Mashujaa wa nyuma ya keyboard
Wewe unajivunia SMG iliyonunuliwa kwa Kodi za haohao unaowadhihaki,unajivunia magwanda,mabuti na mkanda ulionunuliwa na Kodi za hao unaowadhihaki,hata hayo mafunzo uliyonayo Ni Kodi zao,mshahara unaolipwa Ni Kodi zao.
Inawezekana Ni wewe peke yako kwenye ukoo wenu tu ndio una ajira ya Jeshi.
Waonee huruma ndugu zako ambao hawana neema uliyonayo.Acha ubinafsi.
Hawa unaowadharau wanaweza wakakuweka bize wewe na ukasahau na IST yako.
Wakianza kuandamana kudai Hali yao,itabidi wewe uache starehe zako zote za Sasa hivi uende na SMG yako kuwaua.
Unajua kitakachofuata.?
Najua kwa chuki uliyonayo juu Yao utawaua makumi kwa mamia,baada ya hapo unajua kitakachofuata?
Kama umeenda kulinda amani nchi nyingine,unafikiri watumishi Kama wewe kutoka mataifa mengine hawata kuja kulinda amani hapa kwetu?
Nakusihi Sana wa poti wangu usisgemee upande wa dhuruma.
Ulipaswa kukerwa na dhuruma wanazofanyiwa Hawa unawaowadhihaki.
Usiwe mtumwa wa wadhalimu.kumbuka kuna maisha nje ya kazi unyojivunia.
Wewe kwa Raha ulizonazo Leo hiihujafikia hata 1/100 ya Raha alizokua nazo Mkapa.
Mkapa alikuja kujuta juu ya aliyowafanyia hao wapemba na wapinzani kwa ujumla.
Kitabu alichoandika Ni kutubu dhambi zake,Hadi akatamani wapinzani wawe wanashirikishwa kwenye kuhesabu kura.
Sasa Kama Mkapa mtua ambae alikua analindwa na walinzi kila engo anajutia matendo yake,vipi wewe mlinzi usie na hata mlinzi japo nje ya mlango wa nyumbani kwako?
Hiyo kazi uliyonayo isikuondolee utu na kudhani watu wasio na kazi Kama yako hawana Haki ya kuishi kwa sababu tu wamechangia kununua SMG ya serikali kwa Kodi zao ambayo wewe umekabidhiwa ili kuwalinda na leo badala ya kuwalinda unawadhihaki.
Hubiri Hali ndugu,kwa sababu Haki italeta amani,na amani it kufanya wewe uifurahie kazi yako.