Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 naiona CHADEMA kugawanyika sehemu mbili "CHADEMA Asili" na "CHADEMA Wazalendo"

Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 naiona CHADEMA kugawanyika sehemu mbili "CHADEMA Asili" na "CHADEMA Wazalendo"

Nizahiri sasa Tindu Lisu amejipanga na wafuasi wake wanaomuunga mkono iwe jua iwe mvua ni lazima agombee na awe mwenyekiti wa CHADEMA

Pia mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Freeman Mbowe naye amejipanga na watu wake wanaomuunga mkono kutetea tena nafsi yake kama hiyo.

Kwa hali inavyoonyesha hakuna kambi itakayokubali kushindwa kati ya kambi hizi mbili, hali hii itasababisha chama hicho kugawanyika vipande viwili CHADEMA asili ya Mbowe na CHADEMA wazalendo ya Lisu

Baada ya kikao cha leo cha Lisu na wafuasi wake na waandishi wa habari inaonyesha mtia nia huyo hata akipitishwa na chama chake kushindana na boss wake akishindwa hatakubali matokeo ya kushindwa na pengine kujitenga na upande huo wa mwenyekiti na kuondoka na wafuasi wake kuanzisha CHADEMA B

Ingawa kwa maoni yangu CHADEMA wakimpitisha Lisu kugombea uwenyekiti kupambana na Mbowe italeta picha nzuri sana kwenye chama hicho na kuthibitisha kweli kuwa ni chama cha Demokrasia na Maendeleo

Itakuwa jambo la kifahari kama watashindanishwa mafahari hao wawili kwenye uchaguzi wa mwenyekiti na atakayeshindwa akubali matokeo

Lakini kwa hoja za Lisu leo na wafuasi wake inaonyesha hata akipatiwa nafasi ya kugombea akishindwa hawatakubaliana na kushindwa huko kutokana na kutokuwa na imani na uongozi wa Mbowe, watajitenga na uongozi huo kwa imani kuwa Mbowe mbinu zake na uongozi wake kukiongoza chama hicho umefika kikomo

Comasava
Wewe ni kichaa ccm hawawez msajilia chama lissu hawatokubali
 
Wewe ni kichaa ccm hawawez msajilia chama lissu hawatokubali
Ndio shida ya nchi hii hakuna uwazi na demokrasia Lisu si raia wa Tanzania kwa nini azuiwe kusajili chama chake? Kichaa mwenyewe lakini
 
Hivi yule Bon na Genge lake wanaweza kuita mkutano sehemu wakapata watu 20?? Maana naona wanatukana tu na Mbowe kama hujui hawa ndio wanakuvua nguo zaidi unaonekana demokrasia unayosema wala huiamini kama umeongoza miaka 20 achia wengine sio lazima wewe tu....Kwa Upinzani uchwara wa Ntobi na Boni CCM itatawala miaka 200!!!
Aliyosema Nyerere upinzani wa kweli utatoka CCM... Sio hawa Njaa njaa matusi hovyo kabisa
 
Kwa nukuu hiyo uliyomnukuu Mwalimu Nyerere kwa hiyo basi hata Tundu sio mpinzani wa kweli tumsubiri tumsubiri Yohana mbatizaji wetu toka CCM?
 
Back
Top Bottom