Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kwani hakuna Marais wabaya Waliohai?
Kama lengo ni kutafutana ubaya, hatuwezi kosa ubaya WA yeyote.
Lakini kutafuta ubaya wa Wafu ni dalili ya ucheshi wa mwendawazimu.
Hakunaga Hukumu ya Wafu, wanaohukumiwa ni Waliohai.

Hata hivyo kuna Ile hasira ya wahanga ambayo MTU akifa humsema kutuliza hasira na chuki zao. Lakini kumchukia Na kuwa na hasira ya Marehemu Kwa zaidi ya miaka ni Jambo la kipuuzi hasa ukijua amekufa na hatorudi
Hebu jifunze kunyamaza, Hujui wala hufeel pain ambazo watu wamezipata kutoka Kwa huyo ibilisi unayemtetea, labda angeuwawa baba yako mzazi na mama yako mzazi ndio ungejuwa uchungu wake.

Huyo hata ipite miaka 50 ni lazima atashtakiwa tu ili haki itendeke haijarishi yupo kaburini cha msingi ni ile hukumu itakayotolewa ili ikae kwenye kumbukumbu.
 
Kuna watu wameachiwa makovu ya milele na Magufuli, na kuongelea uovu wake ni sehemu ya matibabu kwao. Pia kuongelea uovu wake ni kuwakumbusha waliopo namna watakavyokumbukwa wakishaondoka. Fikiria kidogo muda mwingine mkuu, using'ang'anie uchawa tu.
 
Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa

Magufuli nilimlaani akiwa hai lakini sinaga Laana wala baraka Kwa Watu waliokwisha Kufa.

Kila MTU MTU mpenda Haki alichukizwa na Matendo hayo, ikiwemo Mimi.
 
Kuna mmoja akiona kaboronga kuongoza serikali anaenda kubumba skendo na kumrushia Hayati,wapinzani vichwa panzi wanaidaka hoja na kuitumia kama silaha yao

Wanaiba hela za kutosha kisha wanaibuka kumsingizia Magu alificha china
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.
Mkuu mimi na wewe sote ni wasomi..
Kuna maisha tunayapitia ambayo kiukweli hatukupaswa kuyapitia
 
Kuna watu wameachiwa makovu ya milele na Magufuli, na kuongelea uovu wake ni sehemu ya matibabu kwao. Pia kuongelea uovu wake ni kuwakumbusha waliopo namna watakavyokumbukwa wakishaondoka. Fikiria kidogo muda mwingine mkuu, using'ang'anie uchawa tu.

Mimi siwezi kuwa chawa Mkuu.

Najua wapo ambao wanamakovu ya milele lakini lazima wasamehe kwani Mungu ndiye mjuzi WA yote, tena aliwasaidia kuwalipia kisasi.
Au walitakaje zaidi
 
Shetani ndio Uovu wenyewe,lakini binadamu hata awe muovu kiaje hakosi jema moja.

Tofautisha Shetani na binadamu.
Vyovyote vile Magufuli lazima atajwe na watu wamjue pande zote ili ule uovu wake usije kujirudia tena kwenye taifa letu na yale mazuri yake watu watayaishi na yaendelezwa. Haiwezekani kutokusemwa hiyo haipo kuna sehemu alikosea kama mwanadamu.
 
Magufuli nilimlaani akiwa hai lakini sinaga Laana wala baraka Kwa Watu waliokwisha Kufa.

Kila MTU MTU mpenda Haki alichukizwa na Matendo hayo, ikiwemo Mimi.
Huna sababu ya kumlaani ila waliopata mateso yake kama lissu hawezzi kumsahahu kwa namna yoyote, wala familia ya Ben saannane na wengine waliotekwa kamwe hawatamsahau kila wakati wa sala au maombi watamlaani tu. wewe kwa sababu hakuna ulichopoteza kwenye utawala wake zaidi ya marinda huna cha kumkumbuka
 
Magufuli nilimlaani akiwa hai lakini sinaga Laana wala baraka Kwa Watu waliokwisha Kufa.

Kila MTU MTU mpenda Haki alichukizwa na Matendo hayo, ikiwemo Mimi.
Sasa Kwa taarifa yako kama unapenda Magufuli asisemwe kama kimya, ukianzisha thread ya Magufuli unatutowa pangoni ambao hata hatukuwa na mpango wa kucomment humu leo zaidi ya kusoma tu.

Uelewa wako unapoishia wengine ndio unapoanzia hapo, kwahiyo kuwa makini usicheze na hisia za watu kwenye vitu sensitive kama vya huyu muuwaji.
 
Huna sababu ya kumlaani ila waliopata mateso yake kama lissu hawezzi kumsahahu kwa namna yoyote, wala familia ya Ben saannane na wengine waliotekwa kamwe hawatamsahau kila wakati wa sala au maombi watamlaani tu. wewe kwa sababu hakuna ulichopoteza kwenye utawala wake zaidi ya marinda huna cha kumkumbuka

Haina maana yoyote Ile.
Kama alivyofanya Magufuli ilivyokuwa haina maana ndivyo hivyohivyo Kwa mahasimu wake wafanyavyo
 
Ndipo wengi waliporudi nyuma wakaacha kuandamana naye... Yesu akawauliza wanafunzi, na nyie mwataka kuondoka?
 
Sasa Kwa taarifa yako kama unapenda Magufuli asisemwe kama kimya, ukianzisha thread ya Magufuli unatutowa pangoni ambao hata hatukuwa na mpango wa kucomment humu leo zaidi ya kusoma tu.

Uelewa wako unapoishia wengine ndio unapoanzia hapo, kwahiyo kuwa makini usicheze na hisia za watu kwenye vitu sensitive kama vya huyu muuwaji.

Unapoambiwa kauli ya "haina maana yoyote" unaelewa Jambo Gani Mkuu?
 
Tunajifunza kwa kina mambo yaliyopita (yaliyotendwa na wafu), kwa lengo la kutatua changamoto za wakati huu na hata ujao.
Ni wapumbavu pekee wanaojenga hoja kwamba wafu wasitajwe.
Ni muhimu kuweka kumbukumbu za mema na mabaya ya vizazi vilivyopita kwa lengo la kubotesha kizazi hiki na vile vijavyo.
Ni bahati mbaya sana, siasa zetu zimejaa wapumbavu huku watu wenye akili nzuri na busara wakikaa pembeni.
 
Umemshauri vyema kabisa
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
 
Back
Top Bottom