Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Hii notion ya kijinga ya kuamini kuwa Wahaya, wachaga, Wanyakyusa ni watu hatari wasiopaswa kuongoza siasa za nchi yetu itakwisha lini miongoni mwa wajinga na wachochezi uchwara wa ukabila nchini mweitu?

Mwakasege ni Mnyakyusa watu mahubiri yake wanayaamini, Saida Karoli ni Mhaya nyimbo zake wanazipenda na LUDOVICK UTOH ni Mchaga watu kazi yake wanaifanyia Rejea dhidi ya ubadhirifu uliojaa ndani ya serikali. lakini hawa wote wakithubutu kuingia kwenye Siasa wanaitwa ni watu hatari na wakabila.

Gazeti la Rai toleo la leo limenifanya nijiulize kama vurumai ndani ya CHADEMA ni suala la mapambano ya kupigania Demokrasia ua ni mchezo mchafu unaofanywa na wapinzani wa CHADEMA ili kukisambaritisha chama hicho kabla ya uchaguzi wa mwakani.

Hivi ni Sahihi kusema "Sitta asulubiwa na waislamu ndani ya Kamati Kuu na Halimashauri Kuu" kwa sababu tu wajumbe wengi ndani ya Vikao hivyo ni waislamu na yeye ni mkristo?

Kosa la Mbowe ni kuzaliwa Mchaga Kabila moja na mwanzilishi wa CHADEMA Edwin Mtei? mbona Warioba,Musuguri,Butiku na wengineo walikuwamo ndani ya serikali iliyoongozwa na Ndugu yao Julius Nyerere. Jee na Mwalimu naye alikuwa Mkabila?

Unapatikana wapi mkuu nikupe kumi bora!!! Tufahamu kuwa Tanzania ina makabila zaidi ya 120!!! Na mimi mpaka leo ninajichanganya na kila kabisa ndani ya ofisi, nyumba za ibada, tunashirikiana shughuli mbalimbali bila kujali. Ni automatic kuwa kwa mtu yeyote duniani undugu upo ila inapokuja suala la utendaji tunaangalia utendaji zaidi. Na hivyo basi hata Chadema mnosema ni chama cha wachagga kwanza waanzilishi ni wachagga na wakajiunga wengine wakiwemo wachagga na makabila mengine na chama kikawa na nguvu sana baada ya kufa kwa NCCR-Mageuzi. Leo hii kwa sababu 2010 is around the corner mnaanza kukibomoa??? Au ndiyo response kwa ile kampeni za Sangara??? Ohooo tuwe makini.

Nataka wana JF wenzangu ambao wana uchungu na nchi hii na wanataka ikomboleke, wajihadhari sana na vibaraka wa CCM na mafisadi ambao wapo hapa jamvini kutumaliza. Wako kazini sasa usiku na mchana, na wanalipwa heavily kwa kazi hii!! Amini usiamini ila habari ndiyo hiyo.
 
Jamani hivi mbona yaonyesha hoja zenu zimeegemea kuwa Zitto kachemsha kwa sababu kazungumzia Wachagga!.. Mbona hii issue ya Wachagga imekuwa deal na hoja kubwa sana!.. kuna kitu gani hapa lakini nisichokijua?.. Je, tumeyapima malalamiko ya Zitto ktk kabila hilo ndnia ya chama? kumbukeni Wangwe pia alilalamika haya haya na alichukiwa na kijiwe kizima hadi siku alokufa.. ndio nikaona watu wakaanza kuja na sympathy zao kisha wakageuza game zima kuanza kumpachika masifa...
Kwa nini hatukutaka kuangalia, kuchunguza na hata kuweka ukutani picha ya Ukabiula ambayo marehemu Wangwe alituonesha. Leo kafuata mwingine hata kama anafanya haya kwa hasira zake lakini je kuna Ukweli?..
Jamani hata Hitler pamoja na ushenzi wake wote aliweza kutabiri na kusema ukweli kuhusu wayahudi. Hitler alisema Wayahudi watakuja tawala dunia tusipowaangalia, leo hii hakuna anayebisha!
 
Mkandara,

Kwoti ya Zitto (kama sikosei kwenye gazeti la mwananchi) ilihusu mwandishi wa gazeti mmoja (ambaye ni mmachame) kuwa kabila moja na kiongozi wa Chadema (ambaye zitto alikuwa akimlalamikia). Kuunganisha watu tu kwa vile wametoka sehemu moja ni ubaguzi wa kikabila usio na nafasi yoyote katika Tanzania ya leo na Zitto should have known this.

Hiki (pamoja na mengine) ndicho kiliwagusa watu wengi wanaomlaumu Zitto hapa.
 
Mwafrika,

..watu wako mstari wa mbele kushutumu Wachaga kwa hili na lile.

..sasa mbona wanapofanya mema hawawataji kwa kabila lao?
 
Yaani wewe na wenzio chuki na wivu wenu umewaharibu akili kabisa. Yaani mnapomshambulia Zitto hadi kupanga mikakati yenu ya kutumia magazeti kumuua kisiasa hamuoni kama mnabomoa nafasi yake na ya chama chenu.

Kwani si nyie na upambe na chuki zenu ndio mlikuja hapa na kuanza kusema kuwa Zitto anatumiwa na CCM wakati ninyi wenyewe ndio mabingwa wa kupokea "support" ya hao CCM wakati mnagombea uheshimiwa. Yaani mlipomuona Zitto amekubali kujitoa baada ya ushauri/shinikizo la wazee kutokana na heshima yake kwao ninyi mkatafsiri kuwa ni weak na kuanza kuendeleza sumu zenu kama mlivyowafanyia wengine wengi waliowahi kushindana na maslahi yenu.

Yaani mlipokuwa mnamdanganya Mzee Slaa na Mtei kuwa kuna hongo inatembezwa na Zitto ambaye ndio kioo cha kukuwa kwa matumaini makubwa ya watanzania kwa chama chenu hamkuwa mnaona maslahi yake wala ya chama chenu.

Na mlivyogubikwa na prejudices mmeona kwa kuwa sumu ya kuhamia CCM haifanikiwi malengo yake sasa mmegeukia CUF kwa saabu yeye ni muislamu. Halafu watu wakiwatupia nanyi sumu ya ukabila mnakimbia kuwaona wajinga.

Kaka, msijidanganye kuwa mtamuweza Zitto kirahisi kama wenzako hapo kabla na wewe sasa mlivyowaweza wengi wengine. Zitto ni nuru ya matumaini ya wengi wenye kuamini katika demokrasia makini na kamwe hatutanyamaza kuacha hizi propaganda zenu hivyohovyo mlizokariri zikituzimia nuru hiyo..

Na kwa taarifa yako atakayeondoka CHADEMA ni wakuja kama wewe na wenzako ambao Zitto alifanya kuwabeba kwenda huko na sio Zitto aliyeijua CHADEMA wakati wewe unavaa kikaptura kwenda shuleni.

omarilyas

- Mkuu Omar, tupo pamoja sana mkuu tunahitaji sana mawazo tofauti kama yako.

Respect.

FMEs!
 
Mwafrika,

..watu wako mstari wa mbele kushutumu Wachaga kwa hili na lile.

..sasa mbona wanapofanya mema hawawataji kwa kabila lao?

Jokakuu,

Hili ni tatizo linalosumbua baadhi ya watu ambao hudhani kuwa wao ni victims tu wa wenzao (katika kila jambo). Mtu atajaribu kitu, akishindwa au kukikosa basi ataanza kutafuta kabila au dini nyingine iliyomfanya asipate.

Watu wanaowachukia wachaga bila sababu yeyote ile ya msingi ni lazima wakemewe kwa nguvu zote na hili jamvi.
 
.....
Kama kuna kosa ambalo sitamsamehe Zitto, ni lile la kujitoa kugombea uenyekiti........pili Chadema pia kama chama wamechemsha big time.............

- Mkulu Ogah, saafi sana na tupo pamoja sana hapo.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Mkandara,

Kwoti ya Zitto (kama sikosei kwenye gazeti la mwananchi) ilihusu mwandishi wa gazeti mmoja (ambaye ni mmachame) kuwa kabila moja na kiongozi wa Chadema (ambaye zitto alikuwa akimlalamikia). Kuunganisha watu tu kwa vile wametoka sehemu moja ni ubaguzi wa kikabila usio na nafasi yoyote katika Tanzania ya leo na Zitto should have known this.

Hiki (pamoja na mengine) ndicho kiliwagusa watu wengi wanaomlaumu Zitto hapa.
Sawa huyo mwandishi alisema nini? Bila shaka alidai kuwa Zitto ni mkabila kwa kumpigia debe Muha mwenzake kuchukua Uenyekiti wa vijana.. ndiko walikoanzia au sio!
 
Kwa nini hatukutaka kuangalia, kuchunguza na hata kuweka ukutani picha ya Ukabiula ambayo marehemu Wangwe alituonesha. Leo kafuata mwingine hata kama anafanya haya kwa hasira zake lakini je kuna Ukweli?..
Jamani hata Hitler pamoja na ushenzi wake wote aliweza kutabiri na kusema ukweli kuhusu wayahudi. Hitler alisema Wayahudi watakuja tawala dunia tusipowaangalia, leo hii hakuna anayebisha!

Asante mkuu, nasema kuwa sisi kama JF we need to address this issues, CHADEMA wasifikiri magazeti yanasaidia, swala ni box la kura! wananchi wengi wanajua haya, ni wajibu wa CHADEMA KUONDOA ili wingu, tusipowashauri sisi tunaowapenda muambiwe na nani? hatutaki kubaki kuandika post nyiiingi miaka 5 tena ijayo kisa tunataka CHADEMA waingie madarakani.

Siasa ni mchezo mchafu, hali yeyote yenye uncertainity ni balaa kwenye kupata kura, huko vijijini CCM wataenda na maneno haya haya, sasa mnataka mbishane na Mkandara humu na waberoya haisaidii kitu, swala ni kuwaza muibuke vipi , mpate kura!

Chama lazima kiwe na sura ya kitaifa. Tunaposema hivi tunaumia kuwa wale tunaowaaamini ndio wanatugeuka, tusiposema, is even worse for you CHADEMA!

muda bado upo!

Kisiasa na kuwadanganya wananchi ni kitu rahisi kabisa you need to do this assignment!
 
Mhh .. kweli?

Unaumia kweli?
 
Sawa huyo mwandishi alisema nini? Bila shaka alidai kuwa Zitto ni mkabila kwa kumpigia debe Muha mwenzake kuchukua Uenyekiti wa vijana.. ndiko walikoanzia au sio!

Mkandara,

Sidhani kama ni vyema kwa Zitto kutoa matamko makali dhidi ya kabila mojawapo la makabila ya Tanzania just because mwandishi wa habari kamuuliza swali la kipuuzi.

Kama kweli Zitto anataka kuwa raisi wa Tanzania (kulingana na wapambe wake hapa), basi lazima Zitto ajue kuwa wamachame, wachaga, na watu wa dini zote (wakiwemo wakristo) watategemea kuwa treated fairly bila uonevu wowote ule toka kwa raisi wao.

Katika hili Zitto alizidi kulikoroga na naona bado marafiki zake (wakiwemo vijana wa ccm hapa JF) wanazidi kuendeleza hii vita dhidi ya wachaga.
 
Mwafrika,
Hapana mkuu Zitto alimjibu mwandishi isipokuwa mlochukulia vibaya ni nyie..Sema tu Zitto kama kiongozi hakutakiwa kabisa kurudishiana na mlalahoi Kibanda amabye alikuwa akitetea unga wake..
Makosa ya Zitto yanajulikana vizuri, kama kiongozi hakutakiwa kusema mengi alosema lakini wakati huo huo tumeona makkosa mengi yakifanyika pia upande wa pili.. ikiwa ni pamoja na Mzee wetu Mtei kumshutumu Zitto indirectly kuwa anatumiwa na mafisadi! - kama ndivyo, What was the point ya mzee huyu na wenzake kwenda kuzungumza naye kutijtoa ikiwa wanaamini Zitto katumwa na mafisadi! Utaweza vipi kuipata suluhu toka kwa mtu anayetumiwa na Mafisadi..

Kisha kibaya zaidi ni kwamab Viongozi wa Chadema na hawa wapambe wamekuja sema mengi machafu baada ya Zitto kukubali kujitoa..
Alipokuwa bado hajakubali hatukusikia hata mtu mmoja akiinua kidole zaidi ya kuomba Zitto ajing'atue na kwamba hakutumia uungwana lakini baada tu ya kujitoa mtumeeee sii amtusi hayo... Hivyo mimi namlaumu Zitto but at the same time tuwalaumu wote waliosababisha haya.
Mbona Mbowe wmenyewe hakusema kitu jamani.. Hata kama kawatumia watu imemsaidia kitu gani?.. hakuna hivyo mimi naamini kabisa Ugonvi wa Zitto na Mbowe ni ugonvi uloingiliwa na wapuuzi wengi wakatujaza ujinga..
 
Mimi ni mtu ambaye bado naamini kuwa Zitto hana nia njema na Chadema. Bila kujali wengine wamesema nini, mimi naona Zitto amebadilika sana na wala sio Zitto yule wa Buzwagi.

Mimi na wewe hatuna uthibitisho wa nani ni nani hapa jamvini kwa hiyo mie nawewe hatuna uhakika wa nani ni kiongozi wa chadema hapa na nani sio kiongozi (ila anajaribu kujipresent kama kiongozi).

Kwa hili huwezi kuwalaumu watu ambao huna hakika kama wamesema. Mie nakubali lawama zote kuwa nimempinga Zitto hapa kwa namna alivyoendesha hili zoezi na katika hili ninasimamia imani yangu.

Mengine yote uliyosema natumaini kuwa viongozi wa chadema watakusoma na kufanyia kazi ushauri wako.
 
teh teh teh teh
unasimamia imani ipi?
 
teh teh teh teh
unasimamia imani ipi?

Imani kuwa jua likizama bahari ya hindi jioni, huingia kwenye shimo kubwa na kisha kutokezea kwenye vilima vya makongo inapofika asubuhi au kinyume chake (wakati wa kiangazi).
 
Mwafrika,
Mkandara,

Mimi ni mtu ambaye bado naamini kuwa Zitto hana nia njema na Chadema. Bila kujali wengine wamesema nini, mimi naona Zitto amebadilika sana na wala sio Zitto yule wa Buzwagi.
Mkuu naheshimu sana mawazo yako na nategemea mtu kama Zitto itabidi afanye kazi ya ziada kurudisha imani kama hii..Nachoomba tu kwa mola kila siku ji kwamba tuhuma kama hizi ziwe ni Uongo na kwamba hasira , na maamuzi ya haraka haraka ndiyo yanampoza Zitto kwani wapo marafiki zangu wasomi wazuri tu lakini tatizo lao kubwa ni kushindwa kuvumilia maumivu na kujiamini kwao imekuwa kilema cha maamuzi yao mengi..ndio maana mwanzo nikasema kwamba A sneetch ni liability kwa chama.. na nadhani mimi ndiye nilikuwa mtu wa kwanza kumlaumu Zitto bila kumwachia pumzi.. Kwa sababu nina hakika kwamba JF ni mahala petu, kijiwe chetu ambacho tunakosoana na kuelekezana zaidi ya kutoleana matusi.. matusi yanaondoa hadhi yetu, JF, viongozi na hata vyama vinavyoongelewa..
JF na moja ya makosa makubwa ya wote waliohusina ni kutumia kijiwe hiki kama uwanja wa matusi kiasi kwamba zikaingiliwa hadi familia..
Nje ya hapo mkuu wangu tuko pamoja, tutafika tu haya ndio majaribio Ya Mungu ktk imani zetu, mfano mdogo mwezi jana tu nimepata tiketi nne za traffic yaani kiola nachofanya naona kinapinduka tu ghafla..lakini siku zote naweka imani kuwa siku nzuri bado ipo usoni...
 
Habari zenu waungwana wa jf ,mimi nimekua nikiangalia mIjadala kibao ya siasa humu ndani lakini bado najiuliza swali moja gumu sana. Na swali lenyewe ni kwamba hivi kweli watu wote humu ndani mnaamini kwamba chadema ama chama kingingine chochote kkikiingia madarakani basi wizi ufifadi utaisha ? Ama pia mnahisi maisha yenu yatabadilika ?mhh ! Acheni kujidanganya ndugu zangu.mimi mtazamo wangu ni kwamba maisha ya wale watakao ingia madarakani ndio yatabadilika ila sisi wengine tutaendelea kuwa pale pale.kwa sababu watakao chukua nchi hawatoki mbinguni ama pia hawatokua sio binaadamu na kwa mantiki hiyo watafanya yale yale ya kiubinadamu ambayo ni tamaa,wizi,uongo na kadhalika msikae makjidanganya eti nimeona humu jamvini kuna watu wana diriki kusema watu fulani ni wakombozi !!! Mhhh jamani tuache Mambo haya, yani kukaaa nakusema Cuf ama Chadema na vyama kadhalika wakichukua madaraka basi wizi utaisha ama maisha yakua bora ? 'it is crazy'.

Naomba mnipe mfano wa nchi moja Ama mbili tatu hapa afrika ambayo chama cha upinzani ama baada mtu mpya kua Raisi mambo yamekua kama mbinguni ?jamani yote haya ni siasa.acheni kujidanganya jameni wote hawa watu ni binadamu kama sisi sote na wananjaa kama sisi sote,wakisha pata kazi hua wanatusahau kama jinsi tulivyo sisi binaadamu.

Nawakilisha

Radikali -aka Rk
 
Last edited:
Habari zenu waungwana wa jf ,mimi nimekua nikiangalia majadala kibao ya siasa humu ndani lakini bado najiuliza swali moja gumu sana. Na swali lenyewe ni kwamba hivi kweli watu wote humu ndani mnaamini kwamba chadema ama chama kingingine chochote kkikiingia madarakani basi wizi ufifadi utaisha ? Ama pia mnahisi maisha yenu yatabadilika ?mhh ! Acheni kujidanganya ndugu zangu.mimi mtazamo wangu ni kwamba maisha ya wale watakao ingia madarakani ndio yatabadilika ila sisi wengine tutaendelea kuwa pale pale.kwa sababu watakao chukua nchi hawatoki mbinguni ama pia hawatokua sio binaadamu na kwa mantiki hiyo watafanya yale yale ya kiubinadamu ambayo ni tamaa,wizi,uongo na kadhalika msikae makjidanganya eti nimeona humu jamvini kuna watu wana diriki kusema watu fulani ni wakombozi !!! Mhhh jamani tuache upuuzi huo, yana kukaaa nakusema cuf ama chadema na vyama kadhalika wakichukua madaraka basi wizi utaisha ama maisha yakua bora ? 'it is crazy'.

Naomba mnipe mfano wa nchi moja hapa afrika ambayo chama cha upinzani ama baada ya kua na raisi mpya mambo yamekua kama mbinguni ?jamani yote haya ni siasa.acheni kujidanganya jameni wote hawa watu ni binadamu kama sisi sote na wananjaa kama sisi sote,wakisha pata kazi hua wanatusahau kama jinsi tulivyo sisi binaadamu.

Nawakilisha

radikali -aka rk
Hii "Breaking News??
 
Mhhh jamani tuache upuuzi huo, yIna kukaaa nakusema Cuf ama Chadema na vyama kadhalika wakichukua madaraka basi wizi utaisha ama maisha yakua bora ? 'it is crazy'.

Naomba mnipe mfano wa nchi moja Ama mbili tatu hapa afrika ambayo chama cha upinzani ama baada mtu mpya kua Raisi mambo yamekua kama mbinguni ?jamani yote haya ni siasa.acheni kujidanganya jameni wote hawa watu ni binadamu kama sisi sote na wananjaa kama sisi sote,wakisha pata kazi hua wanatusahau kama jinsi tulivyo sisi binaadamu.

Nawakilisha

Radikali -aka Rk

Kwanza - hiii sio breaking news.
Pili - wewe ni nani kuita mawazo ya wengine kuwa ni upuuzi.
Tatu - huu ulioandika nao ni upuuzi (kwa kipimo chako)?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom