Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa wagombea: Pemba wahimizana kuandika usia kabisa maana sasa wako tayari kwa lolote

Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa wagombea: Pemba wahimizana kuandika usia kabisa maana sasa wako tayari kwa lolote

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Katika hali inayoashiria uwezekano wa umwagaji mkubwa wa damu huko Zanzibar hasa kisiwani pemba, wananchi wa huko wakiwa na hasira kali kutokana na kuenguliwa wagombea wao, wamejiapiza kukabiliana na chochote kilicho mbele yao hata ikibidi kupoteza maisha yao.

Wamehimizana kila mmoja kuandika usia kabisa kwa sababu chochote kinaweza kutokea.

Kwa kweli kama Taifa hatukupaswa kufika hapa, Wazanzibar wamevumilia mengi, wamevumilia ishu ya uchaguzi wa mwaka 2015, wakavumilia kuingiliwa na kuvurugwa chama chao kikuu cha CUF, sasa leo kweli wavumilie kweli kunyimwa chaguo la kumchagua mtu wamtakaye? —aaah wakubwa, oneni aibu

Lakini Kama wananchi wakimwaga damu zao kwa sababu ya michezomichezo hii ya kunyima haki wananchi, Tume ya Uchaguzi NEC na watawala, hawatakwepa lawama, damu za wananchi wasio na hatia zitakuwa mikononi mwao.

Hapa chini ni video ikionyesha wananchi wakijiapiza kwa lolote!

 
Kipindi Serikali inasisitiza amani, naomba ikumbuke kusisitiza pia haki, halikadhalika jeshi la polisi na tume ya uchaguzi, mnasisitiza amani itawale katika nchi yetu lakini mnasahau kusisitiza pia haki itawale, haya yanayoenda kutokea pemba kiukweli Mwenyezimungu atuepushe viongozi mliopewa dhamana ya kutuongoza mkumbuke wajibu wenu nikutenda haki, kisha amani itatamalaki yenyewe bila hata kuisisitiza.

Angalia video ,ndipo tulipofika huku.


 
Hili ndilo hutasikia toka CCM, NEC, Wakurugenzi, viongozi wa dini, TBC... Utasikia tu amani. Hakuna kuongelea haki! Yaani hata wagombea wako wote wakikatwa, kubali ili kuwe na amani!
Hapo ndio unafiki ulipo, tunaomba watendewe haki nduguzetu Wazanzibar warudishiwe viongozi wao, kam kukataliwa basi watakataliwa kwenye sanduku lakura
 
Alidhani akinunua mindege ambayo sasa inapigwa vumbi na kuingiza hasara kubwa kwa Taifa na kufanya miradi kama bado yuko Ujenzi basi itatosha kumpa ushindi wa TSUNAMI. Sasa kagundua hapendwi hata chembe na uchaguzi huru hachomoki atapigwa chini asubuhi subuhi hivyo kaamua kufanya uhuni mapema kabisa wa kuengua wagombea wa Vyama vingine kihuni, kugomea kuwepo na Tume Huru ili kutimiza uhuni na ujambazi wake wa kuendelea kubaki madarakani kupitia mtutu wa bunduki hali kadhalika kule Zenj maccm hayapendwi hivyo yameamua kule nako yaengue wagombea na mtutu kutumika tena kama 2015, 2010, 2000 na 1995 kung'ang'ania madaraka kimabavu. Nina wasiwasi mwaka huu kutatokea mauaji makubwa sana na ya kutisha.
 
Ili mradi huo ushenzi, udhalimu na uhuni wa kisiasa unataka kupingwa kwa nguvu zote huko Znz, sina shaka hilo litatokea manake Zanzibar, hususani Pemba sio wanafiki kama watu wa Bara.

Na hakika hakuna kiongozi mpumbavu kwa nchi kama Tanzania kama yule anayejaribu kutaka kuvuruga siasa za Pemba kwa sababu kila mwenye akili timamu nchi hii anafahamu Wapemba huwa hawataki ungese wa aina yoyote!

Sie wengine tumeshaishi sana na Wapemba huku tukiwaita Wakojan, hawa jamaa hawaogopi kitu! Kwanza Mpemba aliye mathalani Arusha, wala haoni taabu kubeba begi lake kwenda Pemba au Unguja kwa ajili tu ya kwenda kupiga kura!! Hakuna kiumbe wa jamii nyingine kwenye Jamhuri ya Muungano anayeweza kufanya hivyo ukimtoa Mpemba!

Na kingine ninachowapendea Wapemba, ule ujinga wa "sasa ni mtu wa nyumbani" kama tulio nao Bara wao hawana! Sitawasahau watu wa Kanda ya Ziwa, hususani baadhi ya Wasukuma walivyoisaliti CHADEMA mwaka 2015 kwa sababu tu CCM walimweka Msukuma mwenzao!

Pale Zanzibar CCM wakimweka hata Mpemba; Wapemba watamkataa tu kwa sababu wasichotaka Wapemba ni takataka yoyote kutoka CCM!!

Sasa kujaribu ku-mess na watu wa aina hiyo ni kutaka kujaribu kuliangiza taifa kwenye machafuko!

Majahili ya CCM badala ya kutumia njia za kifedhuli wanatakiwa wakae watafakari kwanini takataka yoyote yenye elements za Bara haitakiwi kwenye siasa za Pemba! Na wakumbuke, kule Pemba CCM walianza kukataliwa hadi Babu zao wa ASP!
 
Huko lazima kinuke ila kwa hofu, wanaweza kurudisha walioenguliwa.

Safari hii itakuwa ni zaidi ya yaliyotokea 2001.

Kinachokera ni hawa watu kufanya uhuni na hujuma za wazi kabisa alafu bado wanawaletea watu Kejeli,dharau na kiburi kisa tu ulevi unaotakana na madaraka na kujisahau.

Chochote kitachotokea Zanzibar kitakuwa na athari kisiasa na huku Bara maana foul zinazofanywa huko ni sawa na yanayoendelea huku Bara.

Ngoja tuone jueri yao itaishia wapi.
 
Ili mradi huo ushenzi, udhalimu na uhuni wa kisiasa unataka kupingwa kwa nguvu zote huko Znz, sina shaka hilo litatokea manake Zanzibar, hususani Pemba sio wanafiki kama watu wa Bara
Nafaham kiapo cha raisi nipamoja nakulinda mapinduzi ya Zanzibar, lakini sio kulinda kwa kumwaga damu zawatu wanaohitaji haki itendeke, kiukweli nashindwa kuelewa wenye madaraka kwa nini wasiongoze kwa haki tu?.
 
Huko lazima kinuke!

Hayati Mkapa alijuta mpaka siku anaondoka duniani kumwagika kwa damu ya wazanzibar mwaka 2001. Alijitahidi sana kadri ya ushawishi wake kuwaasa viongozi waliokuja baadae waiangalie Zanzibar kwa jicho la umakini maana uonevu kwa wale watu unaweza pelekea hata hao watu kuukataa muungano wenyewe, ikifikia hatua ya wao kuukataa muungano hata upeleke majeshi milioni utaishia kumwaga damu zaidi tu lakini kamwe hutopata ridhaa yao!.
Kama kuna watu wenye akili na wanatafakari waufanyie kazi ushauri ule wa Mkapa la sivyo nao wataburuzwa ICC kwa umwagaji wa damu za wananchi!
 
Back
Top Bottom