo. Ni pale alipokuwa anakiri kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti kwa kuheshimu ‘ushauri wa wazee' badala ya nguvu ya demokrasia.

Alijitetea kwamba amefanya hivyo baada ya wazee kumwabia kwamba kugombea kwake kunaweza kukisambaratisha chama.
Hiki ni kichekesho. Ina maana Zitto hana akili za kutosha wala upeo wa kuona jambo lipi linaweza kusambaratisha chama na lipi haliwezi kusambaratisha chama, mpaka aambiwe na wazee?

Ina maana Zitto hajimudu kichwani, hana uwezo wa kupima uzito wa mambo, ndiyo maana akaaamua jambo baya bila kujua, mpaka alipoambiwa na wazee ndipo akajua?

Sasa wa nini huyu kuwa mbunge na mwakilishi wa watu kwenye jimbo ambalo namo kuna wazee? Si awapishe wazee; maana yeye hana busara ila wao? Wa nini huyu siku nyingine kupigiwa kura kuongoza watu wenye uwezo wa kuona mema na mabaya wakati yeye hawezi kuona mema na mabaya mpaka aambiwe na wazee?

Ingemwachia Zitto heshima kutochukua kabisa fomu ya kugombea kuliko kuchukua fomu kwa jeuri ya demokrasia na kisha kujiondoa kwa jeuri ya ‘ushauri wa wazee'.

Amesahau kwamba yeye ni tofauti na mwana CHADEMA mwingine yeyote. Zitto ni alama ya CHADEMA na nguzo ya upinzani nchini. Uamuzi wowote wa kijasiri unaofanywa naye lazima unawagusa wengi nchini na kuvuta zaidi mshikamano wa mapambano ya kuiendeleza nchi.

Lakini uamuzi wowote wa kilegelege kama huu wa ‘ushauri wa wazee' unawaponda wengi mioyo na kuwakatisha tamaa. Uamuzi wa ‘ushauri wa wazee' aliochukua Zitto umetia doa rekodi ya demokrasia ya CHADEMA.

Maana; kama Zitto amekiri kwa kinywa chake mwenyewe kwamba wazee wamemwambia akigombea uenyekiti chama kitasambaratika, ina maana wanajua na yeye ameeleweshwa, kwamba demokrasia ikiheshimiwa ndani ya CHADEMA chama kitasambaratika.

Hii ndiyo kusema kwamba CHADEMA inasamabaratishwa na demokrasia na kuimarishwa na ‘ushauri wa wazee'.

Kwa kuwa Zitto ametamka kauli ya aibu kwamba amekataa ‘rushwa' ya wazee kwamba atoe jina lake kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti ili apewe ukatibu mkuu, ina maana amekiri kwamba kuna rushwa ndani ya CHADEMA, na kwamba huenda hata Mbowe ametetewa na wazee kwa sababu wana maslahi fulani binafsi na uongozi wake. Basi tusimsikie Zitto akipokea cheo chochote kingine ndani ya CHADEMA; maana kakiri mwenyewe kwamba amekataa cheo kama mbadala wa fomu yake ya kugombea. Akipewa akapokea tutajua ‘changa' tayari.

Vyovyote vile baada ya kuyumba katika suala lile la Dowans na ukigeugeu huu aliouonyesha katika uchaguzi huo wa CHADEMA, chati ya umaarufu wa Zitto haiwezi kubakia vilevile ilivyokuwa mwaka jana au juzi.

Nimalizie kwa kumuasa Mh. Zitto kutokosea tena na kufanya maamuzi legevu kiasi hicho. Huenda jamii isimhukumu sana kwa kosa la leo; maana ni la pili tu baada ya lile la kusisitiza TANESCO inunue mitambo chakavu ya kampuni inayotuhumiwa kwa ufisadi ulioitikisa sana nchi. Lakini akiendelea hivi na akafanya kosa la tatu, huo utakuwa ndiyo mwisho wake kisiasa!
 
- Yaani inazidi kuchekesha, Zitto kaondoa jina lake mwenyewe lakini yupo hapa akilia lia na viongozi wa Chadema wapo hapa wakilia inachekesha sana, huku wote wanajua kuwa Zitto aliondoa jina kwa hiari yake mwenyewe!

Hilo la kulia lia ni tatizo la Zitto mwenyewe ila yeye mwenyewe kasema kuwa ameondoa jina lake.

- Demokrasia haijawahi kusema kwamba kumrekebisha kiongozi dawa ni kumnyima uongozi bila ya kura za wananchi, sasa Chadema mnamnyima Zitto fomu kule CCM Nchimbi anamnyima Nape fomu, halafu mnasema nini sasa hapa hivi huoni hiyo balance kwamba hakuna tofauti!

Bado unarudia kile kilichosemwa hapa tayari. Yaani umeanza kucheza korasi ya wimbo wako mwenyewe.

- Kwa hiyo kwa sababu alisema Invisible mimi sitakiwi kusema? Aaahgggrrr inachekesha sana, mmelikoroga sasa mlinywe tu, walikubaliana na Invisible kwa hiyo wengine tusiseme tena, hapana ninasema hivi Chadema wameharibu sana na hawana tofauti kabisa na CCM, dawa ni kufuta vyama vyote vya siasa Tanzania, na kupiga marufuku viongozi wote wa sasa kugombea tena, kwa sababu wote hawafai!

Kwa sababu ulitaka kujidai kuwa wewe ndiye wa kwanza hapa kuliona kosa la Zitto kuombwa atoe jina lake. Wengi hapa walishaona hilo na walikubaliana na huu mtizamo kuwa ni makosa kumuomba Zitto atoe jina lake. Hata hivyo, mwisho wa siku ni kuwa, Zitto alitoa jina lake.

- Habari za vikao vya Chadema za nini na zote zipo hapa kwenye hii thread tena mpaka za Wangwe zipo, saafi sana unafiki siku zote una mwisho wake na sasa umefika aibu iliyoje siku inapofika kama hii, siku moja miaka ya 90s, niliwahi kuhudhuria mkutano wa Mtei, pale Sheridan Street New York nyumbani kwa Mkuu wa NICCO Mzee Felix Mosha, I mean Mtei alinipatia muongozo mmoja mrefu wa Chadema ninao mpaka leo ambao unapingana kabisa na haya yaliyofanyika, tena kwa mbali sana sasa eti mnaweza ku-spin hapa mkajisafisha na hii aibuu?

Eti Chadema mko better kuliko CCM after this aibuuu?

Respect.

Field Marshall Es!

Hayo yote bado ni mambo yako binafsi na sidhani kama inabidi yachukuliwe kama ultimate facts kwenye hili swala.
 
CCM yako ya kifisadi itakufa kabla ya Chadema. Umeanza kuiombea Chadema kufa karibu mwaka sasa.

Huko poraandi wangekuwa wanafundisha uchawi nadhani ungekuwa umewaua viongozi wote wa chadema.

chama chochote chenye kunuka damu ya watu sharti kife, ccm ndo hao hao model wa chadema hawa wote lazima wafe.

Lakini usingekuwa mgumu wa roho na wewe ungetubu maana damu ya wangwe yalilia toka undongoni.

Hujui siku wala saa pale mwanawaadamu atakaposhuka,Amini nakuambieni Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la pembeni.
 
Maana; kama Zitto amekiri kwa kinywa chake mwenyewe kwamba wazee wamemwambia akigombea uenyekiti chama kitasambaratika, ina maana wanajua na yeye ameeleweshwa, kwamba demokrasia ikiheshimiwa ndani ya CHADEMA chama kitasambaratika.

Hii ndiyo kusema kwamba CHADEMA inasamabaratishwa na demokrasia na kuimarishwa na ‘ushauri wa wazee’.

Kwa kuwa Zitto ametamka kauli ya aibu kwamba amekataa ‘rushwa’ ya wazee kwamba atoe jina lake kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti ili apewe ukatibu mkuu, ina maana amekiri kwamba kuna rushwa ndani ya CHADEMA, na kwamba huenda hata Mbowe ametetewa na wazee kwa sababu wana maslahi fulani binafsi na uongozi wake.

Back to the subject, naona sasa na wengine ndio wanajitokeza saafi sana, hapa Raia Mwema tupo pamoja sana!

Respect.

FMEs!

-
 
1. Sababu ya tatu ya kumuunga mkono Zitto ilikuwa tamaa yangu ya kuishuhudia CHADEMA ikitekeleza kwa vitendo kile ambacho imekuwa ikikikemea sana dhidi ya CCM;

2. nacho ni kwamba CCM imekuwa na utamaduni wa kuvumiliana na kusulubiana kwenye kinyang’anyilo cha ugombea urais ili aliye madarakani kwa miaka mitano ya kwanza aachiwe kumalizia kipindi cha pili; na kwamba rais wa nchi atokanaye na CCM asipingwe inapofika wakati wa kugombea uenyekiti wa chama.

3. CHADEMA wamekuwa wakiuponda sana utaratibu huu kwamba ni wa kizamani, unaokandamiza demokrasia, na unaoinyima CCM na nchi nafasi ya kupata viongozi bora.

- More hoja nzito, tunaendelea kuzichambua hawa Raia Mwema si unajua wanakubalika sana kwa hoja nzito, sasa ni vyema tukala hoja zao kwanza.

Respect.

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom