Kusema tu ule ukweli, jimbo letu la Kyela limekuwa kama halina Mbunge tangu aondoke Livingstone Mwakipesile mwaka 1995. Wilaya ya Kyela pamoja na kuwa ni miongoni mwa wilaya kongwe kabisa hapa Tanzania lakini ipo nyuma sana kimaendeleo, yani huwezi linganisha kabisa na wilaya kama Rungwe Mashariki au hata wilaya ya Busokelo iliyoanza juzi juzi tu.
Wilaya ya Kyela imeshindwa hata kukarabati barabara zinazozunguka katikati ya mji, huduma mbovu za maji, miuondo mbinu mibovu ya barabara utadhani wilaya haina mapato. Nakumbuka kipindi Mh Rais anafanya ziara Wilayani Kyela, uongozi wa hapo wilayani walijaribu kuziba ziba mashimo ya barabara kuu itokayo Kasumulu kwenda Kyela ili tu ionekane ni nzima wakati ukweli ni kwamba barabara hiyo ni kimeo sana.
Mbunge hana muda na jimbo lake, angalau Dr. Tulia ameonyesha moyo wa upendo kupitia Tulia Foundation wananchi wanafaidika na mikopo midogo midogo.
Hivyo basi Tunakuomba Dr Tulia uje ugombee ubunge katika wilaya yetu, tuna imani sana na wewe kwamba angalau unaweza kuleta maendeleo chanya katika wilaya ya Kyela