Wewe unaishi wapi ambako shetani hatajwi?Shetani tungekuwa tumtaja kama tufanyavyo kwa Magufuli basi wengi tungekuwa wachamungu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unaishi wapi ambako shetani hatajwi?Shetani tungekuwa tumtaja kama tufanyavyo kwa Magufuli basi wengi tungekuwa wachamungu.
Hata huku kwetu Magufuli ni kiongozi shujaa, mafala wachache wasiotaka kukubali kwasababu binafsi hawazuii hilo.Ujerumani Hitler ni kiongozi shujaa.
Ni kama Ghadafi tuu
Ni suala la kihisia zaidi ambalo linatumia muda mwingi kuliko kujadili yaliyopo ambayo tunaweza kufanya mabadiliko.Atasemwa mpaka machozi yaa watu yatakapokauka.
Wewe ni nini unachokifanya hapa kama sio kumtaja?? Tena ukamuanzishia na uzi kabisa.Anatajwa na Wajerumani? Au kina Nani?
Kutaja taja Wafu kila mara ni dalili ya kuchanganyikiwa.
Unataja Watu ambao hawana chochote chakufanya
Kutajwa tu sio shidamaana wapo wenye kumuabudu kabisa hivyo wanamtaja, mie nikiangalia hali ilivyo naona maovu mengi kuliko mema tafsiri yake shetani ana wafuasi wengi tunaona na kusikia mambo ya shetani kwa wingi kuliko kusikia anavyolaaniwa shetani.Wewe unaishi wapi ambako shetani hatajwi?
wafu hawajui neno lolote, ila marehemu atatajwa sana kwa mambo ya hovyo na mazuri aliyoyafanya ktk hii nchiAnaandika, Robert Heriel
Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.
Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.
Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.
Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.
Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.
Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.
Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.
Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.
Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.
Acha nipumzike SASA.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Awawashindi CCMChadema watakuelewa?
Wapuuzi sana hawa vijana wa chadema
Kuna tofauti ya kuzungumzia histoaria ya mtu na kumsema mtu tunakozungumzia hapa, Nyerere huwa anatajwa sana ila ni tofauti na jinsi alivyomzungumzia Tundu Lissu bungeni ikazuia maneno.1). Dikteta Benito Mussolini alianza kutawala Italy tarehe 31/10/1922, karne nzima iliyopita, akapinduliwa tarehe 25/July/1943..
Hatimaye akanyongwa Kwa sababu ya uovu wake mwaka 1945.
2). Dikteta Joseph Stalin, alitawala Urusi Kwa mkono wa chuma kati ya 1924 na 1953.
3). Dikteta Vladimir Lenin alitawala kuanzia 1917 hadi 1924..
Nk..
Na kuna orodha ndeeefu ya madikteta wa Afrika ambao ni marehemu na wanaendelea kusemwa..
Wote hao wanasemwa na wataendelea kusemwa.
Ndo wewe uzibe watu midomo kumsema dikteta wa juzi hapa?!!!
Moja ya manufaa ya kuwasema waovu wa zamani ni kukumbushana na kuelimishana ili kupunguza uwezekano wa kuibuka muovu mwingine upyaaa!
Watu wengi walionyooka wanamkubali Magufuli.Hapa nilipo mie,watanzania wengi wanaoishi hapa uingereza wanamkubali sana jpm,huwa tuna club yetu ya kukutana kila jmos ya mwezi,huwez amin,wanammiss sn jpm,japo wanakili kuwa alifanya makosa kubinya upinzani,
mwendazake ni jinamizi lililojivika ktk vazi la uzalendo, yaani atatajwa sana, zitto kasema ambao hawataki kusikia akitajwa wamfuate kaburiniKwani hakuna Marais wabaya Waliohai?
Kama lengo ni kutafutana ubaya, hatuwezi kosa ubaya WA yeyote.
Lakini kutafuta ubaya wa Wafu ni dalili ya ucheshi wa mwendawazimu.
Hakunaga Hukumu ya Wafu, wanaohukumiwa ni Waliohai.
Hata hivyo kuna Ile hasira ya wahanga ambayo MTU akifa humsema kutuliza hasira na chuki zao. Lakini kumchukia Na kuwa na hasira ya Marehemu Kwa zaidi ya miaka ni Jambo la kipuuzi hasa ukijua amekufa na hatorudi
Huwezi kumtenganisha mtu na matendo yake.Kuna tofauti ya kuzungumzia histoaria ya mtu na kumsema mtu tunakozungumzia hapa, Nyerere huwa anatajwa sana ila ni tofauti na jinsi alivyomzungumzia Tundu Lissu bungeni ikazuia maneno.
Anatajwa na Wajerumani? Au kina Nani?
Kutaja taja Wafu kila mara ni dalili ya kuchanganyikiwa.
Unataja Watu ambao hawana chochote chakufanyak
Kwa hivyo sio vibaya kukumbusha uovu wake ili wenye madaraka na watakaokua na madaraka siku zojazo wajifunze kuwa Kuna haja ya kuwatendea watu wema, Mana mabaya huambatana na mtendaji wa hayo mabaya. (Lesson)Magufuli nilimlaani akiwa hai lakini sinaga Laana wala baraka Kwa Watu waliokwisha Kufa.
Kila MTU MTU mpenda Haki alichukizwa na Matendo hayo, ikiwemo Mimi.
Mamaako.Ukitoka pangoni ukisema alafu inakua nn?? Wewe ni mjinga mkubwa
Mpuuzi ni wewe usiyejua /usiyeweza kupima/kutafakari machungu waliyonao ya aliowaumiza! Ni upuuzi wa jabu ulio nao wewe. Mke wa azory, Ben and many many others wanajisikiaje muda huu bila kuwa na wapendwa wao? Wewe "ntu" wa ajabu!Anaandika, Robert Heriel
Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.
Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.
Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.
Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.
Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.
Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.
Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.
Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.
Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.
Acha nipumzike SASA.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Maelezo kuntu..Kuna kitu kinaitwa "closure". Kwa kiswahili cha mtaani tunaweza kuita "kufunga mafaili" ya jambo au suala. Katika utawala wa Magufuli kuna mambo mengi mabaya sana yaliyofanyika ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu au tuseme bado yako gizani. Kwa mfano, mauaji ya Akwilina, Lwajabe, miili iliyookotwa kwenye viroba, kupotea kwa Azori, Ben Saanane, risasi za Lissu, kutekwa kwa Mo, Roma, Magoti, wizi wa uchaguzi 2019, 2020. kuzima vyombo vya habari, vyama vya upinzani, ukwapuaji wa fedha za watu benki, bureau de change, n.k. Na majuzi Rais wa sasa kaongezea ufisadi kwenye pesa za "plea bargain" zisizojulikana zilipo.
Yote hayo bado yako gizani. Serikali ya CCM bado haionyeshi utashi wa kuleta CLOSURE kwenye kadhia hizi.
Lazima mkondo wa sheria ufanye kazi, ukweli ujulikane, hukumu sahihi itolewe (hata posthumously ikibidi) na hatua zichukuliwe kwa wahusika waliopo. MUHIMU ZAIDI kwa amani na utulivu wa nchi ni vyema kuwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa (truth and reconcilliation process). Hiyo ndiyo namna bora ya kupata CLOSURE. Maridhiano yanayoendelea ni hatua nzuri lakini haitoshi. Kinachosikitisha sana ni kwamba miaka ya karibuni serikali ya CCM imezidi kuendesha propaganda hatarishi za kuwagawa wananchi.
Kwa wale watakaodai hata awamu zilizopita zina matatizo ya aina hiyo wako sawa ingawa ni wazi kuwa Rais wa awamu ya tano aliyafikisha kwenye kiwango cha kutisha. Yaliyotokea kwa Mwangosi, Zona, Ulimboka na Kibanda awamu ya nne nayo bado "yananing'inia". Hayajapata CLOSURE. Ni doa kubwa kwa serikali ya CCM. Wahenga hawakukosea waliposema "damu ya mtu haipotei bure". Yote haya yataendelea kulitesa taifa kwa miaka mingi ijayo.
Walio na shauku kubwa kutaka Magufuli asisemwe au asitajwe basi waiombe serikali yao ya CCM ichukue hatua kuleta CLOSURE na UTANGAMANO kwa wananchi wote nchini. NA pia wajue wakianzisha mada za kumsifu Magufuli katika mazingira haya ambapo kadhia nyingi za utawla wake hajipata CLOSURE basi wasishangae kujibiwa na wenye kero zao. Waingereza wanaita kujibiwa "in kind".
Ona tutusa hili.Tunamtaje jpm kama sehemu ya mktaba wa maridhiano na mama,japo hata sisi hatupendi kumtaja,lkn maelekezo ni lazima tumnange na kumkashifi na kimxushua mambo mabaya,lengo ni kupunguza nguvu kubwa ya ushawishi alionao kwa watanzania na dunia nzima,Na nikili kuwa tunao wakati mgumu sana mbele ta watanzania,kwani tunaxomewa na kutukanwa,
Haisaidiii....Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa
Una uthibitisho gani kwamba Magufuli aliua mtu? Alimuua nani? Thibitisha...Hebu jifunze kunyamaza, Hujui wala hufeel pain ambazo watu wamezipata kutoka Kwa huyo ibilisi unayemtetea, labda angeuwawa baba yako mzazi na mama yako mzazi ndio ungejuwa uchungu wake.
Huyo hata ipite miaka 50 ni lazima atashtakiwa tu ili haki itendeke haijarishi yupo kaburini cha msingi ni ile hukumu itakayotolewa ili ikae kwenye kumbukumbu.
Sawa, wewe endelea kulialia kama juha uone kama kunakitakacho badilika.Wayahudi wanaomlaani Hitler mpaka Leo unadhani niwajinga wewe ndio mwerevu! Mjinga kabisa wewe!