Kufananisha mafuriko ya Rufiji na yanayotokea sehemu nyingine ya nchi ni kutaka kuficha udhaifu wa viongozi na watendaji

Kufananisha mafuriko ya Rufiji na yanayotokea sehemu nyingine ya nchi ni kutaka kuficha udhaifu wa viongozi na watendaji

Nimeona sasa baada ya mafuriko (na si mafuriko bali "maji kujaa ktk Barabara na majengo yaliyo kando") baadhi ya watu wameona kuwa hilo ndilo jibu la mafuriko ya Rufiji.

Ukweli ni kwamba mafuriko ya Rufiji kamwe hayawezi kuwa sawa na mengine kwa sababu,

1. Ukubwa wa mafuriko na eneo kubwa ambalo sasa inakwenda kumezwa Rufiji nzima haiwezi kuwa sawa na kujaa kwa maji katika mitaro, barabara na sehemu ndogo jirani na miundo mbinu hiyo, tofauti na huko Rufiji ambako tunaona kimo cha nyumba nzima ikizama majini.

2. Hayo yanayoitwa mafuriko ktk maeneo mengine huchukua muda mfupi usiozidi wiki moja kuisha na kisha shughuli zingine kuendelea na hii hudhihirisha sababu yake kuwa ni mvua, yatofauti na Rufiji ambako yalianza tangu kutangazwa kwa bwawa kujaa na hadi sasa hakuna dalili ya kupungua bali ni kuongezeka kwa namna hii ni wazi Rufiji ipo sababu ya ziada ya mafuriko hayo

3. Kufananisha mafuriko yoyote na yale ya Rufiji ni kuwahadaa wananchi na kuwapa viongozi na watendaji nguvu ya kutowajibika ktk uzembe ambao wamekuwa wakiufanya kwa maksudi wakitufanya sisi wananchi kama wajinga.

4. Ikumbukwe kuwa moja ya hoja za kuhalalisha ujenzi wa bwawa la Rufiji ilikuwa ni kupunguza au kumaliza tatizo la mafuriko lililowahi tokea kwa kujenga miundo mbinu mingine saidizi itakayo weza kutumika kwa uzalishaji pale bwawa litakapo kuwa limezidiwa. Sasa tujiulize hali hii iliyo kinyume nini kimetikea?

5. Wanaodai kuwa mvua ni nyingi mwaka huu kiasi cha husabanisha hayo mafuriko ya Rufiji, nao pia ni uongo kwa sababu bado mvua za mwaka huu hazijawa nyingi kufikia vipimo vya miaka ya nyuma ambayo haikuwahi kushuhudiwa ukubwa wa mafuriko ya eneo kubwa karibia lote la Rufiji likizama.

Ukweli usemwe, kuteleza si kuanguka, viongozi, watendaji na chawa wao wasiendelee kuwafanya wananchi wajinga kwa kulazimisha sisi wananchi tuione nyeupe huku kukiwa ni giza Totoro "nyeusi"
Kwa hiyo kama mvua sio nyingi hayo maji yanatoka wapi? Kwani hilo ni bwawa la kuzalisha maji? Kama mvua ingekuwa ndogo unafikiri maji ya bwawa yangefunguliwa? Hivi kusingelikuwa na bwawa je? Bavicha punguzeni ujuaji
 
Kwa hiyo kama mvua sio nyingi hayo maji yanatoka wapi? Kwani hilo ni bwawa la kuzalisha maji? Kama mvua ingekuwa ndogo unafikiri maji ya bwawa yangefunguliwa? Hivi kusingelikuwa na bwawa je? Bavicha punguzeni ujuaji
Mbona hii logic ya kawaida tu, ni hivi bwawa lilikusanya maji mengi Sana, mvua zilizonyesha zimekusanya maji ya mvua (nayo ni mengi) lakini baada ya kutapishwa kwa ghafla kwa maji ya bwawa Ndiyo yameongeza wingi mkubwa na kasi zaidi iliyosambaa mbali zaidi ya mkondo wenyewe.

Na kama bwawa lisingekuwepo maji yangekuwa mengi (na si mengi Sana na kasi yake isingekuwa kubwa kwenda eneo kubwa) kiasi kwamba mafuriko yangekuwa madogo ktk eneo dogo.

Bado wananchi tunauliza,
tuliambiwa uwepo wa bwawa utaondoa mafuriko, na kutakuwepo na miundo mbinu ya pembeni ya kuwezesha uzalishaji baada ya bwawa kutapishwa au kuzidiwa maji. Je viko wapi?
 
Leo kuna mafuriko Kisongo Arusha. Nayo yamesababishwa na Bwawa na Nyerere alilojenga Hayati Rais Magufuli!??
 
Leo kuna mafuriko Kisongo Arusha. Nayo yamesababishwa na Bwawa na Nyerere alilojenga Hayati Rais Magufuli!??
Soma tena uelewe, Arusha ni maji kuzidi usawa wa mikondo yake mifereji na barabara na maji kuingia ktk .baadhi ya majengo yaliyo karibu na mikondo hiyo.

Arusha hakuna nyumba iliyozama kwa ukubwa wake lakini pia baada ya mvua kuisha maji yamepungua.

Ni tofauti na Rufiji ambako karibia Rufiji yote inazama hadi baadhi ya nyumba paa hazionekani, na hakuna dalili za mafuriko hayo kupungua ila yanazidi kuongezeka kwa zaidi ya mwezi sasa.

Hata kama ni mtetezi wa viongozi tukubaliane sote kama wananchi tunaoumizwa na maafa kuwa kuna dosari ktk mafuriko ya rufiji na wala hakuna anayekataa uwepo wa bwawa bali ni kiwataka watendaji kuwajibika kwa namna yoyote ya kuepusha ukubwa wa madhara.

Mfano ni wajibu wa serikali kuwa wangaliweza kuwa walikwisha wahamisha au kuwashinikiza kuondoka hata kabla ya hasara inayotokea sasa.
 
Back
Top Bottom