Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KUFANYA BIASHARA SIO JAMBO RAHISI, MTAJI PEKEE SIO LOLOTE
Anaandika, Robert Heriel
Watu wengi wanapenda kufanya biashara, kuna wengine huwalaumu Ndugu zao au Wazazi wao au waume zao Kwa kushindwa kuwapa mitaji, Jambo Moja la uhakika ni kuwa, hakuna ambaye atakupa mtaji ilhali akijua utapoteza pesa zake.
Biashara ni ngumu Sana Ila pia ni rahisi Sana ukifwata kanuni Fulani. Kabla ya biashara kuna mambo yanapaswa yatangulie, mtaji ni kitu cha mwisho katika mambo ya biashara,
Leo sitasema Sana, Acha niiweke hivi;
I/ Jenga jina lako watu wakufahamu na kukuamini eneo ulilopo, hakikisha iwe sifa njema ya kuvutia.
Jina ndilo huamua Hatma yako.
ii/ Tumia jina lako kutafuta na kujenga mtandao wa watu hasa washirika kimkakati.
iii/ Jenga wahusika ndani yako zaidi ya mmoja.
Hii kwenye nadharia ya Utawiwishaji katika kitabu changu nilisema Kwa mfano, Mimi Taikon, ninajipachua nakutoa Taikon zaidi ya mmoja. Kam ifuatavyo;
Taikon 1
Taikon 2
Taikon 3
Taikon 4
Kila mmoja anauhusika wake kama unauwezo wa kifedha basi ajiri watu wachukue uhusika wako,
Taikon 1 unaweza MPA uhusika wa utakatifu, mwerevu, mwenye Busara, Msomi na sifa zote nzuri.
Huyu atakutana na watu wakubwa, wenye hadhi kwenye jami
Taikon 2 huyu utampa Sifa za unyenyekevu, mpenda wanyonge na Masikini, mtatua kero za jamii, Msuluhishi n.k. huyu atakutana na Tabaka la chini Kabisa
Taikon 3 huyu atakuwa Mafia, mambo ya sirini iwe ya kimungu au kishetani, huyu ni mtu wa dili zenye michongo mirefu. Huyu usimdhihirishe mbele za watu, isipokuwa wahusika maalumu kulingana na Mazingira na wakati.
Biashara ndivyo ilivyo, wateja wanatofautiana hivyo lazima uwe na uhusika tofauti.
iv/ Kazi inayokutambulisha.
Labda mwandishi, mwalimu, Fundi, n.k.
Mbali na biashara hakikisha iwe na Fani nyingine ambayo watu wanaijua.
Mfano, mwanamuziki lakini unauza Duka la nguo.
V/ Tafuta Kibali
Hapa lazima upewe kibali cha Kuendeshea biashara, iwe ukipate Kwa Mungu au Kwa Waganga.
Huwezi fanya biashara yoyote bila kibali kutoka kwenye moja ya pande hizo. Usijedanganywa.
Kama vile unavyosumbuliwa ukiwa huna kibali(Leseni) ya kufanya biashara na TRA ndivyo utakavyohangaika usipopata kibali cha kiroho.
Hili ni Jambo kubwa Sana kwenye biashara.
VI/ mtaji
Hii huja mwishoni kabisa.
Hata mambo ya sijui location hayana umuhimu Kama ukiwa na hayo mambo hapo juu.
Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam