Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
1,932
Reaction score
4,403
Mpaka 2015 private sectors zilikuwa zinashamiri. Jakaya aliacha mazingira mazuri na bora kabisa kwa sekta binafsi kukua na kuboreka. Ila tokea 2016 makampuni ambayo idadi yake haijulikani yamefungwa katika nchi hii, na bado yanaendelea kufungwa. Vijana lukuki wamepoteza ajira katika makampuni hayo.... na wale ambao walijiajiri kwa kufungua makampuni kwa sasa wanalia kilio cha kusaga meno, baada ya kuwindup makampuni yao....

Nilikuwa naongea na Mwanasheria moja jana anasema kazi nyingi anazopata kwa sasa ni kuwindup makampuni. Kwa mwezi anawindup makampuni 46-50 na kwa upande mwingine anafungua 2-3 tu. Sasa cheki hiyo ratio mwenyewe uone.. The private sector is tottaly dead!. Na ndio sector ambayo ingechukua vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo. UD inamwaga kila mwaka, UDOM inamwaga kila mwaka, Mzumbe, Tumaini, Muhimbili, TIA na wengine wengi. zaidi ya vyuo 40.... Sasa vijana hao wote hawawezi kuajiriwa sijui na SUMA JKT, TBA,NHC ambao kwa sasa ndio wanafanya kazi zote mpaka za kufagia barabara wakati hizo zilikuwa ni kazi za vikundi vya wanawake na vijana katika mitaa chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Jakaya kipindi anatoka aliacha makampuni ya ujenzi ya ndani yalioweza kushindana na Wachina kibao. But look now they are all dead. Kivipi, TRA Kuwabambikizia kesi za madeni, kazi kubwa zote wamechukua makampuni ya nje, kazi za ndani zote za serikali anafanya SUMA JKT, TBA, NHC, mpaka na Magereza. Is simpe local contractors can not survive in that circumstance. Ok!.. Mpaka yale maujenzi ya Halmashauri wameleta mfumo wa Force Account ambao ni ulaji wa watu wa manunuzi bila kujua wanauwa private sekta... Tuliona enzi za Jakaya akipambana kuweka mazingira bora, ndio maana tukaona wazawa wakiflourish kama vile SKOL (now is dead), DELEMONTE (now is dead), MILEMBE (now is dead), MECCO (now id dead), CASPIAN (is almost dead kabaki na kazi za Barrik tu)... the list is endless..

Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani. Wahenge wanasema kuuwa uchumi ni suala la siku 2 au tatu ila kuujemga ni miaka 10 t0 20... Hii miaka 5 uchumi umekufa kabisa, mpaka kuja kusimamisha uchumi is not now and haitatokkea kama hatobadilika au kama wananchi tusipoamua kumpa kura Lisu
 
1602393991027.png

Kikwete Kiswahili ana kisanifu utafikiri Mzee Shaban Robert.
 
Muwe mnatumia akili kufikiri.unaposema uchumi umekufa unamaanisha nini wakati huo huo nchi imeingia uchumi wa kati? Na makampuni gani una maanisha ? Maana makampuni hayo yalikuwa hayalipi kodi,hayalipi NSSF, PSSF .leo wamekabwa yalipe mnasema eti sector binafsi imekufa!!

Mfano mmoja ni mwambie.kuna hospital moja ywnye ngazi ya wilaya ilikuwa na manesi wa nne since 1995
wengine ni medical attendants. Na hawa alikuwa wanasaini mikataba miwili mkataba wa wazi na mkataba wa siri ili kikwepa kodi.sector binafsi isiyowajibika Ifage tu.
 
Wa tz wengi maisha yetu tulizoea kuishi kwa ujanja ujanja kaja Magufuli mianya yote kaziba tunaanza kulalamika ila hakuna rais bora kama magufuli kura yangu na yafamilia yangu atapata hakuna shaka ndani yake
 
Hili suala mimi mwenyewe binafsi huwa linanifikirisha sana na hii ni baada ya kusikia baadhi ya sababu nikaona ni zakijinga sana.

Sekta binafsi haziuliwi kwa mtindo huo, bali serikali ilitaiwa ijipange vizuri kushindana na sekta binafsi ili ifikie hatua watu waone Sekta binafsi si lolote si chochote, na watu waanzw kukimbilia serikalini.

Naona sasa hivi kuna hawa SUMA JKT, nawaona mpaka kwenye usafi wa jiji na vituo vya Mwendo kasi na kusafisha mabarabara.

Sababu kwangu mimi kupiga kura ni haramu hata angekuwa nani sipigi kura, ila kwa hili aisee linanishangaza sana.
 
Nyie ni wale mliokuwa mnatengeneza mabarabara na majumba mabovu kwa pesa nyingi sasa mnaumia sasa.
Badilikeni sasa, tengenezeni kwa kiwango cha juu na ghalama ya kawaida inayolingana na mkataba wako,
Kazi zipo nyingi tu.
 
Muwe mnatumia akili kufikiri.unaposema uchumi umekufa unamaanisha nini wakati huo huo nchi imeingia uchumi wa kati? Na makampuni gani una maanisha ? Maana makampuni hayo yalikuwa hayalipi kodi,hayalipi NSSF, PSSF .leo wamekabwa yalipe mnasema eti sector binafsi imekufa!! Mfano mmoja ni mwambie.kuna hospital moja ywnye ngazi ya wilaya ilikuwa na manesi wa nne since 1995
wengine ni medical attendants. Na hawa alikuwa wanasaini mikataba miwili mkataba wa wazi na mkataba wa siri ili kikwepa kodi.sector binafsi isiyowajibika Ifage tu.

Utambue ya kuwa nchi ilishashuswa kutoka huo uchumi wa kati. ambao mlitangaziwa kwa twitter

( Tanzania yashushwa rating ya uchumi wa kati, yadaiwa uchumi wake sio halisi na ukwasi wake hautabiriki hasa katika kupata mikopo ya nje )

Pili Hakuna kampuni iliyokuwa hailipi kodi, makadirio yameongezeka na kodi pia zimeongezeka, na ndio iliyosababisha makampuni lukuki yakafungwa, kwa kipindi cha miaka 5, watu zaidi ya 1M wamepoteza ajira na hakuna ajira zilizoongezeka

NSSF, PSSF serikali hi imeziua, CCM ina madem huko mpaka inashindwa kukopesheka tena
 
Hili suala mimi mwenyewe binafsi huwa linanifikirisha sana na hii ni baada ya kusikia baadhi ya sababu nikaona ni zakijinga sana.

Sekta binafsi haziuliwi kwa mtindo huo, bali serikali ilitaiwa ijipange vizuri kushindana na sekta binafsi ili ifikie hatua watu waone Sekta binafsi si lolote si chochote, na watu waanzw kukimbilia serikalini.

Naona sasa hivi kuna hawa SUMA JKT, nawaona mpaka kwenye usafi wa jiji na vituo vya Mwendo kasi na kusafisha mabarabara.

Sababu kwangu mimi kupiga kura ni haramu hata angekuwa na nani sipigi kura, ila kwa hili aisee linanishangaza sana.
Kabisa.... Jamaa alipoingia alikuwa na mentality kwamba private sector ni maadui wakubwa wa maendeleo ya nchi. But alisahau kuwa ni private sector ndio inaajiri zaidi..... Leo hii mpaka kazi za wanawake wa vikundi kazi zake zimechukuliwa na SUMA JKT..... Uppuzi mkubwa kweli
 
Back
Top Bottom