Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa baadhi ya upinzani ni mkakati wa CCM kupunguza idadi ya kura za Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa baadhi ya upinzani ni mkakati wa CCM kupunguza idadi ya kura za Tundu Lissu

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wanajamvi.

Tukijaribu kwa kina kutafakari njama kuu ya kuengua wagombea wa ubunge wa majimbo yaliyo mengi ni moja ya mkakati wa kuhakikisha unalenga kupunguza idadi ya kura atakazo pata Tundu Lissu. CCM wamegundua kuwa idadi ya wapiga kura walio wengi watakaokwenda kwenye sanduku la kura, wataenda kupigia kura kwa kuhamasishwa zaidi na mbunge wa eneo lake, hamasa ya pili ni kumpigia kura Rais.

Wengi tunaamini kwamba hamasa ya kwenda kupiga kura inachochewa na kumuwezesha mbunge wa eneo lako kuweza kupita/kushinda kwa sababu ni mtu anayegusa maisha yako kwa ukaribu sana. Baada ya hapo kipaumbele namba mbili ni kuhakikisha Rais anapigiwa kura. Hivyo basi kwa namna moja CCM wameshinda katika nyanja hiyo kwa sababu hata Upinzano unaonekana hauna mkakati wowote uliopo kupambana na njama za uenguaji.

Tukumbuke kuwa Idadi kubwa ya wabunge wa CCM katika biunge lijalo itawasaidia kupitisha na kubadilisha katiba itakayo muweka madarakani Rais Magufuli kwa Muhula mwingine wa Tatu kwa visingizio kuwa anastahili kwa yale aliyo yafanya.

"Imbombo Jilipo Mwaka Huu"
 
Vita ipo kote ndani na nje. Ndani kuna mamluki walioongwa kufanya hujuma, na nje wanahakikiaha wana demoralize morali ya wanamageuzi kushiriki uchaguzi.

Morali ilikuwa juu wakati wa utafutaji wadhamini, sasa imeshuka sana. Hizo ni techniques za CCM, kupiga ndani na nje.

Mwaka huu hata wale Chadema damu, wanyongee, muangalie mwenyekiti, utadhani hayupo.

Anyway ni mawazo yangu.
 
Huu ni woga sijui unatoka wapi hawakuhitajika kuengua watu bila sababu huku ni kudhalilisha serikali yetu na chama tawala.
 
Kama ni mkakati basi ni namna ya kujaza form kwa umakini pia kuhakikisha mgombea anajua kusoma na kuandika vizuri wengi wa wagombea hata kusoma hawajui!
 
CCM wana mikakati mizito sana kwa ajili ya kupata ushindi.

Kwanza kupora watu fomu ili wasirejeshe na kupata ushindi wa mezani,

Pili kuteka watu ili siku ya kurejesha fomu wasiweze kuzirejesha na hivyo wapite bila kupingwa.

Tatu,kuwapiga wapinzani wao mapanga ili siku ya kurejesha fomu wawe wamelazwa wakiuguza majereha

Nne kuwakamata kwa kutumia polisi na kuwafungulia kesi za uwongo ili wakose muda wa kurejesha fomu,

Tano,wakurugenzi kukataa kupokea fomu,ama kuziharibu ili zionekane zimekosewa ili watoe ushindi wa Chee kwa mtu wao nk.

Chama kikubwa kama CCM, chama ambacho kimefanya mambo mengi kwa kujenga nchi, mf kujenga reli, madaraja, umeme wa SGR nk hawawezi kufanya ujinga wanaofanya kwani utawafanya mgombea wao adhaulike kwa wananchi, wajikite na kujenga hoja, wawajibu wapinzani wao kwa hoja, wanaogopa nini?
 
kinachotafutwa ni 2/3 tu iliwaweze kubadili katiba peke yao, hasa 2/3 ya Zanzibar , mkakati bado unaendelea wa kuongezewa muda kwa mkulu.
 
Kama ni mkakati basi ni namna ya kujaza form kwa umakini pia kuhakikisha mgombea anajua kusoma na kuandika vizuri wengi wa wagombea hata kusoma hawajui!
Mwenye update hadi sasa rufaa za walioenguliwa status ikoje. Je waliorudishwa kugombea baada ya kukatwa ni wakina nani na majimbo yapi?

Hivi vyama wafanye iwe marufuku mgombea kujaza fomy peke yake. Fomu zijazwe kwa pamoja tena mbele ya mwanasheria ili kudhibiti hujuma ya ndani miongoni mwao.
 
Wapinzani wasipo-mobilize ili wagombea wao walioenguliwa kurudishwa basi tutegemee hali ya vyama pinzani kujifia kabisa natural death kufikia 2025......
 
Upinzania ulishakufa kwani nyie hamkusikia kama ccm imetumia technics hii na nyie mmetumia ipi? Au mlifikiri mtapewa tuu...........ufalme wa mungu tuu unatekwa na wenye nguvu
 
Makamanda mabakuli yatapita huko mlipo msituangushe makamanda.
Na kuhusu zile 6bn michango ya wabunge wa CDM, Mwenyekiti wetu Mbowe amesema hata yeye hajui zilipo hizo fedha.
Msisahau kutuma picha za mabakuli ili kuhamasisha makamanda wengine wachangie pia.
😁 😁 😁
 
Back
Top Bottom