Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama Vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)
Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.
Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!
Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-
1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa(LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.
Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?
Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.
Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Matekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki
Je nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?
Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?
Nipe mfano wa nchi yenye demokrasia ya kweli duniani.
Ninacho jua mimi nchi zote ulimwenguni zilizojaribu kuwa na demokrasia ya kweli ziliangamia. Wagiriki walianziasha demokrasia wakaangamia na warum nao vilevile walikwenda chini. Wengine wanao fuata ni waingereza na baadae watakuja waamerika. Si mnaona mambo yanayotokea huko? Ninkichekesho kweli. Eti nyie ndiyo wa kufanganywa kuwa demokrasia ya kweli iko Amerika. Amerika? "Da lachen sogar die Hühner(hata kuku wanacheka)!"
Wachina na waarabu ndiyo watao-dominate ulimwengu. Mtake msitake.
Ujerumani kwa mfano hivi sasa imesha chukuliwa na waturuki. Rais wa Utruki Erdogan ndiye mwenye kupeleka commands Ujerumani na wafuasi wake wanaitikia.
Wajerumani hata wafanye nini, hawawezi kuwazuia na kuwafukuza.
Na nataka tu mtambue waturuki nao wanazaana ile mbaya kama sisi, kiasi kwamba miaka 50 tu ijayo asilimia kubwa ya wajerumani watakuwa wenye asili ya kituruki.
Mfano ni huu hapa; hawa researchers wawili wa Covid-19 Vaccine ni mke na mme. Ni wajerumanu wenye asili ya kituruki. Hivyo mjionee wenyewe ulimwengu unako kwenda
Biontech and Pfizer have announced that they are on the brink of emergency-use approval for a coronavirus vaccine. The scientists responsible, Ugur Sahin and Özlem Türeci, are from Germany.
amp.dw.com
Hi ni picha moja wapo ya kuwaonyesha nyie walilia demokrasia na haki za bidam kuwa kwenye viwanda vikubwa vya magari na mashine huko ujerumani asilimia kubwa ya wafanyakazi na hata mabosi ni waturuki. Nyie endeleeni kulala na ku-dream demokrasia, mkitegemea kila kitu kitaletwa kenyewe. Nendeni nje mkauangalie ulimwengu sio kukaa kaa Tanzania tu na kulilia vitu msivyo vijua asili yake.
Askofu Gwajima alikwisha waeleza ulimwengu unako kwenda na watu wasio ujua ulimwengu vizuri kwa ujinga wao walimkebei sana. Hapa nawaambia kitu kimoja kuwa huyu Askofu ni mtu anaye ona mbali sana. Anapo piga Safari zake za nje na kuongea na watu, nin mtu anaye yachunguza sana mazingira. Na mimi ninampa right.
Nyie vijana wa leo endeleeni tu na mambo ya kupenda kuiga maneno na vitendo vya watu wengine bila kujiuliza, kwanini?. Tumieni common sense yenu kusoma nyakati! Mtauzwa mchana kweupe!
Demokrasia wanayo taka kutujaza sisi ni demokrasia ya kutuibia rasilimali zetu na sio kingine.