Kuna kitu kinaitwa "closure". Kwa kiswahili cha mtaani tunaweza kuita "kufunga mafaili" ya jambo au suala. Katika utawala wa Magufuli kuna mambo mengi mabaya sana yaliyofanyika ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu au tuseme bado yako gizani. Kwa mfano, mauaji ya Akwilina, Lwajabe, miili iliyookotwa kwenye viroba, kupotea kwa Azori, Ben Saanane, risasi za Lissu, kutekwa kwa Mo, Roma, Magoti, wizi wa uchaguzi 2019, 2020. kuzima vyombo vya habari, vyama vya upinzani, ukwapuaji wa fedha za watu benki, bureau de change, n.k. Na majuzi Rais wa sasa kaongezea ufisadi kwenye pesa za "plea bargain" zisizojulikana zilipo.
Yote hayo bado yako gizani. Serikali ya CCM bado haionyeshi utashi wa kuleta CLOSURE kwenye kadhia hizi.
Lazima mkondo wa sheria ufanye kazi, ukweli ujulikane, hukumu sahihi itolewe (hata posthumously ikibidi) na hatua zichukuliwe kwa wahusika waliopo. MUHIMU ZAIDI kwa amani na utulivu wa nchi ni vyema kuwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa (truth and reconcilliation process). Hiyo ndiyo namna bora ya kupata CLOSURE. Maridhiano yanayoendelea ni hatua nzuri lakini haitoshi. Kinachosikitisha sana ni kwamba miaka ya karibuni serikali ya CCM imezidi kuendesha propaganda hatarishi za kuwagawa wananchi.
Kwa wale watakaodai hata awamu zilizopita zina matatizo ya aina hiyo wako sawa ingawa ni wazi kuwa Rais wa awamu ya tano aliyafikisha kwenye kiwango cha kutisha. Yaliyotokea kwa Mwangosi, Zona, Ulimboka na Kibanda awamu ya nne nayo bado "yananing'inia". Hayajapata CLOSURE. Ni doa kubwa kwa serikali ya CCM. Wahenga hawakukosea waliposema "damu ya mtu haipotei bure". Yote haya yataendelea kulitesa taifa kwa miaka mingi ijayo.
Walio na shauku kubwa kutaka Magufuli asisemwe au asitajwe basi waiombe serikali yao ya CCM ichukue hatua kuleta CLOSURE na UTANGAMANO kwa wananchi wote nchini. NA pia wajue wakianzisha mada za kumsifu Magufuli katika mazingira haya ambapo kadhia nyingi za utawla wake hajipata CLOSURE basi wasishangae kujibiwa na wenye kero zao. Waingereza wanaita kujibiwa "in kind".