Kuepuka Radi kwa kufuga Kondoo

Kuepuka Radi kwa kufuga Kondoo

Status
Not open for further replies.
yes mkuu, ni vigumu pia kwa great thinker kuamini kwamba mtu anaweza kupigwa radi wakati wa jua kali bila wingu hata moja.
Mkuu FUSO umenikumbusha back to 1990's nilikuwa naishi Morogoro,Radi ilipiga mida ya saa 9 mchana kulikuwa hakuna wingu hata moja tulichoshuhudia ni mnazi kukatika katikati na matawi yake kuungua to ashes.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu bona nashukuru kuwa na wewe umemsoma huyo mwana JF mwenzetu alivyo na kashfa za kishamba!

Sasa bona anasema mimi nina matusi!
Wewe unasema nina kashfa za kishamba.!!
Duhh nibebe lipi??
 
Last edited by a moderator:
sidhani kama ni kweli , unajua kondoo huwa hapendi mvua impige usoni na ndiyo maana anaainamisha kichwa chini , na pindi anaposikia kitu cha kumshtua aidha mwanga au mlio huwa ana mtindo wa ku react na kusogea mbele , sasa in local belief wanadai ame fight na radi kumbe hamna lolote zaidi ya mawenge tu ya kondoo

Umakondeni na kufuga kondoo wapi na wapi? Unajua panya tuu wewe......
 
Wanyama wana uwezo mkubwa wa ku-sense natural disasters.Kukiwa na radi inataka kupiga eneo kondoo huanza kubadilika tabia akienda huko na huko kwa hasira ya mapigano mara ingine kugonga miti.ukiona yuko hivyo radi inataka kupiga eneo hilo usikae chini ya mti wowote kukokoa maisha yako na kama uko karibu na daraja kaa mbali nalo. Wachungaji wa mifugo kondoo kawasaidia mara nyingi kujua ujio wa radi na namna ya kujiokoa.

Wakati wa Elnino kabla haijatua kule Asia wanyama kama nyoka,mbwa na paka na wanyama wa mwituni walianza safari ya kutoroka kutoka maeneo tambarare na na kuanza kuhamia milimani ilikuwa ni mass exodus ya wanyama ambayo watu waliona tu kama kituko cha wanyama wakieelekea kwenye miinuko lakini watu hawakujali kuwa ni kwa nini wamekuwa hivyo.Elnino iliposhuka watu wengi walikufa .Watu wangewahi kufuatana na wanyama pengine vifo vingepungua.

Kukiwa na nyoka mfano hatari mahali mbwa ana uwezo wa ku-sense na kubadilisha tabia na mlio na wanyama kama ng`ombe kukiwa na kitu fulani hatari jirani kikubwa hunyanyua mikia juu na kuruka kwa nguvu kwa hasira.Ukiona hivyo mwenye mifugo unatoka na silaha tayari kwa mapambano.

Kondoo ni mnyama atumikaye kwa matambiko na makafara kwa dini zote na washirikina pia.Kwa sababu za miiko kuna mambo siwezi kueleza uwezo mwingine kondoo alionao na anavyotumika ila ninachoweza kusema ni kuwa radi haiwezi piga kondoo milele.Kondoo hapigwi na radi hata siku moja.Radi ni mtoto mdogo kwenye kichwa cha kondoo.

umeeleza vizuri ila umeharibu hapo mwishoni ati kondoo anatumika na dini zote kwa matambiko, tangu nakua sijawahi kuona au kusikia kanisa linafanya tambiko la aina yoyote. Mfano ulioutoa wa tsunami nimeusikia mara kadhaa, ni kweli wanyama wanauwezo wa ku sense imminent of danger na ku react as well
 
Honestly,hata mm nmewah kuckia hlo inaweza ikawa kweli ni kweli radi inavyokuwa inapiga wale kondoo wanarudi kinyumenyume
inaweza ikawa
Ebu fafanua kidogo...yaani, mfano, radi ikipiga mashariki wakati wao(kondoo wameangalia mashariki) watarudi kinyumenyume kuelekea magharibi; au hata ikipiga magharibi wao wakiwa wameangalia mashariki watarudi kinyumenyume kuelekea magharibi au watageuka kuangalia magharibi na kuanza kurudi kinyume nyume kuelekea mashariki...?
 
.....

"A horse can get zapped by less than 2,000 volts and will almost never try the fence again, whether it’s turned on or not. 2,500 volts will easily turn a cow but you better have a good 4,500 volts to even get a sheep’s attention"

This sound a little bit scientific and I have managed to get the source of your information. Source>>>sheep magazine | breeding and raising sheep | sheep business


Lakini Swali la msingi linabaki pale pale, Kondoo anazuiaje Radi ukizingatia Radi uhusisha mamia elfu ya Kilovolts inapopiga?
 
hakuna ukweli wowote hapo ,nimeona watu waliofuga kondoo na kushuhudia banda walilolala kondoo limepigwa na radi nyang'anyang'a.
Ukitoa uthibitisho wa hili inasaidia sana kuipa nguvu sitahiki hoja yako. Mfano ungeweza kutueleza tukio hili lilitokea wapi na lini ili nasi tukafanye udadisi zaidi juu ya hili.
 
....... Baadaye kidogo nilipoondoka mazingira hayo kwa mbali zilitokea sauti kuubwa zilizoambatana na miale ya radi Ambapo mti uliokuwepo eneo karibu na kondoo yule ulichanwachanwa vipande vipande lakini kondoo hakupata jeraha na alirejea mwenyewe baada ya muda mrefu tangu mvua kwisha.......

Hapa mkuu umetupa kitu kutoka "field". tukipata michango kama hii tutaujua ukweli kuhusu uwezo wa kondoo kuzuia Radi.

Lakini kwenye maelezo yako niliyonukuu hapo juu, bado nina mashaka kama kweli wakati Radi inachanacha mti ule kondoo alikuwa palepale kwenye mti. Ikizingatiwa, kwa mujibu ya maelezo yako, wewe binafsi uliswaga mifugo mingine kutoka maeneo yale.

Halafu nina swali moja hivi kwenye mifugo yako siku ya tukio ulikuwa na kondoo mmoja tu?
 
Badala ya kutumia Lightning Conductor kuna umuhimu wa kutumia kondooo sasa
Kwa jinsi mada ilivyokaa (zuia radi)...inabidi kutumia Kondoo kama Lightining Insulator...hapa ni mefanya utani(I am, purely, joking)
 
ndugu tukio hili limetokea nikiwa mdogo wakati nimeenda kumsalimia bibi yangu, siku hiyo watoto wa jirani walikuwa manalala sebuleni chini wanatandika jamvi ila siku hiyo kama MUngu aliwaotesha ,watoto wakaambiwa wakalae kwenye geto la kaka yao ,pale wakalala mbuzi na kondoo siunajua wafugaji ,Usiku ikashuka mvua ya kutosha na radi ambapo mbuzi na kondoo wengi walikufa kwa hiyo radi.Amini usiwe kama TOMASO wa Biblia.
Ukitoa uthibitisho wa hili inasaidia sana kuipa nguvu sitahiki hoja yako. Mfano ungeweza kutueleza tukio hili lilitokea wapi na lini ili nasi tukafanye udadisi zaidi juu ya hili.
 
Mbona kijijini kwetu mvua ikiwa kubwa sana tena ya kuambatana na radi, wanachofanya ni kuchukua chupa yenye konyagi ndani yake na inawekwa mlangon. hakna cha radi wala nini.
Waweza kutuelekeza ni wapi inafanyika hii kitu ?
 
Wote nyie hakuna hata mmoja aliyeishi na kuchunga mifugo - Ukiwa kwenye machunga then mvua kubwa ya radi ikaanza kunyesha hapo ndipo utajua rule ya Kondoo ukitofautisha na mbuzi, ngombe na mbwa!!

Tunahitaji ufafanuzi..mkuu juu ya hili, has hapo kwenye 'rule' ya kondoo, mbuzi na ng'ombe na mbwa wakati wa mvua.
 
ndugu tukio hili limetokea nikiwa mdogo wakati nimeenda kumsalimia bibi yangu, siku hiyo watoto wa jirani walikuwa manalala sebuleni chini wanatandika jamvi ila siku hiyo kama MUngu aliwaotesha ,watoto wakaambiwa wakalae kwenye geto la kaka yao ,pale wakalala mbuzi na kondoo siunajua wafugaji ,Usiku ikashuka mvua ya kutosha na radi ambapo mbuvi na kondoo wengi walikufa kwa hiyo radi......
Ahsante kwa maelezo haya.... kiasi sasa tumepata mwanga wa kilichotokea.
Kwa vyovyote, nadhani,mifugo hiyo ilifungiwa hapo hapo sebuleni. Na hii (kama kweli walikuwa wamefugiwa kiasi wasingeza kutoka hapo sebuleni) inanisaidia kulitafakari kwa kina suala la Mlendamboga juu ya kondoo wake kunusurika radi iliyochanana chana mti.
 
Last edited by a moderator:
Naam niliiona hiyo kitu Shinyanga vijijini. Kwamba radi huja kama jogoo, na inapokutana na kondoo hupigana sana na mara nyingi radi hushindwa.
Mkuu RADI ni umeme unaotokana/generated na msuguano wa mawingu, sasa jogoo anatoka wapi! Adithi kama hizo niliwahi kuzisikia kijijini kwetu nilipo kuwa mdogo - mimi nafikiri radi kabla haija strike aridhi kuna mini-branches zinazo tokana na main lightnig bolt ambazo umeme wake ni mdogo i.e hauwezi kuua binadamu, sasa umeme huo ukipitia kichwani/ubongo kwenda aridhini basi unaweza kumfanya binadamu aone illusion ya mfano wa JOGOO i.e light current ya umeme wa radi kupitia kwenye ubongo unamfanya apate hallucination ya muda na kudhani alimuona Jogoo kweli. Mimi nina mfano hai lakini sio wa kuona Jogoo, Mkoa wa Kagera una incidents nyingi za kupigwa radi hasa hasa vitongoji vilivyo karibu na ziwa Victoria, siku moja nikiwa darasa la kwanza tukiwa darasani radi ilipiga karibu sana na shule, baadhi ya wanafunzi akiwemo mimi mwenyewe tulihisi kitu kama chumvi mdomoni!! Nafikiri kitu kilicho tuhokoa ni a lightnig arrestor iliyo kuwa imewekwa kwenye paa la shule kwa miaka mingi, bila ya kizuhizi hicho cha radi sina shaka siku hiyo tungepigwa radi - kwa nini nina hakika kuwa taste ya chumvi ilitokana na umeme mdogo wa radi, siku moja chukua betri mpya ya tochi weka kidole kwenye base (-ve) yake alafu tumia ncha ya ulimi wako iguse +ve side ya betri - kama betri ni mpya basi taste yake inakuwa ni ya chumvi chumvi, kama betri hiko completely discharged hutahisi chochote. Siku ya tukio la radi shuleni nilipata taste ya chumvi kinywani mwangu, kwa hiyo tusione ajabu sana watu wengine wanapo pata illusion tofauti mfano - kuona Jogoo sijui mweupe au mwekundu!
 
Wakati naishi kijijini tulikuwa tunaambiwa radi huja kwa kupitia maskioni na puani.

Kujikinga na radi mvua ikianza tu, tunaambiwa kukaa chini na kuziba maskio, hadi leo nimeathirika, haijalishi najua vingapi ila mvua ikinyesha ya radi sipendi kusimama simama, nataka nikae chini au kulala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom