Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Hayo makampuni unayoyasema JPM ndio aliyainua Sasa kaipa kampuni ya kienyeji kujenga uwanja wa ndege kiiila siku mnamtukana nayo Bora awape suma jkt,

Tatizo Ni Lissu na matapeli wenzie kutukana wenzao kilasiku, tumejenga flyover nayeye kapita hapohapo kwenda kununua maparachichi mawili kariakoo eti anasema lingejengwa kijijini, ovyo
Mkuu JPM mchagueni nyie, sisi tumechoka kuchagua Rais msimangaji na mbaguuzi.yeye Kwake wanawake ni weupe tuuu....hapanaaa
 
Haahaa atachaguliwa alikopeleka mboga, wanageita na watanzania wengine watampiga wamtakaye asiyewagua...
uzuri wa kura ni siri
acha kupandikiza matamanio ya moyo wako kwenye akili za watu wengine,utapata kiharusi,hutaamini utakachokisikia,binadamu sio watu wazuri
 
Muwe mnatumia akili kufikiri.unaposema uchumi umekufa unamaanisha nini wakati huo huo nchi imeingia uchumi wa kati? Na makampuni gani una maanisha ? Maana makampuni hayo yalikuwa hayalipi kodi,hayalipi NSSF, PSSF .leo wamekabwa yalipe mnasema eti sector binafsi imekufa!! Mfano mmoja ni mwambie.kuna hospital moja ywnye ngazi ya wilaya ilikuwa na manesi wa nne since 1995
wengine ni medical attendants. Na hawa alikuwa wanasaini mikataba miwili mkataba wa wazi na mkataba wa siri ili kikwepa kodi.sector binafsi isiyowajibika Ifage tu.
Wewe binafsi na wanaokuzunguka vipi maisha yenu?yameboreka au yamedoda?
 
Wewe binafsi na wanaokuzunguka vipi maisha yenu?yameboreka au yamedoda?
Hawa vijana wa pale Lumumba nawajua sana wasikupe tabu... Ijumaa wakishapewa pilau ya Mandi pale Lumumba basi akili yao inawaruka. Na hawana majukumu ya kifamilia.... Swali zuri, tokea tumeingia uchumi wa kati maisha yake yameboreka?
 
Kabisa.... Jamaa alipoingia alikuwa na mentality kwamba private sector ni maadui wakubwa wa maendeleo ya nchi. But alisahau kuwa ni private sector ndio inaajiri zaidi..... Leo hii mpaka kazi za wanawake wa vikundi kazi zake zimechukuliwa na SUMA JKT..... Uppuzi mkubwa kweli
Hajawahi kujiajiri hata kuuza genge la nyanya. Maisha yote ameajiriwa na serikali. Akiona matajri anaamini ni majizi. Akaanza na kuwafanya malaika waishi kama mashetani bila sababu yoyote.
 
Ni kweli kuna changamoto ya makampuni kufungwa kutokana na kodi. Mimi kwa maoni yangu sababu ni :
1. Pamoja na umuhimu wa makampuni kulipa kodi bila kukwepa kuna umuhimu sasa wa kupitia sheria za kodi pia ili kupunguza faini na riba zisizolipika kwa vile kuzilipa lazima zitakula mtaji wa mfanya biashara. Bora kidogo na biashara ziendelee ili kuwa na kodi endelevu kwa manufaa ya taifa
2.kuna umuhimu wa kuhuisha kodi na tozo ili kupunguza utitiri wa kodi na hapo hapo kupanua wigo wa kodi kwa kuingiza sekta isiyo lazima ichangie ulipaji kodi mf. Taxi bubu hazilipi kodi
3. Serikali iongeze mitandao ya ukusanyaji kodi hadi ngazi za kata na hii iongeze uwekezaji katika raslimali watu ndani ya TRA kwa idadi ujuzi na wledi
3. Rushwa na kubambikia kodi vikomeshwe kwa kuweka mifumo ya ndani ya TRA ya ufuatiliaji mienendo ya watumishi na mifumo yenye uwazi ya ukadiriaji mapato
4.kuwe na vetting endelevu ya mienendo na tabia ya watumishi wa TRA.
Rais alikwishatoa maelekezo ya kuboresha mazingira ya ulipaji kodi na uondoaji vikwazo lakini hatua au mapinduzi ya kisheria kidogo sana yamechukuliwa kulingana na maelekezo hayo. Ninaamini mazingira yakiboreshwa kodi endelevu itakusanywa na kuwa na malengo yanayotimilika kwa kipindi kirefu na biashara kushamiri na kodi hiyari bila shuruti kulipwa kutokana na uwezo na faida ya kampuni bila ya kodi lazimishi(coercive tax regime)Ninaamini Rais Magufuli atayafuatilia haya kipindi kijacho cha utawala wake kwa vile ni msikivu na amekwishayatolea maelekezo kwa mamlaka husika. Tumchague apate fursa tena tuone.
 
Kampuni zinakufa sio kwa sababu zilikuwa zinakwepa kodi, ni kwa sababu hakuna Tenda kutoka serikalini, serikali inatoa tenda kwa serikali na serikali inailipa serikali, hata ukiendelea kukwepa kodi, kama biashara yako ilitegemea zaidi kufanya kazi na serikali lazima kampuni itajifia natural death. Ndio kitu kilichofanywa na awamu hii
 
Dah mdau umenikumbusha Fasjet Airlines. Just imagine familia mgapi zilikua zinafurahi kuwepo kwa Fastjet. Kuanzia wafanyakazi na familia zao mpaka abiria wapya ambao hawajawahi panda ndege walianza kupanda kwa bei nafuu.

Kampuni ilikuja pigwa katafunua ya hatari mpk ikaondoka ili iipishe Atcl. Na viongozi wa serekali walifanya party kabisa kuanguka kwa Fastjet.

Kwani kungekua na shida gani Fastjet iwepo na ATCL iwepo. Si ndio ajira zingekuwepo mara dufu?

Serekali inapiga domo ajira zitaongezeka lkn in reality ukiangalia kilichofanyika ndani ya miaka mi5 ni kuwatoa walioajiriwa wengi na kuwaajiri wachache.
 
Yawezekana unatetea makampuni yaliyoishi kwa ubabaishaji maana kuna miradi mingi imekuja kukamilishwa kwenye awamu hii ya utawala kwa usimamizi wa karibu ikiwa ni pamoja na sababu ulizozitaja.

Hivyo basi, ingekuwa jambo jema na la uchambuzi ukaorodhesha, hata kwa mifano michache, miradi ya hayo makampuni binafsi ya ujenzi iliyokamilishwa kwa kiwango, ndani ya makadirio ya muda na gharama.
 
Dah mdau umenikumbusha Fasjet Airlines. Just imagine familia mgapi zilikua zinafurahi kuwepo kwa Fastjet. Kuanzia wafanyakazi na familia zao mpaka abiria wapya ambao hawajawahi panda ndege walianza kupanda kwa bei nafuu.

Kampuni ilikuja pigwa katafunua ya hatari mpk ikaondoka ili iipishe Atcl. Na viongozi wa serekali walifanya party kabisa kuanguka kwa Fastjet.

Kwani kungekua na shida gani Fastjet iwepo na ATCL iwepo. Si ndio ajira zingekuwepo mara dufu?

Serekali inapiga domo ajira zitaongezeka lkn in reality ukiangalia kilichofanyika ndani ya miaka mi5 ni kuwatoa walioajiriwa wengi na kuwaajiri wachache.
Mambo ya ovyo kweli kweli!.......
 
Back
Top Bottom