Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa
Tungekuwa muda mwingi tunazungumzia mabaya ta shetani na watu wote wajue ubaya wa shetani kama ifanyikavyo kwa Magufuli basi naamini wengi tungekuwa wachamungu.
 
Kuna kitu kinaitwa "closure". Kwa kiswahili cha mtaani tunaweza kuita "kufunga mafaili" ya jambo au suala. Katika utawala wa Magufuli kuna mambo mengi mabaya sana yaliyofanyika ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu au tuseme bado yako gizani. Kwa mfano, mauaji ya Akwilina, Lwajabe, miili iliyookotwa kwenye viroba, kupotea kwa Azori, Ben Saanane, risasi za Lissu, kutekwa kwa Mo, Roma, Magoti, wizi wa uchaguzi 2019, 2020. kuzima vyombo vya habari, vyama vya upinzani, ukwapuaji wa fedha za watu benki, bureau de change, n.k. Na majuzi Rais wa sasa kaongezea ufisadi kwenye pesa za "plea bargain" zisizojulikana zilipo.

Yote hayo bado yako gizani. Serikali ya CCM bado haionyeshi utashi wa kuleta CLOSURE kwenye kadhia hizi.

Lazima mkondo wa sheria ufanye kazi, ukweli ujulikane, hukumu sahihi itolewe (hata posthumously ikibidi) na hatua zichukuliwe kwa wahusika waliopo. MUHIMU ZAIDI kwa amani na utulivu wa nchi ni vyema kuwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa (truth and reconcilliation process). Hiyo ndiyo namna bora ya kupata CLOSURE. Maridhiano yanayoendelea ni hatua nzuri lakini haitoshi. Kinachosikitisha sana ni kwamba miaka ya karibuni serikali ya CCM imezidi kuendesha propaganda hatarishi za kuwagawa wananchi.

Kwa wale watakaodai hata awamu zilizopita zina matatizo ya aina hiyo wako sawa ingawa ni wazi kuwa Rais wa awamu ya tano aliyafikisha kwenye kiwango cha kutisha. Yaliyotokea kwa Mwangosi, Zona, Ulimboka na Kibanda awamu ya nne nayo bado "yananing'inia". Hayajapata CLOSURE. Ni doa kubwa kwa serikali ya CCM. Wahenga hawakukosea waliposema "damu ya mtu haipotei bure". Yote haya yataendelea kulitesa taifa kwa miaka mingi ijayo.

Walio na shauku kubwa kutaka Magufuli asisemwe au asitajwe basi waiombe serikali yao ya CCM ichukue hatua kuleta CLOSURE na UTANGAMANO kwa wananchi wote nchini. NA pia wajue wakianzisha mada za kumsifu Magufuli katika mazingira haya ambapo kadhia nyingi za utawla wake hajipata CLOSURE basi wasishangae kujibiwa na wenye kero zao. Waingereza wanaita kujibiwa "in kind".
Umemaliza yote mkuu
 
Amini usiamini wanasiasa wanaomtaja magu kwa ubaya wake na kujitia upofu wa mazuri yake,2025 ndio watakuwa vinara wa kumsifia jpm kishingo upande ili wapate kura.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Ukitaka kumsifia unaruhusiwa, na kama unamtetea mtetee kimpango wako. Hao marais wabaya walioko hai waongelee ww. Sisi tuko na dhalimu Magufuli fullstop.
Kwahiyo umekubali hoja ya mleta mada kwamba mmeng'ang'ania kueleza maovu ya mtu aliyekufa kwa sababu ya hisia zenu tu ila hakuna faida kuzungumzia maovu ya mtu aliyekufa hayupo tena na kuacha kuzungumzia waovu waliyo hai ambao bado wanaendelea kutenda maovu?
 
Umeandika jambo la mbolea sana mkuu.
 
Kuna kitu kinaitwa "closure". Kwa kiswahili cha mtaani tunaweza kuita "kufunga mafaili" ya jambo au suala. Katika utawala wa Magufuli kuna mambo mengi mabaya sana yaliyofanyika ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu au tuseme bado yako gizani. Kwa mfano, mauaji ya Akwilina, Lwajabe, miili iliyookotwa kwenye viroba, kupotea kwa Azori, Ben Saanane, risasi za Lissu, kutekwa kwa Mo, Roma, Magoti, wizi wa uchaguzi 2019, 2020. kuzima vyombo vya habari, vyama vya upinzani, ukwapuaji wa fedha za watu benki, bureau de change, n.k. Na majuzi Rais wa sasa kaongezea ufisadi kwenye pesa za "plea bargain" zisizojulikana zilipo.

Yote hayo bado yako gizani. Serikali ya CCM bado haionyeshi utashi wa kuleta CLOSURE kwenye kadhia hizi.

Lazima mkondo wa sheria ufanye kazi, ukweli ujulikane, hukumu sahihi itolewe (hata posthumously ikibidi) na hatua zichukuliwe kwa wahusika waliopo. MUHIMU ZAIDI kwa amani na utulivu wa nchi ni vyema kuwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa (truth and reconcilliation process). Hiyo ndiyo namna bora ya kupata CLOSURE. Maridhiano yanayoendelea ni hatua nzuri lakini haitoshi. Kinachosikitisha sana ni kwamba miaka ya karibuni serikali ya CCM imezidi kuendesha propaganda hatarishi za kuwagawa wananchi.

Kwa wale watakaodai hata awamu zilizopita zina matatizo ya aina hiyo wako sawa ingawa ni wazi kuwa Rais wa awamu ya tano aliyafikisha kwenye kiwango cha kutisha. Yaliyotokea kwa Mwangosi, Zona, Ulimboka na Kibanda awamu ya nne nayo bado "yananing'inia". Hayajapata CLOSURE. Ni doa kubwa kwa serikali ya CCM. Wahenga hawakukosea waliposema "damu ya mtu haipotei bure". Yote haya yataendelea kulitesa taifa kwa miaka mingi ijayo.

Walio na shauku kubwa kutaka Magufuli asisemwe au asitajwe basi waiombe serikali yao ya CCM ichukue hatua kuleta CLOSURE na UTANGAMANO kwa wananchi wote nchini. NA pia wajue wakianzisha mada za kumsifu Magufuli katika mazingira haya ambapo kadhia nyingi za utawla wake hajipata CLOSURE basi wasishangae kujibiwa na wenye kero zao. Waingereza wanaita kujibiwa "in kind".
Ndio maana mleta mada haoni faida ya kutumia muda mwingi na nguvu kueleza au kufukua maovu ya awamu ya tano ili hali hata awamu zilizopita hakukuwa na hiyo closure na ndio kwanza hao viongozi wamejiwekea kinga ya kutokushtakiwa.
 
Kwa hiyo yeye ndio alie piga risasi,yeye ndio aliewateka hao ulio waoanisha hapo juu,kwani wangapi walitekwa na wakapatikana,haya ikatokea taarifa kwamba hao waliotekwa yaweza ikawa ni wao kwa wao waliofanyiana unyama huu,au huyo aliepigwa risasi kapigwa na watu wake wa karibu kutokana na maslahi baina yao wao kwa wao,jee familia ngapi zenyewe kwa zenyewe zinauana kwa njia mbali mbali sembuse kwenye vyama?,haya wangapi wanafaidika na barabara ya morogoro road jee inawasaidia wagonjwa wangapi kuokolewa maisha yao kutokana na kuwa na miundo mbinu rafiki,jee hao wakazi waliokuwa wanaishi maeneo ya kimara tokea kuundwa kwa Tanzania hawakuwahi kulipwa stahiki zao kabla,jee wana uhakika walipo kuja nunua maeneo hao walio wauzia wao hawakulipwa kabla?
Yule mzee alikuwa Muuaji na halitapingika hilo,,, shetani kabisa Yule tutamlaani kila siku na kuanika mabaya yake hadi vizazi vijavyo vijue kweli tuliwahi kuwa na Shetani Ikulu
Tungekuwa muda mwingi tunazungumzia mabaya ta shetani na watu wote wajue ubaya wa shetani kama ifanyikavyo kwa Magufuli basi naamini wengi tungekuwa wachamungu.
 
Tungekuwa muda mwingi tunazungumzia mabaya ta shetani na watu wote wajue ubaya wa shetani kama ifanyikavyo kwa Magufuli basi naamini wengi tungekuwa wachamungu.
kwani hujui kwamba yule mzee ni Jamii hiyo hiyo ya shetani
 
Marehemu alikua dikteta killer jambazi kibaka mwehu af unataka tumsifie

Maisha kla mtu anauhuru wa kusema na kuongea ttzo lenu wafuasi wa marehemu mnatabia km za marehemu mnataka wote tuwe na mawazo sana huo ni udikteta km wa baba yenu jiwe
Sawa alikuwa dikteta na jambazi na muuwaji, sasa kutumia muda mwingi kuzungumzia hayo mabaya yake (kuliko kuzungumzia mabaya yaliyopo sasa) je kunaleta faida au ni suala kihisia kupunguza hasira?
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Shetani utaachaje kimtaja kwa ushenzi wake?
 
Hebu jifunze kunyamaza, Hujui wala hufeel pain ambazo watu wamezipata kutoka Kwa huyo ibilisi unayemtetea, labda angeuwawa baba yako mzazi na mama yako mzazi ndio ungejuwa uchungu wake.

Huyo hata ipite miaka 50 ni lazima atashtakiwa tu ili haki itendeke haijarishi yupo kaburini cha msingi ni ile hukumu itakayotolewa ili ikae kwenye kumbukumbu.
Mungu ni Mwema siku zote
 
basi kaa huko unyamaze kimya kuna watu bado wana vidonda wakivitizama tu wanamkumbuka huyo muuaji na kuongea kwao inawapa faraja
This is collective therapy for all victims of Magufuli era and need to start identifying the people who were his foot soldiers because he didn’t do the work alone he gave the order’s and they were followed by??
 
Nikweli Shetani anashawishi watu ndiyo maana aliweza pia kumshawishi Magufuli awatendee wengine uovu na sisi tunakemewa wengine wasije kushawishiwa kama Magufuli.
Ukiwa na maana wasiwe viongozi aina kama ya Magufuli Kwamba hapo unakusudia wanasiasa? Kwa sababu hapa Magufuli anazungumziwa kama kiongozi ila shetani anawishi uovu kila mtu hadi sie tusio viongozi.
 
Back
Top Bottom