Kufananisha Subaru SJG na LC 300 series ni matusi!

Shida mnanunua magari kwa sababu umeyaona Serikali inayatumia ila ungekua na chaguo la kuona magari tofauti mengi usingeandika ulichoandika hapa...
Tumemeza Mkuu...tusamehe..ila huko barabarani..kuna ligi ambazo ni moto😀😀
Huwa nawaza sana hizi magari kuna tumechezo chezo usipoelewa unataka nini basi umepotea.
 
Tumemeza Mkuu...tusamehe..ila huko barabarani..kuna ligi ambazo ni moto😀😀
Huwa nawaza sana hizi magari kuna tumechezo chezo usipoelewa unataka nini basi umepotea.
Hii hapa ni yard ya magari hapo four ways Johannesburg pana gari za kutosha ukiwa na hela utatoka na gari yeyote nzuri tu hapo sio kwa haya tuliyoyameza..
 
Hii debate hata Mimi nilifuatilia kule Instagram...
Huyu dogo kwenye ishu za mambo ya ufundi wa magari anajua Sana ila kuna muda huwa anapenda kufurahisha genge tu
Ila Kwa Subaru forester SJG za Singapore hii inaweza kabisa kushindana na LC 300 bila shida, subaru za Singapore ni noma Sana kwenye mbio
 
Subaru ni gari mazee sema wazee tunaona vijana wanaongea tu niliwahi kuwa na Ford ya 2024 naitafuta Daslm kutokea Tunduma nilipofika Iringa nikakutana na bwana mdogo mmoja ana Subaru moja matata sana ahaa kila nikitoa mguu yupo mpaka daslm wakati hiyo mashine gari nyingi zitasoma namba ilikua usiku nikasema hawa wadogo kumbe gari zao ni za ukweli pia..
Niliwahi kuleta Subaru moja siwezi kutuma picha maana nilishaiuza aisee nilitembea bila kuchoka kutoka Jozi mpaka Tunduma mwanzo nilijua ni gari nzito kumbe sio..
 
Ikiwa kwenye tope inazama inavuta na inatoka au unazungumzia inavuta ikiwa nje ya tope?
Soma vizuri na uelewe hiyo 'vuta' nimemaanisha nini; usipoelewa tena rudi nikufafanulie vizuri,sawa?
 
Hata hivyo huyo jamaa alijitahidi Sana maana kuifukuza ford ranger kutoka iringa Hadi DAR sio mchezo hata kidogo
 
Hayo malc300 kwenye mbio ni gari ya kawaida tu ndiyo maana zinapitwa hata na subaru wewe hujiulizi kwanini hao watu wa masubaru huwezi kuta wakishindani mbio na marange rover
 
Ikiwa kigezo ni KUCHANGANYA SPEED upesi wakati wa kuanza kuondoka……. Yes kuna magari mengi sana madogo yanaweza kuizidi LC300 kwenye KUANZA

LAKINI hii haiondoi ukweli kwamba LC300 ni gari BORA tena mbali kabisa kuliko Subaru SJG karibu kwenye kila idara…..,,, Hawapo Daraja moja hata kidogo

Mind you that
DAR to DOM
Ikiwa kila kitu kitakua sawa, mfano madereva wenye ujuzi sawa, barabara iwe nyeupe kama msafara wa rais😂,

Kuanzia Dar hadi kama kibaha hivi SJG itaongoza halafu taratibu zikianza kona na vilima hapo ndio LC300 atakuja kucover na kuipita SJG
Mwisho wa safari mshindi atakua LC300
Lakini ikiwa barabara itakua busy mara upunguze speed halafu uanze kuchanganya tena ku overtake, mijini nk……. Hapo Subaru ataweza kumsumbua LC300

Kwenye Rough road ndio kabisaaaa
Mfano Singida via Itigi to Mbeya…… yaani LC300 atakua kashafika mbeya kaoga na yuko zake baa ana bia kama ya 5 hivi ndio Subaru ataingia Mbeya
 
Muache kutuchosha sasa lc 300 haina maajabu yoyote kwenye mbio hata muitete vipi mara mlimani sijui nini ,mara rough road
 
Hahahaha
Hatari sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…