Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Mpaka 2015 private sectors zilikuwa zinashamiri. Jakaya aliacha mazingira mazuri na bora kabisa kwa sekta binafsi kukua na kuboreka. Ila tokea 2016 makampuni ambayo idadi yake haijulikani yamefungwa katika nchi hii, na bado yanaendelea kufungwa. Vijana lukuki wamepoteza ajira katika makampuni hayo.... na wale ambao walijiajiri kwa kufungua makampuni kwa sasa wanalia kilio cha kusaga meno, baada ya kuwindup makampuni yao....

Nilikuwa naongea na Mwanasheria moja jana anasema kazi nyingi anazopata kwa sasa ni kuwindup makampuni. Kwa mwezi anawindup makampuni 46-50 na kwa upande mwingine anafungua 2-3 tu. Sasa cheki hiyo ratio mwenyewe uone.. The private sector is tottaly dead!. Na ndio sector ambayo ingechukua vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo. UD inamwaga kila mwaka, UDOM inamwaga kila mwaka, Mzumbe, Tumaini, Muhimbili, TIA na wengine wengi. zaidi ya vyuo 40.... Sasa vijana hao wote hawawezi kuajiriwa sijui na SUMA JKT, TBA,NHC ambao kwa sasa ndio wanafanya kazi zote mpaka za kufagia barabara wakati hizo zilikuwa ni kazi za vikundi vya wanawake na vijana katika mitaa chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Jakaya kipindi anatoka aliacha makampuni ya ujenzi ya ndani yalioweza kushindana na Wachina kibao. But look now they are all dead. Kivipi, TRA Kuwabambikizia kesi za madeni, kazi kubwa zote wamechukua makampuni ya nje, kazi za ndani zote za serikali anafanya SUMA JKT, TBA, NHC, mpaka na Magereza. Is simpe local contractors can not survive in that circumstance. Ok!.. Mpaka yale maujenzi ya Halmashauri wameleta mfumo wa Force Account ambao ni ulaji wa watu wa manunuzi bila kujua wanauwa private sekta... Tuliona enzi za Jakaya akipambana kuweka mazingira bora, ndio maana tukaona wazawa wakiflourish kama vile SKOL (now is dead), DELEMONTE (now is dead), MILEMBE (now is dead), MECCO (now id dead), CASPIAN (is almost dead kabaki na kazi za Barrik tu)... the list is endless..

Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani. Wahenge wanasema kuuwa uchumi ni suala la siku 2 au tatu ila kuujemga ni miaka 10 t0 20... Hii miaka 5 uchumi umekufa kabisa, mpaka kuja kusimamisha uchumi is not now and haitatokkea kama hatobadilika au kama wananchi tusipoamua kumpa kura Lisu
Kodi zimefilisi makampuni mengi ya ujenzi. Kodi zisizokuwa halisi. Sijui wana benefit nini hawa watu kuua hizi biashara
 
uzi bora kabisa
nadhani hii ni hoja ya msingi ambayo Tundu Lissu angetembea nayo nchi nzima naseme ataletaje suluhisho
nchi imehsribika kabisa
Mimi nimeshuhudia makampuni kibao hapa Arusha yamekufa kibudu Nathan Engineering
Hamfrey Construction
Madava Engineering nk.
jamani tungane tuliokoe taifa hakuna pahala palipo salama sekta binafsi watumishi wote kuanzia walimu madaktari majeshi yote yanalia
yaani walioko salama labda wakuu wabaoketi meza moja na mkulu
 
Ungekua ulianza biashara zako ukilipa kodi Leo usingekua hapa ukilialia. Usikate tamaa, fanya ku restructure biashara yako uweze kuongeza faida bila kukwepa ya kaisari... kinachofanyika sasa ulitakiwa kukifanya bila shurti siku nyingii
Halafu nani alikuambia wao hawalipia kodi?
Alicholalamikia ni serikali kutaka kufanya kazi zote, hivyo private ina shrink. Sio kila kampuni iliyofungwa walikuwa wezi.
Sasa hivi mnawaambia watu wakajiajiri, yani kwa mfano mtu afungue kampuni ya construction, uwezekano wa kufeli ni 80% kutokana na kukosa kazi.
Ajira za sasa ni kuuza mihogo, kununua nguo karikoo na kuziuza online n.k
Sasa badala ya kuwaambia watubku restructure, government ndio ifanye kuji restructure, wawe wabunifu kuongeza na kuboresha vyanzo vya mapato, waache ushamba.
Hawa watu walioishi katika nyumba za nyasi, kulala na mbuzi chumbani,sijui kuoga umande ni wazito kubadilika, kwa dunia na Tanzania ilivyo ni muda wa kuwafanya washauri na wafuasi tu.
 
Kodi zimefilisi makampuni mengi ya ujenzi. Kodi zisizokuwa halisi. Sijui wana benefit nini hawa watu kuua hizi biashara
Ukweli ni kwamba hakukua na ulipaji kodi sahihi na hii ilipelekea serikali kupoteza kiasi cha kushindwa hata kuboresha miundombinu huku makampuni kupata faida zisizokua za kweli.
Makampuni mengi yaliweza kumudu matumizi mengi yasiyokua ya lazima sababu tuu pesa ilikua nyingi. Sasa kwakuwa kodi zinalipwa sawasawa wenye makampuni wanatakiwa kujipanga upya kwa kuangalia upya gharama za uendeshaji huku wakiongeza ufanisi
Kulalamika hakutusaidii chochote kwa sasa
 
Uchumi wetu umeyumba kama ulivyoyumba kwingine kote duniani. NGO nyingi zimesimisha miradi na kupumzisha watu kazi na hii kwa sababu ya mdororo huko Ughaibuni.

Kwa sisi ndani ukiachilia mbali athari za mdororo wa kidunia tunazo changamoto zetu. Na hizi ni muhimu tuzitazame objectively.

Shida kubwa ya kampuni nyingi za kitanzania zilikuwa haziendeshwi kitaasisi. Nyingi zilikuwa zinaendeshwa kama magenge tu.. pesa inaingia inatumika hovyo..hatukuona umuhimu wa ku-hire tax experts and proper managers.. hapo tulichokuwa tunafanya ni maandalizi ya anguko kuu.

Pili toka tuingie Kwenye Nchi za Uchumi wa kati.. uhitaji wa kuongeza wigo wa walipa kodi ulikuwa lazima... Kwa mujibu wa sheria za kodi hakuna jipya sema wameamua kusimami tu.. kama ulikuwa na mtu wa kodi atakuambia haya yalikuwepo sema hayakuwa yakisimamiwa..

Makampuni mengi hayakujua na hayakuhitaji kujua. Yalijiendesha kimimi ndio maana mfumo wa kitaasisi unapokuja kuwa imposed mengi yanatetereka. Na ni kweli kampuni nyingi zinawindup lakini nyingi ni kampuni changa na nyingine hazikuwahi hata kuoperate.. kwa Brela hii ni njema ilikuwa na Data za makampuni meengi yasioyooperate.

Makampuni mengi yanayofunguliwa kwa sasa yamekuwa makini zaidi na uwezekano wao kukua ni mkubwa. Wanaingia katika biashara na mfumo sahihi wa kitaasisi na sio kampuni mtu(za mfukoni).. wanatunza taarifa na ni rahisi kuwaauddit na kujua ukubwa wao na maendeleo kitu kilichokuwa kigumu sana hapo mwanzo.

Hii itapelekea kuzaliwa kwa mergers ambazo zitakuwa imara zaidi na huenda zikawa na uwezo wa kuwa listed kwenye soko la hisa, kukuza mitaji yao, kupanua operations na kuongeza ajira.

Sio kila kitu ni kibaya.. ninaelewa frustrations zinazotokana na mabadiliko ya mfumo.. japo ni lazima tubadilike. Hakuna namna. Sekta haijakufa its just taking a new shape and form.. like it has always been and will always be. Change is inevitable.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ungekua ulianza biashara zako ukilipa kodi Leo usingekua hapa ukilialia. Usikate tamaa, fanya ku restructure biashara yako uweze kuongeza faida bila kukwepa ya kaisari... kinachofanyika sasa ulitakiwa kukifanya bila shurti siku nyingii
Halafu nani alikuambia wao hawalipia kodi?
Kila mtu analia ugumu wa maisha,kuna haja gani kurudia kosa October
 
Wa tz wengi maisha yetu tulizoea kuishi kwa ujanja ujanja kaja Magufuli mianya yote kaziba tunaanza kulalamika ila hakuna rais bora kama magufuli kura yangu na yafamilia yangu atapata hakuna shaka ndani yake
Ka create mianya ama kaiziba? Mbona hatuambiwi taratibu zilizofuatwa kwenye manunuzi ya ndege? Huo sio mwanya?
 
Mimi nasikitika sana kusoma mtu analaumu Suma JKT kupewa kazi hapa nchini kwani Suma ni ya watu wa wapi Kenya? Kampuni nyingi kipindi cha JK zilikuwa kampuni za briefcase ukienda kule bandarini kulikuwa na clearing agents zaidi ya 15000 hata ofisi hawana lakini utakuta account zao za benki kuna malipo wanapokea kutoka serikalini. Uchumi wa madawa ya kulevya na fedha nyingi kuonekana mitaani sababu ya wale punda wakishatelemsha mzigo na kupokea malipoyao mjini hakutoshi. Fedha za malipo ya watu waliochukua fedha benki na masandarusi mmeshasahau, na malipo ya hovyo kwa watu wa magari waliohudumia mikutano isiyukwisha, matumizi ya Ngurdoto na wale jamaa wa marekani weusi Sullivan fedha zilimwagwa kama wenda wazimu sasa huu ndio uchumi watu wanaulilia kutoka kwa JK wakati alishindwa hata kufufua reli tu ya Dar, Tanga, Moshi na Arusha kilichotakiwa ni ukarabati tu. Shule za serikali zilikuwa hoi taabani hazikuwa na ukarabati tangu mkoloni aondoke nilienda kuangalia shule yetu ya zamani ya Ilboru hivi juzi sikuamini macho yangu ni sawa na kumchukua mzee aliyechoka na kumrudisha kwenye ujana. Acheni jamani na mahaba yenu feki. Ilboru ipo hadhi ya chuo kikuu.
 
Mpaka 2015 private sectors zilikuwa zinashamiri. Jakaya aliacha mazingira mazuri na bora kabisa kwa sekta binafsi kukua na kuboreka. Ila tokea 2016 makampuni ambayo idadi yake haijulikani yamefungwa katika nchi hii, na bado yanaendelea kufungwa. Vijana lukuki wamepoteza ajira katika makampuni hayo.... na wale ambao walijiajiri kwa kufungua makampuni kwa sasa wanalia kilio cha kusaga meno, baada ya kuwindup makampuni yao....

Nilikuwa naongea na Mwanasheria moja jana anasema kazi nyingi anazopata kwa sasa ni kuwindup makampuni. Kwa mwezi anawindup makampuni 46-50 na kwa upande mwingine anafungua 2-3 tu. Sasa cheki hiyo ratio mwenyewe uone.. The private sector is tottaly dead!. Na ndio sector ambayo ingechukua vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo. UD inamwaga kila mwaka, UDOM inamwaga kila mwaka, Mzumbe, Tumaini, Muhimbili, TIA na wengine wengi. zaidi ya vyuo 40.... Sasa vijana hao wote hawawezi kuajiriwa sijui na SUMA JKT, TBA,NHC ambao kwa sasa ndio wanafanya kazi zote mpaka za kufagia barabara wakati hizo zilikuwa ni kazi za vikundi vya wanawake na vijana katika mitaa chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Jakaya kipindi anatoka aliacha makampuni ya ujenzi ya ndani yalioweza kushindana na Wachina kibao. But look now they are all dead. Kivipi, TRA Kuwabambikizia kesi za madeni, kazi kubwa zote wamechukua makampuni ya nje, kazi za ndani zote za serikali anafanya SUMA JKT, TBA, NHC, mpaka na Magereza. Is simpe local contractors can not survive in that circumstance. Ok!.. Mpaka yale maujenzi ya Halmashauri wameleta mfumo wa Force Account ambao ni ulaji wa watu wa manunuzi bila kujua wanauwa private sekta... Tuliona enzi za Jakaya akipambana kuweka mazingira bora, ndio maana tukaona wazawa wakiflourish kama vile SKOL (now is dead), DELEMONTE (now is dead), MILEMBE (now is dead), MECCO (now id dead), CASPIAN (is almost dead kabaki na kazi za Barrik tu)... the list is endless..

Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani. Wahenge wanasema kuuwa uchumi ni suala la siku 2 au tatu ila kuujemga ni miaka 10 t0 20... Hii miaka 5 uchumi umekufa kabisa, mpaka kuja kusimamisha uchumi is not now and haitatokkea kama hatobadilika au kama wananchi tusipoamua kumpa kura Lisu
Tatizo mtu asyejua pesa asiyejua biashara ndo mpngaji na muellekezaji. Na anaabudiwa na kusujudiwa. Ni mtu gani anajua kila kitu.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Muwe mnatumia akili kufikiri.unaposema uchumi umekufa unamaanisha nini wakati huo huo nchi imeingia uchumi wa kati? Na makampuni gani una maanisha ? Maana makampuni hayo yalikuwa hayalipi kodi,hayalipi NSSF, PSSF .leo wamekabwa yalipe mnasema eti sector binafsi imekufa!!

Mfano mmoja ni mwambie.kuna hospital moja ywnye ngazi ya wilaya ilikuwa na manesi wa nne since 1995
wengine ni medical attendants. Na hawa alikuwa wanasaini mikataba miwili mkataba wa wazi na mkataba wa siri ili kikwepa kodi.sector binafsi isiyowajibika Ifage tu.

Well and good

Kama amefagia vitaasisi na vikampuni (vya sekta binafsi) ambavyo vilikuwa haviwajibiki ktk kulipa kodi nk nk

Sasa hebu tujibu swali hili muhimu, kwamba, serikali yake inafanya na imefanya juhudi gani kuandaa mazingira bora kwa ajili ya private sector inayowajibika kustawi?

Iweje awe anaamuru kandarasi za umma/serikali za majenzi, upishi na chochote kile zifanywe na TBA, SUMA JKT, Magereza, JWT ambazo ni taasisi za serikali tena pasipo ushindani?

Si unakumbuka alilipa Jeshi la wananchi (JWT) kazi ya kununua korosho mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kazi ambayo ilipaswa ifanywe na makampuni ya sekta binafsi kwa ushindani? Hakujua madhara ya maamuzi yake haya kiuchumi?

Kiongozi wa nchi (Rais) wa namna hii anakuwa anajua namna kusimamia na kuendesha uchumi kweli?

Let's be honest, Magufuli ndiye problem ktk nchi hii!!

He must go out ama la Mungu akimjalia kuendelea, basi ni lazima abadilike ingalau kwa kuazima akili njema ya kuongoza nchi toka kwa wenye nazo else ataiharibu nchi hii kuliko maelezo!!

Bahati mbaya nyingine kwake ni kuwa hata chama chake CCM kiko mfukoni mwake mwenyewe peke yake.

CCM ya kina Polepole na Bashiru is useless. Haina ubavu wala uwezo wa kumrejesha njiani anapokuwa off line..!

Ni shida juu ya shida..
 
Ccm ikishinda ni sababu ya Magufuli. Ikishindwa pia ni sababu ya Magufuli. Wajumbe walimchagua kwa 100% kimkakati but sio reflection ya wanachi.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hawa vijana wa pale Lumumba nawajua sana wasikupe tabu... Ijumaa wakishapewa pilau ya Mandi pale Lumumba basi akili yao inawaruka. Na hawana majukumu ya kifamilia.... Swali zuri, tokea tumeingia uchumi wa kati maisha yake yameboreka?
Tena wanaheabika humu.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nasikitika sana kusoma mtu analaumu Suma JKT kupewa kazi hapa nchini kwani Suma ni ya watu wa wapi Kenya? Kampuni nyingi kipindi cha JK zilikuwa kampuni za briefcase ukienda kule bandarini kulikuwa na clearing agents zaidi ya 15000 hata ofisi hawana lakini utakuta account zao za benki kuna malipo wanapokea kutoka serikalini. Uchumi wa madawa ya kulevya na fedha nyingi kuonekana mitaani sababu ya wale punda wakishatelemsha mzigo na kupokea malipoyao mjini hakutoshi. Fedha za malipo ya watu waliochukua fedha benki na masandarusi mmeshasahau, na malipo ya hovyo kwa watu wa magari waliohudumia mikutano isiyukwisha, matumizi ya Ngurdoto na wale jamaa wa marekani weusi Sullivan fedha zilimwagwa kama wenda wazimu sasa huu ndio uchumi watu wanaulilia kutoka kwa JK wakati alishindwa hata kufufua reli tu ya Dar, Tanga, Moshi na Arusha kilichotakiwa ni ukarabati tu. Shule za serikali zilikuwa hoi taabani hazikuwa na ukarabati tangu mkoloni aondoke nilienda kuangalia shule yetu ya zamani ya Ilboru hivi juzi sikuamini macho yangu ni sawa na kumchukua mzee aliyechoka na kumrudisha kwenye ujana. Acheni jamani na mahaba yenu feki. Ilboru ipo hadhi ya chuo kikuu.
Kama usemacho hapa ni sahihi, basi alipaswa kurekebisha hayo na kisha aandae mazingira ya kuilea na kuikuza private sector ambayo ndiyo injini ya uchumi ktk nchi yoyote ile...

Kinyume chake, aliziondoa hizo unazoziita "kampuni za kwenye briefcase" lakini hafanyi lolote kuijenga upya sekta binafsi yenye tija kulingana na "standards" zake ili imsaidie kuendesha uchumi wa nchi yake....

Yeye anaamini kuwa serikali inaweza kufanya yote, inaweza hata kununua korosho za wakulima wa mikoa ya kusini..

Huku ni kufeli kwa Sera za uchumi za Magufuli big time. Cha ajabu nyie wengine mnaona sawa tu..

Akiendelea hivi, hatutafika popote zaidi kutengeneza matatizo makubwa kama taifa ambayo kuyarekebisha huko mbeleni itakuwa shida kubwa sana!!
 
Mpaka 2015 private sectors zilikuwa zinashamiri. Jakaya aliacha mazingira mazuri na bora kabisa kwa sekta binafsi kukua na kuboreka. Ila tokea 2016 makampuni ambayo idadi yake haijulikani yamefungwa katika nchi hii, na bado yanaendelea kufungwa. Vijana lukuki wamepoteza ajira katika makampuni hayo.... na wale ambao walijiajiri kwa kufungua makampuni kwa sasa wanalia kilio cha kusaga meno, baada ya kuwindup makampuni yao....

Nilikuwa naongea na Mwanasheria moja jana anasema kazi nyingi anazopata kwa sasa ni kuwindup makampuni. Kwa mwezi anawindup makampuni 46-50 na kwa upande mwingine anafungua 2-3 tu. Sasa cheki hiyo ratio mwenyewe uone.. The private sector is tottaly dead!. Na ndio sector ambayo ingechukua vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo. UD inamwaga kila mwaka, UDOM inamwaga kila mwaka, Mzumbe, Tumaini, Muhimbili, TIA na wengine wengi. zaidi ya vyuo 40.... Sasa vijana hao wote hawawezi kuajiriwa sijui na SUMA JKT, TBA,NHC ambao kwa sasa ndio wanafanya kazi zote mpaka za kufagia barabara wakati hizo zilikuwa ni kazi za vikundi vya wanawake na vijana katika mitaa chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Jakaya kipindi anatoka aliacha makampuni ya ujenzi ya ndani yalioweza kushindana na Wachina kibao. But look now they are all dead. Kivipi, TRA Kuwabambikizia kesi za madeni, kazi kubwa zote wamechukua makampuni ya nje, kazi za ndani zote za serikali anafanya SUMA JKT, TBA, NHC, mpaka na Magereza. Is simpe local contractors can not survive in that circumstance. Ok!.. Mpaka yale maujenzi ya Halmashauri wameleta mfumo wa Force Account ambao ni ulaji wa watu wa manunuzi bila kujua wanauwa private sekta... Tuliona enzi za Jakaya akipambana kuweka mazingira bora, ndio maana tukaona wazawa wakiflourish kama vile SKOL (now is dead), DELEMONTE (now is dead), MILEMBE (now is dead), MECCO (now id dead), CASPIAN (is almost dead kabaki na kazi za Barrik tu)... the list is endless..

Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani. Wahenge wanasema kuuwa uchumi ni suala la siku 2 au tatu ila kuujemga ni miaka 10 t0 20... Hii miaka 5 uchumi umekufa kabisa, mpaka kuja kusimamisha uchumi is not now and haitatokkea kama hatobadilika au kama wananchi tusipoamua kumpa kura Lisu
Uzi Bora kabisa huu.. umeandika mambo ya msingi sana, ila ingekuwa vzr kama ungeandika kiswahili pekee bila kuchanganya changanya na kiingereza ili wote tuelewe..
 
Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani.
Akikuambia atabadilika hiyo itakuwa ahadi hewa, usithubutu kudanganywa.. Hapo dawa ni kuchagua Lissu, period
 
Kusema kweli itakuwa jambo geni kwa mara ya kwanza rais wa ccm ku serve kwa kipindi kimoja. Ndio maana mbinu zozote zinatumika.
Japo wanamshambulia sana Lissu, ukweli ni kwamba jamaa ana uwezo mkubwa sana.
Ujue ukiwa rais wa nchi unakuwa miongoni mwa watu mashuhuri wasiozidi 300 na hivi kuwa global figure. Unawakilisha watu wako katika jumuiya ya mataifa. Unakuwa msemaji wao. Hivo unatakiwa uwe na uwezo maalumu katika nafasi hii. Kiukweli Lissu ana uwezo na wanaompiga vita ni kwa sababu hiyo tu ya woga. Ni fitina tu lakini wanaelewa ukweli. Mfuatilie hotuba zake mtagundua uwezo wake. That man anatufaa watanzania na anafit kwenye dunia ya leo.

Back
Top Bottom