“Kufanikisha kazi si lazima niwepo” - Rais Xi Jinping wa China

“Kufanikisha kazi si lazima niwepo” - Rais Xi Jinping wa China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1.jpg

Mei 9, 2014, Xi Jinping alipofanya ukaguzi mkoani Henan, aliangalia hali ya ukuaji wa ngano kwenye mashamba ya Zhangshi Wilaya ya Weishi

Baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama, Bw. Xi Jinping alipotoa hotuba mara kwa mara alisisitiza nia yake kuhusu kusukuma mbele mageuzi, huku akitetea kujikomboa kifikra ili kupanua shughuli zetu na kufanya uvumbuzi. Machoni mwa maofisa na watu, Xi ni kiongozi aliyejikomboa kifikra na kutupia macho mbele na mwenye ari kubwa ya kufanya mageuzi.

Bw. Xi alipofanya kazi mjini Xiamen, ambao ni moja ya maeneo maalumu ya uchumi nchini China, aliongoza kazi ya kutunga “Mikakati ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Mji wa Xiamen ya Mwaka 1985-2000”, baadaye mikakati hiyo imekuwa mwongozo muhimu wa serikali ya mji huo katika kutunga sera za uchumi, mipango ya maendeleo na utekelezaji wa mipango hiyo. Akiwa ofisa mwandamizi wa idara za mageuzi ya mifumo na usimamizi na ujenzi wa Mji wa Xiamen, alifanya utafiti na kubuni hatua mbalimbali za kusukuma mbele mageuzi na kufungua mlango katika eneo maalumu la uchumi. Alifanya juhudi za kuuwezesha Mji wa Xiamen upate haki ya uchumi kama mkoa, na kuongoza uratibu na utatuzi wa masuala mengi muhimu katika kupata haki hiyo, na kuupatia mji huo mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu.

2.jpg


Disemba 30, 2012, Xi Jinping alipokwenda kutoa pole kwa watu wenye matatizo ya kiuchumi wa Wilaya ya Fuping mkoani Hebei, alimtembelea mzee Tang Rongbin na familia yake katika Kijiji cha Luotuowan cha Wilaya ya Longguan

Wakati alipofanya kazi katika Wilaya ya Zhengding mkoani Hebei, Bw. Xi aliambiwa na wengine, kwamba kikundi cha kutengeneza tamthiliya ya Ndoto Kwenye Jumba Jekundu kilikuwa kinatafuta sehemu yenye mandhari zinazofaa kwa ajili ya tamthiliya hiyo. Baada ya kuafikiana na kikundi hicho, aliishawishi serikali ya wilaya hiyo kutenga fedha kujenga Jumba la Rongguo na siku za baadaye likawa bustani ya utalii. Mwaka huo, mapato ya Jumba la Rongguo yalifikia Yuan zaidi ya milioni 10, ambayo ni makubwa kuliko uwekezaji wake. Wakati huo Bw. Xi aliondoka Zhengding na kwenda kuanza kazi mjini Xiamen. Jumba la Rongguo limeinufaisha sana Wilaya ya Zhengding. Baada ya tamthiliya ya kuonyeshwa kwa Ndoto Kwenye Jumba Jekundu, tamthiliya nyingine zipatazo zaidi ya 170 zilitengenezwa huko na idadi ya watalii waliotembelea jumba hilo walifikia zaidi ya milioni moja kwa mwaka.

3.jpg


Xi Jinping alipokuwa Fuzhou akicheza na binti yake
Wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Fujian, Bw. Xi alianzisha kampeni dhidi ya uchafuzi wa chakula mwaka 2001 na kujenga mradi maalumu wa kutoa “vyakula visivyo na uchafuzi”, na kupongezwa na umma.

Mwaka 1999, Bw. Xi alikuwa mtu wa kwanza aliyetoa pendekezo la kujenga “Fujian ya Kidigitali”, ambalo lilipitishwa rasmi kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la Mkoa wa Fujian mwaka 2000.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa kikundi cha uongozi wa ujenzi wa “Fujian ya Kidigitali”. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, mtandao usioonekana wa “Fujian ya Kidigitali” ulikamilika na kutoa huduma bora kwa ajili ya uzalishaji mali na maisha ya umma, shughuli za kijamii na usimamizi wa miji, na kubadilisha mtindo wa maisha ya watu. Hadi kufikia mwaka 2010, Fujian ulikuwa mkoa pekee uliowezesha matumizi ya kadi moja ya kulipia katika hospitali zote mkoani.

4.jpg


Xi Jinping anakagua kazi za uhifadhi wa mazingira mkoani Fujian

“Tunapotamani milima ya dhahabu na fedha, hatuwezi kupuuza kazi ya kulinda mazingira ya asili.” Bw. Xi anatilia maanani sana kazi za kulinda mazingira ya asili na kupendekeza kufanya mazingira mazuri yahimize maendeleo mazuri ya uchumi na kuwanufaisha watu wa vizazi vijavyo. Kutokana na kukabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu ya Changting mkoani Fujian, mwaka 2002 alitangulia kutoa mpango wa kimkakati wa kujenga mkoa wenye mazingira mazuri ya asili na mkoa wa Fujian ulikuwa mmoja wa mikoa iliyotangulia kufanya majaribu ya kutekeleza mpango huo. Baada ya juhudi za miaka zaidi ya 10, milima iliyoachwa ya sehemu ya Changting ilifunikiwa tena na miti na majani, huku Fujian ukiwa mkoa pekee wenye maji, hewa na mazingira bora zaidi nchini China.

5.jpg

Mwezi Januari, 2007, Xi Jinping alipokuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Zhejiang aliwapikia wazee walioishi katika Nyumba ya kutunza wazee ya Pingdu ya Wilaya ya Qingyuan mkoani Zhejiang

Mwaka 2002, Bw. Xi alianza kufanya kazi katika mkoa wa Zhejiang, ambao ni moja kati ya sehemu zilizoendelea zaidi kiuchumi nchini China. Baada ya kufanya ukaguzi na utafiti kwa wingi na kwa kina, Bw. Xi alitoa na kuongoza utekelezaji wa “Mikakati ya Nane Nane”4, yaani “kusukuma mbele hatua nane kubwa kwa kutumia nguvu bora katika pande nane”, na utekelezaji wa mikakati hiyo iliweka msingi imara kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu wa mkoa huo.

Kuhusu mageuzi ya kimsingi ya njia ya kuendeleza uchumi, na marekebisho ya kimkakati ya muundo wa uchumi, Bw. Xi alitoa mfano wa hali ilivyo ya “ndege wawili”, kwamba alihimiza mkoa huo “kufufuka kama finiksi” kwa “kubadilisha ndege tunduni”, maana yake ni kuunganisha juhudi za kuhimiza makampuni ya Mkoa wa Zhejiang kuendeleza shughuli zake nje ya mkoa huo na kuingiza makampuni bora ya nje kuanzisha shughuli zao mkoani humo, na kufanya ushirikiano na mawasiliano kati ya sehemu mbalimbali, ili kupata nafasi ya kuingiza “ndege” hodari anayetaga mayai mengi na kuruka juu zaidi huku akila kidogo. “Kufufuka kama finiksi”, maana yake ni kuwa na ujasiri wa kujichoma kama finiksi, kuacha kabisa njia isiyo na ufanisi mkubwa ya kuendeleza uchumi ili sekta za viwanda na makampuni vifufuke na kuboreshwa upya.


6.jpg

Mei 23, 2014, Xi Jinping alipofanya ukaguzi katika Kampuni ya ndege za kibiashara ya China aliongea na wanateknolojia wa Kituo cha usanifu na utafiti cha kampuni hiyo

Mwaka 2007, Bw. Xi aliteuliwa kuwa ofisa mwandamizi wa Mji wa Shanghai. Baada ya kufika mjini humo, aliendelea kutetea utandawazi wa Kanda ya Delta ya Mto Changjiang. Kuhusu mpango wa maendeleo ya Shanghai katika siku za baadaye, aliona kuwa mji huo kabisa hauwezi na hauruhusiwi kujiendeleza peke yake, mpango wa maendeleo yake unapaswa kutungwa kulingana na mipango ya maendeleo ya sehemu nzima ya Delta ya Mto Changjiang, na Mji wa Shanghai unatakiwa kuwa kiongozi wa maendeleo ya kanda hiyo.

Maneno yanayoonesha “Moyo wa Mji wa Shanghai” yalikuwa “Shirikiana na pande zote, Tafuta ubora wa juu”. Bw. Xi aliongeza mengine ya “Kuwa na Busara, Moyo Mkubwa na Unyenyekevu”. Vyombo vya habari vya Shanghai vilitoa maelezo vikisema, maneno hayo ya nyongeza si kama tu yameonesha upungufu wa Shanghai katika utendaji wa kazi yake, na kupanua “Moyo wa Mji wa Shanghai”, bali pia ni ahadi ya ngazi ya juu iliyofikiriwa zaidi ya mji huo kwa kuelekea “dunia ya nje”. Maofisa na watu wengi wa sehemu nyingine mbalimbali wamepongeza na kusema, “Shanghai imebadilika.”
 
China ina kiongozi bora sana kuwahi kutokea kwenye nchi yao sema tu wamagharibi hawawezi kukuambia hili Waziwazi, wanaweza kukuaminisha zelensky ni bora kuliko Xi.
 
China ina kiongozi bora sana kuwahi kutokea kwenye nchi yao sema tu wamagharibi hawawezi kukuambia hili Waziwazi, wanaweza kukuaminisha zelensky ni bora kuliko Xi.
China ina viongozi bora toka wakati wa Comrade Mao Zedong wakafatia wakina Deng Xiaoping, Jiang Zemin, Hu Jintao na Sasa Xi Jinping kitu pekee kilichobora ni CPC kwa sababu hii ndio unazalisha na kusimamia viongozi wawe bora
 
Back
Top Bottom