Kufananisha mafuriko ya Rufiji na yanayotokea sehemu nyingine ya nchi ni kutaka kuficha udhaifu wa viongozi na watendaji

Kwa hiyo kama mvua sio nyingi hayo maji yanatoka wapi? Kwani hilo ni bwawa la kuzalisha maji? Kama mvua ingekuwa ndogo unafikiri maji ya bwawa yangefunguliwa? Hivi kusingelikuwa na bwawa je? Bavicha punguzeni ujuaji
 
Kwa hiyo kama mvua sio nyingi hayo maji yanatoka wapi? Kwani hilo ni bwawa la kuzalisha maji? Kama mvua ingekuwa ndogo unafikiri maji ya bwawa yangefunguliwa? Hivi kusingelikuwa na bwawa je? Bavicha punguzeni ujuaji
Mbona hii logic ya kawaida tu, ni hivi bwawa lilikusanya maji mengi Sana, mvua zilizonyesha zimekusanya maji ya mvua (nayo ni mengi) lakini baada ya kutapishwa kwa ghafla kwa maji ya bwawa Ndiyo yameongeza wingi mkubwa na kasi zaidi iliyosambaa mbali zaidi ya mkondo wenyewe.

Na kama bwawa lisingekuwepo maji yangekuwa mengi (na si mengi Sana na kasi yake isingekuwa kubwa kwenda eneo kubwa) kiasi kwamba mafuriko yangekuwa madogo ktk eneo dogo.

Bado wananchi tunauliza,
tuliambiwa uwepo wa bwawa utaondoa mafuriko, na kutakuwepo na miundo mbinu ya pembeni ya kuwezesha uzalishaji baada ya bwawa kutapishwa au kuzidiwa maji. Je viko wapi?
 
Leo kuna mafuriko Kisongo Arusha. Nayo yamesababishwa na Bwawa na Nyerere alilojenga Hayati Rais Magufuli!??
 
Leo kuna mafuriko Kisongo Arusha. Nayo yamesababishwa na Bwawa na Nyerere alilojenga Hayati Rais Magufuli!??
Soma tena uelewe, Arusha ni maji kuzidi usawa wa mikondo yake mifereji na barabara na maji kuingia ktk .baadhi ya majengo yaliyo karibu na mikondo hiyo.

Arusha hakuna nyumba iliyozama kwa ukubwa wake lakini pia baada ya mvua kuisha maji yamepungua.

Ni tofauti na Rufiji ambako karibia Rufiji yote inazama hadi baadhi ya nyumba paa hazionekani, na hakuna dalili za mafuriko hayo kupungua ila yanazidi kuongezeka kwa zaidi ya mwezi sasa.

Hata kama ni mtetezi wa viongozi tukubaliane sote kama wananchi tunaoumizwa na maafa kuwa kuna dosari ktk mafuriko ya rufiji na wala hakuna anayekataa uwepo wa bwawa bali ni kiwataka watendaji kuwajibika kwa namna yoyote ya kuepusha ukubwa wa madhara.

Mfano ni wajibu wa serikali kuwa wangaliweza kuwa walikwisha wahamisha au kuwashinikiza kuondoka hata kabla ya hasara inayotokea sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…