Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Acha watu waongee , tunaongelea Nyerere ambaye hayupo tena kila siku lakini hujawahi kusema chochote, tofauti yao nini au unataka tusifie tuu, wewe kila siku unaandika na hatukuiti umechanganyikiwa, acha hayo mambo yako
 
Ukiwa na maana wasiwe viongozi aina kama ya Magufuli Kwamba hapo unakusudia wanasiasa? Kwa sababu hapa Magufuli anazungumziwa kama kiongozi ila shetani anawishi uovu kila mtu hadi sie tusio viongozi.
Kikubwa mwanadamu yoyote hupaswi kuwa mwovu na usijiinue sana hadi kujifananisha na malaika na kujiuona hukosei, Magufuli alipitiliza kujiona yeye ni yeye na hakuna kama yeye.
 
Kuna kitu kinaitwa "closure". Kwa kiswahili cha mtaani tunaweza kuita "kufunga mafaili" ya jambo au suala. Katika utawala wa Magufuli kuna mambo mengi mabaya sana yaliyofanyika ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu au tuseme bado yako gizani. Kwa mfano, mauaji ya Akwilina, Lwajabe, miili iliyookotwa kwenye viroba, kupotea kwa Azori, Ben Saanane, risasi za Lissu, kutekwa kwa Mo, Roma, Magoti, wizi wa uchaguzi 2019, 2020. kuzima vyombo vya habari, vyama vya upinzani, ukwapuaji wa fedha za watu benki, bureau de change, n.k. Na majuzi Rais wa sasa kaongezea ufisadi kwenye pesa za "plea bargain" zisizojulikana zilipo.

Yote hayo bado yako gizani. Serikali ya CCM bado haionyeshi utashi wa kuleta CLOSURE kwenye kadhia hizi.

Lazima mkondo wa sheria ufanye kazi, ukweli ujulikane, hukumu sahihi itolewe (hata posthumously ikibidi) na hatua zichukuliwe kwa wahusika waliopo. MUHIMU ZAIDI kwa amani na utulivu wa nchi ni vyema kuwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa (truth and reconcilliation process). Hiyo ndiyo namna bora ya kupata CLOSURE. Maridhiano yanayoendelea ni hatua nzuri lakini haitoshi. Kinachosikitisha sana ni kwamba miaka ya karibuni serikali ya CCM imezidi kuendesha propaganda hatarishi za kuwagawa wananchi.

Kwa wale watakaodai hata awamu zilizopita zina matatizo ya aina hiyo wako sawa ingawa ni wazi kuwa Rais wa awamu ya tano aliyafikisha kwenye kiwango cha kutisha. Yaliyotokea kwa Mwangosi, Zona, Ulimboka na Kibanda awamu ya nne nayo bado "yananing'inia". Hayajapata CLOSURE. Ni doa kubwa kwa serikali ya CCM. Wahenga hawakukosea waliposema "damu ya mtu haipotei bure". Yote haya yataendelea kulitesa taifa kwa miaka mingi ijayo.

Walio na shauku kubwa kutaka Magufuli asisemwe au asitajwe basi waiombe serikali yao ya CCM ichukue hatua kuleta CLOSURE na UTANGAMANO kwa wananchi wote nchini. NA pia wajue wakianzisha mada za kumsifu Magufuli katika mazingira haya ambapo kadhia nyingi za utawla wake hajipata CLOSURE basi wasishangae kujibiwa na wenye kero zao. Waingereza wanaita kujibiwa "in kind".
wanaoweza kukuelewa ni wachahe kwa andiko zuri la weledi kama hili! Fikiria mke wa Ben anajisikije , wazazi wa Ben, and many many others who their loved ones disappeared during Magufuli's era!
 
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
Uovu gani aliufanya magufuli kushinda viongozi waliotangulia?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Shetani Hadi kesho anatajwa, se mbuse jombii.
 
Sawa, wewe endelea kulialia kama juha uone kama kunakitakacho badilika.
Magufuli alisha waumbua wajombazenu walamba asali na wapinzani wachumia tumbo, akikuambia hataki ujinga kwenye rasilimali za nchi he was not joking.

Mnajitia mastress ya kijinga bila kujua.
Wengine mnatumwatu,mjitoe akili 24/7 muwe mna pambana na Marehemu.

Saazingine muwe mnawalaumu wazaziwenu kwa kuzembea kuwapeleka shule,maisha hayana short cut, cheti feki unajuwa ninacho maanisha.
Sawa, pesa za Plea bargain ziko wapi?
 

Attachments

  • IMG-20230208-WA0035.jpg
    IMG-20230208-WA0035.jpg
    39.1 KB · Views: 1
Kikubwa mwanadamu yoyote hupaswi kuwa mwovu na usijiinue sana hadi kujifananisha na malaika na kujiuona hukosei, Magufuli alipitiliza kujiona yeye ni yeye na hakuna kama yeye.

Yule mzee alilewa madaraka sana!
 
Anayetaka udhalimu wa Magufuli usisemwe anataka kufunika uvundo ili na wengine nao wakifanya uvundo utataka tuwafichie aibu ya uvundo wao pindi wakifa. Hatuwezi kujenga nchi ya kulindalinda uovu
 
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
We gasho kweli!

Vipi familia ya Mwangosi yenyewe inajisikiaje?

Vipi familia za wale watu 5 waliouwa na bomu la mkono kule kwenye mkutano wa machadema kule soweto arusha wao wanajisikia raha sana ee?

Vipi familia ya Ulimboka wanajisikia raha sana maana walitawaliwa na mwanademcrasia eti?

Kichwa hicho kiwe na ubongo siyo mavi
 
Hili linasababishwa na maumivu au majeraha ya ndani na kushindwa kusamehe na kuachilia kabisa, kumbuka unayemtaja kwa mabaya hakusikii, wewe ndio unaendelea kuteseka kwa sabb ya kumbeba mtu Moyoni mwako. Jifunze tu kusamehe ili maisha mengine yaendelee
 
Ukitoka pangoni ukisema alafu inakua nn?? Wewe ni mjinga mkubwa
Matola na tindo wao hata waume zao wakishindwa kusimamaisha ili wawapande humsingizia Magufuli!

Tindo yeye stress anadai kwamba Magu alimfanyia ukatili mkubwa.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Huwezi kumtenganisha mtu na matendo yake.
Kuna manabii wa Mungu walishafariki maelfu ya miaka nyuma, lakini bado wanatajwa na matendo yao, mazuri na mabaya
Ndio nimekwambia hata Nyerere huwa anatajwa sana ila sio kwa aina ile aliyomzungumzia Tundu Lissu bungeni ikazua maneno, sasa huwezi kumtenganisha mtu na matendo yake basi tungekuwa tunamzungumzia Nyerere hadi leo kwa mabaya yake kama alivyoyaelezea Lissu lakini mbona haipo hivyo?
 
Ndio nimekwambia hata Nyerere huwa anatajwa sana ila sio kwa aina ile aliyomzungumzia Tundu Lissu bungeni ikazua maneno, sasa huwezi kumtenganisha mtu na matendo yake basi tungekuwa tunamzungumzia Nyerere hadi leo kwa mabaya yake kama alivyoyaelezea Lissu lakini mbona haipo hivyo?
Kwa Nyerere, mazuri yake ni mengi kuliko mabaya..
Kwa jiwe ni kinyume chake!
 
Awazaungumzie hao wabaya walioko hai kimpango wake, kama vipi na ww msaidie kwenye hilo. Sisi tuko na dhalimu magu.
Usipanic hapa tunajadiliana kwa hoja tu wala usifikiri kuna mtu atakulazimisha kitu, mwisho wa siku ni uamuzi wako hata ukiamua utembee uchi barabarani na kusema ni kwa sababu ya kumlaani Magufuli hiyo ni wewe ila sie tutasema umechanganyikiwa kwa sababu hoja yako ya kukufanya utembee uchi ya kipuuzi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom