Kufanya biashara ya ubia partnership na mbongo bora pesa yako ujenge nyumba ya wapangaji

Kufanya biashara ya ubia partnership na mbongo bora pesa yako ujenge nyumba ya wapangaji

Usiwekeze kwa mtu ambae hana cha kupoteza , mtu ambae hajatia hata 100 usiweke pesa yako hapo

Muda pekee hautoshi, nae aweke pesa , sisi hapa tuna 50/50
Tuelezea aina ya biashara ili tujifunze nasi.
 
Biashara za kuaminiana Hapa Bongo
Fanya na wapemba, wasomali au wale waislamu Safi wale wanaosali swala 5 .

Naongea kutokana na uzoefu
sio Maneno ya kuambiwa au kuskia kwa watu.

NB: Mimi Ni mtu wa bara afu mkatoliki[emoji1431]
 
Hii imewasaidia sana. Kwa hili wamepiga gap kubwa sana kwa dini nyingine hizi za kwetu.
Acheni kujidanganya ndugu.Mmefanya utafiti?Vibaka,magerezani wamejaa kina nani? Mitaani kulikokubuhu uongo uongo na utapeli wamejaa dini gani? Acheni sentiments za kidwanzi hili ni tatizo kote na hakuna mwenye afadhali,likemewe kwa nguvu zote.
 
Mtu hujawai hata kufuga kuku au kuuza mayai utotoni alfu unakuan kupata dola 100000 kwanin usipigwe vzr

Biashraa lzm uwe na uzoefu hata na cjcjote ndio utawaelewa watu
 
Watanzania wenzangu mnao toka ughaibuni kwa lengo la kuwekeza nyumbani na kufanya biashara ya ubia na hao waswahili walio zeekea hapa hata hajawahi kuvuka mpaka kuenda Kenya au Uganda muwaogope sana kufanya nao partenership.

Utakufa kwa pressure stress au fatique hao watu bado hawajastaharabika kama Ulaya mnavo ona kwamba bishara zinazo shamiri sana ni zile za ubia/partnership na watu wana aminiana.

Watanzania/waswahili wenzetu wana kila aina ya vitabia vibomvu awe msomi au sio msomi kama haja wahi kuishi nje ya Tanzania usimuamini kibiashara. Wengi ni:
  • Waongo
  • Sio waminifu kibiashara
  • Wezi
  • Wavivu wa kufanya kazi
  • Matapeli.
  • Wanapenda raha sana
  • Hupenda kuongea sana na simu hata wakati wa kazi.
  • Limbukeni
  • Wana showoff za kishamba
  • Wanaamini kwenye uchawi.
  • Wanafiki nk.
Ili limetokea kwangu ndugu na rafiki zangu zaidi ya watano the most recent ni huyu rafiki yangu wakaribu alio toka Norway baada mwaka jana ya kuka huko miaka zaidi ya 10 kukusanya mtaji. kamuka asubuhi mbia wake kakimbia na mtaji wote na ofisi imefungwa na simu zake zote hazipatikani.

Jamaangu kachanganyikiwa zaidi $35,000 zimepotea anajipanga upya tena kwasbb hawezi kurudi ughaibuni tena. Jamani lindeni pesa/mitaji haipatikani kirahisi kaa mbali na marafiki wasio kuongezea thamani yoyote kwenye maisha yako.
Kwa hiyo watanzania wote ni kati ya hao ndugu zako watano? Partnership inasumbua sana kwa Africa, lakini hata ughaibuni bado ni shida.
 
Kwa hiyo watanzania wote ni kati ya hao ndugu zako watano? Partnership inasumbua sana kwa Africa, lakini hata ughaibuni bado ni shida.
Hi ni sampling tu, wewe ukiwa nataka kujua maharage kama yameiva unabonyeza kila harage au unacheki mawili tu?
 
Watanzania hawa wa sasa hata mtu akikupa promise usiamini; watu wanawaza kupiga; Taasisi na visheria za Serikali too many red tapes na kila mtu anaamini bakshishi / rushwa ni haki yake; yaani akifanya kitu lazima umlipe akikupa tender lazima mgawane (kwahio hata ukiwa huko ukatuma pesa huku kwa mdau wako huenda utendaji ukawa mgumu kutokana na mambo ya ajabu ajabu / unpredictability ya nchi yetu...)

Ila sifa hii sio sifa ya Watanzania enzi za Mwalimu (wale walikuwa waaminifu) wakti huu watu wanajiona wajanja kukuibia au kukuangamiza (partnership atataka aibe ili ajenge kwake / yake) In short if you can..., do it alone usichoweza bora ufanye outsourcing
 
Ahahahahaha..nikiwa form 5 boarding, nilijichanga changa vile vi pocket money nikamuomba mama pale dukan kwake niweke vinywaji nikampa pesa ya kreti kama 7 kwa kuanzia (ilikia 2008)...eeehhh narud likizo ya mwisho kumaliza kidato cha sita kala pesa zangu zote....hakuliongelea hilo wala kuomba msamaha nami nikatulia kimyaaaa 😂😂😂
2008 mimi nilikua class 2
 
Kwamba zile Karo, na tujipesa twa hapa na pale unadhani alitoa wapi au na yeye akianza kudai pesa za lactogen?

Ofcourse ni wajibu wake kukupa ziwa na uji na hata kaptula yenye viraka ila moccasin, raba mtoni na saa ya kukonyeza hizo ni extra...; Kwahio Mkuu piga Kimya.... (ili mambo yaende huwa tunasema wakubwa hawakosei)

Funika Kombe Mwanaharamu Apite....
 
Ni kwel lakin mbona hata hizo pocket money ni wao ndio walikua wakinipa so ilihakiwa anitie moyo kwa kuona sichezei pesa wanazonipa bali nazi thamini. Ila yeye akaona kama sina matumiz nazo sijui??? 😅😅
 
Watanzania wameshajenga culture ya kuiba sehemu ya kazi. Infact kuiba kazini inaonekana kama ndiyo ujanja na usipoiba unakuwa mjinga kwa jamii.
Shida sio kuiba. Mishahara tunalipana midogo halafu wale ma top wawili watatu wao ndio wanakatiana mafungu marefu. Shida huanza hapo ukigundua pia wanawapigaga nyie wa chini. 😀
 
Ni kwel lakin mbona hata hizo pocket money ni wao ndio walikua wakinipa so ilihakiwa anitie moyo kwa kuona sichezei pesa wanazonipa bali nazi thamini. Ila yeye akaona kama sina matumiz nazo sijui??? 😅😅
Basi tu pesa haikai na ilipata matumizi mengine, am sure angekuwa na za ziada angekuongezea au huenda yeye sio business minded kama wewe..., ukweli ni kwamba Biashara nyingi za Bongo ni zima moto hizo soda zipo dukani ili wageni wakija pia wanye kuliko kununua kwa mangi; sukari ikiisha ni dukani kwahio kanakuwa ni ka mradi fulani hivi kasikokuwa bali kanapigana tafu na wanafamilia (nipe nikupe)
 
Back
Top Bottom