Naomba nikujibu maswali yako kutokana na jinsi nilivyotafuta mwenyewe majibu na kufahamu. Usiamini ninachosema ila chunguza na wewe upate majibu yako.
Kufa ni nini? Mwanadamu ni muunganiko wa huu MWILI na UFAHAMU. Na kila chenye uhai kina consciousness (ufahamu) lakini viumbe vinatofautiana hali na nafasi ya ufahamu na mwanadamu ndiye kiumbe chenye ufahamu wa juu zaidi. Ufahamu ni neno linalotumika kumaanisha hali zifuatazo- kujitambua (kujifahamu mimi ni nani na hiki ni nini), kumbukumbu zitokanazo na milango ya ufahamu (macho, masikio, pua, na kadhalika hukupa taarifa na ndio maana huitwa milango ya ufahamu), uwezo wa kufanya maamuzi, utambuzi na akili kwa ujumla. Ufahamu sio ubongo. Mpaka sasa ushahidi unaokubalika 100% ni kuwa UFAHAMU ni energy/nguvu. Ndani ya ubongo kuna seli maalum kupitisha umeme. Kumbukumbu ni umeme. Ufahamu ni umeme. Wazo ni Umeme. Hisia ni umeme. Unaweza usifahamu ni umeme kutokana na umeme uliouzoea majumbani lakini frequency yake ni umeme.
Kwa mwanadamu tunasema kufa ni UFAHAMU unapouacha MWILI lakuna hakuna kifo cha UFAHAMU au MWISHO WA UFAHAMU. Mwili ni matter (kitu) kama vitu vingine. Ufahamu ni umeme, na kama ni energy tunafahamu dhahiri sheria YA ULIMWENGU kuwa Energy yoyote haiwezi kufa wala kuharibiwa bali hubadilika katika hali moja kwenda nyingine. Mpaka leo hakuna energy inayokufa hivyo ni dhahiri kuwa UFAHAMU hauna mwisho.
Mwanzo wa kila kitu duniani ulianza katika UFAHAMU. Haijulikani katika ufahamu wa nani lakini bila UFAHAMU kuwepo, huu uumbaji na mageuzi ya ulimwengu yasingeanza. Hivyo Ufahamu umejigawa katika Ufahamu mingi na lengo ni Ufahamu mdogo kurudi katika ufahamu mkuu na kuwa Ufahamu mmoja kama mwanzo.
Kutopumua, ubongo kutofanya kazi na mapigo ya moyo kuacha sio kwamba Umekufa bali kilichokufa ni mwili tu. Mwili huu ni kama kitu chochote ukionacho kilivyo. Unajengwa na vitu (Chakula ni matter), Unazeeka (kama vile mwamba uliokaa muda mrefu), Unaumwa (kuingiliwa na uhai mwingine, vitu au chembechembe zozote zisivyo sahihi), Unakufa (Kufa kwa mwili ni kuurudisha katika uasili wake baada ya kuchoka), na mwili ukifa unarudi ardhini kwani umejengwa na chembechembe za dunia hii (Kila chakula kimetoka katika ardhi hii lakini tofauti ya chakula na vitu vingine ni kuwa hali ya chakula inaendana na mwili, hivyo chakula ni chembechembe zinazoendana na mwili na kuujenga mwili, kama vile mbao haiwezi kujengwa na mawe wala mawe hayawezi kuwa mbao ni kutokana na muundo wa chembechembe za kila kitu ulimwenguni upo kiupekee).
Hivyo kufa ni kukupa nafasi ufahamu wako kuchukua identity au hali mpya kwani kila kilichopo katika hali ya kifizikia kina mwisho, sema tu kila kitu kinatofautiana mwisho wake na kingine kwa muda tofauti tofauti. Lakini ufahamu hauna mwisho kwani ufahamu ni energy/nguvu kani. Na Ufahamu ndio NAFSI (Katika imani nyingine zinazoita nafsi au roho).