Kufananisha Subaru SJG na LC 300 series ni matusi!

Kufananisha Subaru SJG na LC 300 series ni matusi!

Shida mnanunua magari kwa sababu umeyaona Serikali inayatumia ila ungekua na chaguo la kuona magari tofauti mengi usingeandika ulichoandika hapa...
Tumemeza Mkuu...tusamehe..ila huko barabarani..kuna ligi ambazo ni moto😀😀
Huwa nawaza sana hizi magari kuna tumechezo chezo usipoelewa unataka nini basi umepotea.
 
Tumemeza Mkuu...tusamehe..ila huko barabarani..kuna ligi ambazo ni moto😀😀
Huwa nawaza sana hizi magari kuna tumechezo chezo usipoelewa unataka nini basi umepotea.
Hii hapa ni yard ya magari hapo four ways Johannesburg pana gari za kutosha ukiwa na hela utatoka na gari yeyote nzuri tu hapo sio kwa haya tuliyoyameza..
20260206_121809.jpg
 
Motech-i anapambanisha haya magari kwenye suala la mbio tu, yaani kukimbizana barabarani mfano useme kuwe na ligi ya nani atawahi kufika Dodoma n.k

Labda uzi wako ungejikita hapo zaidi ya hizo physics nyingine ambazo yule fundi hakuwa anazilinganisha...
Hii debate hata Mimi nilifuatilia kule Instagram...
Huyu dogo kwenye ishu za mambo ya ufundi wa magari anajua Sana ila kuna muda huwa anapenda kufurahisha genge tu
Ila Kwa Subaru forester SJG za Singapore hii inaweza kabisa kushindana na LC 300 bila shida, subaru za Singapore ni noma Sana kwenye mbio
 
Subaru ni gari mazee sema wazee tunaona vijana wanaongea tu niliwahi kuwa na Ford ya 2024 naitafuta Daslm kutokea Tunduma nilipofika Iringa nikakutana na bwana mdogo mmoja ana Subaru moja matata sana ahaa kila nikitoa mguu yupo mpaka daslm wakati hiyo mashine gari nyingi zitasoma namba ilikua usiku nikasema hawa wadogo kumbe gari zao ni za ukweli pia..
Niliwahi kuleta Subaru moja siwezi kutuma picha maana nilishaiuza aisee nilitembea bila kuchoka kutoka Jozi mpaka Tunduma mwanzo nilijua ni gari nzito kumbe sio..
 
Ikiwa kwenye tope inazama inavuta na inatoka au unazungumzia inavuta ikiwa nje ya tope?
Soma vizuri na uelewe hiyo 'vuta' nimemaanisha nini; usipoelewa tena rudi nikufafanulie vizuri,sawa?
 
Subaru ni gari mazee sema wazee tunaona vijana wanaongea tu niliwahi kuwa na Ford ya 2024 naitafuta Daslm kutokea Tunduma nilipofika Iringa nikakutana na bwana mdogo mmoja ana Subaru moja matata sana ahaa kila nikitoa mguu yupo mpaka daslm wakati hiyo mashine gari nyingi zitasoma namba ilikua usiku nikasema hawa wadogo kumbe gari zao ni za ukweli pia..
Niliwahi kuleta Subaru moja siwezi kutuma picha maana nilishaiuza aisee nilitembea bila kuchoka kutoka Jozi mpaka Tunduma mwanzo nilijua ni gari nzito kumbe sio..
Hata hivyo huyo jamaa alijitahidi Sana maana kuifukuza ford ranger kutoka iringa Hadi DAR sio mchezo hata kidogo
 
Hii debate hata Mimi nilifuatilia kule Instagram...
Huyu dogo kwenye ishu za mambo ya ufundi wa magari anajua Sana ila kuna muda huwa anapenda kufurahisha genge tu
Ila Kwa Subaru forester SJG za Singapore hii inaweza kabisa kushindana na LC 300 bila shida, subaru za Singapore ni noma Sana kwenye mbio
Hayo malc300 kwenye mbio ni gari ya kawaida tu ndiyo maana zinapitwa hata na subaru wewe hujiulizi kwanini hao watu wa masubaru huwezi kuta wakishindani mbio na marange rover
 
Wanabodi za wikiendi! Nimekuwa nikifuatilia huu mjadala unaoendelea Instagram kuhusu Subaru SJG vs Land Cruiser 300. Kuna hoja zinatolewa kwa confidence sana kwamba Forester SJG inaweza kuipiku LC300. Binafsi nikaona ni vyema tuweke hisia pembeni, tuangalie uwezo wa magari haya kwa uhalisia wa kiufundi na matumizi halisi ya mazingira yetu ya Tanzania.

Kwanza kabisa, ni muhimu kuelewa haya ni magari ya madaraja mawili tofauti kabisa. Land Cruiser 300 ni full size heavy duty SUV iliyoundwa kwa kazi nzito, safari ndefu, kuvuta mizigo na kupita maeneo magumu. Subaru Forester SJG ni compact SUV yenye AWD nzuri sana kwa matumizi ya kila siku na barabara za mazingira yetu.

Hapo tu tayari tunalinganisha ndizi na nanasi!!

Ukianza na suala la nguvu na torque, hapa LC300 inaongoza bila mjadala. Sasa kule insta kuna dogo naona alipata 'D' ya fizikia naona anadanganya umma nikasema acha nami nitoe maoni yangu hapa!

Injini LC 300 series za V6 twin-turbo (hasa diesel 3.3L kwenye baadhi ya matoleo) zina torque kubwa sana inayofika karibu 700Nm (hii torque ni magari machache sana hapa bongo yanafikia US wanafikia hii sababu ya aina ya magari wanayopendelea kumiliki yaani premium higher performance vehicles).
Hii 700 si torque ya kimasihara asee! sio mchezo (kwa asieelewa torque hii ni kama nguvu ya mtu anayesukuma mlango mzito kadri anavyokuwa na nguvu ndivyo mlango unavyofunguka kirahisi).

Torque ya LC ni ya kuvuta trailer, kupanda milima na kusukuma gari zito kwenye matope au mchanga mzito bila kusumbuka. Sasa hii forester SJG hata ile ya turbo 2.0XT, ina nguvu nzuri kwa daraja lake lakini haiwezi kulinganishwa na torque ya LC300. Hii ni physics tu ya watengenezaji, si mapenzi ya brand naona dogo kule analeta tu mapenzi ya subaru!

Ukija kwenye mfumo wa uendeshaji, Subaru anajulikana kwa 'symmetrical AWD' yake ambayo ni bora sana kwa utulivu wa ndinga barabarani, mvua, kona na barabara za udongo zisizo kali. Lakini LC300 iko level nyingine. Ina low-range gearbox, diff lock, crawl control, multi-terrain select na mfumo wa E-KDSS unaosaidia suspension kujirekebisha kwenye off-road ngumu. Hii ina maana LC300 imeundwa kupita sehemu ambazo Forester itahitaji dereva awe makini sana au aishie kugeuza.

Ground clearance na uwezo wa kuvuka maji na matuta pia ni tofauti. LC300 iko juu zaidi, ina clearance kubwa na uwezo wa kuvuka maji marefu zaidi. Hii ndiyo sababu utaona mashirika, miradi ya ujenzi, safari za porini na hata watu wa mikoani wanaitegemea sana Land Cruiser. Ni gari la kuaminika kwenye mazingira ambayo barabara si lami tu.

Kwenye suala la kuvuta trela na kubeba mizigo, LC300 inaweza kuvuta hadi tani 3.5 bila shida. Hapa Forester haipo hata karibu. Forester ni nzuri kwa familia, safari za kawaida na matumizi ya mjini na highway, lakini si gari la kuvuta trela nzito au kubeba kazi nzito kila siku.

Lakini kusema SJG inaweza kuipiku LC300 kwa uwezo wa jumla wa kiutendaji na off-road ya kueleweka kama kule kwetu igowole, hapo tunakuwa tunajipa moyo tu. LC300 imejengwa kwa filosofi ya 'durability', torque na mazingira tata.

Kwa mazingira yetu kibongobongo, ukiongelea safari za mbali, barabara mbovu, kuvuka mito, kubeba mizigo au matumizi ya kikazi, LC300 bado ni mfalme. Ukiongelea matumizi ya kila siku, gharama nafuu za uendeshaji na comfort ya familia, Forester SJG inafanya kazi vizuri sana.

Mwisho wa siku, si kila comparison ni battle. Wakati mwingine ni kuelewa gari limeundwa kwa kazi gani. LC300 na Forester SJG kila moja ina nafasi yake lakini kwenye uwezo wa kiufundi na off-road serious, LC300 iko daraja lingine kabisa madogo na timu subaru acheni LC awe LC hata LC series ya nyuma inamkalisha huyo subaru wenu.View attachment 3546983

Wanabodi mliowahi kumiliki au kuendesha zote mbili kwenye mazingira ya Tanzania, mna uzoefu gani halisi? Tupeane uhalisia badala ya ushabiki wa brand.
Ikiwa kigezo ni KUCHANGANYA SPEED upesi wakati wa kuanza kuondoka……. Yes kuna magari mengi sana madogo yanaweza kuizidi LC300 kwenye KUANZA

LAKINI hii haiondoi ukweli kwamba LC300 ni gari BORA tena mbali kabisa kuliko Subaru SJG karibu kwenye kila idara…..,,, Hawapo Daraja moja hata kidogo

Mind you that
DAR to DOM
Ikiwa kila kitu kitakua sawa, mfano madereva wenye ujuzi sawa, barabara iwe nyeupe kama msafara wa rais😂,

Kuanzia Dar hadi kama kibaha hivi SJG itaongoza halafu taratibu zikianza kona na vilima hapo ndio LC300 atakuja kucover na kuipita SJG
Mwisho wa safari mshindi atakua LC300
Lakini ikiwa barabara itakua busy mara upunguze speed halafu uanze kuchanganya tena ku overtake, mijini nk……. Hapo Subaru ataweza kumsumbua LC300

Kwenye Rough road ndio kabisaaaa
Mfano Singida via Itigi to Mbeya…… yaani LC300 atakua kashafika mbeya kaoga na yuko zake baa ana bia kama ya 5 hivi ndio Subaru ataingia Mbeya
 
Muache kutuchosha sasa lc 300 haina maajabu yoyote kwenye mbio hata muitete vipi mara mlimani sijui nini ,mara rough road
 
Ikiwa kigezo ni KUCHANGANYA SPEED upesi wakati wa kuanza kuondoka……. Yes kuna magari mengi sana madogo yanaweza kuizidi LC300 kwenye KUANZA

LAKINI hii haiondoi ukweli kwamba LC300 ni gari BORA tena mbali kabisa kuliko Subaru SJG karibu kwenye kila idara…..,,, Hawapo Daraja moja hata kidogo

Mind you that
DAR to DOM
Ikiwa kila kitu kitakua sawa, mfano madereva wenye ujuzi sawa, barabara iwe nyeupe kama msafara wa rais😂,

Kuanzia Dar hadi kama kibaha hivi SJG itaongoza halafu taratibu zikianza kona na vilima hapo ndio LC300 atakuja kucover na kuipita SJG
Mwisho wa safari mshindi atakua LC300
Lakini ikiwa barabara itakua busy mara upunguze speed halafu uanze kuchanganya tena ku overtake, mijini nk……. Hapo Subaru ataweza kumsumbua LC300

Kwenye Rough road ndio kabisaaaa
Mfano Singida via Itigi to Mbeya…… yaani LC300 atakua kashafika mbeya kaoga na yuko zake baa ana bia kama ya 5 hivi ndio Subaru ataingia Mbeya
Hahahaha
Hatari sanaaa
 
Back
Top Bottom