Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Sababu kwangu mimi kupiga kura ni haramu hata angekuwa nani sipigi kura, ila kwa hili aisee linanishangaza sana.
Sabb ya imani ya dini, au?!
Watu wasiotaka kuchukua hatua Kama wewe ndo wanasababisha ccm wanatawala miaka na miaka bila tija yoyote
 

Sio kweli. Hizi kodi zinazorudiwa kila siku hazikamiliki ? Mfano mdogo tu...2019 TRA inafanya mahesabu na unaambiwa ulipe kodi kiasi fulani. 2020, TRA hao hao wanarudi kwenye yale yale mahesabu na wanakuja tena na kiasi kingine cha kulipa. Is that how it works? Investors wawe wazawa au wa nje wanawaangaliaje kwenye mambo kama hayo? Mtakusanya wapi kodi kama kampuni kinaendelea kufungwa? I think, mnakusanya kodi ambayo wala sio kodi. Ni kula mitaji ambayo wala hamkuwekeza
 
Hakuna haja ya kuendelea kukuelewesha sabab ushachagua kutokusikiliza.

Siasa sio mpira, usikariri
Wenye kupanga tanking ni Moody au world Bank and it's affiliates organisation??
 
Sabb ya imani ya dini, au?!
Watu wasiotaka kuchukua hatua Kama wewe ndo wanasababisha ccm wanatawala miaka na miaka bila tija yoyote
Achilia mbali imani ya dini, ila akili tu iliyo salimika inakataa mchakato wa upigaji kura, watu kuomna uongozi na mfumo mzima wa uendeshaji mambo chini ya Mwamvulo wa Demokrasia.

Kwani hatua tu ni mpaka umpigie yule aliye dhidi ya CCM au hata kutokupiga kura kabida nayo ni kuchukia hatua, au huku si kuchukua hatua ?
 
Sasa nimeelewa😁
Ukiona TRA wamekuongezea kiasi cha kodi rudi kwenye hesabu zako kama sio wewe basi anayekufanyia hesabu kuna mahali alitengeneza mambo ili kupunguza kodi halafu upande wa pili akashindwa kutengeneza. Sasa documents zinapowafikia lazima wataona na kama wamekuambia ulipe tena wamekupendelea, kwa hilo huwa wanakupiga adhabu ya kutosha. Hii imewatokea wengi, hata mimi iliwahi kunikuta kwa kuamini report iliyoandaliwa na mtu wangu kumbe ndani alivuruga
Kama kampuni ni yako jaribu kupata ukweli wa nini kilitokea ili lisijirudie tena
 
Shida ni kwamba hata uki appeal bado unatakiwa ulipe aslimia fulani kubwa tu wakati ukisubiria majibu ya rufaa yako.
 
Mkuu, hatua inayosaidia kuangusha mfumo mbovu ni nzuri zaidi
 
Mara nyingi Tra wanakulainisha tu kwa Kodi kubwa ili rushwa itoke kirahisi
 
Mkuu, hatua inayosaidia kuangusha mfumo mbovu ni nzuri zaidi
Si kweli na hili huwezi kuthibitisha. Tunaweza kusema ya kuwa serikali inafanya uonezi kwa makampuni binafsi hasa hasa madogo ila kuna makampuni haiwezi kuyaondoa sababu nchi haina mpango huo na haiwezi kufanya baadhi ya kazi.

Ngoja nikupe mfano, serikali yenyewe inadai imekuja kubaini ya kuwa kwenye hii miradi kuna upigaji mkubwa sana. Sasa kama ni kweli,hapa kunaonyesha udhaifu mkubwa wa serikali yenyeww kupitia watendaji wake. Mkandarasi au mtu binafsi huwa hapigi deal mwenyewe bali anapiga deal na serikali husika. Kwahiyo serikali ilitakiwa kwanza iwaajiri watu ambao hawana tamaa na kuweka mfumo mzuri juu ya hilo.

Kinachokuja kutokea ni miradi mingi inayofanywa na serikali yenyewe ina kuja kuwa na ubora mdogo sana, na hapa kuna sababu za kumridhisha mtawala na si uhaslisi. Mifano iko mingi katika hili.

Lakini labda nikuulize,ni mfumo gani huo unao ukusudia na ni hatua zipi ?
 
Unafungua biashara survival strategy yako ufanye kazi na serikali tu, sio kwamba umefanya demand analysis ya soko zima. Wakati unasoma biashara ukufundishwa effect za changes in consumption trends za wateja na jinsi ya kujikinga?

Biashara ya namna hiyo zife tu hakuna creativity. Kungekuwa na high streets retails leo kweli nchi za wenzetu zama hizi za online shopping bila ya maduka makubwa ku adapt mazingira ya leo.

Serikali imeamua hela yake inataka iende mbali value for money na miradi yake iishe on time; hata hizo taasisi za serikali zinazo sua sua miradi wananyang’anywa with minimal legal consequences za kupelekana mahakamani for breach of contract.

Zama zimebadilika tatizo sio Magufuli isipokuwa wafanyabiashara wasiotaka kubadilika; fungua biashara nyingine sio lazima ufanye kazi na serikali tu.
 
Uchumi wa vitabuni huo ndiyo yale boss wa tra akistaafu anafungua biashara mwaka anafilisika
 
Uchumi wa vitabuni huo ndiyo yale boss wa tra akistaafu anafungua biashara mwaka anafilisika
Ni kwa sababu hawana survival strategy (sina uhakika ntaingia google nirudi na takwimu rasmi) hila wanadai katika biashara laki moja zinazofunguliwa nchi za mabeberu karibu 2/3 hufa ndani ya miaka miwili, zilizobaki kama 3/5 hufa ndani ya miaka 5 na katika miaka 10 unakuta zimebaki biashara kama 5000 tu kati ya laki zilizoanzishwa pamoja. kati ya hizo 5000 zilizobaki kama 100 ndio ukuwa kuelekea kuitwa biashara za kati.

Tatizo kubwa linatajwa ni poor planning and the ability to adapt to changing external environment, yaani mtu anafungua biashara kwa lengo la kuhudumia serikali tuu. Hizo ndio akili gani, serikali ikibadili mfumo wake wa manunuzi wanakuja kulia.

Shughuli anayofanya Magufuli leo sio optional ni lazima nchi aiwezi chochea speed ya ukuaji wa uchumi bila ya miundombinu in 10 years time ndio watu watakuja faidika na kuelewa kinachofanywa leo.
 
Uchumi wa vitabuni huo ndiyo yale boss wa tra akistaafu anafungua biashara mwaka anafilisika
Kampuni za ujenzi mubadirike tunategemea sasa muingie mikataba na sisi wananchi wakawaida mtujengee nyumba kwa bei nafuu maana mlikimbilia serikalini kwakuwa mlipiga hela sasa rudini nyumbani kazi zipo tu
 
Kampuni za ujenzi mubadirike tunategemea sasa muingie mikataba na sisi wananchi wakawaida mtujengee nyumba kwa bei nafuu maana mlikimbilia serikalini kwakuwa mlipiga hela sasa rudini nyumbani kazi zipo tu
Si ndio hapo yaani wao mteja ni serikali tu. Wanunue viwanja na kuanza kujenga nyumba za bei nafuu mteja sio serikali tu.
 
Tra walifanya sifa kutangaza mapato kila mwezi.
Walitamani kila mwezi uwe na makusanyo ya juu kuliko mwezi uliopita..
Ule mchezo wa halmashauri za mikoa kushindana mapato .
(Wahusika ili kupata sifa za ukusanyaji wanambana mfanya biashara kupita kiasi)

Haya mambo yamewaumiza sana wafanya biashara na kupelekea mitaji yao kuanguka.
 
Kampuni za ujenzi mubadirike tunategemea sasa muingie mikataba na sisi wananchi wakawaida mtujengee nyumba kwa bei nafuu maana mlikimbilia serikalini kwakuwa mlipiga hela sasa rudini nyumbani kazi zipo tu
Mkuu una nyumba ?
Namaanisha nyumba uliyojenga kwa kutumia mafundi wa kawaida mitaani.
Gharama zake umezionaje?
 
Matokeo ya hizo kodi yanareflect kwenye kushamiri kwa hiyo biashara. Ikiwa makadirio yanapelekea kufungwa kwa biashara ,hayo hayawezi kuwa makadirio sahihi kwa maana mfanya biashara analipa kodi nyingi kuliko faida anayotengeneza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…