Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Tunaamini mtu aliyeelimika, anakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto za jamii. Ingawa kuna baadhi ya watu wanaamini, kuwa na vyeti vingi ndio kuelimika; ambapo si kweli.
Kuwa na vyeti vingi bila kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za jamii, ni sawa na kusoma magazeti ya udaku na baadaye ukapewa vyeti kwa kufanikiwa kusoma magazeti hayo. Ambapo vyeti vyako vinakuwa havina maana zaidi ya kuthibitisha ulisoma magazeti hayo.
Pia ile dhana ya kusema mimi nimesoma sana, inatakiwa iendane na uwezo wako wa kutatua kero au changamoto za jamii. Vinginevyo, unakuwa huna tofauti na yule aliyesoma magazeti ya udaku na kutunukiwa uthibitisho wa kusoma magazeti hayo.
Pia mtu aliyeelimika uongea kwa kujiamini ‘confidence’ na pia um-‘challenge’ boss wake pale ambapo anaenda ndivyo sivyo. Mtu aliyeelimika huwa hawazi kukosa ugali leo, bali anaamini hata ukimfukuza kazi , yeye ataishi tu, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutatua changamoto za jamii, ikiwa ni pamoja na kujiajiri na utengenezaji wa ajira kwa wengine.
Je, wewe umeelimika?