Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,295
- 10,928
Hii notion ya kijinga ya kuamini kuwa Wahaya, wachaga, Wanyakyusa ni watu hatari wasiopaswa kuongoza siasa za nchi yetu itakwisha lini miongoni mwa wajinga na wachochezi uchwara wa ukabila nchini mweitu?
Mwakasege ni Mnyakyusa watu mahubiri yake wanayaamini, Saida Karoli ni Mhaya nyimbo zake wanazipenda na LUDOVICK UTOH ni Mchaga watu kazi yake wanaifanyia Rejea dhidi ya ubadhirifu uliojaa ndani ya serikali. lakini hawa wote wakithubutu kuingia kwenye Siasa wanaitwa ni watu hatari na wakabila.
Gazeti la Rai toleo la leo limenifanya nijiulize kama vurumai ndani ya CHADEMA ni suala la mapambano ya kupigania Demokrasia ua ni mchezo mchafu unaofanywa na wapinzani wa CHADEMA ili kukisambaritisha chama hicho kabla ya uchaguzi wa mwakani.
Hivi ni Sahihi kusema "Sitta asulubiwa na waislamu ndani ya Kamati Kuu na Halimashauri Kuu" kwa sababu tu wajumbe wengi ndani ya Vikao hivyo ni waislamu na yeye ni mkristo?
Kosa la Mbowe ni kuzaliwa Mchaga Kabila moja na mwanzilishi wa CHADEMA Edwin Mtei? mbona Warioba,Musuguri,Butiku na wengineo walikuwamo ndani ya serikali iliyoongozwa na Ndugu yao Julius Nyerere. Jee na Mwalimu naye alikuwa Mkabila?
Unapatikana wapi mkuu nikupe kumi bora!!! Tufahamu kuwa Tanzania ina makabila zaidi ya 120!!! Na mimi mpaka leo ninajichanganya na kila kabisa ndani ya ofisi, nyumba za ibada, tunashirikiana shughuli mbalimbali bila kujali. Ni automatic kuwa kwa mtu yeyote duniani undugu upo ila inapokuja suala la utendaji tunaangalia utendaji zaidi. Na hivyo basi hata Chadema mnosema ni chama cha wachagga kwanza waanzilishi ni wachagga na wakajiunga wengine wakiwemo wachagga na makabila mengine na chama kikawa na nguvu sana baada ya kufa kwa NCCR-Mageuzi. Leo hii kwa sababu 2010 is around the corner mnaanza kukibomoa??? Au ndiyo response kwa ile kampeni za Sangara??? Ohooo tuwe makini.
Nataka wana JF wenzangu ambao wana uchungu na nchi hii na wanataka ikomboleke, wajihadhari sana na vibaraka wa CCM na mafisadi ambao wapo hapa jamvini kutumaliza. Wako kazini sasa usiku na mchana, na wanalipwa heavily kwa kazi hii!! Amini usiamini ila habari ndiyo hiyo.