Namwongelea Mbunge wangu Mwigulu Nchemba - huyu jamaa hapo zamani alikuwa akitokeza sana humu JF na kujibu hoja au hata kuanzisha hoja. Kwa mfano kuna hoja iliwahi kutokea kuhusu utata wa yeye kutumia jina la mtu mwingine na akajitetea vizuri tu. Mheshimiwa huyu kwa sasa amekuwa kimya sana hajibu hoja na watu wanasema yupo zake kijijini kwao Makunda anafuga na kulima sana. Ninachojiuliza ni kitu gani kimembadili kiasi hicho huyu Mheshimiwa? Ashakuwa na uhakika hapati Ubunge?
Je anahofia wapinzani wake wa zamani na wa sasa ndani na nje ya Chama chake katika uchaguzi ujao? Au amenyamaza ili kumrudishia imani Rais ajifikirie kumrudisha kwenye Baraza la Mawaziri? Ukimya huu unashangaza sana.
Hata hivyo baadhi ya wadau wamekuwa wakidai Mwigulu amanenyamaza kwa kuwa anakabiliwa na wapinzani kibao wakiwepo wale waliojaribu kugombea kupitia Chama Chake Mwaka 2015 ambao ni kama Juma Kilimba (Mbunge wa Zamani na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida) David Jairo (inadaiwa anajisema anaingia tena mwaka huu na kajipanga kweli), Fadhili Nkurlu (ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama) Jumbe Katala (naye amejipanga kihaswa), Nalaila Kiula (anadaiwa kurudi kwa nguvu), Timothy Lyanga, Dr. Zaipuna Yonah n.k ambao mara nyingi wamejaribu kushindana naye.
Wengine wanaosemwa ambao walishindana naye wakiwa upinzani ni Profesa Kitila Mkumbo (Katibu Mkuu Maji) na Jesca Kishoa (Mbunge wa CHADEMA anayetarajiwa kuhamia CCM). Kuna majina mapya pia kama Eng. William Shila wa ulemo, Kitandu Ugula (ambaye ni Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni na Kiongozi wa CCM Kata anayotoka Mwigulu), Diwani wa sasa wa Kata ya Ulemo, Amosi Makala (ambaye baada ya kukosa Morogoro anatarajiwa kurudi kwao Iramba), Marthar Mlata (ameamua kugombea kupitia jimbo), na wengine wengi ambao nitaendelea kuleta majina yao.
Wengine wanadai kawa kimya kwa kuwa chochote atakachokisema kinaweza kuwa na athari katika kutetea jimbo lake ikiwa ni pamoja na tuhuma za kuanza kampeni mapema.