Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Kuhusu hao ambao hawajajengwa tangu wadogo ni ngumu sana lakini kama kungekuwa na sheria ngumu katika mahakama zetuKuwajenga watoto tangu wakiwa wadogo... nimekuelewa mkuu.
Nimeona maelezo ya mzee Wa NJEE YA BOX (Mh. Kigwangala) mitandaoni, nimeona maelezo yake jinsi alivyoibiwa, na watu aliowaamini. Pia ulisoma michango (comments) za watu wengine nao wanalalamika kuibiwa na ndugu nk. Suluhisho kwa watu ambao hawajajengwa tangu wangali wadogo ni lipi mkuu, kwa uzoefu wako?
Ambao ndio chanzo cha wala rushwa
Mimi nimeishi na kutembea sehemu nyingi duniani
Kuna nchi zingine nimekaa miaka mpaka 10 huko middle east ambapo ukiiba unakatwa mkono
Kwa kweli unaacha gari milango wazi unaingia shopping na kurudi hukuti hata paka kaingia
Sisemi na sisi tuwakate mikono ingawa mnawachoma moto waizi wa kuku na kuwashangilia waizi wa billions
Kama mahakama wataacha rushwa na kufuata sheria na kuwafunga kila wanapopata ushahidi wa kuwaweka jela basi na iwe hivyo
Angalia suala la majizi ya bandari TPA mahakama bado wanavutana ili mwisho wawafutie kesi
Hawa ndugu wanaoiba pia nao ni mtihani mkubwa yaani unamtumia hela akujengee yeye anazila tu na kukupigia picha ya jengo la mtu huyo sijui utamfanya nini
Taumbeane tu mema ila kuamini hata ndugu huko ni ngumu labda muwe na uelewa mmoja