Kufa ni kufanya nini?

Kufa ni kufanya nini?

Hivi dini maana yake ni nini???
Cc; Jimena, Aretasludovick

Dini ni neno la kiarabu ambalo tafsiri yake ni NJIA kama alivyoieleza mkuu aretasludovick hapo juu 👆👆👆👆

kwa ufupi dini ni njia mengine ni mbwembwe tu, mana kupitia dini ndo watu huanza kujiona bora kuliko wengine
 
Last edited by a moderator:
scary staffs.nadhani kifo ndo kitu nnachokihofia zaidi duniani.Hivi humu ndani kuna asiyeamini kama kuna kifo or anayechukulia kifo kama playing game.?
 
Dini ni njia.
Kama kiongozi wa hiyo dini/njia amesema wanaume ni wanawake na wanawake ni wanaume, basi haina budi kukubali. Tena kwa 100%.

Lakini kumbuka dini ya kweli ipo moja tu! Hizi nyingine ni blah blah tu.

dini hiyo ya kweli ni ipi mkuu???
 
scary staffs.nadhani kifo ndo kitu nnachokihofia zaidi duniani.Hivi humu ndani kuna asiyeamini kama kuna kifo or anayechukulia kifo kama playing game.?

usiogope kifo mkuu, maana hata ukiogopa utakufa tuuu... ila furaha ni kuwa kuna maisha baada ya kifo.
 
Naomba kuelimishwa juu ya hiki kitu kufa.

Tukisema mtu kafa kinachokufa ni nini? Je, kutopumua ni kufa? Brain kutofanya kazi ni kufa? Mapigo ya moyo yakiacha kufanya kazi ndio kufa au roho kutoka ndio kufa?

Napata shida mno nisaidieni maana naanza kuhisi watu wanaweza kuwa wanazikwa wazima.

Naomba nikujibu maswali yako kutokana na jinsi nilivyotafuta mwenyewe majibu na kufahamu. Usiamini ninachosema ila chunguza na wewe upate majibu yako.

Kufa ni nini? Mwanadamu ni muunganiko wa huu MWILI na UFAHAMU. Na kila chenye uhai kina consciousness (ufahamu) lakini viumbe vinatofautiana hali na nafasi ya ufahamu na mwanadamu ndiye kiumbe chenye ufahamu wa juu zaidi. Ufahamu ni neno linalotumika kumaanisha hali zifuatazo- kujitambua (kujifahamu mimi ni nani na hiki ni nini), kumbukumbu zitokanazo na milango ya ufahamu (macho, masikio, pua, na kadhalika hukupa taarifa na ndio maana huitwa milango ya ufahamu), uwezo wa kufanya maamuzi, utambuzi na akili kwa ujumla. Ufahamu sio ubongo. Mpaka sasa ushahidi unaokubalika 100% ni kuwa UFAHAMU ni energy/nguvu. Ndani ya ubongo kuna seli maalum kupitisha umeme. Kumbukumbu ni umeme. Ufahamu ni umeme. Wazo ni Umeme. Hisia ni umeme. Unaweza usifahamu ni umeme kutokana na umeme uliouzoea majumbani lakini frequency yake ni umeme.

Kwa mwanadamu tunasema kufa ni UFAHAMU unapouacha MWILI lakuna hakuna kifo cha UFAHAMU au MWISHO WA UFAHAMU. Mwili ni matter (kitu) kama vitu vingine. Ufahamu ni umeme, na kama ni energy tunafahamu dhahiri sheria YA ULIMWENGU kuwa Energy yoyote haiwezi kufa wala kuharibiwa bali hubadilika katika hali moja kwenda nyingine. Mpaka leo hakuna energy inayokufa hivyo ni dhahiri kuwa UFAHAMU hauna mwisho.

Mwanzo wa kila kitu duniani ulianza katika UFAHAMU. Haijulikani katika ufahamu wa nani lakini bila UFAHAMU kuwepo, huu uumbaji na mageuzi ya ulimwengu yasingeanza. Hivyo Ufahamu umejigawa katika Ufahamu mingi na lengo ni Ufahamu mdogo kurudi katika ufahamu mkuu na kuwa Ufahamu mmoja kama mwanzo.

Kutopumua, ubongo kutofanya kazi na mapigo ya moyo kuacha sio kwamba Umekufa bali kilichokufa ni mwili tu. Mwili huu ni kama kitu chochote ukionacho kilivyo. Unajengwa na vitu (Chakula ni matter), Unazeeka (kama vile mwamba uliokaa muda mrefu), Unaumwa (kuingiliwa na uhai mwingine, vitu au chembechembe zozote zisivyo sahihi), Unakufa (Kufa kwa mwili ni kuurudisha katika uasili wake baada ya kuchoka), na mwili ukifa unarudi ardhini kwani umejengwa na chembechembe za dunia hii (Kila chakula kimetoka katika ardhi hii lakini tofauti ya chakula na vitu vingine ni kuwa hali ya chakula inaendana na mwili, hivyo chakula ni chembechembe zinazoendana na mwili na kuujenga mwili, kama vile mbao haiwezi kujengwa na mawe wala mawe hayawezi kuwa mbao ni kutokana na muundo wa chembechembe za kila kitu ulimwenguni upo kiupekee).

Hivyo kufa ni kukupa nafasi ufahamu wako kuchukua identity au hali mpya kwani kila kilichopo katika hali ya kifizikia kina mwisho, sema tu kila kitu kinatofautiana mwisho wake na kingine kwa muda tofauti tofauti. Lakini ufahamu hauna mwisho kwani ufahamu ni energy/nguvu kani. Na Ufahamu ndio NAFSI (Katika imani nyingine zinazoita nafsi au roho).
 
sijakuelewa bado kwenye suala la ufahamu kuacha mwili, maana umesema nafs/ufaham ni kujitambua inayotokana na milango ya fahamu kama pua, macho n.k
na ufaham umesema ni energy na energy haifi... .. . sasa ni sabab gani inasababisha ufaham uachanee na mwili(uthibitisho)
 
Ubongo ukiacha kufanya kazi
Hakuna cha soul sijui spirit or body imefanyanini.
Wala dini hawezi tuambia kitu ni science tu.

wakati umelala je ubongo unakua unafanya kazi? au mtu unapopigwa nusu kaputi ubongo unakua unafanya kazi???
 
Sasa mkuu tunaomba ututafasirie neno imani kwa ufasaha...

Tatizo si ipi tafsiri fasaha,maana kuna tafsiri nyingi tu ila hoja yangu ni kwamba wanaotafsiri kuwa imani kama ni uongo wapo nje ya maana ya hilo neno.
 
Ndio unakuwa unafanya kazi kwani waga unatumia nn kuota?

sasa kama umelala na ubongo unakuwa unafanya kazi kwann unashindwa kusens vitu vinavyoendelea nje yako, kwa mfano mtu ukiwa umelala usingizi mzito/nusu kaputi ni vigumu kunusa,kuhisi,kuona hata kama macho yapo wazi,kusikia n.k

ninavojua japo si kwa undani sana kuwa kazi ya ubongo ni ku interpret, sasa kama kuna sauti ila hausikii, kuna harufu ila hunusi, kuna maumivu ila huisi, kuna picha au taswira ila huoni n.k inakuaje tuseme ubongo unafanya kazi?

Au kazi za ubongo ni zipi hasa?
 
sasa kama umelala na ubongo unakuwa unafanya kazi kwann unashindwa kusens vitu vinavyoendelea nje yako, kwa mfano mtu ukiwa umelala usingizi mzito/nusu kaputi ni vigumu kunusa,kuhisi,kuona hata kama macho yapo wazi,kusikia n.k
ninavojua japo si kwa undani sana kuwa kazi ya ubongo ni ku interpret, sasa kama kuna sauti ila hausikii, kuna harufu ila hunusi, kuna maumivu ila huisi, kuna picha au taswira ila huoni n.k inakuaje tuseme ubongo unafanya kazi???.
Au kazi za ubongo ni zipi hasa???.

Ndugu nikuulize kitu
Sasa ukiwa na udingizi mzito unamaanisha unakuwa umekufa au?
Wewe unachanga na kitu kinaitwa *consciousness*
To sense something means you are conscious about something. Hiyo ndio unayomaanisha
 
Ndio maana mkuu naomba unieleweshe,
kwani ubongo kazi yake ni nini???
 
usiogope kifo mkuu, maana hata ukiogopa utakufa tuuu... ila furaha ni kuwa kuna maisha baada ya kifo.

Maisha baada ya kifo? yanategemea nini?I mean hayo ni kwa watu wote? na kwanini tusiishi moja kwa moja pasi na kufa?
 
Back
Top Bottom