Kuelimika ni kuwa na vyeti vingi?

Kuelimika ni kuwa na vyeti vingi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Tunaamini mtu aliyeelimika, anakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto za jamii. Ingawa kuna baadhi ya watu wanaamini, kuwa na vyeti vingi ndio kuelimika; ambapo si kweli.

Kuwa na vyeti vingi bila kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za jamii, ni sawa na kusoma magazeti ya udaku na baadaye ukapewa vyeti kwa kufanikiwa kusoma magazeti hayo. Ambapo vyeti vyako vinakuwa havina maana zaidi ya kuthibitisha ulisoma magazeti hayo.

Pia ile dhana ya kusema mimi nimesoma sana, inatakiwa iendane na uwezo wako wa kutatua kero au changamoto za jamii. Vinginevyo, unakuwa huna tofauti na yule aliyesoma magazeti ya udaku na kutunukiwa uthibitisho wa kusoma magazeti hayo.

Pia mtu aliyeelimika uongea kwa kujiamini ‘confidence’ na pia um-‘challenge’ boss wake pale ambapo anaenda ndivyo sivyo. Mtu aliyeelimika huwa hawazi kukosa ugali leo, bali anaamini hata ukimfukuza kazi , yeye ataishi tu, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutatua changamoto za jamii, ikiwa ni pamoja na kujiajiri na utengenezaji wa ajira kwa wengine.

Je, wewe umeelimika?
 
Hapana kuna wengi wenye makaratasi ila ni wa hovyo.

Elimu huonekana kwenye matendo.
 
Kwa hiyo kumbe kuelimika ni kujiajiri tu basi kwa mtazamo wako serikali ya Tanzania ni pumbavu haiwezekani iwekeze

Mkishapata vi Mia mbili hamsini mkashiba kunde mnakuwa na mawazo finyu
Mfano; usipo ajiriwa, kwa kutumia elimu yako itakusaidiaje? au utatafuta tena kuajiriwa?
 
Tunaamini mtu aliyeelimika, anakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto za jamii. Ingawa kuna baadhi ya watu wanaamini, kuwa na vyeti vingi ndio kuelimika; ambapo si kweli.

Kuwa na vyeti vingi bila kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za jamii, ni sawa na kusoma magazeti ya udaku na baadaye ukapewa vyeti kwa kufanikiwa kusoma magazeti hayo. Ambapo vyeti vyako vinakuwa havina maana zaidi ya kuthibitisha ulisoma magazeti hayo.

Pia ile dhana ya kusema mimi nimesoma sana, inatakiwa iendane na uwezo wako wa kutatua kero au changamoto za jamii. Vinginevyo, unakuwa huna tofauti na yule aliyesoma magazeti ya udaku na kutunukiwa uthibitisho wa kusoma magazeti hayo.

Pia mtu aliyeelimika uongea kwa kujiamini ‘confidence’ na pia um-‘challenge’ boss wake pale ambapo anaenda ndivyo sivyo. Mtu aliyeelimika huwa hawazi kukosa ugali leo, bali anaamini hata ukimfukuza kazi , yeye ataishi tu, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutatua changamoto za jamii, ikiwa ni pamoja na kujiajiri na utengenezaji wa ajira kwa wengine.

Je, wewe umeelimika?
Kuchamba kwingi huondoka na Mavi,tumewashuhudia wenye Elimu kubwa wakiwa ndio wapumbavu
 
Upumbavu hautokani na elimu bali unaanziana mtazamo wa mtu mhusika. Unaweza ukawa na elimu ukaonekana mpumbavu na bado unaweza usiwe na elimu ya kutosha ukaonekana mpumbavu.
Wewe unasemaje kwa Hilo???
 
Back
Top Bottom