RugambwaYT
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 1,444
- 2,032
Mkuu, usiumie kichwa. LC300 ni next level. Ina speed sana kulinganisha na Land Cruisers za nyuma yake, na magari mengine mengi tu.Ikiwa kigezo ni KUCHANGANYA SPEED upesi wakati wa kuanza kuondoka……. Yes kuna magari mengi sana madogo yanaweza kuizidi LC300 kwenye KUANZA
LAKINI hii haiondoi ukweli kwamba LC300 ni gari BORA tena mbali kabisa kuliko Subaru SJG karibu kwenye kila idara…..,,, Hawapo Daraja moja hata kidogo
Mind you that
DAR to DOM
Ikiwa kila kitu kitakua sawa, mfano madereva wenye ujuzi sawa, barabara iwe nyeupe kama msafara wa rais😂,
Kuanzia Dar hadi kama kibaha hivi SJG itaongoza halafu taratibu zikianza kona na vilima hapo ndio LC300 atakuja kucover na kuipita SJG
Mwisho wa safari mshindi atakua LC300
Lakini ikiwa barabara itakua busy mara upunguze speed halafu uanze kuchanganya tena ku overtake, mijini nk……. Hapo Subaru ataweza kumsumbua LC300
Kwenye Rough road ndio kabisaaaa
Mfano Singida via Itigi to Mbeya…… yaani LC300 atakua kashafika mbeya kaoga na yuko zake baa ana bia kama ya 5 hivi ndio Subaru ataingia Mbeya
Ila kwa upande speed, inazidiwa au inaweza kuzidiwa na magari mengine mengi tu. Hata ya Toyota, hasa yale yaliyotengenezwa kwa ajili ya mbio (e.g GR Corolla, GR Yaris, Rav4 Prime).
Ila haya yote hayatii mguu kwenye LC300 kama gari. Sababu haikutengenezwa kwa sababu ya kukimbizana. SUV zote hazijatengenezwa kwa mbio, physics (e.g higher centre of gravity, body on frame contruction, body roll, uzito mkubwa etc) yake inakataa.
SUV Inaweza kuwa na mbio kuliko gari dogo kwenye straight line, ila kwenye kona ikawa hatari kupita kwa kasi kubwa. Wakati gari dogo vile centre of gravity yake iko chini, linaweza kupita kwenye kona kwa kasi zaidi bila kuhatarisha maisha ya gari na dereva.