Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Leo mbona tutafaidi ma blogu ya chadema...

Sorry, kama unatafuta UCHADEMA basi usiende huko maana huko ni UTANZANIA na UAFRIKA tu...CHADEMA kama ilivyo CCM kwangu mimi ni viunganishi tu vya barabara ya UTANZANIANJEMA.

omarilyas
 
Ungekuwa unatoa hoja zako honestly naamini ungepitia makala niliyoandika katika hiyo blog hapo na ukajua kwa nini nasimama katika mstar huu hapa. Tatizo kwa kuwa mna utando wa kufikiri na muono wenu wa kisiasa unakuwashaped na CNN zenu tu basi mmekuwa wazembe kiasi cha kuja na conclusion zilizojichokea.

Alipochagua kuingia ndani ya tume ya madini kujua ukweli wa hali ilivyo katika sekta hiyo na kupata nafasi ya kuingiza maoni yake humo ambayo mengi yapo katika ripoti hiyo mkamuona kalaghaiwa na Kikwete.

Alipoamua kusimama kushindana na Mbowe mnakuja na kutumia na CCM na hao MAFISADI wenzenu ambao walichowazidi ni kuwa wao wana access zaidi yenu na hivyo kufaidika kuliko ninyi kama aliyosema PENGO.

Sasa amekuja hapa kuwaeleza kuwa mbinu zenu za kusambaza sumu na kumfrustrate kama mlivyozoea kuwafanyia wengine hapo awali haziwezi kuwasaidia zaidi ya kuwaumiza wenyewe mnakimbilia kuwa anatoa siri. Nani kasema mtanzania hapaswi kujua siri chafu kama hizo?

Aliposimama kupinga kutumika katika spining ya CCM inayoongozwa na Mwakyembe na wenziwe kuwadanganya watanzania kuwa there is a hope in CCM mkakimbilia kuwa amenunuliwa.

Cheap minds, cheap conclusions, cheap spinings

Kuhusu UMALAIKA kamwe sina imani za kuamini kuna kiumbe hapa duniani anaweza kuwa na umalaika na ndio maana mimi na yeye huwa tunatofautiana mengi sana na huwa namweleza bila ya kusita. Sasa mnataka muendelee kumwaga sumu zenu hapa halafu mnategemea ninyamaze. La hasha, hilo halitawezekana kama ambavyo mbinu zenu za kumchanganya ili awazilie chama ama mumfanye mliyoanza kuyazoea.

omarilyas

Siri zipi hizo alizozitoa Zitto?

Kama unasema kuwa ni siri za uozo, na Zitto anasema kwamba yeye alishiriki kuufanya kama huo aosema kama alipanga mkakati wa kummaliza Wangwe na kumzushia kuwa anatumiwa na Mafisadi. Kama kweli Zitto alipanga mambo hayo, kumbe basi ni mtu muovu sana!

Lakini mbona habari za Wangwe kutumiwa na CCM zilisemwa na gazeti la Mwananchi kabla ya CHADEMA? Kwa habari yao ya uchunguzi ndio wakaandika mpaka fax namba ya CCM

Vipi leo Zitto aseme maneno yote yalikuwa ni uongo mtupu?

serayamajimbo
 
Omar

Kama Kubenea, Kibanda, Ansbert Ngurumo na Jesse wanampinga Zitto katika haya anayoyafanya ni watu makini zaidi ambao nawaunga mkono kwa hoja zao kuliko Balile, Muhingo, Msacky na Charles Charles wanaomtetea.
Nakubaliana nawe kuwa Jesse Kwayu na Kibanda ni watu makini lakini kukubali kufuata maelekezo ya kummaliza RAFIKI yao kwa shinikizo la mabosi wao haliwezi kuachwa kwa sababu ya hulka ya umakini wao...Mbona mwenzao amerebel? Lakini pia historia yao si unaijua....

Balile, Muhingo, Charles Charles, Kubenea wala sishangazwi kwani hakuna la zaidi ya haya niliyoyategemea. Kwa Charles Charles, Muhingo na Balile wanaendeleza libeneke lao na Mbowe na hapa kwao Zitto ni chambo tu...wanaua ndege wawili kwa jiwe moja..

Ngurumo kwa kweli sipati jibu na kwa kuwa naepuka chep conclusions basi naacha kwa sasa kumake my judgement...

Zitto anasema Kibanda anafanya hivyo kwa kuwa ni Mkristu na mfanyakazi wa Mbowe, hebu muulize kwamba Kubenea muislamu na si mfanyakazi wa Mbowe kwanini anampinga?

Zitto anasema kwamba Jesse Kwayu anampinga kwa kuwa ni mchaga mmachame, lakini hailezi ni kwa vipi Mchaga Msacky anamuunga mkono na kupotosha habari za CHADEMA kwenye Mwananchi.

Lakini leo Zitto badala ya kujibu hoja za Nipashe anamtuhumu Jesse kwa kuwa ni mmachame!
Hapa alikosea....naamini alikuwa akihoji ni vipi magazeti yanayomshambulia yote yanamilikiwa na mtu anayetoka kabila ama mahala pamoja na bosi wake Mbowe ambaye wameshindana...

Lakini pia kama ilivyo propaganda ya kuwa CUF ni chama cha waislamu, CCM ni chama cha mafisadi ambapo vyama vyote hivi vimeshindwa kuwa na umakini unaotakiwa kuzishinda propaganda hizo kutoka kwa washindani wao ndvyo ilivyo kwa upande wa propaganda ya kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga. Kutumia magazeti yanayomilikiwa na Mbowe na Mengi ni kumshambulia na kusambaza sumu dhidi ya Zitto ambaye katika fikira za wengi (sio mimi) wanaona kuwa anashindana na CHAGA MAFIA ni tactical mistake ambayo pamoja na mengine inahalalisha propaganda chafu ya ukabila.

Inaelekea Zitto ana chembe za udini, ukabila na ubaguzi;
Kama wengine wanatumia ukabila kufanikisha mbinu zao chafu dhidi yako na wewe ukasema kuwa wanatumia ukabila unakuwa na chembe za ukabila basi hapo utatuhukumu wengi....Na pia inaelekea humjui vizuri Zitto
 
Kilichomtokea Zitto kwenye kamati ya madini ya Kikwete anakijua mwenyewe na nadhani ni wakati muafaka wa Kikwete kulipa fadhila kwa Zitto.

Tatizo kubwa linalosibu nchi yetu ni hivi vichwa vyenye muono wa SIASA ZA MATUMBO ambazo hazijui kitu zaidi ya siasa za kulalama, Kushutumu na kutengeneza majungu.

Ukiulizwa kama umesoma hata muhtsari wa ripoti hiyo unatkuta hakuna kitu halafu unakimbilia kutengeneza maconclusion yako bila hata kujua yaliyomo humo na hata kuchunguza ni upi mchango wa Zitto katika ripoti hiyo.

Watanzania wengi wanaomshutumu Zitto kukubali kushiriki katika tume za kitaifa kama ile ya Afrika Mashariki na ile ya Madini wamelemewa na taathira ya ushindani ni udui. Nothing constructive can come from ur simple minds.

Mnashindwa kumwajibisha JK na wenzake kuteeleza maoni ama ushauri wa tume hiyo mnakimbilia kumlaumu Zitto kwa kukubali kushiriki huko. Hivi bila ya Zitto kushiriki katika kamati hiyo CHADEMA mngeweza kujua kwa undani jinsi sekta ya madini hapa Tanzania ilivyo na kuweza kutengeneza misimamo inayoheshimika na kuenekana imenda shule katika sekta hiyo...yaani anachoona mwenzenu ni strength ninyi mnakimbilia kuona ni weakness....Mnaboaaaa

Cha ajabu wakati mnahoji na kutengeneza fikira potofu kuhusu kuteuliwa kwa Zitto katika kamati ya madini mkanyamaza kimya hata kuhoji uteuzi wa Arfi katika kamati ya APRM...Natumai unajua APRM stand for what!

omarilyas
 
Waungwana, hebu tujaribu kusoma haya ya huyu mwandishi bila kuegemea upande wowote. Sijaweka jina la mwandishi na ambao wanamfahamu wasimtaje ili mada yake ijadiliwe vema. Kwa kifupi ni kuwa, Mwandishi ana Digrii ya Siasa na Mahusiano ya Nchi Kimataifa (Political Science and International Relations from University of Dar Es Salaam).

WAMEBAKA NA KUDUMAZA KADEMOKRASIA KETU

August@2009

Wakati watanzania walio wengi wanaamka na kuonyesha utayari wa kuchukua jukumu la kuleta mabadiliko ya kweli ambayo yataliwezesha taifa letu kusonga mbele katika harakati za kujenga mfumo wa kidemokrasia nchini, ndugu zetu wa CHADEMA wameamua kubaka na kudumaza mfanikio madogo yaliyoweza kupatikana hadi hivi sasa.

Kwa kifupi tukio la kumshinikiza ama kumshawishi kama ambavyo wanapenda watu wajue, kiongozi wao mahiri Zitto Kabwe kuacha kushindana kidemokrasia na Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe katika kugombea nafasi ya mwenyekiti kinatafsirika kwa maneno machache sana. CHADEMA wamebaka na kudumaza harakati za demokrasia nchini.

Kama kuna chama ambacho watanzania hasa vijana walikuwa na matumaini makubwa ya kuwaondoa katika madhila ya ukiritimba wa miaka mingi ulioshiwa na tija wa CCM, basi chama hicho kilikuwa ni CHADEMA.

Natumia neno kilikuwa na matumaini kwa kuwa naamini kuwa kwa hali ilivyo sasa ni vigumu na kama sio kitu kisichowezekana kwa watanzania kuendelea na imani waliyoanza kuijenga kwa chama hicho kuwa kingeliweza kuwakomboa kutoka kwa maovu ya CCM ambayo yanaonekana kukosa dawa.

CHADEMA wamefanya yale ambayo hata mahasimu wao CCM hawakutegemea kuyaona. Wameweza kutupa baharini nafasi ya kipekee ya kuhakikisha ushindi wa kutosha kwa chama hicho katika chaguzi zinazokuja na kuamua kujichimbia kaburi la kisiasa. Yaani wameamua kujiunga na historia ya vyama ambavyo vilikuwa tishio kwa CCM, kuanzia enzi za NCCR Mageuzi hadi CUF ambavyo kwa sasa vimebaki historia tu kama vyama mbadala vya CCM.

Hapa nisingependa kuzungumzia ni nini CHADEMA ingeweza kufaidika ama kuathirika endapo wangelimchagua Zitto Kabwe kama mwenyekiti wao mpya. Ninachojaribu kuchambua ni faida gani CHADEMA kama chama na wapenda demokraisia nchini wangeliweza kupata na hasara gani ambazo uamuzi wa kumshawishi ama kumshinikiza Zitto kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Ukweli ni kuwa kitendo cha mwanachama mwenye ushawishi mkubwa kama alivyo Zitto Kabwe kuthubutu kusimama kushindana na Mwenyekiti aliyeko madarakani kilifungua nafasi kubwa sana kwa CHADEMA. Kitendo hicho kimeweza kuonyesha kwa vitendo kuwa chama chao ni kweli chama cha demokrasia na maendeleo na maneno hayo sio kauli mbiu tu.
Wapo watu wengi, vijana kwa wazee ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na CHADEMA.

Na kama ilivyo utamaduni wa watanzania, wengi wao bado walikuwa wanasubiri uhakikisho kuwa CHADEMA ni mbadala makini wa CCM ili wajiunge katika harakati za kuleta mabadiliko makubwa kisiasa. Wengi wao kuingia kwa Zitto katika kinyang’anyiro hicho ilikuwa ni ishara kuwa CHADEMA inaweza kuaminiwa kwa yale wanayoyasema kwani wanaonyesha kuyatenda.

Ukiangalia kwa undani utaghamua kuwa kule kuingia tu katika kinyang’anyiro hicho kwa Zitto Kabwe kulikuwa ni mtaji mkubwa kwa CHADEMA na zaidi kwa maendeleo ya demokrasia nchini.

Kitendo cha Zitto Kabwe ambaye amekuwa kama kioo cha mafanikio ya wanasiasa vijana wenye uthubutu wa kusimama kupambana na mfumo kandamizi uliokuwa ukiwatisha kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani kuthubutu kuingia katika kinyang’anyiro hicho kulikuwa ni mwaliko wa wazi kwa maelfu ya vijana kujiunga na CHADEMA.

Kama CHADEMA wangeweza kuendelea na kufanya uchaguzi wao na mwishoni mshindwa akamkumbatia mshindi basi ni wazi hilo lingejenga imani kubwa kwa chama hicho miongoni mwa wapenda mabadiliko makini ambao hadi sasa wanashindwa kuamini vyama vyetu vya kisiasa na wanasiasa kwa ujumla.

Kwa watanzania ambao tungependa kuona kunakuwa na mfumo ambao unawezesha nchi yetu kuwa na demokrasia ya kweli yenye kujenga umakini wa kisiasa katika kuchagua viongozi wetu na kufanya maamuzi makubwa na madogo ya kikatiba, kisheria, kisera, kifalsafa na kiutawala. Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na chama ambacho kitaweza kwanza kuondoa ukiritimba wa CCM katika vyombo vya maamuzi na baadae kutupa chaguo mbadala pale itakapowezekana kubadilisha chama tawala.

CHADEMA ilishaanza kujenga muono huo miongoni mwa watanzania walio wengi. Zitto Kabwe ni mmoja wa watu ndani ya CHADEMA ambao wameweza kujenga hisia miongoni mwa jamii kuwa kama wangendelea vizuri ni muonekano wa kidemokrasia na maendeleo, basi wangeweza kujenga imani miongoni watanzania hao. Yaani CHADEMA walikuwa ndio wanaelekea katika kufanikiwa kujenga imani kuwa lipo chaguo mbadala la CCM katika nchi yetu.

Ukweli ni kwamba baada ya kuyafanya waliyoyafanya, ni wazi kama ilivyo vigumu kwa viongozi wa CCM kuzungumzia vita dhidi ya ufasadi mbele ya watanzania, kwa CHADEMA itakuwa ni vigumu kwa viongozi wao kusimama kuongelea umuhimu wa demokrasia na kupiga vita ukandamizaji nchini na kuaminika ama hata kueleweka.

Ni wazi CHADEMA wamejifunga uhalali hata wa kuongelea UFISADI ambayo imekuwa ajenda yao muhimu katika miaka ya kariuni. Kwani hapa wameonyesha ufisadi wa hali ya juu dhidi ya misingi ya kidemkrasia ambayo ina nafasi kubwa katika kufikia maamuzi ya kisiasa miongoni wa wapenda mabadiliko katika nchi yetu.

Kitendo walichokifanya, tena kwa kumkandamiza Zitto Kabwe ambaye ni alama ya uthubutu na umakini miongoni mwa vijana ambao ndio mtaji mkuu katika chaguzi zinazokuja, CHADEMA wamewaondolea hata nafasi waliyokuwa nao baadhi ya vijana wao katika kushinda kwenye chaguzi zijazo.

Ni wazi kutokana na hali iliyotokea kuanzia sasa itakuwa vigumu sana kwa vijana wa CHADEMA ambao walikuwa nyota zinazotegemewa kubadili sura ya siasa katika uchaguzi ujao kuweza kuwashinda vijana wenzao wa CCM. Hii inatokana na ukweli kuwa hata wao o wamejijengea taswira ya ama kuunga mkono, kubariki ama kunyamazia nguvu za wazee ndani ya chama chao zikifisadisha misingi ya kidemorasia ambayo wao walipaswa vijana hao walipaswa kusimama kidete kuitetea na kuipigania. Ni wazi kuwa kuanzia sasa itakuwa vigumu kwa vijana wa CCM kusimama mbele ya vijana wenzao katika chaguzi zijazo na kuwashawishi kuwa wao ndio chaguo la mabadiliko ya kweli.

Zaidi, sababu ya kumshikiza Zitto kuacha kushindana na Mwenyekiti wao aliyekuwepo madarakani ili kuepusha mpasuko ndani ya chama ni sababu inayoleta maswali zaidi ya majibu.

Kwa chama ambacho kinasema kinapigania demokrasia na maendeleo nchi kuamini kuwa kuwaacha viongozi wawili kushinda katika uchaguzi ni tishio la umoja wa chama ni sawa na kukubaliana na fikiria mgando zilizomo miongoni mwa wahafidhina ndani ya CCM kuwa kuruhusu ushindani wa haki na huru kati ya vyama vya siasa nchini ni kuhatarisha amani na maelewano ya nchi yetu.

Pia, kusema kuwa Mbowe akipata mshindani mkali kutaleta mtafaruku ndani ya chama kunatoa sura ya ama wazee kumuogopa Mbowe ama kukiri kuwa CHADEMA hawawezi kufanya siasa za kiungwana na zisizo na chuki ambazo zingeleta mgawanyiko. Ni wazi fikira kama hizo sio tu zitazuia wengi wengine kujiunga na chama hicho lakini pia si ajabu tukasikia kuendelea kwa mlolongo wa wanachama na viongozi wa chama hicho kuondoka na kwenda kujiunga na jinamizi walilolizoea yaani CCM.

Ndio maana baada ya kuona hili nimekuwa nikijiuliza sana ukweli wa sababu za viongozi na wanachama kadhaa wa CHADEMA ama kuhama, kusimamishwa ama kufukuzwa uanachama katika miaka ya karibuni. Nimekuwa nikijiuliza kama ni kweli hawa walikuwa vidudu mtu vinavyohatarisha ustawi wa chama ama kuna tatizo la kiuongozi ndani ya chama hiki. Kutokana na maamuzi yaliyofanyika hivi karibuni nachelea kuamini kuwa wapo walio ondoka CHADEMA baada ya kushindwa kuvumilia kuvunjika moyo katika nia yao ya kujenga mabadiliko ya ndani ili kuweza kushawishi mabadiliko ya nje.

Na katika hili, ni wazi muathirika si Zitto, si Mbowe na wala sio CHADEMA tu bali ni mustakali mzima wa mapambano ya kujenga demokrasia nchini.

Kitendo cha kuonyesha taswira ya kuwa kuna uwezekano wa kiongozi wa CHADEMA kuwa tayari kutumia mbinu zozote zile, halali na haramu, makini na hovyohovyo, salama na hatari ili kulinda nafasi yake kileleni, kinaonyesha kuwa ile ndoto ya vyama vya upinzani kuungana ili kukishinda chama dola cha CCM zinaendelea kubaki hivyo, yaani ni ndoto tu.

Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa kitendo hiki kinahalalisha propaganda ya CCM na dola kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wamegubikwa na ubinafsi na hawana nia ya kuwakomboa watanzania kama wasemavyo.

Na hapa napenda kuwashauri wana CHADEMA kuacha kutumia ujanja wa CCM kama sababu ya yaliyotokea na yanayoendelea kuwakumba. Kufanya hivyo ni sawa na kuwaunga mkono watwala wetu wa sasa ambao daima hawachoki kuwalaumu wazungu ama wakoloni kwa umasikini na madhila waliyowezesha katika nchi yetu kutokana na makosa yao wenyewe. Ilichofanya CHADEMA ni kujianika mbele ya mashamulizi ya CCM na maadui wengi. Na itakuwa ajabu sana kama madui hao wataacha nafasi hii kuwashambulia na hata kuwamaliza kabisa wakati huu nyeti wa kuelekea katika chaguzi za kitaifa.

Zaidi, kitendo walichokifanya CHADEMA kinawapa nafasi na nguvu zaidi maadui wa demokrasia kuendelea kudhihaki harakati za demokrasia nchini. Wapo ambao wamekuwa wakipita mitaani kusema kuwa wanaopiga kelele kutaka demokrasia hawana nia ya kweli ya kuleta demokrasia ya kweli bali ni mbinu tu ya kuweza kujipatia madaraka na baadae kufanya yaleyale ambayo wanayalalamikia wakati wasipokuwa madarakani.

Hatua ya kumshikinikiza Zitto Kabwe kutotumia haki yake ya kidemokrasia ya kuomba ridhaa ya kuongoza chama chake kwa wanachama wenzake kinahalalisha mitazamo ya maadui wa demokrsia kama hao.

Ni wazi, uamuzi wa wazee wa CHADEMA kumshinikiza Zitto Kabwe kujitoa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chake kwa kuhofia uwepo wa siasa chafu zitakazoweza kugawanya chama chao ulichofanikiwa ni kuhalalisha matumizi ya siasa chafu na hovyohovyo na hivyo kudumaza kabisa ndoto na juhudi za watanzania wanaopenda kuona mfumo wa demokrasia makini unatawala nchini mwetu.

Baada ya kufuatilia kwa karibu mwenendo wa siasa zetu wakati wa uchaguzi uliopita (2005) na baadae kupata taarifa za ufisadi mkubwa uliokuwa na na bado unaendelea katika nchi yetu mara baada utawala Mwalimu Nyerere, nilikuja katika hitimisho kuwa CCM na wadau wake wamelibaka taifa letu, na sasa nachelea kuhitimisha kuwa CHADEMA wamebaka kademkorasia ketu ambako katika miaka ya hivi karibuni tulianza kujenga imani na matarajio nako.
 
Last edited:
Wakuu zangu,
Mtasema yooote mabaya kuhusiana na Zitto lakini ukweli utabakia kwamba Zitto nimtu makini sana ktk Uongozi. Tatizo la Zitto ni uchungu mkubwa ambao humpa hasira akashindwa kujizuia..Ni kama maradhi ambayo huibuka tu pale anapoguswa sehemu za kipimo cha imani yake kwa wananchi.

Nimezungumza na watu wengi sana wanaomfahamu Zitto na wengi wanakiri kuwa hakuna mtu msafi ktk Bunge letu zaidi ya Zitto hata ndani ya chama chake mwenyewe. Hupokea posho na malipo mengine kwa kufahamu kuwa ni poshio au malipo halali ya huduma zake lakini kamwe Zitto hawezi chukua cha juu ili kushinikiza muswada au hoja Bungeni au nje.

Kwa hiyo wakuu zangu tumpeni sifa yake ndugu yetu Zitto na tumseme pale anapokosea kwani mwenzetu mdomo wake hauna break kama Mkandara anapoguswa hapa JF.. simwachii mtu ktk uwanja huu mdogo lakini hata siku moja siwezi kuropoka, kukurupuka ovyo inapofikia maswala mazito kama haya. Kibanda anamjua vizuri Zitto na alifanya makusudi kumtoa nyoka Pangoni huku akisubiriwa na panga..Maskini wa watu Zitto akatoka huko alikokuwa bila kuangaza hook waliyoiweka ajinyonge.

Mambo yote haya toka Zitto kujiandikisha hadi kujitoa na matusi mengine yote yamekuja ghafla kwa kasi kubwa kiasi kwamba inanipa wasiwasi sana na vikundi vinavyoibuka ndani ya Chadema.. Inawezekana kuwa wao ndio Mafisadi maanake kwetu Ukerewe wanasema ukimsikia mtu akisema sana kuhusu Wachawi basi jua yeye ndio mchawi nambari moja. Pia inawezekana kuwa hawa jamaa zangu kina Kibanda ni waoga wa maisha.. wakisikia hata Unyasi ulopepewa huruka maili nzima wakifikiri akuna Nyoka kumbe wasiwasi yao wenyewe.

Nina hakika Viongozi wa Chadema watayaweka mambo yote sawa..
Hiyo demokrasia inayoliliwa na wengi haiwezi patikana nchi yoyote duniani..Unataka kugombea Uenyekiti ni lazima uwe na sifa fulani na Zitto hana.. Zitto hawezi kugombea Urais nchini kwa sababu yuko chini ya umri unaotakiwa.. sasa msinambie eti hakuna Demokrasia kwa kuwepo na Umri ktk kinyanganyiro cha Urais.
Binafsi nitaendelea kuheshimu maamuzi ya chama chochote kile iwe CCM au Chadema inapofikia mgombea ktk kukiongoza chama kwa sababu kila chama kina mipango yake, sheria zake, taratibu zake na kadhalika..Jambo la mwisho nitakalo mshauri ndugu Zitto ni kwamba ktk siasa hutakiwi mashambulizi kama haya ya kina Mama Clinton..
Una jambo rohoni lifikishe ktk vyombo vinavyohusika na kama halikupatiwa ufumbuzi well utajua umesimama wapi kimya kimya mwanaume unatafuta uwanja mwingine!.. Tupo wengi tu tutakufuata ila jaribu kupunguza jazba maanake kama ingekuwa ushahidi mahakamani mkuu unalia jela sasa hivi kwa makosa ambayo hukuyafanya.
 
Last edited:
Zitto anadalili za U-Augustine Mrema.

Sidhani kama Augustine Mrema alikuwa na udini, ukabila na ubaguzi, tumweke pembeni huyo nadhani.

Zaidi ya hilo, nadhani Serayamajimbo umeongea ya maana sana sana, tena bila kutukana tukana wala jazba za mkizi kama CHADEMA insiders wengi wa humu. Incredible job there.

Zamani (si sana, labda up to 2005 election) tulizoe kuchagua viongozi ambao hatuwajui, background zao, hujui aliwahi kusema na kuandika nini, au ali handle vipi mitafaruku na wenzake katika taasisi alizopitia.

Lakini katika enzi hizi za Jamii Forums nadhani mtu kama Zitto ameshajitia kitanzi, asahau ndoto za kugombea kiti kama cha Urais. Ameshaongea mambo ya ajabu kuhusu Wachaga v/s Waha v/s Wafipa na rekodi zimebaki.

Naweza kumsamehe yote, ya jazba, kunyoosheana vidole na wenzake, na kila kitu, isipokuwa hili la udini na ukabila kwa kweli limenitisha mno.
 
Dilunga,
Mkuu wangu Zitto katupiwa Chambo na akakimeza bila kujua kuna ndoana ya Papa.. . Sii yeye aloanza kuzungumzia habari za Udiini na Makabila ila ukisoma maelezo mengi yaliyotangulia yamemweka yeye kuwa Ni mtu wa Kigoma na yule mgombea wa vijana pia ni mtu wa Kigoma, Mama yake ni sijui nani wa Kigoma..Hivyo ikabidi ajisafishe kwanza kumbe ndio walitaka aingie ktk uwanja huo..

Sasa ukikuta mtu mhuni kama mimi nitaweka yangu vile vile yanayolingana na uzito wa hoja kama hizi lakini kosa kubwa la Zitto kacheza bila viatu Uwanja wa taifa.. matokeo yake kapigwa njumu na ngwala kibao kiasi kwamba sasa hivi yuko nyumbani anachua maumivu yake..

Mimi naweza kuongopa chama Chadema kuwa cha Udini na Ukabila kuliko kumwogopa Zitto mtu mmoja kwani inahitaji kuwa na nguvu (Power) for one to practice ubaguzi huo..Na nachelea kusema inawezekana kuwa Zitto ni kikwazo cha baadhi ya watu wanaotaka kujenga Udini ndani ya chama Chadema hivyo anaanza kutafutiwa sumu yake. Hizi pia ni habari ambazo nimezipata kwamba Udini umeingia sana Chadema hasa kutokana na maswala ya waraka!..
Inatisha na nawaomba viongozi wa chama hiki kujichunga sana na tuhuma kama hizi kabla hazijafika mikoani..
 
Kweli kabisa ... sasa inasubiriwa tu ni wizara gani atapewa maana toka aimalize issue ya Buzwagi kiaina kwa kuingia kamati ya Kikwete, wakulu wa chama la kijani walikuwa wanamuandalia zawadi ya nguvu.

Mnajua mnachekesha sana. Hivi si Zitto huyuhuyu mliokuwa mkimshauri akubali ule mwaliko wa kuingia katika baraza la mawaziri mara baada ya serikali ya Lowassa kuvunjika? Ama mnataka kubisha kuwa hamkuwa mkimshauri akubali na yeye akang'amua janja ya nyani akachomoa.

Na kama Zitto anaendekeza siasa za matumbo kama ninyi ni vipi alikubali kuacha kujiunga nao wakati ule huku akiendelea na CHADEMA na ajiunge sasa kwa kuingia kujiunga na jahazi lilokuwa likizama kabla hamjawaokoa na haya makosa mliyoyafanya sasa....

omarilyas
 
Wakuu zangu,
Mtasema yooote mabaya kuhusiana na Zitto lakini ukweli utabakia kwamba Zitto nimtu makini sana ktk Uongozi. Tatizo la Zitto ni uchungu mkubwa ambao humpa hasira akashindwa kujizuia..Ni kama maradhi ambayo huibuka tu pale anapoguswa sehemu za kipimo cha imani yake kwa wananchi.

Nimezungumza na watu wengi sana wanaomfahamu Zitto na wengi wanakiri kuwa hakuna mtu msafi ktk Bunge letu zaidi ya Zitto hata ndani ya chama chake mwenyewe. Hupokea posho na malipo mengine kwa kufahamu kuwa ni poshio au malipo halali ya huduma zake lakini kamwe Zitto hawezi chukua cha juu ili kushinikiza muswada au hoja Bungeni au nje.

Kwa hiyo wakuu zangu tumpeni sifa yake ndugu yetu Zitto na tumseme pale anapokosea kwani mwenzetu mdomo wake hauna break kama Mkandara anapoguswa hapa JF.. simwachii mtu ktk uwanja huu mdogo lakini hata siku moja siwezi kuropoka, kukurupuka ovyo inapofikia maswala mazito kama haya. Kibanda anamjua vizuri Zitto na alifanya makusudi kumtoa nyoka Pangoni huku akisubiriwa na panga..Maskini wa watu Zitto akatoka huko alikokuwa bila kuangaza hook waliyoiweka ajinyonge.

Mambo yote haya toka Zitto kujiandikisha hadi kujitoa na matusi mengine yote yamekuja ghafla kwa kasi kubwa kiasi kwamba inanipa wasiwasi sana na vikundi vinavyoibuka ndani ya Chadema.. Inawezekana kuwa wao ndio Mafisadi maanake kwetu Ukerewe wanasema ukimsikia mtu akisema sana kuhusu Wachawi basi jua yeye ndio mchawi nambari moja. Pia inawezekana kuwa hawa jamaa zangu kina Kibanda ni waoga wa maisha.. wakisikia hata Unyasi ulopepewa huruka maili nzima wakifikiri akuna Nyoka kumbe wasiwasi yao wenyewe.

Nina hakika Viongozi wa Chadema watayaweka mambo yote sawa..
Hiyo demokrasia inayoliliwa na wengi haiwezi patikana nchi yoyote duniani..Unataka kugombea Uenyekiti ni lazima uwe na sifa fulani na Zitto hana.. Zitto hawezi kugombea Urais nchini kwa sababu yuko chini ya umri unaotakiwa.. sasa msinambie eti hakuna Demokrasia kwa kuwepo na Umri ktk kinyanganyiro cha Urais.
Binafsi nitaendelea kuheshimu maamuzi ya chama chochote kile iwe CCM au Chadema inapofikia mgombea ktk kukiongoza chama kwa sababu kila chama kina mipango yake, sheria zake, taratibu zake na kadhalika..Jambo la mwisho nitakalo mshauri ndugu Zitto ni kwamba ktk siasa hutakiwi mashambulizi kama haya ya kina Mama Clinton..
Una jambo rohoni lifikishe ktk vyombo vinavyohusika na kama halikupatiwa ufumbuzi well utajua umesimama wapi kimya kimya mwanaume unatafuta uwanja mwingine!.. Tupo wengi tu tutakufuata ila jaribu kupunguza jazba maanake kama ingekuwa ushahidi mahakamani mkuu unalia jela sasa hivi kwa makosa ambayo hukuyafanya.

.....agreed, ukiwa na uchungu sana na usipoweza kuji-control unaweza kufanya vitu visivyokubalika......the boy need counseling.......na ushauri hutolewa sana kwake kupitia hapa JF.........Bob hivi unaweza ukaamini yale maandiko aliyotundika Zitto hapo nyuma?,

Bob, mabaya mengi yanafanyika iwe kwenye vyama na hata serikalini, suala ni "TIME" gani ya ku-react na kuwa effective..........unaweza kufanya jambo zuri at the wrong time umati.....utakushangaa na kujikuta not effective..............Bob, as we always been saying since BCS we need to FIGHT A GOOD FIGHT.........

Kama kuna kosa ambalo sitamsamehe Zitto, ni lile la kujitoa kugombea uenyekiti........pili Chadema pia kama chama wamechemsha big time.............

.........nakuhakikishia hapo CCM wamepumua na kusema "check mate"
 
Dilunga,
Mkuu wangu Zitto katupiwa Chambo na akakimeza bila kujua kuna ndoana ya Papa.. . Sii yeye aloanza kuzungumzia habari za Udiini na Makabila ila ukisoma maelezo mengi yaliyotangulia yamemweka yeye kuwa Ni mtu wa Kigoma na yule mgombea wa vijana pia ni mtu wa Kigoma, Mama yake ni sijui nani wa Kigoma..Hivyo ikabidi ajisafishe kwanza kumbe ndio walitaka aingie ktk uwanja huo..

Sasa ukikuta mtu mhuni kama mimi nitaweka yangu vile vile yanayolingana na uzito wa hoja kama hizi lakini kosa kubwa la Zitto kacheza bila viatu Uwanja wa taifa.. matokeo yake kapigwa njumu na ngwala kibao kiasi kwamba sasa hivi yuko nyumbani anachua maumivu yake..

Mimi naweza kuongopa chama Chadema kuwa cha Udini na Ukabila kuliko kumwogopa Zitto mtu mmoja kwani inahitaji kuwa na nguvu (Power) for one to practice ubaguzi huo..Na nachelea kusema inawezekana kuwa Zitto ni kikwazo cha baadhi ya watu wanaotaka kujenga Udini ndani ya chama Chadema hivyo anaanza kutafutiwa sumu yake. Hizi pia ni habari ambazo nimezipata kwamba Udini umeingia sana Chadema hasa kutokana na maswala ya waraka!..
Inatisha na nawaomba viongozi wa chama hiki kujichunga sana na tuhuma kama hizi kabla hazijafika mikoani..

Achaneni na hawa wazee wa busara.Wameshatia agano la kunywa damu za watu.
 
Dilunga,
... Sii yeye aloanza kuzungumzia habari za Udiini na Makabila ila ukisoma maelezo ...

Unajua Mkuu Mkandara, Zitto hatumpimi kwenye mizani ile ile tunayopimiwa kina Dilunga na wewe na sijui Sikonge, Mwafrika etc. Why, because who the hell is Dilunga? Who the heck is Chuma or SerayaMajimbo sijui MpakaKieleweke? Vivuli vya watu tu! Au some sleazy editors ambao have nothing to lose na zogo la CHADEMA. Kina Kilanda ni wahariri wanaotaka kuuza magazeti tu. Zitto ni kiongozi mwandamizi wa upinzani, na mheshimiwa mbunge. Hawezi kutupiwa jiwe na sijui Eric Ongara, Kilanda, halafu akarudishia vijembe vya kikabila tukasema hakuanza yeye. Zitto ndio mkubwa kisiasa. Hata mama mtu akikuta watoto wanagombana anaweza kumuwashia moto mkubwa mdogo asiguswe japo ndio aliyeanzisha ukorofi, why, because mkubwa should know better, mkubwa has heavier responsibilities. Umeona Mbowe alivyotulia?

Zitto amelikoroga.

Zitto amezungukwa na kina nani hivi? Kina Kikwete na Edwin Mtei? Ndio wanao mshauri njia? I mean, the man needs somebody to tell him Zitto mdogo wangu, siku nyingine ukija kwenye maskini za kisiasa don't drug your mother with you! Just don't let your mother speak for you, they gonna drug you and your mother into the mix! Umeona headlines za leo? "MAMA ZITTO AFYATUKA"! Sio Bi. Shida Salum, Mwenyekiti wa Walemavu, no, "Mama Zitto amfyatukia Dr. Slaa!" mara sijui "First Lady".... nikadhani First Lady wa JF, kusoma nakuta Mama Zitto, I said damn, this thing done gotten cuckoo now!
 
. Hata mama mtu akikuta watoto wanagombana anaweza kumuwashia moto mkubwa mdogo asiguswe japo ndio aliyeanzisha ukorofi, why, because mkubwa should know better, mkubwa has heavier responsibilities. Umeona Mbowe alivyotulia?

Wewe nawe,
Wakati mwingine unapoint wee ila wakati mwingine unalazimisha kwa nguvu hamna kitu na mwisho hadi unatemea mate, pyuuuu. Na bado point zinagonga mwamba.

Umesema sawa kabisa kuwa Mkubwa inabidi achapwe viboko.

Haya nenda kamchape viboko Mzee Mtei (baba mkwe) kwa kubwabwaja ovyo.
 
Kuna mstari kwenye biblia unaosema something to this effect: "watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima".

Vikongwe vinne vya Chadema ndiyo vilivyokosa hekima na busara.Mtei huwezi kuingia kwenye kikao huku ukijua kuna mgongano wa kimaslahi.unampendelea Mkweo-Mbowe wazi wazi?
tumia busara na hekima.

hivi wewe kitila bado una hamu na hao vikongwe wa Chadema? umesoma makala ya KIBANDA jumatano hii kwenye Tanzania Daima? kaendelea kukuita mjinga.badala ya kuleta suluhu yeye anakadhania kuleta migongano.KIBANDA MVI ZIMEANZA KICHWANI LAKINI HUNA BUSARA NA HEKIMA.
 
[/B][/COLOR][/SIZE]

Nani kasema kuwa Masatu ni mtu wa Musoma? Musoma haina mafisadi kama Masatu, huyu atakuwa tu mtu wa kisiwani mafia.

Mmezijua mbinu hizo na nani? ha ha ha ... punguza muda huko madrasa za suicide bombings labda utapata cha maana cha kuandika

Unajua unapokutana na sentiments kama hizi miongoni mwa wanaCHADEMA wanaopambana na Zitto unaweza kuanza kujiuliza kama issue hapa ilikuwa ni kupingwa Mbowe tu ama kuna mengine yamejificha.

Halafu Zitto akimjibu mtu kama huyu mtamwita mdini, mbaguzi, mkabila....

Hivi hamuoni waathirika wa chuki za kidini na kikabila kama hawa?

omarilyas
 
Unajua Mkuu Mkandara, Zitto hatumpimi kwenye mizani ile ile tunayopimiwa kina Dilunga na wewe na sijui Sikonge, Mwafrika etc. Why, because who the hell is Dilunga? Who the heck is Chuma or SerayaMajimbo sijui MpakaKieleweke? Vivuli vya watu tu! Au some sleazy editors ambao have nothing to lose na zogo la CHADEMA. Kina Kilanda ni wahariri wanaotaka kuuza magazeti tu. Zitto ni kiongozi mwandamizi wa upinzani, na mheshimiwa mbunge. Hawezi kutupiwa jiwe na sijui Eric Ongara, Kilanda, halafu akarudishia vijembe vya kikabila tukasema hakuanza yeye. Zitto ndio mkubwa kisiasa. Hata mama mtu akikuta watoto wanagombana anaweza kumuwashia moto mkubwa mdogo asiguswe japo ndio aliyeanzisha ukorofi, why, because mkubwa should know better, mkubwa has heavier responsibilities. Umeona Mbowe alivyotulia?

Zitto amelikoroga.

Zitto amezungukwa na kina nani hivi? Kina Kikwete na Edwin Mtei? Ndio wanao mshauri njia? I mean, the man needs somebody to tell him Zitto mdogo wangu, siku nyingine ukija kwenye maskini za kisiasa don't drug your mother with you! Just don't let your mother speak for you, they gonna drug you and your mother into the mix! Umeona headlines za leo? "MAMA ZITTO AFYATUKA"! Sio Bi. Shida Salum, Mwenyekiti wa Walemavu, no, "Mama Zitto amfyatukia Dr. Slaa!" mara sijui "First Lady".... nikadhani First Lady wa JF, kusoma nakuta Mama Zitto, I said damn, this thing done gotten cuckoo now!
Mkuu nakubaliana na wewe 100% na ndio maana mimi nimekuwa mstari wa mbele kumlaumu Zitto. Najua makosa alofanya na pengine kinachomwangusha nikile kiburi cha mzee wetu Wassira(Tyson) isipokuwa yeye akitumia mdomo..
Hiki ndicho kitu kinachomponza Zitto but in all Huyu ni mtu wetu. Tumemweka kitimoto hapa ili tupate kumwongoza, kumwoyesha njia na kijiwe hiki cha JF kiwe sehemu yake ya kujifunza na sii kumtosa kwani bado kabisa tunamhitaji pamoja na kwamba kati yetu wapo wengi sana waliokata tamaa kwani 2010 ni karibu sana.
Yet naamini kabisa tunaweza kujirekebisha sote na Zitto akawa miongoni mwetu kwa sababu ukisoma hoja zote toka tumemshutumu Zitto amekuwa msomaji na bila shaka anayasoma mengi mazito..Lakini kwa mara ya kwanza amekuwa mtulivu, msikivu na mvumilivu.
Mkuu wangu mengi yamezungumzwa nje kabisa ya mada hizi na hasa kama ulivyozungumza inahitaji moyo mkubwa sana kujizuia kutoputa na kusema liwalo na liwe!
Imetosha wakuu zangu tujenge nchi hizi habari za Zitto zimechukua nafasi kubwa ya mazungumzo yetu kiasi kwamba tumesahau kabisa matatizo ya nchi yetu, tumesahau kabisa kwamba tunakabiriwa na matatizo wazito zaidi mbele ambayo yanahitaji nguvu yetu sote pamoja..
Warumi waliweza sana kutumia wafungwa kwenda pigana vita, watu hawa waliwa majambazi, wauaji, vibaka na kaddhalika kushinda vita kubwa zilziowakabiri. Mwisho wa yote waliwazawadia majambazi hao na kuwapoa mwanzo mpya.
Ku smell mkuu kasmell tena kishenzi..isipokuiwa makosa yakem yanasameheka. Udini hana isipokuwa ailijisahau na kufdikiri JF ni kijiwe cha kila mtu kiasi kwamba alivua Ubunge wake, Ukatibu wake na kuvaa joho la Kibembe. hapo ndipo alipovuka mstari na kuingia kama raia wengine..Ni makosa na naomba sana tumsamehe kama kiongozi bwana mdogo anayechipukia...
Tumetukanwa na Mkapa tena katika mkutano wa taifa na hatukuwa na jibu zaidi ya kushika matama yetu. He might be nothing but trouble, yet we can't live without him! katika vita hii tuliyokuwa nayo.
 
Last edited:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom