Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Mimi siwezi kuwa chawa Mkuu.

Najua wapo ambao wanamakovu ya milele lakini lazima wasamehe kwani Mungu ndiye mjuzi WA yote, tena aliwasaidia kuwalipia kisasi.
Au walitakaje zaidi

Huwezi kumlazimisha mtu kusamehe, specially kama hayakuhusu. Maumivu ni yao, maamuzi ni yao.
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.
Historia haifutiki. Maisha aliyoishi ni kitabu amekiandika hivyo lazima kisomwe kama alivyokiandika mwenyewe na ni ujinga kuwapangia wasomaji kurasa za kukisoma kitabu hicho.
 
Kumtaja JPM kwa mabaya ni kuwakwaruza Watanzania walio wengi kwenye mshono. Muacheni apumzike kwa amani mwamba wetu.
 
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
Unataka kusema Duniani huko wanamtambua kwamba Tanzania iliwahi na kiongozi muovu na kwamba huyo kiongozi anaingia kwenye list ya vuongozi waovu duniani?
 
Ttzo wafuasi wa marehemu mnatabia km za marehemu ,
Mnatak watu wote wamseme vizuri marehemu wakat kla mtu anauhuru wa kuongea na kusema vle anataka

Marehemu alikua Mwizi jambazi kibaka dikteta killer na wafuasi wake wengi izo ndo tabia zenu pia mnatetea mateso aliyosababishia watanzania wenzenu

Mkimtukuza nyie uyo mungu mtu wenu inatosha why mnakua na tabia za kishoga kutaka kla mtu ausifie na kuutukuza ushoga wakat wengne sio mashoga
 
Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa
Kwa hiyo yeye ndio alie piga risasi,yeye ndio aliewateka hao ulio waoanisha hapo juu,kwani wangapi walitekwa na wakapatikana,haya ikatokea taarifa kwamba hao waliotekwa yaweza ikawa ni wao kwa wao waliofanyiana unyama huu,au huyo aliepigwa risasi kapigwa na watu wake wa karibu kutokana na maslahi baina yao wao kwa wao,jee familia ngapi zenyewe kwa zenyewe zinauana kwa njia mbali mbali sembuse kwenye vyama?

Haya wangapi wanafaidika na barabara ya morogoro road jee inawasaidia wagonjwa wangapi kuokolewa maisha yao kutokana na kuwa na miundo mbinu rafiki,jee hao wakazi waliokuwa wanaishi maeneo ya kimara tokea kuundwa kwa Tanzania hawakuwahi kulipwa stahiki zao kabla,jee wana uhakika walipo kuja nunua maeneo hao walio wauzia wao hawakulipwa kabla?
 
Kama shetani anatajwa na dini zote kwanini Magufuli asitajwe kwa aliyo yatenda.? Mwinyi alisema maisha ya mwanadamu ni hadithi tu. Magufuli kosa lake alijiona Mungu mtu na ni yeye pekee ndiye mwadilifu na wengine wote ni wezi tu.
Shetani yupo hai na anatajwa kwa sababu anashawishi watu maovu hivyo bado anatenda hazungumziwi kama habari ambayo imeshapita.
 
Usitushangae Mkuu,

Uwezo wetu ndo umeishia hapo. Hushangai mpaka Leo tunalaumu ukoloni hata baada ya miaka 60 ya uhuru. Hatufiki mbali kwa sababu Kila muda tunaangalia nyuma kutafuta wa kumlaumu badala ya ubunifu wa kupambana kutatua changamoto zinazotukabili.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom